Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini.

Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar. 10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.

Angalizo ni kwamba, TUNDU LISSU amefungiwa kufanya kampeni zozote katika majukwaa kwa siku saba. Hivyo kama atapanda jukwaani kwa namna yeyote ile ndani ya muda uliyowekwa, hakuna namna atakwepa mkono wa sheria. Ni vyema akafuata taratibu alizopewa ili kuepusha malalamko baadaye.
 
Anapambana na aliyeshika mpini. Busara ilikuwa ni chama chake kitoe tamko siyo yeye binafsi.
Tundu hayupo kwa maslahi ya chama chake wala wananchi, yeye yuko kwa maslahi ya Robati Amstadamu. Na anamlipa fadhila kwa kafuata kila amri anayopewa huku akisahau alipo
 
Aendelee tuu Sasa anapayuka nini😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ndio maana walitaka kumchukua mapema wanajua mziki wake!!!!! Sasa naelewa. Huyu jamaa anajielewa na anajua haki zake. Ni kama raia wa Kenya huyu ndugu
 
Consequence zakuendelea kufanya kampeni zinaweza ku justify hatua ingine kubwa zaidi na ya kuumiza.Naamini NEC wakimkata kuendelea na uchaguzi hakuna kitakachotokea (kama ilivyotokea kwa JECHA).Atumie busara na ajenge hoja!!
Kama hilo linawezekana ni bora afanye hivyo ili wamuengue mapema. Maana najua hata akishinda hawatamtangaza
 
Mnatumia udhaifu huo kukandamiza watu? Eti asishiriki ili mpite bila kupingwa?

Muache atuonyeshe njia na kujua namna ya kupambania haki zetu.

Mbali ya kampeni, Lissu anatufungua macho
 
Unadhani hayo yakitokea wewe na familia yako mtabaki salama?

Acheni kuchochea watu kuumizana kwa maslahi ya watu wachache
 
Anatafuta triggering factor...ya kuanzisha vurugu. Yawezekana ni moja ya kazi alizopewa, maana inasemwa si mwananchi mwenzetu yule. Fuatilieni ukweli wa hili.
Kazungumza kwa mujibu wa sheria. Kama mmefuata sheria, mpeni vifungu.

Acheni kujificha kwenye koti la vurugu
 
Nashangaa sana na Comment za humu.

Wengi wanaona kama LISSU ni Mkorofi na anatafuta chokochoko ; Ukweli ni kwamba CCM ni dhulumati na wana siasa za kishamba zilizopitwa na wakati, yaani Ujima.

CCM Hii Hii ndio iliyofuta uchaguzi Zanzibar kwa kuendekeza dhulma na kuuficha ukweli. Kitendo kile ni jibu tosha nani si mwema katika nchi.

Kabla ya kuwaza kwamba Lissu anataka kuharibu Amani ya Nchi; tuwaze kwanza CCM ndio chama chenye kuleta Vurugu. Yaani CCM inajiona ina haki kila mahala. Ni ulofa kwa Karne hii. Tukuwe watu wazima basi.

Kama uchaguzi , CCM itashinda hata kwa mkono ; sasa upuuzi wa nini ! Si wamuache huyo Lisu afanye linalomfaa. Yaani siasa za Kitanzania ni Ufala sana .
 
ogopa sana mtu aliyebishana na kifo,usibishane nae atakuumiza kwa kila kitu.
 

Sawa Bw Mahera umesikika..
 
Umezoea kuroga mnaroga mpaka mchana
 
UPUUZI MTUPU!! Mbona huyo anayejiita KICHAA yeye hiyo Tume FAKE haimsumbui pamoja na kukiuka taratibu kila siku?

 
Consequence zakuendelea kufanya kampeni zinaweza ku justify hatua ingine kubwa zaidi na ya kuumiza.Naamini NEC wakimkata kuendelea na uchaguzi hakuna kitakachotokea (kama ilivyotokea kwa JECHA).Atumie busara na ajenge hoja!!
Huo uwezekano hakuna kabisaaa. Sumu haijaribiwi kwa kuimeza
 
Uchaguzi hauendeshwi na maagizo wala matamko ya tume ila ni kwa mujibu wa sheria, kwo wakifuata sheria na yeye atafuata ila vinginevyo haiwezekani kabisa kumtii shetani hatakama umemkuta madhabahuni
Hafati maelekezo ya tume,anashindana na tume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…