Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Ungejikita katika kujadili hoja yangu kuhusu aina tatu za uhusiano wa mataifa, huku pia ukijibu maswali yangu baada ya maelezo yangu katika kila eneo, suala hili serikali ya Kwimba, Itigi, Monduli,n.k, suala ambalo kwa ustadi mkubwa sana unajaribu ku-spin ili kuajengea watu kiini macho zaidi, attending hoja yangu ile na kuijibu in full, ingeangusha juhudi zako zote za ku-spin suala hili la serikali, ambalo awali ulikuwa unajadili jamhuri moja kama vile ndio serikali moja, na baadae ukajisahihisha; Kwa vile umekataa kujadili suala la aina ya ushikiano wa mataifa, ni matumaini yangu kwamba wapo waliofuatilia nachojaribu kusema na wamenielewa;
Okay tuachane na hili kwanza.
 
Asante Mkuu;

Kwa hoja hii, sasa kwa vile hapo ulipo una mkataba wa muungano na sheria ya muungano:


  • Tukianza na Mkataba wa Muungano, 1964, tazama ibara ya 4 (a hadi k) na ibara ya '5' (a hadi c);

  • Kisha, nenda kwenye Sheria ya muungano na utazame ibara zifuatazo: Kifungu cha pili kinachotoa maana ya sheria na pia kifungu cha 5(a, i hadi xi);

The discrepancy utakayoikuta ndio msingi wa hoja yako, na ndio hoja yanguya msingi ambayo tumekuwa tunazungushana kwa masaa zaidi ya 24, kwani discrepancy hiyo ndio haswaaaa kiini macho kinachobeba mada hii, na vile vile kwa kiasi kikubwa hoja ya LISSU;

Nadhani mimi na wewe sasa tunaweza kusonga mbele kujadili hoja nyinginezo;
Okay,
Kwanza kabisa, tukubaliane kuwa two republics zilikubaliana zifanye one sovereign republic.(4) cha sheria ya muungano.
Pili angalia kifungu cha nne (a} cha mkataba (siyo sheria) kuhusu nani anaweza kurekebisha existing laws za Tanganyika na Zanzibar (tafadhali angalia neno "hereafter").
Twende taratibu tusijadili vipengele vingi kwa wakati mmoja.
 
Swadaktaa!!!

Hakuna mabo ya Tanganyika yasiyo ya muungano na hayajawahi kuwepo.

Kwa hiyo hakuna mambo yasiyo ya Muungano kwa upande mwengine(Tanganyika) wa Muungano, mambo yasiyo ya muungano yapo kwa Zanzibar pekee?

Kama jibu litabakia kuwa hakuna...je Tanganyika na Zanzibar waliunganisha mambo yepi? mangapi?

Kobello

Unapokasimu madaraka yako, maana yake ni kuwa umekufa? umeuawa? umejifuta?
Je kukasimu madaraka ina maana ipi? Au kukasimu ni kufanya mazingaombwe/kiini macho?
 
Kwa hiyo hakuna mambo yasiyo ya Muungano kwa upande mwengine(Tanganyika) wa Muungano, mambo yasiyo ya muungano yapo kwa Zanzibar pekee?

Kama jibu litabakia kuwa hakuna...je Tanganyika na Zanzibar waliunganisha mambo yepi? mangapi?

Kobello

Unapokasimu madaraka yako, maana yake ni kuwa umekufa? umeuawa? umejifuta?
Je kukasimu madaraka ina maana ipi? Au kukasimu ni kufanya mazingaombwe/kiini macho?
Serikali ikikasimu madaraka yake kwa serikali nyingine, hiyo serikali imekufa.... haipo.
Ndiyo, mambo yasiyo ya muungano yapo Zanzibar pekee, Zanzibar ina serikali kama ya halmashauri ya wilaya ya Ilala.
kwa sababu nayo ina executive (meya or whatever), legislature (madiwani,mbunge) na judiciary mahakama za wilaya au city courts. Ila ina jurisdiction ndogo kulinganisha na ya muungano.
 
EMT,

nashukuru kwa Hotuba hii ya Tundu Lissa, sasa nadhani tuna nyenzo zote muhimu za kutusaidia kubaini zaidi kiini macho hiki, lengo likiwa ni kuboresha muungano wetu, sio kuuvunja;

cc: jmushi1

Mchambuzi kwanza tukubaliane kimisngi kuwa lengo ni KUBORESHA na si kuvunja

The idea that the union came into being under dubious circumstances [that is, law making bodies of two republics were not involved or the general population of parties concerned were in the dark] is founded. But that is not sound to discredit the union as whole.

Hizo articles of union nazo ziko vague, hazielezi kwanini tuliungana na nani alitoa baraka ya kisheria na kama alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo au la, ili muungano uwe hai kisheria. Lakini hilo si muhimu kwa kuwa, mtoto ni mtoto kama ni illegitimate au legitimate. Akiwa hai yuko hai na ana haki kama mtoto mwingine yeyote.

Lakini ningependa tukubaliane kuwa kuna uwezekano kuwa Muungano si wa Nyerere na karume peke yao kama baadhi ya watu kutoka Pemba wanavyotaka tuamini, lazima other senior officers were involved. Na nina hakika kuwa at that hour walitumia busara kutokana na mazingira ya saa ile, na kufanya uamuzi sahihi kwa saa ile, kwa matumaini kuwa yatakuwa na manufaa kwa siku zijazo. In a way, rais ni legal representative wa nchi, kwa hiyo kama ana executive powers za kufanya maamuzi kwa niaba ya nchi, basi uamuzi wake unaweza ukawa na thamani ya kisheria.


Tukianza kupitia neno kwa neno kwenye artciles of union tutaona weaknesses nyingi sana kwa kuwa iliandialiwa katika mazingira ya ukilaza. walioandaa hawakuwa na mwanga wa kutosha na mazingira yao wakati ule yalikuwa ya kidikteta na hali ya hewa ulikuwa ni ukombozi kisiasa. Lakini kusema muungano haufai kwa kuwa ulianza vibaya, na hauna msingi wa kisheria, si hoja yenye maana sana.

Lakini hebu tuangalie hoja za sasa. Anayesema anataka Zanzibar iwe huru maana yake nini? Na Zanzibar itakuwa tofauti kwa namna gani na sasa baada ya kuwa huru? Kuna hoja nyingi mbazo kwangu huwa naona ni za kipuuzi.

1. Serikali ya Muungano inaizua Zanzibar kuomba misaada kutoka kwa waarabu. This is complitelte bull.... kwa kuwa sidhani kama lengo la uhuru ni kuwa ombaomba.
2. Zanzibar ina mafuta, serikali ya muungano ina hila ya kuataka kutumia mafuta ya Zanzibar ndio maana inang'ang'ania muungano. This is also bull kwa kuwa tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa kuna traces za mafuta na sio mafuta ambayo yanaweza kuchimbwa commercially.
3. OIC au uanachama katika jumuiya za kimataifa and such kind of things, ambavyo siamini kama kweli vitastrengthen uhuru wa Zanzibar zaidi ya kuwaingiza kwenye mikono ya waarabu.
4.....

Angalia ni vipi ZNZ italipa gharama za idara zile za muungano zikiwa nje ya muungano, ni vipi itapoteza soko kwa wafanyabiashara wake waoneemeka huku bara, ni vipi wanaweza kumudu chakula kutoka bara kwa Forex, na kuingia bara kwa visa. Au wazenji wote wa bara kuwa foreigners na kuanza kuishi kwa vibali. Angalia econimics ya Zanzbiar kwanza. Ukiangalia hata Seif Sharif Hamadi Mwenyewe unaweza kuona kaka yake ana hoteli pale kisutu kama hawapendi muungano sijui kwanini walijenga ile hoteli pale kistu na zile biashara zao za jumba la sinema kule Mbeya.
Kwa hiyo ukisikia siasa unaona haziendani na realities za uchumi. So let us think of this without Seif Sharif's infulence na siasa zake.


Kwa upande wa bara kimisngi hakuna hoja kubwa, labda hoja ni kuwa jamaa some how ni infestors hapa bara, [Yes infestors, not Investors], na kuwa wanatagemea mengi kutoka bara, lakini sioni ubaya kwa kuwa wao ni sehemu ya Tanzania.

Anayesema anataka Tanganyika aseme how will it be different from current Tanzania, na aseme vipi tunaweza kudeal na Zanzibar huru ambayo itakuwa hot bed ya magaidi Afrika mashariki baada ya waarabu kuanza kumiminika kule na kutumia fedha kwa kuwahonga wale wanaopenda kuwa ombaomba kujifucha na kupanga shughuli zao za kigaidi (idea ambayo Seif fancy alot) . Au ambayo watu wake wataanza kukumbilia kwa ndugu zao wa bara baada ya kuona usultani umerudi tena na weaknesses za upweke.

The idea that Tanzania bara is going to be affected by losing territorial waters bado haina msingi kwa kuwa hata sasa hatuna tunalotumia kwa hiyo bahari kubwa tuliyonayo zaidi ya kuvua samaki wawili na kuongelea. Japo naweza kukubalina na wanaosema Tanzania bara hainufaiki na muungano, bado sinajona ni wapi tunaingia hasara kutokana na muungano.


My point is, we have muungano now, Kimisngi ni jambo zuri kiuchumi lakini unatakiwa kuboreshwa ili unufaishe zaidi pande zote mbili, na si kuwa mzigo na chanzo cha kuwalaumu wabara .
 
Serikali ikikasimu madaraka yake kwa serikali nyingine, hiyo serikali imekufa.... haipo.
Ndiyo, mambo yasiyo ya muungano yapo Zanzibar pekee, Zanzibar ina serikali kama ya halmashauri ya wilaya ya Ilala.
kwa sababu nayo ina executive (meya or whatever), legislature (madiwani,mbunge) na judiciary mahakama za wilaya au city courts. Ila ina jurisdiction ndogo kulinganisha na ya muungano.

Kobello

Serikali ya Zanzibar ina serikali kama halmashauri ya wilaya ya Ilala.
Unakusudia kusema serikali ya Zanzibar ni kama serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala.

Tanzania ina serikali kama halmashauri ya wilaya ya Ilala?
Serikali ya muungano ni kama serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala pia?

1. Nini uhusiano ulipo baina ya serikali ya Jamhuri ya muungano na serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala?

2. Ni uhusiano upi ulipo baina ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar?

Unaelewa kuwa kuna orodha ya mambo ya muungano? Yale mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano ni mambo ya nani?
 
Nguruvi3,

Cc: Kobello

Kuna swali la Kobello ambalo umejaribu kulijibu, bado majibu yako yanarudi kwenye neno sheria ya mwaka 1964.

  1. Naomba ufafanuzi kama sijaelewa. Je, kuna kitu kinaitwa sheria ya 'Article of union'?
Hakuna kitu kinachoitwa SHERIA YA ARTICLE OF THE UNION na sijajenga hoja ya namna hiyo; Kilichopo ni Sheria ya Muungano, 1964; Na kama alivyosema Kobello, ni sahihi kwamba dhumuni la Sheria hii ilikuwa ni ku ratify Mkataba wa Muungano, 1964; Kwa maana hii, Muungano ulianza kwa Mkataba, na ulikuwa unasubiri sheria ya kuu halalisha, ndio maana Sheria ya Muungano, 1964, ikalenga kuupa Mkataba huu nguvu na uhalali wa kisheria; Lakini ninapopishana na Kobello ni sehemu ndogo sana. Kwa kifupi ni hivi:

Tofauti na matarajio kwamba Sheria ile ingefuata makubaliano yaliyomo ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964, uchakachuaji ukaanza; Kwanza - Bunge la Tanganyika ndio lililo pitisha Sheria hiyo ya Muungano, which was OKAY, kwani Mkataba wa Muungano ulisema pia kwamba – Katiba ya Tanganyika itakuwa katiba ya Muda (mwaka mmoja), ili taasisi ndani yake zifanye kazi kama hizi kwa ajili ya Muungano; Lakini, Mkataba wa Muungano ibara ya 3(a hadi d) ikaweka sharti kwamba Katiba ya Tanganyika itakuwa na uhalali wa kuwa katiba ya muda ya Tanganyika iwapo tu, ITAFANYIWA MAREKEBISHO kama yalivyo orodheshwa kwenye ibara ya ‘3' ya Mkataba wa Muungano, 1964; Sasa mvutano wa kisheria baina ya Mkatab wa Muungano na Sheria ya Muungano kwamba nani ndio mwenye uhalali, ukaanza pale Katiba ya Tanganyika ilipoachwa ifanye kazi kwa masuala ya JMT, bila ya marekebisho per articles of the union; Tatizo likaanzia hapa, Kwahiyo Katiba ile haikuwa na uhalali wa Kisheria, kupitia chombo cha kutunga sheria, kutunga sheria ile;

Tatizo la pili ambalo likajitokeza ni kwamba – hata Sheria yenyewe ya Muungano, nayo ikachakachua kipengelea muhimu sana cha Mkataba wa Muungano, hivyo kuzidi kukosa uhalali wa kisheria juu ya masuala ya Muungano; Tutazame kidogo hili; Ibara ya ‘5' ya Mkataba wa Muungano, 1964 inasema hivi:

"SHERIA ZILIZOPO TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZIENDELEE KUWEPO NA ZITUMIKE NDANI YA MAENEO YA NCHI HIZO";

Na katika sehemu muhimu kuliko zote ambazo Sheria ya Muungano ilitakiwa to ratify ilikuwa ni ibara hii As it is, hakuna cha kutoa, hakuna cha kuongeza; lakini ebu tazama Sheria hii namba 22 ya Muungano ilichofanya, pale ilipotamka haya:

"SHERIA ZILIZOPO VITABUNI NA ZISIZOANDIKWA WAKATI WA MUUNGANO HUO UKIANZISHWA, LAKINI HAZIJUMUISHI KATIBA YA TANGANYIKA KATIKA KULE KUITHIBITISHA KWAKE KUWEPO KWA SERIKALI YA TANGANYIKA AU SHERIA NYINGINE AU TAMSHI AMBALO LITAPOTEZA NGUVU ZAKE KUTOKANA NA KUANZA KUTUMIKA KATIBA YA MUDA"

Suala la ku-note hapa ni neno ZISIZOANDIKWA WAKATI WA MUUNGANO HUO, meaning kuna vijisheria vingine nje kabisa ya Mkataba wa Muungano vikaingizwa kwa hila; vile vile, Sheria hii mbali ya kwenda kinyume na Makubaliano ndani ya mkataba, pia ikaanza mchakato wa KUUA TANGANYIKA, lakini kwa kuanzia, kwa KUUA KATIBA YA TANGANYIKA, tofauti kabisa na ilivyokubaliwa chini ya Mkataba wa Muungano; Kifungu cha ‘7' sheria hii kilitamka hivi kuhusu hilo:

"Wakati katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano itakapoanza kutumika, Katiba ya Tanganyika itakoma kuwa na nguvu kwa ajili ya Serikali ya Tanganyika kama sehemu tofauti ya Jamhuri ya Muungano"

Kumbuka matatu hapa:

La Kwanza - Mkataba uliagiza mchakato maalum ufuatwe kuleta katiba ya kudumu ya JMT, kupitia ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964; Lakini cha ajabu ni kwamba, Bunge la JMT (ambalo tayari tumeona sio halali kwa masuala ya JMT hapa), lika hairisha indefinitely mchakato wa katiba mpya;

La Pili – Bunge hili lika hamisha JMT kutoka kwenye katiba ya Muda ambayo ilikuwa ni ile ya Tanganyika kama ilivyo (badala ya kuwa ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho maeneo fulani, Per Articles of the Union, 1964, ibara ta tatu - ili Zanzibar nayo wawe na nguvu), Bunge hili (haramu), lika hamisha JMTT kutoka kwenye katiba hii haramu ya Muda, na kuingiza JMT kwenye Katiba nyingine ya Muda, 1965;

Na tatu, -kumbuka, miaka miwili baadae yani 1967, Bunge hili hili, kupitia sheria namba 24, likaizika rasmi TANGANYIKA, na kuibatiza then then Tanganyika kuwa TANZANIA;

Nadhani mpaka hapo unaona naposema uchakachuaji nina maana gani hasa - Sheria ya Muungano, 1964 ilifungua njia ya kuvuruga kila kitu kilichoafikiwa ndani ya Mkataba wa muungano, 1964, kama tulivyo ona – lakini la muhimu hapa pia ni kuvuruga lengo halisi la Mkataba ule la kuwa na shirikisho la serikali tatu;

Na hii ndio maana kwa kipindi kirefu sana, nyaraka ile (Mkataba wa Muungano, 1964), ilikuwa ukikutwa nayo ni sawa na kukutwa na tani moja ya Dhahabu chumbani kwako enzi za UJAMAA; Ebu jiulize, kwanini ilikuwa hivi???

Ndio maana hadi leo hii, Mkataba wa Muungano unabakia kuwa nguzo kuu ya Muungano wetu, na ndio maana hakuna anayezungumzia suala la Sheria ya Muungano, 1964, kwani kwa yaliyotokea, ni aibu!

2. Katika post# 8, umesema muungano umeipora Zanzibar autonomy tena baada ya kupigana katika mapinduzi.

  1. Je, unadhani muungano unapaswa kufuata njia ya uhuru au ni makubaliano baada ya kuwa huru?
Muungano ni lazima utokee baina ya nchi huru mbili au zaidi, kwani bila ya taifa kuwa huru, mkataba huo haukubaliki chini ya sheria za kimataifa; Mkataba wa Muungano, 1964, unakubalika kimataifa kwa sababu as of 1964, nchi zote mbili za Tanganyika na Zanzibar zilikuwa ni dola na pia jamhuri mbili huru, kwa mujibu wa sheria za kimataifa; Kwahiyo kimataifa, hauna shida, TATIZO ni uhalali wake na pia nguvu yake kisheria katika nchi shirikishi, kwa sababu nilizojadili;

b)Umeorodhesha mambo 11 ya Article of union. Je, endapo tungebaki na hayo 11, autonomy ya Zanzibar ingekuwa intact au bado ingekuwa imeporwa?

Swali zuri sana; Hata kama masuala yale kumi na moja yangebakia kama yalivyo, hili peke yake lisingepelekea autonomy; autonomy ingekuja iwapo Muungano ungeheshimu aina za serikali zilizokusudiwa, sheria zilizoagizwa zitumike katika kipindi cha mpito, na nini mchakato uliokubaliwa utumike ndani ya kipindi cha MWAKA MMOJA, Per Articles, hasa:


  • Kwa kurekebisha Katiba ya Tanganyika ili iwe na nguvu ya kuwa katiba ya JMT, huku the original Katiba ya Tanganyika, iendelee kuwa katiba ya Tanganyika, huku Zanzibar ikitegemea kupata nguvu zake za kikatika kupitia utekelezaji wa Mkataba wa Muungani, ibara ya ‘7'.

Haya yote hayakutekelezwa, na badala yake, kilichotokea ni matukio ya kukiuka Mkataba wa Muungano kama nilivyojadili hapo juu: Bunge la JMT kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika (ambayo haikafanyiwa marekebisho ili iwe na uhalali kisheria JMT) kupitisha sheria upesi upesi ya kuhairisha indefinateky - sharti la Mkataba wa Muungano, ibara ya ‘7' (mchakato wa katiba mpya ya JMT), bunge hilo hilo kupitisha katiba nyingine tena ya Muda ya JMT; Kwa mara ya kwanza na kinyume yale masuala 11 ya muungano ambayo hayakutaja vyama vya siasa na shughuli zao, tunaona TANU inakuwa sehemu ya Katiba hiyo, huku ASP ikipewa masharti kwamba ASP ijiunge na TANU, but until then, TANU will run the show - Katiba ya nchi ikatambua TANU peke yake katika masuala ya Muungano kwa kipindi cha 1965 – 1977;

Msisitizo wangu katika kujibu swali lako hili: Kwa mantiki rahisi tu, unapoleta nchi mbili kuwa chini ya jamhuri moja na kuamua masuala fulani yawe ya Muungano hivyo chini ya serikali kuu (e.g. JMT), maana yake ni kwamba YALE YOTE YASIYO YA MUUNGANO, By Default, yanabakia kuwa chini ya serikali shirikishi (Tanganyika na Zanzibar); Na kama nilivyo jadili, kilichotokea ni uchakachuaji wa mkataba na sheria zilizo pelekea Zanzibar kuzidi kupoteza autonomy yake, na pia kifo Tanganyika – kikatiba na pia kama serikali shirikishi;

3.Katika post# 69 umesema sheria mama ya mwaka 1964 ilikiukwa. Je, bado unaamini Article of union ni sheria?

Hii sio sheria bali ina nguvu kubwa ya kisheria kuliko nyaraka nyingine yoyote inayo halalisha Muungano, kama nilivojadili huko juu; Sababu yake nadhani nimejadili katika sehemu za awali za bandiko hili;

b)Umesema nguzo ibaki makubaliano ya 1964. Je, hapa una maana tubaki na United Republic of Tanganyika and Zanzibar?

Swali nzuri; Hapakuwa na United Republic of Tanganyika and Zanzibar, bali United Republic of Tanzania, inayotokana jamhuri mbili huru za Tanganyika na Zanzibar; Lakini kama maana yako unaposema - United Republic of Tanganyika and Zanzibar – ni maana hii hii niliyoelezea, basi jibu langu ni NDIO, lakini IWAPO TU – bado wananchi wa Tanganyika na wa Zanzibar bado watataka Muungano wetu uendelee kwa kufuata makubaliano ndani ya Mkataba wa Muungano, 1964;

Muhimu - Mkataba wa Muungano, 1964, kama ilivyo mikataba mingine yenye kufuata uhusiano wa mataifa wa mfumo wa Shirikisho, Mkataba huu una ‘Provision' ya wazi kabisa kwamba iwapo nchi shirikishi hazitapendezwa na Muungano, basi ni RUKSA kujitoa; Huu ni ushahidi zaidi kwamba Muungano chini ya Mkataba ule, ulilenga mfumo wa Shirikisho; Ndio maana hata Mwl. Nyerere aliwahi nukuliwa na gazeti la Observer, Uingereza *1968) akisema:

"Iwapo UMMA wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha…
Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendeleaiwapo washiriki wake wataamua kuukana."

Kauli ya Nyerere ni muhimu kwetu leo kwa maana tatu:

Kwanza, msimamo wako na Joka Kuu kwamba tuachane na muungano unatokana na tabia za wazanzibari zinazoendana na kauli ya Nyerere hapo juu; Kwahiyo, iwapo mnataka kumtumia Mwalimu kuongezea nguvu msimamo wenu, basi Mwalimu mnae katika hilo, hasa iwapo itahitajika kuelimisha UMMA, kwani UMMA huu umeshapigwa porojo nyingi sana kwamba Mwalimu hakuwa na lingine la kujadili kuhusu hatima ya Muungano wetu;

Pili, vyama vya siasa pia vinaweza challenge position ya CCM juu ya hili, hasa ikizingatiwa kwamba hoja ya baadhi ya viongozi wa CCM kuhusu Serikali ya Tanganyika ni kwamba, Nyerere hakutaka hilo, na hakuna lingine la kujadili; Nyerere alitaka Muungano, lakini alikuwa tayari kuachana nao; Vyama vya siasa vinaogopa sana kubeba hoja ya Muungano, na nilikuuliza swali la namna hii mapema leo;

Na Tatu, maneno haya ya Mwalimu (ambayo yapo mengine mengi tu), yanazidi kuweka bayana kwamba Mkataba ulilenga Shirikisho, vinginevyo mabadiliko baada ya kusainiwa mkataba, yalitokana na nia njema tu, hasa njozi ya kuifanya JMT iwe na Serikali moja siku za usoni, ikiwezekana akiwa bado hai, lakini kwa kuanzia, serikali mbili, kwani alijua fika kwamba ili wazanzibari wakubali, Mkataba ule ilibidi uweke mfumo wa serikali tatu;

4. Katika post#8 umesema solution ya tatizo tulilo nalo ni Serikali 3.

  1. Kwa vile Article of union iliunda United republic of Tanganyika and Zanzibar, na ulisema turudi katika makubaliano ya mwaka 1964, Ni wapi unaposimamia? Tuwe na republic of Tanganyika and Zanzibar au Tuwe na Republic of Tanganyika, Republic of Zanzibar and Republic of Tanzania?

Naomba niliweke hili vizuri kidogo; Articles of the Union iliunda Jamhuri Moja – Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliojumuisha dola mbili huru, na kuweka mazingira ya shirikisho kama nilivyojadili elsewhere;

Now, kuhusu kurudi katika makubaliano ya 1964, nina msimamo huo kwa sababu bado nina amini katika Muungano wetu kwa mfumo uliotarajiwa na Mkataba wa Muungano – yani tuwe na United Republic of Tanzania yenye mfumo wa serikali tatu yani ile ya JMT, Tanganyika na Zanzibar; Kawaida, Jamhuri zote hufuata moja ya mifumo ifuatayo ya serikali:


  • Mfumo wa Serikali Moja;
  • Matangamano ya Serikali za Majimbo;
  • Mfumo wa Shirikisho;

Kwenye bandiko langu namba 94 nimefafanua mifumo hii, huku nikijenga hoja kwamba Mkataba wa Muungano, 1964, ulilenga Mfumo wa shirikisho;

b) Kwanini unadhani kuwa solution ya tatizo hili ni serikali 3?
Naomba kwanza niseme kwamba, Serikali tatu sio solution pekee, ila ni msimamo nilionao sasa hivi mpaka pale UMMA utakavyoamua kupitia referendum, na nitaungana na maamuzi yoyote yatakayoafikiwa kupitia mchakato huo; Vingine options kuu kwa mtazamo wangu ni nne:


  • Kwanza, Serikali tatu - hii ni kama nilivyoelezea, hasa kwa mtazamo kwamba – nia ya Muungano per articles ilikuwa ni NJEMA, lakini utekelezaji ndio ulikuwa mbovu, Kwahiyo turudi kutekeleza tulicho chakachua, but again, referendum ikiamua options nyingine, nitaunga mkono;


  • Option ya Pili ni Serikali Mbili: Ingawa hatujafanya referendum juu ya muundo huu wa sasa, lakini nakubaliana na mtazamo wako na Joka Kuu kwamba kwa hali ya leo, Muungano upo "Beyond Repair"; Nadhani referendum juu ya option hii majibu yake ni very predictable, unless sijui nini kitokeee; Personally I don't believe in this option, na ndio msingi wa hoja yangu katika mada hii;


  • Option ya Tatu – Serikali Moja – iwapo serikali mbili haiwezekani, moja ndio kabisa; kama ni kukubalika, basi option hii itapita by referendum kwa upande wa "Tanzania Bara" peke yake, sio Zanzibar;


  • Option ya Mwisho ni ile ya kuuvunja Muungano, ambayo nadhani wewe na Joka Kuu mpo humu; kwangu, hii ni option number two – na nitaiunga mkono pale referendum juu ya Serikali tatu itakataa; Hata referendum upande wa ZNZ ikikataa serikali tatu, huku Bara ikikubali, nitahamia rasmi kwenye kambi yako, joka kuu na Mzee Mwanakijiji;

(c) Kwa vile makubaliano ya mwaka 1964 yalichakachuliwa kwa mujibu wako, je, tukiamua kurudi kule kwenye mambo 11 tutahitaji serikali ya 3 au tutabaki na ilivyokuwa mwaka 1964.

Kwanza, masuala ya Muungano kuwa kumi na moja haikuwa na maana kwamba orodha hii ingezidi kuongezeka, pengine ingezidi kupungua, lakini kwa sababu kadhaa, wahusika wa Muungano huu treated Mkataba ule kwa mtindo wa Daima mbele, Nyuma mwiko – hasa kwa kujaribu ku-fast track uelekee serikali moja in the near future, na ndio maana tukaona orodha ya masuala ya Muungano ikianza kuongezeka ndani ya kipindi kifupi sana cha Muungano;

Kwahiyo tukiamua kurudi kwenye Mkataba wenye masuala 11, masuala ya Muungano yataweza kuongezeka au kupungua; Duniani kuna mifano mingi ya Serikali kuu zinazofuata Mfumo wa shirikisho ambazo zimekuwa zinapunguza masuala yaliyo chini ya serikali kuu na kuyarudisha kwa serikali shirikishi kwa sababu mbali mbali zenye kulenga maslahi ya taifa;.

Naomba niongezee pia katika hili kwamba - kwa kawaida, serikali kuu inatakiwa kuwa ndogo relative to the whole, lakini chini ya Mfumo wetu wa JMT, ni kinyume, na ndio kielelezo cha inefficiency and wastes as of now, ingawa UMMA unazidi kuaminishwa UONGO kwamba ndio mfumo nafuu kwa mlipa kodi; Ujue pia kwamba - hata ikitokea orodha ya masuala ya Muungano wa JMT yanapungua na kubakia kwa mfano Matano, maana yake ni kwamba mengine yote yasiyokuwa ya Muungano by default yanaangukia kwa serikali husika – hence umuhimu wa serikali tatu unakuwa pale pale, especially kama uamuzi ni Muungano per articles of the Union, 1964;

5. Je, unadhani kuwa uthabiti wa muungano wowote ni lazima ujengwe katika sheria.

Sio sheria tu, bali sheria yenye uhalali wa kikatiba, na katiba hii lazima itokane na masharti ya Muungano, 1964, ibara ya ‘7', kwani hivyo ndivyo katiba halali ilipangwa izaliwe, na hata leo, kama tuna nia ya dhati ya kulinda Muungano wetu, ni lazima turudi kwenye hii ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964, kwani hivyo ndivyo chombo chenye uhalali (sio mamlaka tu kam ilivyo sasa), wa kutunga sheria za JMT (bunge), kitapatikana kupitia Katiba yenye legitimacy & credibility mbele ya walio wengi katika Tanganyika na Zanzibar; Lakini kwa vile Muungano wetu haujajengwa kupitia sheria halali – Katiba ya JMT, 1977, huku structure ya Katiba ya sasa ikiwa based on Muungano ulio kinyume na Articles of the Union, 1964, Mgogoro wa Kikatiba katika JMT Will Always Remain To Be THE ZANZIBAR QUESTION, huku taratibu pia ukianza kuchukua sura ya THE TANGANYIKA QUESTION, iwapo matatizo yaliyojitokeza hayatafanyiwa kazi haraka;

Nina ya nyongeza lakini niweke kituo kwanza kwa haya machache

Asante mkuu, nasubiri kwa hamu maswali mengine toka kwako, lakini muhimu zaidi your counter arguments; I believe kwamba, kama ilivyo mimi, You are Not here to reason to Win Arguments, and instead To See the Truth;

Nafurahishwa sana na michango yako kwani - ni constructive na inatupeleka Mbele;
 
Serikali ikikasimu madaraka yake kwa serikali nyingine, hiyo serikali imekufa.... haipo.

Ndiyo, mambo yasiyo ya muungano yapo Zanzibar pekee, Zanzibar ina serikali kama ya halmashauri ya wilaya ya Ilala.
kwa sababu nayo ina executive (meya or whatever), legislature (madiwani,mbunge) na judiciary mahakama za wilaya au city courts. Ila ina jurisdiction ndogo kulinganisha na ya muungano.

Mkuu Kobello, naomba upitie bandiko langu namba 94 nililojadili mahusiano ya mataifa na aina ya mifumo mikuu in that context; Sielewi kwanini unakwepa again and again, kwani suala la Temeke, Ilala, haya yote yapo ndani ya Jamhuri moja, mjadala wetu ni je, tunaendesha serikali chini ya mfumo gani iwapo tunaleta Jamhuri huru na zenye dola zake kuwa jamhuri moja? Kumbuka kwamba ili Jamhuri moja iweze ungana na nyingine, ili kutambulika kisheria ngazi ya kimataifa, ni lazima jamhuri hizi kwanza ziwe jamhuri huru;

lala, Temeke, hayo ni maeneo yaliyopo ndani ya jamhuri mmoja iliyo huru, ambapo mfumo wake wa serikali unachagua either kuwa more decentralization or more centralization, kama njia ya kuwa karibu zaidi na wananchi/walipa kodi, na shughuli inaishia hapo; But when it comes to Jamhuri huru zaidi ya moja kuungana, lazima zifuate mfumo wa mahusiano YA MATAIFA, ambayo kama nilivyojadili ni serikali kufuata kati ya mifumo hii:


  • Serikali Moja;
  • Matangamano ya Serikali Za majimbo;
  • Mfumo wa Shirikisho;

Matumizi yako ya dhana ya Government unataka kufanya na sisi tuanze kukuiga na Spining, kwani hata Vyuo vikuu kuna Serikali ya Wanafunzi, au sio; Nia yako kweli ni kwenda huko na mjadala huu muhimu kwa taifa letu?

cc: nonda
 
Okay,
Kwanza kabisa, tukubaliane kuwa two republics zilikubaliana zifanye one sovereign republic.(4) cha sheria ya muungano.
Pili angalia kifungu cha nne (a} cha mkataba (siyo sheria) kuhusu nani anaweza kurekebisha existing laws za Tanganyika na Zanzibar (tafadhali angalia neno "hereafter").
Twende taratibu tusijadili vipengele vingi kwa wakati mmoja.

Kabla ya kuangalia unachoelekeza, ni lazima kwanza uangalie:

  • Je ibara ya 3 (a,b,c & d) ya Mkataba wa Muungano, 1964, imetekelezwa?
  • Je, ibara ya 7 (a &b) ya Mkataba wa Muungano, 1964, imetekelezwa?

Ukipuuza haya, mjadala wetu juu ya hili utakuwa hauna tija; Hii ni kwa sababu, kutokana na hayo yote mawili kutotekelezwa aidha kwa bahati mbaya au makusudi, Rais wa JMT ambae pia alikuwa rais wa Tanganyika as of the date ya Kuweka sahihi kwenye makubaliano ya Muungano, Rais huyu pamoja na chombo chake cha kutunga sheria (Bunge) akamzidi mwenzake in terms of mamlaka pamoja na ukweli kwamba jamhuri hizi mbili ziliingia zikiwa huru na zenye dola kamili, hivyo zenye marais na mabunge ambayo yalitakiwa yawe sawa, Per Mkataba wa Muungano, 1964; Nimetoa mifano mingi jinsi gani Bunge la Tanganyika, ambalo lilikuwa batili kwa hoja nilizoweka, lilivyoanza kufanya maamuzi ya kisheria - ovyo ovyo na kuvuruga Muungano uliokusudiwa;
 
Kobello


Unakusudia kusema serikali ya Zanzibar ni kama serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala.

Tanzania ina serikali kama halmashauri ya wilaya ya Ilala?
Serikali ya muungano ni kama serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala pia?

1. Nini uhusiano ulipo baina ya serikali ya Jamhuri ya muungano na serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilala?

2. Ni uhusiano upi ulipo baina ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar?

Unaelewa kuwa kuna orodha ya mambo ya muungano? Yale mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano ni mambo ya nani?
1&2: Uhusiano uliopo ni kuwa serikali ya muungano ni superior kuliko hizo ulizozitaja zote.
3. Naelewa, mambo yasiyo katika orodha ni mambo ya serikali ndogo za Zanzibar na Ilala.Kwa mfano, kuna sheria ya kutokula mchana mwezi wa ramadhani Zanzibar na kuna sheria ya kutokuuza nyanya mtaa wa Congo Manispasa ya Ilala. Hizo si sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na kuna sheria ya Uhamiaji Tanzania ambayo hizo serikali ndogo zote lazima zifuate.
 
when it comes to Jamhuri huru zaidi ya moja kuungana, lazima zifuate mfumo wa mahusiano YA MATAIFA, ambayo kama nilivyojadili ni serikali kufuata kati ya mifumo hii:


  • Serikali Moja;
  • Matangamano ya Serikali Za majimbo;
  • Mfumo wa Shirikisho;

cc: nonda
Vipi kuhusu Inner Mongolia Na China?
 
Mchambuzi,
Kwanza nikushukuru kwa maelezo ya kina. Na pia kwa masahihisho, nilichokusudia ni kile ulichokijibu kuhusu Republic of Tanganyika and Zanzibar, ahsante

Kwa jibu lako kuwa tunaweza kurudi katika makubaliano ya mwaka 1964 napenda kusema kuwa hilo halitawezekana.
Kwa mujibu wa maelezo yako ya bandiko # 94 kilichokusudiwa katika mwaka 1964 ilikuwa kuunda shirikisho.
Ukatoa maelezo ya namna shirikisho linavyoweza kuundwa.

Hoja hiyo inasaidia sana katika hoja yetu tunaoona muungano uvunjwe. Nasema hivyo kwasababu tukirudi katika shirikisho lililokusudiwa mwaka 1964, shughuli za mambo ya nje na ulinzi na usalama zinapaswa kuwa za pamoja.
Kwasasa hivi Zanzibar inataka mamlaka kamili kwa neno dola kamili.

Sidhani kuwa kuna uwezekano wa kuwa na dola kamili isiyo na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa maana hiyo Zanzibar inataka kuondoa Ulinzi na usalama katika yale 11.

Lakini pia inataka kiti UN na kwa msingi huo inataka mambo ya nje yatoke katika yale 11.
Kama ni hivyo basi kwanini tusivunje muungano kwanza wa yale 11 na kama upo ulazima watu wakae kuamua aina ya muungano?Hapa ndipo hoja ya kuvunja muungano inapopata nguvu.

Swali langu la je muungano unapaswa kujengwa katika misingi ya sheria tu! Hapa nilitaka kusikia maoni yako kuhusu namna gani muungano unajengwa na kama tulikuwa sahihi au tutakuwa sahihi.
Nakubaliana na jibu kuwa muungano ni lazima ujengwe katika sheria halali.

Tusisahau kuwa sheria ni mambo yanayoshikilia muungano (binding) lakini muungano hautokani na sheria!
Maana yangu ni kuwa hakuna mahali palipowahi kuwa na sheria halafu muungano ukatokea. Ni lazima kuwe na mambo yanayojenga muungano kwanza ili yalindwe na sheria.

Baadhi ya mambo hayo ni muingiliano wa jamii, mahusiano ya kijamii na Uchumi wa jamii. Hili la uchumi ndilo linaonekana kuwa nguzo kubwa kwa karne tuliyo nayo.

Tunaweza kurudi mwaka 1964, 1965, 1967, 1977, 1984 kwa kuangalia sheria ziliziokuwepo na kukubaliana wapi tusimame.
Kwa bahati mbaya hilo sio tatizo la muungano wetu kwa sasa.

Tatizo la muungano wetu kwa sasa ni kuacha zile value tulizodhani zinaweza kutuleta pamoja kama mahusiano ya jamii na uchumi (economy and social fabric).
Kwa mantiki hiyo hata kama tutakuwa na sheria nzuri mpya, au tukarejea zile za mwaka 1964 au zozote zitakazoondoa kiini macho hatuwezi tena kuwa society yenye utangamano bali tutarithisha vizazi vyetu matatizo tuliyo nayo.

Mfano, katika mazingira ya kudhani kuwa gesi na mafuta ni muhimu kuliko uchumi na mahusiano ya jamii, kuna sheria gani nzuri itakayotuleta pamoja?
Kwasababu hizo, kwasasa tumeshapoteza value za kuwa na muungano, na njia nzuri ni kuvunja muungano!
Hadi pale kutakapokuwepo na ushawishi uliozidi kipimo katika referendum( najua halitatokea kwasababu tumeshapoteza value), the only solution and best option on the table is separation.
 
Mchambuzi

Kimsingi nakubaliana na hoja yako kuu, kwamba Muungano unatakiwa kuwa wazi na uboreshwe. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo sikubaliani na wewe.

Nakubaliana na kukuunga mkono kutokana na kujadili suala hili kwa hoja. Na siku zote wasio na elimu na wajinga, yaani ambao hawana uwezo wa kujibu hoja kwa hoja, ndio wanaotoa vitisho. Nasikitika sana kuona kuwa unatishiwa, unachosema ni haki ni kweli, na ni vema tukijadili wazi ili tukielewe, hili suala la issue ya Muungano Nyerere aliamua kulifutika wakati ile G55 ilipokuwa inataka kurudisha Tangayika, lakini halikuwa addressed, ndio maana it keeps coming, hata kama mtu akikutisha usiongee leo au hata akikufumba mdogo, mwingine kesho atatumie lugha nyingine kuongea hilo hilo.

Tatizo kubwa ni kwamba hata leo bado hakuna msingi imara wa Muungano, ndio maana kuna baadhi ya mawaziri ndani ya serikali zote mbili wanaaupinga na wanautilia shaka, lakini hadharani wanasema tofauti na wanavyosema vichochoroni. Bado hatujia kama Taifa (URT) tunasimama wapi kuhusu suala hili.

Ukiangalia leo ZNZ, what if CUF inashika dola, policy yake kuhusu Muungano ni ipi? How will that be compatible with that of TLP, TADEA, or DP kama wakiwa madarakani. No body knows. What i am they to say here Muungano umebase kwenye consent ya CCM bara na CCM Visiwani, na sio watanzania au wazanzibar. Hii ni weakness ambayo hadi sasa hakuna anayeifikiri.

Ndio maana mjadala kuhusu Muungano unabase kwenye maoni ya watu kama Seif Sharif Hamad na Tundu Lissu na sio maslahi ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar). Mpaka sasa hatujui ni kwanini tuliungana, nini kilichofanya nchi zetu ziungane, na nani hasa was behind muungano. Kusema sisi ni ndugu wa damu ni uongo, kwa sababu ukiangalia Msumbuji unaweza kusema kuwa wana wangoni na wamkonde nao ni ndugu wa damu, ukiangalia burundi na Rwanda kuna wengi tu ambao nao wanaweza kuwa ndugu zetu wa damu, Kenya kuna wamasai na wajaluo wengi. Kama mchambuzi unafahamu ni kwanini tuliungana ni vema ukanifahamisha kidogo labda nawez ana kuwa la kuongea.

Kingine naona kuna porojo nyingi kwenye siasa zetu, wanaosema kuwa katika miaka ya 40 ya muungano, au miaka 50 ya uhuru tumefanikiwa katika mambo ya kijamii, kiuchumi etc etc...siku zote naona ni waongo, kwa sababu ukitoka nje ya nyumba yako(sehemu ambayo ndio ukomo wa kazi yako na nguvu zako binafsi) ukiangalia nje ambako ndio mwanzo wa kazi ya serikali, kila unachoona ni failure failure failure, hakuna kitu chochote cha maana ambacho tunaweza kuwaonesha watu wenye akili kuwa serikali yetu imefanya hivi au hiki. Kuna traces za kazi alizofanya Nyerere baada ya kutake over kutoka kwa mkoloni, kama barabara, viwanda, shule etc etc lakini baada ya hapo hakuna chochote kikubwa tunachoweza kuonesha mbele ya watu. Kwa hiyo kauli za tumethubutu, tumejaribu, na kusonga mbele kimsingi ni uongo.....tumekwama.

Kwa hiyo ukisikia Waziri yoyote anakwambia tumefanikiwa, tumefanya hivi......kimsingi ni siasa tu za kujustify uwepo wao, lakini in reality huoni anything tangible. Kama ulivyosema we are operating under the supreme leader who in Tanzania happen to be politics. CCM.

Mchambuzi unajua kama tukisema tuige nje, yaani tuchague kama tunataka serikali moja, serikalia za majimbo au serikali ya Shirikisho, utaona kuwa kila moja kati ya hizo haifai mazingira ya Tanzania. Mifumo hiyo inategemea demographics, leve of development, na sababu hasa ya kuamua kuungana. Sasa sijui wewe unaona ipi inafaa kati ya hizo tatu. Sikubaliani na wewe kuwa bila Tangayika Muungano hauwezekani. What if Zanzibar dies like Tanganyika did? Muungano hautawezekana?

Tanzania tuna issues kubwa sana za kujadili, Muungano thing can wait. Sasa hivi tatizo kubwa kwa Tanzania ni kwamba hatuna leadership, kuna utapeli mwingi (aka ufisadi), umaskini, haki, miundo mbinu nk nk, these are burning issues, Muungano is in no way a cause of that. Hata kama ukiimarika au kufa dakika hii, hayo makubwa yatakuwepo. Ingekuwa vizuri kama tukielekeza jocho kwenye hayo.
 
Tanzania tuna issues kubwa sana za kujadili, Muungano thing can wait. Sasa hivi tatizo kubwa kwa Tanzania ni kwamba hatuna leadership, kuna utapeli mwingi (aka ufisadi), umaskini, haki, miundo mbinu nk nk, these are burning issues, Muungano is in no way a cause of that. Hata kama ukiimarika au kufa dakika hii, hayo makubwa yatakuwepo. Ingekuwa vizuri kama tukielekeza jocho kwenye hayo.

Tanzania tuna issues kubwa sana za kujadili,

Mojawapo ni muungano unatumia resources zetu hasa akili zetu.

Muungano thing can wait.

Muungano must go ili kupisha burning issues za uchumi na maendeleo.

Sasa hivi tatizo kubwa kwa Tanzania ni kwamba hatuna leadership, kuna utapeli mwingi (aka ufisadi), umaskini, haki, miundo mbinu nk nk, these are burning issues, Muungano is in no way a cause of that.

Leadership imejificha nyuma ya muungano ili mambo mengine yasipewe kipaumbele. Leadership ipo ipo lakini haina uhalali wala matakwa ya wananchi ndiyo maana inatimiza matakwa ya kifisadi. Mimi siwalaumu kwa sababu tumekubali mazingira na taratibu za kipuuzi zinazowaweka madarakani. Zikiwepo kutokulinda kura zetu.

Hata kama ukiimarika au kufa dakika hii, hayo makubwa yatakuwepo.

Hautaimarika ila ni lazima ufe dakika hii ili hayo makubwa yaliyopo yatafutiwe ufumbuzi.


Ingekuwa vizuri kama tukielekeza jocho kwenye hayo

Sawa na la muungano ni kikwazo kikubwa kinachozuia mjadala na mikakati endelevu ya kujadili mambo ya msingi ya haki, uchumi na mstakabali wa maendeleo wa pande zote.

UJUE MAMBO YA MUUNGANO HAYATAKAA YAISHE KWA SABABU YAKO HIVYO YAKIISHA MTAJADLI MAMBO YA MSINGI NJE YA MTANDAO WA UFISADI. KWA HIYO KUFA KWA MUUNGANO NI UKOMBOZI WA KIUKWELI
 
1&2: Uhusiano uliopo ni kuwa serikali ya muungano ni superior kuliko hizo ulizozitaja zote.
3. Naelewa, mambo yasiyo katika orodha ni mambo ya serikali ndogo za Zanzibar na Ilala.
Na kuna sheria ya Uhamiaji Tanzania ambayo hizo serikali ndogo zote lazima zifuate.

Kobello

Unaelewa kuwa kuna kitu kinaitwa mgawanyo wa mamlaka/madaraka?
Umeshawahi kusikia au unafahamu kuwa Tanzania ina Muungano wenye serikali mbili (as per kiini macho)na mamlaka tatu kisheria?

Zanzibar ( au Ilala)kufuata Sheria za uhamiaji ni kwa sababu ya udogo wa serikali hii au ni kwa sababu uhamiaji imo katika mamlaka ya serikali ya Muungano?(jambo la muungano)

Usuperior (ukuu) wa serikali ya muungano upo kihisia au kisheria? Kama ni kisheria, sheria ipi inaipa serikali ya muungano hadhi/cheo cha serikali kuu dhidi ya Serikali ya Zanzibar?

Au sheria ipi inatamka kuwa serikali ya Zanzibar ni sub-ordinate kwa serikali ya Muungano?

Ni uhusiano upi uliopo baina ya serikali kuu na serikali za mitaa,wilaya,mikoa?

Serikali ya Zanzibar ipo kwenye kundi lipi?

Je Zanzibar ni mtaa, wilaya, mkoa au state?
Je Tz bara(Tanganyika) ni mtaa, wilaya, mkoa au state?
 
Nguruvi3,


Kwa jibu lako kuwa tunaweza kurudi katika makubaliano ya mwaka 1964 napenda kusema kuwa hilo halitawezekana.
Kwa mujibu wa maelezo yako ya bandiko # 94 kilichokusudiwa katika mwaka 1964 ilikuwa kuunda shirikisho.
Ukatoa maelezo ya namna shirikisho linavyoweza kuundwa.

Hoja hiyo inasaidia sana katika hoja yetu tunaoona muungano uvunjwe. Nasema hivyo kwasababu tukirudi katika shirikisho lililokusudiwa mwaka 1964, shughuli za mambo ya nje na ulinzi na usalama zinapaswa kuwa za pamoja.
Kwasasa hivi Zanzibar inataka mamlaka kamili kwa neno dola kamili.

Sidhani kuwa kuna uwezekano wa kuwa na dola kamili isiyo na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa maana hiyo Zanzibar inataka kuondoa Ulinzi na usalama katika yale 11.

Lakini pia inataka kiti UN na kwa msingi huo inataka mambo ya nje yatoke katika yale 11.
Kama ni hivyo basi kwanini tusivunje muungano kwanza wa yale 11 na kama upo ulazima watu wakae kuamua aina ya muungano?Hapa ndipo hoja ya kuvunja muungano inapopata nguvu.

Una hoja ya msingi hapa, ndio maana nikasema hili suala la Muungano na uwe wa mfumo gani wa serikali, ije referendum tujue moja. Referendum iulize swali moja tu kwamba – Kwa vile tulikosea, na kama tunataka tuimairishe Muungano wetu, Je turudie Mkataba wa Muungano, 1964 chini ya serikali tatu?
Vinginevyo ningependa kuendelea kuamini kwamba hizi ***** ***** za dola kamili ni siasa tu za wanasiasa, na nitaacha kuamini hivyo pale tu – referendum itakapofuata mtazamo wa wanasiasa;

Muungano na sheria…

Nadhani Sheria unayozungumzia hapa ni sheria mama – yani katiba; Kama nipo sahihi, nadhani pia utakubaliana na mimi kwamba Mkataba wa Muungano, 1964, ilikuwa ni Katiba Mpya ya Muungano; Mkataba huu ukaweka masharti kwamba Katiba ya Kudumu ipatikane ndani ya mwaka mmoja kupitia tume ya katiba na baadae bunge la katiba – per ibara ya ‘7' ya Mkataba wa Muungano, 1964; Lakini kama tulivyojadili, hili halikutokea;

Baadhi ya mambo hayo ni muingiliano wa jamii, mahusiano ya kijamii na Uchumi wa jamii. Hili la uchumi ndilo linaonekana kuwa nguzo kubwa kwa karne tuliyo nayo.

Tunaweza kurudi mwaka 1964, 1965, 1967, 1977, 1984 kwa kuangalia sheria ziliziokuwepo na kukubaliana wapi tusimame.

Kwa bahati mbaya hilo sio tatizo la muungano wetu kwa sasa.

Tatizo la muungano wetu kwa sasa ni kuacha zile value tulizodhani zinaweza kutuleta pamoja kama mahusiano ya jamii na uchumi (economy and social fabric).
Kwa mantiki hiyo hata kama tutakuwa na sheria nzuri mpya, au tukarejea zile za mwaka 1964 au zozote zitakazoondoa kiini macho hatuwezi tena kuwa society yenye utangamano bali tutarithisha vizazi vyetu matatizo tuliyo nayo.

Nakubaliana na hoja yako hapa na ningependa kuongezea kwamba – Katika masuala yasiyokuwa ya Muungano – kwa Tanganyika na Zanzibar, Katiba za ndani ya nchi hizi mbili (sio ile ya JMT), validity zake na pia political legitimacy zake zitatokana na internal historical processes za wananchi wa Jamhuri ya Tanganyika, na kwa upande wa Zanzibar, hivyo hivyo; Validity na political supremacy haitatokana na katiba ya JMT; Hii ni kama tutakuwa na uelewa juu ya nini maana ya Katiba ya nchi huru; Na kwa mantiki hii, ndio maana Zanzibar wamejipatia katiba yao, na vile vile Tanganyika inabidi irudi na iwe na katiba yake;

Katiba ya Zanzibar itaunda serikali ya Zanzibar, na Katiba ya Tanganyika itaunda serikali ya Tanganyika, na kinyume cha hapo ni kujiingiza kwenye matatizo ambayo tumeyaona yakiendelea hivi leo kutokana na ukiukwaji wa mkataba wa Muungano, 1964, kama tulivyojadili; kwa maana nyingine, kujichanganya katika hili, maana yake hatujakomaa au hatuna uelewa wa maana ya mfumo wa serikali wa shirikisho maana yake ni nini; Muungano hauwezi kufanya kazi kwa nguvu za kisiasa tu, bali iwapo haya yatakuwa satisfied:

  1. Mgawanyiko wa jurisdiction unakuwepo;
  2. Kila upande unajaribu kwa kila namna kuheshimu mgawanyiko huu bila ya hila za kuingiliana;
  3. Kuna chombo chenye sura ya kimahakama kutatua iwapo kutakuwa na migogoro ya aina yoyote;
  4. Na pia – serikali shirikishi na wananchi wake wana NIA ya dhati ya kutumia mahakama kila itakapotokea disputes zinazohusiana na juridisction;

Lakini muhimu zaidi ni kama ulivyosema – mafanikio ya Muungano yatategemea political will, Muungano pia lazima uwe socially viable, na vile vile uwe na uhalali wa kihistoria katika pande zote mbili;
 
Kobello,

Usijaribu ku – spin dhana ya Serikali;

Hoja zako juu ya hili inafanania na hoja nyingine nilizowahi sikia huko nyuma kwamba serikali za mitaa hazina katiba zake zenyewe; Serikali mbili tulizonazo leo haziwezi kufananishwa na Serikali Kuu na Serikali Za mitaa, vinginevyo ni sawa na kufafanisha embe na nazi; Tofauti kuu iliyopo na iliyo wazi kabisa ni kwamba – tofauti na serikali za mitaa, ambayo ipo subordinate kwa serikali kuu, serikali mbili au zaidi ndani ya mfumo shirikisho au Muungano wowote – THESE ARE NOT SURBODINATE TO EACH OTHER: Badala yake, serikali shirikishi are co-ordinate and of equal power and jurisdiction in their own sphere; THEY ARE MASTERS IN THEIR OWN HOUSE;

cc: nonda
 
...hadi pale kutakapokuwepo na ushawishi uliozidi kipimo katika referendum( najua halitatokea kwasababu tumeshapoteza value), the only solution and best option on the table is separation.

Mkuu Nguruvi3,

Mchakato wa separation tunauanzaje:


  • Kwa kuvunja kwanza muungano au kwanza kwa kuunda Tanyanyika?

Mimi mtazamo wangu ni tuanza na Tanganyika kwanza kwa kuifufua jamhuri hii; Na Kama ni kuanza na Tanganyika;


  • Tunaanza kwa kutengua Sheria namba 24 ya mwaka 1967 iliyofuta Tanyanyika au sio lazima kurudi kwenye sheria hii?


  • Kwa mtazamo wako, je, kitendo cha kuanza na Tanganyika maana yake pia ni kuvunja Muungano?
 
Back
Top Bottom