Pascal Mayalla, unahitaji sana kutokuwa 'biased' kujadili suala la shambulizi dhidi ya Tundu Lissu!!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
745
633
Ndugu Paskali salaam,

Una kila haki ya kutoa maoni yako. Na kwa kuwa haki hii ni ya kikatiba, basi hakuna mtu anayeweza kukunyang'anya. Nimesoma kwa makini sana makala yako Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi! Je, anahusika? - JamiiForums ambayo kiukweli, na kimsingi, ni mawazo yako.

Vilevile nimesoma wachangiaji kwenye uzi huu; wapo wanaobeza na wapo wanaokubaliana na wewe, lakini nimesikitika kuwa, wanaokubaliana na wewe wanaishia kusema 'BAVICHA HAWAWEZI KUKUELEWA'.

Mimi niseme, na awali nimesema, suala la Tundu Lissu na shambulio hilo la SEPT 7 linahitaji utulivu wa hali ya juu ukiondoa njaa, ushabiki wa chama na unafiki, ili kujua ukweli ndani yake.Unahitaji kutokuwa 'biased' kabisa ili kuujua ukweli. Sasa, kwa kuwa tayari umetumia haki yako hiyo ya maoni, naamini unajua kuwa wajibu wako pia kusikiliza na maoni ya watu wa pande zote, kwa kuwa hakuna haki bila wajibu, na hivyo naomba na mimi nitumie uhuru huohuo kutoa maoni yangu.

SUALA LA SILAHA ZILIZOTUMIKA!
Umesema kuwa, silaha zilizotumika ni AK 47. Kitu cha kwanza tu Bwana Mayalla nikuombe hapa ni uthibitisho kuwa, silaha zilizotumika ni AK 47, kwa sababu sikuwahi kujua kama Tundu Lissu alishambuliwa kwa silaha nzito kama hizi. Na kwenye ushahidi huo, ningependa uwaambie wasomaji wako kuwa umejuaje kama zilizotumika zilikuwa ni AK 47.


Pamoja na hil, Bw. Paskali, nimeona umeenda mbali hata kutoa elimu ya kijeshi ukisema kuwa, kwa mwanajeshi aliye na mafunzo sahihi ya kijeshi, asingeweza kukosa shabaha zote; alihitaji risasii moja tu ambayo ingepiga aidha kwenye moyo ama kichwani. Nikuambie tu kwamba, wapo wanajeshi ambao, pamoja na kuwa ni wanajeshi, huwa wanakosa shabaha tu za kawaida, tena wakiwa wanafundisha. Na ndiyo maana, kati ya wanajeshi wengi, wapo walenga shabaha (snippers) wachache. Kwa nini wasiwe wanajeshi wote? Kwa hiyo, hapa mimi nataka kupingana na wewe suala la shabaha lisitumike kusema kuwa, Lissu alishambuliwa na 'wahuni' wa kawaida.

Umesema kweli kabisa kuwa, AK 47 huwa na kasha (magazine) yenye risasi arobaini. Shambulizi la Lissu halikufanywa na mtu mmoja, bali zaidi ya mmoja. Risasi zilizobainika kufyatuliwa (kwa mujibu wa matundu yaliyokuwa kwenye gari) ni thelathini na nane. Hapa napata wasiwasi, kama hakuwa mmoja, mimi nadhani matundu ya risasi yangekuwa zaidi ya hayo yaliyobainishwa. Hili nalo linanitia mashaka kuamini kuwa, waliomshambulia Lissu walitumia aina ya mashine ulizozitaja.

KUHUSU DEREVA NA USHAHIDI WA SHAMBULIO LENYEWE!

Ndugu Mayalla,
Mara baada tu ya tukio, dereva alikuwapo palepale hospitali mjini Dodoma, tena kabla ya kwenda Nairobi. Hapa najiuliza, jeshi la polisi lilishindwa nini kumtia nguvuni ili asaidie upelelezi kabla hajaondoka?


Lakini pia, baada ya hapo, dereva alisafiri na boss wake kwenda Nairobi, na amekaa naye huko siku nyingi. Nafikiri Kenya ni nchi mwanachama wa Afrika Mashariki. Jeshi letu la polisi lilishindwa nini kutumia nafasi hiyo ya pili ili kumpata dereva na kisha kutoa ushahidi wa tukio?

KAMA SERIKALI INAHUSIKA, BASI LISSU ANGEMALIZWA PALEPALE HOSPITALINI AIDHA KWA KUPEWA INCOMPATIBLE BLOOD, AMA KUCHELEWESHEWA HUDUMA!

Vilevile hii hoja, kaka yangu Paskali, ni ya kijinga sana, labda kama hujasoma profession yoyote ndiyo unaweza kusema hoja kama hii. Daktari anaapa, katika fani yake, kutokuwa chanzo cha kifo kwa mtu yeyote. Na pale waliomshughulikia Lissu walikuwa ni madaktari wengi. Napata mashaka kwamba, je wangehongwa wote, na wakakubali, kupoteza maisha ya Lissu? Kwa hiyo nataka nisikubaliane nawe kuwa, Lissu anatakiwa kuishukuru serikali. Lissu anapaswa kumshukuru Allah na kuwashukuru madaktari kwa weledi wao kitaaluma!

SASA HEBU TUFIKICHE VICHWA VYETU NA AKILI ZETU TIMAMU KAKA PASKALI
Baada ya shambulio la Lissu, kuna vitimbwi vya kila aina vilianza kutokea. Baadhi ya hivyo vitimbwi ni hivi;

  1. Kuna wazee wa Kiislamu walikaa Tanga kutaka kusoma dua'h rasmi kwa ajili ya kitendo hicho kiovu cha kutaka kummaliza mwanasheria wao. Jeshi la polisi lilifanya kila aina ya figisu, ubabe na mambo mengine kuzima dua'h hiyo.
  2. Watanzania wanaompenda mwanasheria wao na mtanzania mwenzao, walichapisha ma-T-shirt yenye sura ya Lissu na maneno 'Pray for Lissu'. Kila aliyekuwa akivalia ma-T-shirt hayo, basi naye alipata tabu sana kukimbizana na polisi,
  3. Hadi leo, hakuna tamko la amiri jeshi mkuu juu ya kuvitaka vyombo vya ulinzi kuwabaini haraka sana waliofanya shambulizi hili,
  4. Matibabu ya Lissu na gharama zake yanapingwa bungeni na hadi serikalini,
  5. Kamera za kiusalama (CCTIV) zilizokuwa eneo la tukio ziliondolewa. Hadi sasa, hakuna mtu yeyote ndani ya serikali anayehoji 'whereabouts' za kamera hizo,
  6. Kila aliyeenda kumsalimia Lissu Mjini Nairobi, serikali ilimchukia sana, na zipo za chini kuwa, hata 'vice' alilazimisha tu kwenda kumuona, kwa kuwa mama wa watu ana hofu ya Mungu kama ilivyo ada ya Wazanzibar wengi, na;
  7. Jana ya tarehe 7, kongamano la kukumbuka mwaka mmoja toka Lissu ashambuliwe lilivurugwa na kupigwa vita na jeshi la polisi.
Kwa uchache wa masuala haya ndugu yangu, kaka yangu, Paskali, unapata picha gani? Ndiyo maana nikasema, suala la shambulio la Lissu linahitaji akili iliyotulia ili kujua ukweli wake, na kabla hujaanza kuliteta, ondoa njaa, uchama na unafiki.

Mimi napata mashaka juu ya uwezo wako wa kuchambua masuala kama haya endapo utakuwa bado unao tena, maana, kama alivyosema mchangiaji mmoja kwenye uzi wako, toka umeitwa bungeni, umekuwa si Paskali ambaye alikuwa na maswali magumu kama ya Ansbert Ngurumo, Sami Awami na Absalom Kibanda; si Paskali aliyemuuliza Mhe. Rais swali gumu hata akashindwa kujibu, akaambulia kuelezea maana ya jina la muuliza swali.

Rai yangu ni hii:
Kuwa jagina wa kuchambua masuala anuai ya kitaaluma na ya kisiasa kunahitaji kipaji. Kipaji hiki huwa hakina hata chembe la unafiki, hata kama kikiwa kimezungukwa na njaa kali ama uchama.


Historia inaonesha, kila Mtanzania anapoanza kunyemelewa na kile chama chetu, 'chama-dola', basi taratibu huanza kupoteza uwezo wake wa kufikiri. Tulikuwa na bright persons kama kina Kabudi, Mkumbo na Mtatiro. Toka waanze kuenenda kwenye njia ya chama kile, hawana tena uwezo wa kuchambua mambo, zaidi ya kuungurumisha matumbo yao yanayodai chakula kutoka kwa mfalme.

Nakutakia kazi njema ndugu yangu!!
 
Pascal alikuwa anataka kujenga hoja indirectly kuwa watu wasiojulikana walishirikiana na dereva wa Lissu katika ilie shambulio kitu ambacho mazingira ya tukio zima(kama yalivyoelezwa). yanakataa.

Ukimsoma utagundua anakiri ni watu wasiojukikana(ambao wote tunajua wanamtumikia nani) ndio walitekeleza lile shambulio na ndio maana akachomekea swala la uchunguzi wa kimaita kuwa gumu ila alitaka pia kumtuhumu dereva wa Lissu kushirikiana na watu wasiojulikana na hapo ndipo alipochemka.
 
Kwenye suala la Lissu Pascal anatumika , sasa hivi tunachokifanya ni kuchunguza amelipwa kiasi gani alipewa na nani au iliingizwa a/c gani na ni benki gani , ni wapi na lini , majibu tutayaleta hapahapa

Tuna uzoefu wa kutosha sana kuchunguza mambo haya na ndio maana hela zote alizopewa Lipumba tunajua zilikoingilia na kutokea . Lengo la uchunguzi huu ni kuondoa unafiki na kuchora mstari ili wale ambao wameshikamana na wauaji dunia iwafahamu .
 
Pascal wa sasa sio yule tena, amepoteza umakini kwa kiwango cha juu kabisa. Nahisi kuna kitu kinamtiwa wasi wasi sana mpaka kupoteza umakini na ujasiri, nae engekaa kimya tu kama wakina Mzee warioba na wakina issa shivji si lazima kuandika.
 
Kati ya watu nilio kuwa nawaheshimu ni paskali huyu jamaa nilikuwa namuona kama huwa analifanyia kazi jambo ndio
Anakuja nalo jukwaani lakini nimegundua jamaa ni mnafiki Sana brother pascal heshima unajishushia sio kila kitu lazima ukisemee au unataka uvishwe taji kwa mambo ya hovyo hovyo kama haya
Rudi kwenye misingi yako
 
Jana Paskali nilimwambia siyo kila kitu ukitoa hoja utakuwa sahihi na kwa hili la shambulio la Lissu kuna mambo mawili.

moja yawezekana kuna watu wanamtumia kupotosha au

Hili jambo hana uelewa nalo na namna nzuri ya kuepusha hiyo bias kama hana uelewa nalo ni vyema akakaa kimya ila kama anatumika acha aendelee atajua yeye na Mungu wake.
 
Back
Top Bottom