Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Maelezo ya Lissu alipohojiwa na CLOUDS
Nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking. Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao

Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Lissu

MASWALI
1. Je risasi zilipigwa kutoka nyuma yake?

2. Mbona gari lake lilionekana kuwa risasi zilikuwazimepigwa ubavuni. Kama niko sahihi hii iliwezekana vipi wakati hakukuwa na nafasi ya wao kuegesha gari hapo?

Maana yake ni kuwa nafasi kati ya gari na gari kwenye maegesho isIngeweza kumfanya mpigaji atumie bunduki kwa usahihi mpaka asogee karibu sana na hii ingemfanya amtambue aliyemshambulia.

3. Kwa nini dreva wake kama mtu aliyekuwa kwenye tukio anamzuia asitoe maelezo yake?
 
Mleta mada ni wazi wewe sio mtaalamu wa kupeleleza jambo hili na maswali unayouliza yanaweza hata yasiulizwe na mtaalamu wa uchunguzi. Jaribu kushughulika na mambo uliyo na uwezo nayo!!

Vijana wa nchi hii tutadharauliwa kwa ujumla wetu kumbe dharau ilipaswa kuelekezwa kwako tu.
 
Unafanya makosa makubwa sana kudhani kila aliyeko humu ni kijana- mie siyo kijana
 
Unafanya makosa makubwa sana kudhani kila aliyeko humu ni kijana- mie siyo kijana
Haya basi, tufanye hivi. Kuna wazee wanadharauliwa kwa ujumla lakini kumbe anapaswa kudharauliwa mmoja tu. Jikite kwenye ushauri - fanya mambo ya maana maishani mwako, achana na vitu vidogo vidogo ambavyo havikuongezei afya wala kipato.

Wewe sio mtaalamu wa uchunguzi katika jambo hili. Lissu huyu hapa, badala ya kuuliza humu - fanya taratibu akamatwe akajibu haya unayouliza Polisi au Mahakamani. Kwa kuwa sio kijana, utaona busara katika ushauri huu.
 
Haya basi, tufanye hivi. Kuna wazee wanadharauliwa kwa ujumla lakini kumbe anapaswa kudharauliwa mmoja tu. Jikite kwenye ushauri - fanya mambo ya maana maishani mwako, achana na vitu vidogo vidogo ambavyo havikuongezei afya wala kipato. Wewe sio mtaalamu wa uchunguzi katika jambo hili. Lissu huyu hapa, badala ya kuuliza humu - fanya taratibu akamatwe akajibu haya unayouliza Polisi au Mahakamani. Kwa kuwa sio kijana, utaona busara katika ushauri huu.
Ushauri wa kijinga sana
 
Haya basi, tufanye hivi. Kuna wazee wanadharauliwa kwa ujumla lakini kumbe anapaswa kudharauliwa mmoja tu. Jikite kwenye ushauri - fanya mambo ya maana maishani mwako...
Unajua utaalamu wangu au unanichukulia juujuu siyo? Tuheshimiane sawa
 
Tatizo umeelekeza akili yako kwenye mabishano. Tufanye hajapigwa risasi alijipiga
Wala siko huko- kwa alivyoeleza ni sahihi hajapigwa risasi atakuwa aliletwa hapo na dreva wake akiwa majeruhi tayari. Hebu fikiria unachema ulisoma chuo na kuhitimu mwaka fulani ila huwezi kumtaja hata mwanafunzi mmoja uliyesoma naye- maana yake hujawahi soma chuo hicho unachosema
 
Kuwa wakili, ila usidhurumu! Unajua inauma eeh!

Halafu udhulumu wenye nazo? Utakuwa hujipendi
 
Unajua utaalamu wangu au unanichukulia juujuu siyo? Tuheshimiane sawa
Nakuheshimu lakini sidhani unajua hilo. Una assumptions nyingi katika jambo hili ndio maana nimesema wewe haiwezekani ukawa mtaalamu. Ukiwa ni lawyer, ni bush lawyer tu!! Moja ya assumptions - kuwa amlete dereva ili ahojiwe. Una chochote kinachoonesha anamzuia dereva asitoe maelezo?? Lakini dereva huyo atoe maelezo wapi? kwako au Polisi? Na ndio niliposema je kuna jalada la uchunguzi liko wazi?? Nikamalizia kwa jambo unalokwepa kuzungumzia - Lissu huyu hapa. Kamata na fungua jalada ili maswali yako pamoja na mengine yajibiwe.

Kama ilivo ada, mnapokuwa challenged huwa mnakimbilia "tuheshimiane". Vumilia tu!! Umeleta mada hii hapa - acha ijadiliwe. Swala la kuheshimiwa utaliinjoy vizuri katika mazingira unayodhibiti. Hapa humdhibiti mtu na bila kukukosea heshima, utapambana na hoja. Acha vitisho!!
 
Nakuheshimu lakini sidhani unajua hilo. Una assumptions nyingi katika jambo hili ndio maana nimesema wewe haiwezekani ukawa mtaalamu. Ukiwa ni lawyer, ni bush lawyer tu!! Moja ya assumptions - kuwa amlete dereva ili ahojiwe. Una chochote kinachoonesha anamzuia dereva asitoe maelezo?? Lakini dereva huyo atoe maelezo wapi? kwako au Polisi? Na ndio niliposema je kuna jalada la uchunguzi liko wazi?? Nikamalizia kwa jambo unalokwepa kuzungumzia - Lissu huyu hapa. Kamata na fungua jalada ili maswali yako pamoja na mengine yajibiwe.

Kama ilivo ada, mnapokuwa challenged huwa mnakimbilia "tuheshimiane". Vumilia tu!! Umeleta mada hii hapa - acha ijadiliwe. Swala la kuheshimiwa utaliinjoy vizuri katika mazingira unayodhibiti. Hata humdhibiti mtu na bila kukukosea heshima, utapambana na hoja. Acha vitisho!!
hebu msikilize unless awe anaumwa psychological trauma
 
Back
Top Bottom