Tundu Lissu na CHADEMA wamekata tamaa baada ya kukataliwa na Vijana

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,254
9,704
Ndugu zangu watanzania,

Tegemeo la chadema miaka yote ilikuwa Ni kwa kundi la vijana,Hakika na kwa hakika vijana wa nchi hii walitumika na kutumikishwa Sana na chadema,wazazi wengi Sana wamebaki wanalia machozi kila Siku baada ya watoto wao na vijana wao kufukuzwa vyuoni kwa sababu ya utovu wa Nidhamu na mavurugu yaliyokuwa yanasababishwa na viongozi wa chadema walio kuwa wanawadanagnya vijana na mwisho wa siku wanaishia kufukuzwa vyuo.

Vijana wengi wamekatisha ndoto zao,wamejeruhiwa,wamevunjwa miguu na kuteguliwa viono kwa sababu ya Chadema,vijana wengi wamefukuzwa kazi kwa sababu ya Chadema kuwadanganya na kuwaaminisha kuwa watawasaidia kisheria mahakamani na wanakwenda kuchukua nchi na watawapa vyeo,vijana wengi walifirisika na kupoteza mitaji yao kwa sababu ya kuipigania chadema wakiamini kuwa Ni chama Cha ndoto Yao, na kweli ikaonekana ushujaa na uzalendo kwa kijana kuwa Chadema na kuitwa Kamanda na kuvaa magwanda yao

Mwisho wa siku wakati vijana wamepoteza muelekeo na dira ndipo wakaja kugundua na kufahamu ukweli kuwa Chadema Ni chama Cha kilaghai na kikundi Cha wasaka tonge na madaraka hasa ya ubunge na udiwani,wakaona kuwa viongozi wao wanawachuuza tu na kuwa hawana Uzalendo wowote juu ya nchi yetu.

Wakagundua kuwa Ni CCM pekee ndio chama chenye kuwajali kuwasikiliza kuwapa kipaombele katika mikakati ya kiuchumi,kuwawezesha na kuwakwamua kiuchumi na kuwaendeleza katika juhudi zao, wakagundua ni CCM pekee yenye uchungu na Taifa hili na ambayo imeonyesha ushupavu na umadhubuti katika kuliongoza Taifa letu,Ndio sababu vijana wengi kuanza kurejea CCM na kuchukua kadi za CCM chama ambacho kina Sera na ajenda zinazogusa maisha Yao.

Baada ya Chadema kuanza mikutano yake na kupewa majibu ya kukataliwa na watanzania hasa vijana walio kuwa Tegemeo kwao wamebaki wamekata Tamaa Sana,wamekata pumzi na nguvu za Kuendelea na mikutano Yao,,hawaelewi Ni vipi watasonga mbele wakiwa wanaonekana Kama wasaliti wa Taifa letu.

Tundu Lisu amebaki anaeleza habari zile zile za miaka yote tangia amekwenda ulaya, siyo yeye Wala chadema wenye ushawishi wa kisera na kiajenda kwa watanzania, Hakuna wanachokieleza kinachoweza mshawishi Bibi wa kule kijijini kuwaunga mkono,hawana Sera ya kumgusa mkulima kuweza kuwaunga mkono, Hawana Sera juu ya uzalishaji wa ajira kwa vijana, Hawana Sera Wala ajenda juuu ya uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kama afanyavyo Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani.

Kimebaki Ni chama Cha kuokoteza vihabari,Ni chama kilichokosa Safu ya uongozi yenye kuleta matumaini hata kwa wafuasi wake,ndio maana ya kuona kila mmoja akiwa na msimamo wake,Ni chama ambacho hakina mizizi katika mioyo ya watanzania, Hakuna mwenye akili Timamu anayeweza kuipigania chadema Hadi kuhatarisha maisha yake kwa Sasa ,hayupo mtanzania wa namna hiyo, maana kila mmoja ameshatambua kuwa Chadema Ni kundi la wasaka tonge tu

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Nafasi za ma DC zimejaa piga moyo konde usichoke kesho ni nzuri kuriko Jana 2024 Kuna uchaguzi wa Wenye viti na wajumbe wa mitaa ukajalibu huko pengine zali laweza kua upande wako lukasi mwashambwa awe ukaukwaa uheshimiwa tia bidii kufanikiwa sio mchezo
Nimeridhika na kilimo
 
Huu uzi
IMG_7083.jpg
 
Back
Top Bottom