Dkt. Slaa: Tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Balozi Mteule na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amesema tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na watu ‘wasiojulikana’ ni jambo la kawaida na ameitaka jamii kuliacha Jeshi la Polisi kukamilisha upelelezi na kutoa majibu.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha Clouds juu ya hali ya kisiasa ya Tanzania na mustakabali wa maisha yake baada ya kuondoka CHADEMA, amesema hafurahishwi na baadhi ya watu kuwataja hadharani watuhumiwa wa tukio hilo kwasababu linaharibu uchunguzi wa polisi.

“Mimi kinachoniudhi ni hii watu kusema hadharani kwamba kuna hiki na hiki tunasuspect (tunahisi) waliofanya ni fulani. Sheria inasema ukihisi nenda polisi katoe taarifa sio unaenda kwenye vyombo vya habari”, amesema Dkt. Slaa.

Amesema hawezi kuzungumzia kwa undani suala la Lissu kupigwa risasi, ikizingatiwa kuwa watu wengi wamepigwa risasi nchini na kazi ya kuwabaini wahalifu waliomshambulia ni ya polisi sio viongozi wa siasa au wananchi.

“Lakini kama binadamu hakuna anayependa binadamu yeyote aumizwe lakini matukio haya ya kuumizwa yametokea nchi hii kwa watu wengi sana. Na mimi sio chombo cha dola kujua kwamba unanyoosha kidole kwa kitu ambacho hatukiamini; mimi ni msomi”, amesema Dkt. Slaa na kuongeza kuwa,

“Ukitoa taarifa za upelelezi unaharibu upelelezi. Mimi niko Canada mauaji yapo kila siku na watu wanapotea, wanapigwa risasi wakiulizwa polisi wanakwambia suala hilo liko kwenye upelelezi tukifikia hatua nzuri tutatoa taarifa”.
 
Dr Slaa kasema tukio lile ni jambo la kawaida? Kama ni kweli ameongea haya maneno nitamtoa maanani moja kwa moja!

Nadhani anataka kutumika kuendesha propaganda kuwa Lissu hakushambuliwa kwasababu za kisiasa!

Ukisoma btn the lines, kusema ni jambo la kawaida, ni sawa na kudownplay tukio zima! Of which nimeshangazwa sana!

Ubalozi aliopewa, naona mojawapo ya masharti, ni “ubalozi wa propaganda dhidi ya Lissu”

Sasa karata ya serikali ya ccm dhidi ya Lissu ni Slaa, mark my words!
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
 
Yeye ile list of shame alikwenda kutoa taarifa Polisi au TAKUKURU? Au anavyokomaa kuwa Lowasa ni fisadi kuna taarifa yoyote aliyoipeleka TAKUKURU?
Huyu ni msaliti wa Ukatoliki, haaminiki hata kidogo. Achana naye. CCM damu sasa, what else do you expect na ameahidiwa ubalozi, hawezi kulikoroga. Kutoka kuosha vyombo hotelini, leo ni diplomat, hawezi kuuona ubaya wa Lisu kupigwa risasi na huyo anayetuhumiwa.
 
Kajichanganya sana kwenye swali linalomuhusu Lissu, huku yeye anasema alipotaja List of shame alikua na maadui wengi na aliwaita waandisha akawaambia, huku upande wa pili akisema amekimbilia Canada kwa sababu ni moja ya nchi zinazoheshimu haki za binadam, kwa nini hakukimbilia Polisi..

Kaongea vizuri sana kwenye mambo mengine, ila lilipokuja swala la Lissu hekima aliamua kuiweka pembeni... anaonekana ana hasira sana na Lissu
 
ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu j.forum ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua lissu risasi.nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.
note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Quite a comedian
Polisi mpaka leo hawajui aliyemuua Mawazo
Polisi hawajui alipo Saanane
Hawajui alipo mwandishi wa mwananchi
Aliyewateka Roma na Ulimboka ni kitendawili hata kama wenyewe wanawafahamu
Nini kina kufanya udhani suala la Lissu litatuliwa?
 
Nikifaninisha tukio la Lissu na la ndugu zangu waliopoteza uhai Kibiti, na polisi waliopoteza uhai kwa kushambuliwa wakiwa katika malindo yao naona tukio la Lissu ni la kawaida tu. Viachwe vyombo husika vifanye kazi yao katika uchunguzi wa matukio haya.
 
Yeye mwenyewe alipokuwa katibu wa Chama cha upinzani mke wake alipigwa mapanga na alikaa India kwa kipindi kirefu akitibiwa Polisi walimpa hitimisho la uchunguzi?

Tundu Lissu amepigwa risasi mchana katika makazi ya watumishi waandamizi wa serikali anasema ni tukio la kawaida.
 
Ni kweli kabisa na kila siku nimeendelea kusema humu JF ya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unathibitisha mtu aliyemdungua Lissu risasi. Nikaendelea kuwapa member walalamishi wasiotaka kuelewa wakereketwa wa upande wa pili kama wana evidence wapeleke polisi haki itendeke washukiwa wafikishwe kortini.

Note;"huna haki ya kuzungumza pasipo kuwa na ushahidi wa kile unachokizungumza"
Kama hakuna ushahidi wa kutosha turudishe Zila Camera tu eneo la tokeo
 
Back
Top Bottom