Mkuu Kobello,
Napenda kurudia tena kwamba mimi sio mwanasheria, lakini nimejifunza kwamba bila kutumia muda wa ziada kuwa mwelewa wa sheria, hoja zako juu ya muungano zitatawaliwa na siasa zaidi, na hautaishiwa hoja; Lakini iwapo hoja zitaegemea sheria, basi utarudia yale yale tu kimsisitizo;
Nimeona kabla sijapitiwa na mambo mengine, nijibu hoja yako ifuatayo:
Sikubaliani na wewe kuwa Articles of the Union zilikuwa ndiyo sheria mama
Bandiko namba 77 katika mjadala wetu huu ndio msingi wa hoja yako hiyo juu, lakini pia umezungumzia mengine kadhaa, lakini yoye ukilenga kuhalalisha muungano wetu chini ya mfumo wa sasa, huku ukijaribu kukitetea CCM, tangia enzi za TANU kwamba walifuata taratibu zote. Ningependa kujibu hoja zako hizikama ifuatvyo:
Kwanza, bila ya CCM itakayojirudi na kukubali kwamba ilikosea kuhusu:
- Uendeshaji MUUNGANO; na
- Mauaji ya Azimio la Arusha
Kifo cha CCM yenye kukana hayo hakipo mbali. Ndio maana suala la muungano linaipa CCM presha kubwa kwani ni yenyewe (enzi za tanu), ndio iliuwa Tanganyika kwa mujibu wa sheria ya bunge, sheria namba 24, ya mwaka 1967. Kwahiyo defense strategy kama hizi unazotumia ku-spin facts ni kitu ambacho lazima tukitegemee, kwani huko ndiko kupumulia kwenye mashine, na pengine kifo kitaepukika. Vinginevyo CCM is clinically dead, na nikutokana na mambo mawili hayo hapo juu (Muungano & Azimio la Arusha);
Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi, hakika wewe ni such a political spinner; Nitafafanua hili; Unajenga hoja nzuri sana, kwa kutumia vipengele vilivyopo lakini kwa njia ya kupotosha na pia kuaminisha wengine kwamba kinachoonekana ni BLUE, kama wao wanaona ni KIJANI, basi wana matatizo ya akili; Ningependa kujirudia tena, kwani tabia ya kujirudia rudia ovyo ni sehemu ya kuwa na tatizo la akili; Nitajaribu kutumua hoja za Kisheria zaidi Kuliko Siasa, na naomba wadau wengine wanipime kwa hilo na wawe wazi kunikosoa;
Hoja yako ya kupinga hoja yangu kwamba Mkataba wa Muungano haukuwa sheria mama, nitajirudia tena kama taahira kama ifuatavyo, kwa njia ya maswali:
Swali la Kwanza: Je, kabla ya Mkataba wa Muungano, 1964, kulikuwa na kitu gani?
Jibu ni kwamba kulikuwa na taifa la Tanganyika yenye miaka miwili na ushee ya Uhuru, Kulikuwa na Taifa la Zanzibar lenye miezi kama minne ya uhuru wa mapinduzi; Pia kulikuwa na taifa la Uganda, Kenya, n.k.
Swali la Pili: Je, kama ni hivi kwanini Tanganyika haipo?
Jibu ni kwamba, nchi huru za Tanganyika na Zanzibar ziliamua kuingia MKATABA wa KUUNGANA ili kuwa JAMHURI MOJA, Sio SERIKALI MOJA; Tutaona baadae suala hili kwa undani;
Swali la Tatu: Je, Mkataba Ulijengwa kwa Nguvu Ganui ya Kisheria?
Jibu ni kwamba, Mkataba wa Muungano, 1964, ulichukua nafasi ya Sheria Mama, kwa matarajio kwamba, Muungano wetu utapewa nguvu za kikatiba ndani ya mwaka mmoja; Ni hapa ndugu Kobello unapoanza spins zako; Nitafafanua; Unaelezea vizuri sana yaliyojiri huku aidha kwa kujua au kutojua, unaruka mambo mengine muhimu zaidi ya kusaidia kufungua kiini macho hiki cha muungano; Kwa mfano, hoja yako kwamba Katiba ya Tanganyika ilikubaliwa ndio iwe Katiba ya Muda, hakuna anayebisha hili, mpaka hapa tupo sawa; Lakini hauelezei watanzania waliopo humu kwamba, ili hilo lifanikiwe, katiba ya Tanganyika ilitakiwa ifanyiwe marekebisha kwanza, bila ya hivyo, Mkataba wa Muungano, 1964 ungeendelea kuwa nguzo pekee ya kuhalalisha muungano;
Kwa makusudi au kwa kupitiwa, hautaki kujadili yaliyomo katika Mkataba wa Muungano, 1964, hasa pale unapoweka masharti juu ya matumizi ya Katiba ya Tanganyika kuwa Katiba ya Muda ya Jamhuri Mpya ya Muungano wa Tanzania (katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja). Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, ibara ya tatu inasema hivi:
(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:
a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar;
c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.
Bila ya Katiba ya Tanganyika kufanyiwa marekebisho katika maeneo haya, ili kuupatia Muungano wetu Uhalali na Nguvu ya Kikatiba, Katiba ya Tanganyika isingekuwa na uhalali au nguvu ya kutumika kama Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na badala yake, ingebakia na nguvu yake kwa upande wa Tanganyika, kama ilivyokuwa kabla ya Muungano baina ya taifa huru la Tanganyika na Zanzibar; Kwa maana hii, basi Mkataba wa Muungano, 1964, ungebakia kuwa ndio nyaraka peke yake ya kuhalalisha muungano wetu, hivyo kuendelea kuchukua nafasi ya Sheria mama katika kipindi cha mpito;
Mbali na marekebisho haya ya Katiba ya Tanganyika ili ipate nguvu za kikatiba kuendesha Muungano wakati wa kipindi cha mpito, pia kulikuwa na sharti lingine ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, sharti ambalo lilikuwa ni muhimu kuliko yote, kwa maana ya kuupatia Muungano wetu sasa nguvu kamili na uhalali wa kisheria wa kudumu; Sharti hili ambalo pia unakwepa kulijadili kwa mtindo wa ku-spin issues, lipo katika kipengelea cha saba cha Mkataba wa Muungano ambacho kinasema hivi:
vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Nadhani sasa tupo tayari kudadisi kwa undani zaidi kuhusu Mkataba wa Muungano, 1964, na nguvu yake ya kisheria;
Kwanza tukubaliane kwamba wakati wa makubaliano yale, ilitarajiwa kwamba kipengele cha saba cha Mkataba ule kingefanyiwa kazi kwa haraka sana ili Muungano wetu uweze kupata katiba yake ya Kudumu; Sasa nini kilitokea?
Kwanza, kilichotokea ni kwamba Katiba ya Tanganyika haikufanyiwa mabadiliko yoyote kama ilivyokusudiwa;
Pili, tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, nayo haikuteuliwa;
Kwa hoja hizi mbili, mkataba wa Muungano, 1964, uliendelea kuwa ndio nyaraka pekee halali, kinyume cha matarajio na pia madhumuni yaliyokusudiwa;
Mazingaombwe yafuatayo yakaanza:
Moja, katika hali isiyokuwa ya kawaida, ilipofika Julai 10, 1965, Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, likapitisha sheria iliyolenga kuhairisha INDEFINATELY, ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964 amacho kilitoa sharti hili (nirudie tena):
vii) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Badala yake, bunge hili KINYUME NA MKATABA WA MUUNGANO, 1964, ibara ya ‘7', likapitisha Katiba ya Muda (SIO KATIBA YA KUDUMU), chini ya Sheria namba 43 ya 1965.
Msisitizo: Hapa tunaona mazingaombwe kama ifuatavyo: As of 1965:
- Kipindi cha mpito per articles of the union, 1964, kwamba kisizidi mwaka mmoja, kina expire huku ibara ya saba ya Articles of the Union ikiwa haijatekelezwa na vile vile, ibara ya pili nayo ya kurekebisha Katiba ya Tanganyika ili iwe na uhalali wa muda kama katiba ya Jamhuri, nayo haijarekebishwa; Katika hii expiry date, Mkataba wa Muungano unaendelea kuwa the only document that can be regarded as "SHERIA MAMA", whether by accident au kwa makusudi, tutaona in the future kwenye mjadala huu;
- Kwa vile as of 1965, ambapo nchi haina katiba yenye nguvu ya kisheria per articles of the union, kama nilivyoeleza hapo awali, ibara ya saba ya articles ambayo inaweka sharti la kuteuliwa tume huru ya katiba kutoka pande mbili za muungano, sharti hili linakuwa postponed kupitia sheria ya bunge, tena INDEFINATELY, kisha bunge hili hili ambalo halina uhalali wa kikatiba na wala halina uhalalo per articles of the union, 1964, linapitisha katiba nyingine tena (mpya) ya MUDA (sio ya kudumu), chini ya sheria namba 43, 1965; katiba hii ikaendelea kuwepo kwa miaka 12 mpaka pale akili ya kuzidi kuchakachua muungano kwa uhalali wa kisiasa ilipowadia: TANU + ASP = CCM (1)being equated as TANGANYIKA + ZANZIBAR = TANZANIA (1);
Msisitizo: Ndani ya mwaka mmoja wa muungano, tunahamia kutoka katiba YA MUDA ya Tanganyika ambayo haikurekebishwa, kwenda kwenye Katiba nyingine YA MUDA TENA, huku ibara ya ‘7', ambayo ndio nguzo kuu ya muungano, ikihairishw INDEFINATELY;
- Bunge pia mwaka 1967, likapitisha sheria namba 24, iliyompa Rais wa JMT mamlaka ya kubadilisha jina kutoka Tanganyika, kuwa Tanzania; Kwahiyo, Tanganyika iliuwawa kwa mujibu wa bunge la JMT, ambalo hata hivyo kwa waelewa, tayari wanaona kwamba bunge hili halikuwa na uhalali wa kikatiba in terms of its existence, lakini pia kujihusisha na masuala ya ku deal na majina ya nchi shirikishi, kwani suala hili halikuwa la muungano, bali la nchi shirikishi; Suala lingine la kufanya bunge hili lisiwe halali kama bunge la JMT ni kwamba ibara ya 3 (c) haikuwa imefanyiwa kazi, nayo ni:
"(iii) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:
(c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano;
Swala la mwisho ambalo ningependa kuliweka hapa ni lile la TANU, hasa jinsi gani chama hiki kilivyojipenyeza katika masuala ya Muungano, kinyume cha Mkataba wa Muungano, 1964; Kwanza ijulikane kwamba katika Mkataba ule, hakuna sehemu ambapo TANU au ASP, na hata CCM, vinatajwa; masuala ya vyama yalitakiwa yabakie katika nchi husika – Tanganyika na Zanzibar, na muungano ushughulikie masuala yale kumi na moja tu katika kile kipindi cha mpito mpaka katiba mpya itakapopatikana; Katiba mpya haikutokea, na hili nimelijadili tayari;
Kama nilivyojadili, katika Mkataba wa Muungano, 1964, TANU haipo, wala ASP; Lakini cha ajabu, katika Katiba ya Muda ya 1965, tunaona TANU ikiingia humo. Katika ibara ya tatu ya katiba ya muda, 1965, inasema hivi:
- (1) Kutakuwa na Chama Kimoja Cha Siasa Katika Tanzania.
(2) Mpaka hapo TANU itakapoungana na ASP, na kufanya chaa kimoja cha Siasa, Chama hicho cha Tanganyika Kitakuwa ni TANU na kwa Zanzibar Kitakuwa ni ASP;
Natumaini kipengele hiki kinampa makengeza msomaji yoyote na kufikiria nimekikosea; Hivyo ndivyo kilivyo, kwa lugha ya mtaani - FULL KIINI MACHO; Zanzibar hapa ikapigwa teke la kisigino, kwani TANU ikawa Supreme to Katiba ya 1965, na Muungano kwa ujumla; Katika majibu yangu mengine humu, niliweka sehemu ya maneno ya Pius Msekwa aliyosema kwenye kitabu chake cha Towardes Party Supremacy (1977), ambapo, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, analiweka hili bayana;
Vinginevyo, kuanzia tarehe ambayo katiba ya Muda, 1965, ilianza kutumika, ina maana kwamba KANUNI ZA TANU na KATIBA YAKE zikawa zimefanywa kuwa sehemu za Sheria ya Jamhuri ya Muungano; Madhara yake kwa Zanzibar hapa ilikuwa nini? Kwa wale waelewa, kamwe hawawezi kuwalaumu ndugu zetu wa Zanzibar kwa kutafuta autonomy yao ndani ya muungano wetu, per articles of the Union, 1964;
Huu ni mtiririko wa baadhi tu ya matukio, na kama unavyo ona, hoja zangu zimejaa mtazamo wa Kisheria, kuliko Kisiasa kama unavyopenda kuaminisha watu, ambayo yalijeruhi muungano, badala ya kutimiza wajibu wetu wa kulinda na kutetea mkataba wa Muungano, 1964.
Nitazidi kutoa mawazo yangu KISHERIA, hasa kuhusu matukio yaliyotokea baada ya mwaka 1967 Tanganyika ilipouawa kwa mujibu wa sheria za bunge, kinyume na Mkataba wa Muungano; Nitalenga hasa kuzaliwa kwa CCM, 1977, na madhara kwa Mkataba wa Muungano, 1964; Lengo kuu itakuwa kuonyesha jinsi gani CCM ILIYOSHIKA HATAMU, ilivyozidi kukiuka Mkataba wa Muungano, 1964; Ninatarajia ntakuwa mzima na ninaishi by the time Napata muda wa kuliweka hilo humu;