Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Kamati kuu wanatoaje maamuzi ikiwa barua haijapokelewa?
Lissu alitoa msimamo na zaidi alisema anasubiri maamuzi ya kamati Kuu na lolote watakaloamua kamati kuu yeye atafuata. Hivyo tunafuata msimamo huu mpya uliotolewa na kamati Kuu kwa sababu Lissu alisema ndo yatakuwa maamuzi ya mwisho
 
Kamati kuu wanatoaje maamuzi ikiwa barua haijapokelewa?
Lissu alitoa msimamo na zaidi alisema anasubiri maamuzi ya kamati Kuu na lolote watakaloamua kamati kuu yeye atafuata. Hivyo tunafuata msimamo huu mpya uliotolewa na kamati Kuu kwa sababu Lissu alisema ndo yatakuwa maamuzi ya mwisho
 
Kuna watu ndani ya system wamemshauti asiendelee lakini alikuwa anaendelea kama kawaida. Mtego umechomolewa
Ule ulikuwa ni uropokaji tu,Ila watu tunaolewa misingi ya chadema tulikuwa tunamzoom? 😂
 
Salaam Wakuu,

Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.

Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.

Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni

======

UPDATES:

16:54HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.

17:04HRS

Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.

Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.

Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.

Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.

1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utaratibu.

2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.

3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.

4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.


HII HAISHANGAZI

Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.

Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.

Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.

Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.

Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.

Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.

NINI MSIMAMO WANGU?

Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.

Hoja nilizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.

Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.

Uamuzi huu sio wa haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.

View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.

Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.

Ya kwangu kwa leo ni hayo.

Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza

Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji

Swali: Huoni unaleta Ukaidi? Sheria inasema nipewe nakala ya Mashitaka, sijapewa

Sheria inasema apewe masaa 48, sijapewa.

Sheria inasema akishitakiwa natakiwa apewe nakala ya Maamuzi, sijapewa.

Hiyo sio Sheria. So ninyamaze nionekane mwema? Ninyamaze niwapendezeshe wakina Polepole? Sijawahi kunyamaza. Natetea haki yangu

Swali: Huoni unafanya mambo kwa Jaziba?

Lissu: Mimi nina Jeshi? Nilisema Hatutokubali kuibiwa kura, hatutokubali kanuni zisipofuatwa. Kama hizo ndo Jaziba basi nina Kaziba

Swali: Kama Kamati kuu ikisema Usubiri Siku 7?

Jibu: Nitasubiri.

Swali: Barua inasema wamempa barua yako Katibu Mkuu.

Jibu: Haya maadili yalisainiwa na Wagombea.

Kuna maadili ya Chama na Maadili ya Mgombea.

Chadema haikuwa Mlalamikiwa aliyekuwa Mlalamikiwa ni Tundu Lissu. Kama Mlalamikiwa ni Tindu Lissu anayepelekewa ni nani?

Mimi nafuata ratiba ya Tume, Natembea na Askari Polisi amekaa nyuma ya kiti changu, Polisi magari Mawili ya Polisi, kila ninapolala Polisi Wanalinda. Hivyo tume wanajua nilipo, Wasingeshindwa lete barua.

Tume wana hofu kubwa ya kuniita. Wanakiuka maadili ili wasikutane na mimi Uso kwa uso.

Nizungumzie mgogoro wangu na Polisi.

Wito wa Polisi sio barua ya Mapenzi. Wito wa Polisi ni Amri. Kwa sababu ni amri ya Kisheria ina mashariti yake. Polisi hatakiwi kukuita kwa lolote bila kuambiwa Makosa yako.

Nmemsikia Sirro jana eti niende kujieleza Moshi. Kwa kosa lipi?

Mumeona barua ya Wambura, umeona kosa lake? Eti nikajieleze kwa Matamshi. Matamshi gani?

Mimi sina Mpango huo wa kukanyagwa na watu wasiofuata Sheria. Unatakiwa Useme kosa. Sitakuja sababu najitambua. Asiyeelewa haki zake akiitwa na Polisi anaruka anaenda. Sio mimi.

Polisi alinifuata akasema asingefuata Ushauri ingeleta maafa.

Kwamba CCM walikua wanawaambia Polisi piga Mabomu. Watu waligoma kuondoka.

Mimi si nilisindikizwa na Polisi usiku ule hadi kwenye Mkutano pale Moshi nikasema muda umeisha, tawanyikeni wakatawanyika. Kosa langu ni lipi? Mlitaka wapigwe Mabomu?

Nyamongo mimi sikiwa na ratiba. Siku hiyo nlisindikizwa na Polisi OCD yupo mbele mimi katikati Polisi wengine Nyuma. Tulofanya mikitano Mitatu. Polisi wakikuta watu wananisubiri Wanasimamisha msafara nasalimia. Mimi na Nyamongo tuna urafiki kwani Wakati wa Mkapa nilikuwa nawatetea kuhusu Madini, Wasingekubali nipite bila kuongea.

Wale Polisi Walipiga Mabomu hadi yakawaishia watu wakaanza kurusha Mawe. Ikabidi nishuke kwenye gari baada ya kupiga Mabomu. Nikasema fanyeni mnachotaka. Tukafanya mkutano. Hao hao waliotupiga Mabomu baada ya Mkutano wakatusindikiza na Magari 10 mpaka Serengeti.

Kama ni sahihi kwa Magufuli ni sahihi kwa Tundu Lissu.

Feedback ya Mikoani si mnaona Nyomi? Ukweli ni kwamba tulipopita pote tunampiga Magufuli mapema sana. Tunampiga Mwanza, Geita, Kigoma. Na wakiiba hatukubali, Kitanuka. Tunataka kama ni kushindwa tushindwe kihalali.
Nimewahi kuona sehemu Mh Lissu ukisema hukumbuki ni lini ULIKUBALIANA NA WALIMU WAKO UKIWA SHULE.
Kwa mantiki hiyo,naona hilo ndilo liliopo moyoni mwako,kwamba wengine wote hawajui ila wewe tu.
Najua wewe ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA.
Najua pia unafahamu kwamba taasisi za kiserikali huwa zinafanyakazi kimaandishi.
Nafahamu kwamba mtendaji mkuu wa chama cha siasa ni katibu mkuu
Nafahamu unafahamu kwamba mawasiliano yote ya kichama yanapelekwa kwa katibu mkuu wa chama
Nafahamu HUKUWASILIANA NA KATIBU MKUU KAMA AMAPATA BARUA AU LAA
Nafahamu ulijinbu bila kuwasiliana na ye yote.
Nafahamu ulizani tume iltakuandia wewe kama mgombea kinyume na taratibu.
Wewe kama mgombea unatupa picha halisi utakapochaguliwa hutakuwa na subira au usikivu kwa mtu ye yoe,hasa
kwa kauli yako kwamba hukumbuki linmi ulikubaliana na walimu wako.
 
Back
Top Bottom