Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini.

Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar. 10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.

Angalizo ni kwamba, TUNDU LISSU amefungiwa kufanya kampeni zozote katika majukwaa kwa siku saba. Hivyo kama atapanda jukwaani kwa namna yeyote ile ndani ya muda uliyowekwa, hakuna namna atakwepa mkono wa sheria. Ni vyema akafuata taratibu alizopewa ili kuepusha malalamko baadaye.
 
Anapambana na aliyeshika mpini. Busara ilikuwa ni chama chake kitoe tamko siyo yeye binafsi.
Tundu hayupo kwa maslahi ya chama chake wala wananchi, yeye yuko kwa maslahi ya Robati Amstadamu. Na anamlipa fadhila kwa kafuata kila amri anayopewa huku akisahau alipo
 
Salaam Wakuu,

Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.

Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.

Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni

======

UPDATES:

1654HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.

1704HRS

Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.

Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.

Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.

Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.

1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utarsti6.

2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.

3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.

4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.


HII HAISHANGAZI

Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.

Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.

Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.

Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.

Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.

Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.

NINI MSIMAMO WANGU?

Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hiivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.

Hoja nlizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.

Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.

Uamuzi huu sio wq haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.
View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.

Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.

Ya kwangu kwa leo ni hayo.

Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza

Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji

Swali: Huoni unaleta Ukaidi? Sheria inasema nipewe nakala ya Mashitaka, sijapewa

Sheria inasema apewe masaa 48, sijapewa.

Sheria inasema akishitakiwa natakiwa apewe nakala ya Maamuzi, sijapewa.

Hiyo sio Sheria. So ninyamaze nionekane mwema? Ninyamaze niwapendezeshe wakina Polepole? Sijawahi kunyamaza. Natetea haki yangu

Swali: Huoni unafanya mambo kwa Jaziba?

Lissu: Mimi nina Jeshi? Nlisema Hatutokubali kuibiwa kura, hatutokubali kanuni zisipofuatwa. Kama hizo ndo Jaziba basi nina Kaziba

Swali: Kama Kamati kuu ikisema Usubiri Siku 7?

Jibu: Nitasubiri.

Swali: Barua inasema wamempa barua yako Katibu Mkuu.

Jibu: Haya maadili yalisainiwa na Wagombea.

Kuna maadili ya Chama na Maadili ya Mgombea.

Chadema haikuwa Mlalamikiwa aliyekuwa Mlalamikiwa ni Tundu Lissu. Kama Mlalamikiwa ni Tindu Lissu anayepelekewa ni nani?

Mimi nafuata ratiba ya Tume, Natembea na Askari Polisi amekaa nyuma ya kiti changu, Polisi magari Mawili ya Polisi, kila ninapolala Polisi Wanalinda. Hivyo tume wanajua nilipo, Wasingeshindwa lete barua.

Tume wana hofu kubwa ya kuniita. Wanakiuka maadili ili wasikutane na mimi Uso kwa uso.

Nizungumzie mgogoro wangu na Polisi.

Wito wa Polisi sio barua ya Mapenzi. Wito wa Polisi ni Amri. Kwa sababu ni amri ya Kisheria ina mashariti yake. Polisi hatakiwi kukuita kwa lolote bila kuambiwa Makosa yako.

Nmemsikia Sirro jana eti niende kujieleza Moshi. Kwa kosa lipi?

Mumeona barua ya Wambur7, umeona kosa lake? Eti nikajieleze kwa Matamshi. Matamshi gani?

Mimi sina Mpango huo wa kukanyagwa na watu wasiofuata Sheria. Unatakiwa Useme kosa. Sitakuja sababu najitambua. Asiyeelewa haki zake akiitwa na Polisi anaruka anaenda. Sio mimi.

Polisi alinifuata akasema asingefuata Ushauri ingeleta maafa.

Kwamba CCM walikua wanawaambia Polisi piga Mabomu. Watu waligoma kuondoka.

Mimi silisindikizwa na Polisi usiku ule hadi kwenye Mkutano pale Moshi nikasema mida umeisha, tawanyikeni wakatawanyika. Kosa langu ni lipi? Mlitaka wapigwe Mabomu?

Nyamongo mimi sikiwa na ratiba. Siku hiyo nlisindikizwa na Polisi OCD yupo mbele mimi katikati Polisi wengine Nyuma. Tulofanya mikitano Mitatu. Polisi wakikuta watu wananisubiri Wanasimamisha msafara nasalimia. Mimi na Nyamongo tuna urafiki kwani Wakati wa Mkapa nlikuwa nawatetea kuhusu Madini, Wasingekubali nipite bila kuongea.

Wale Polisi Walipiga Mabomu hadi yakawaishia watu wakaanza kurusha Mawe. Ikabidi nishuke kwenye gari baada ya kupiga Mabomu. Nikasema fanyeni mnachotaka. Tukafanya mkutano. Hao hao waliotupiga Mabomu baada ya Mkutano wakatusindikiza na Magari 10 mpaka Serengeti.

Kama ni sahihi kwa Magufuli ni sahihi kwa Tundu Lissu.

Feedback ya Mikoani si mnaona Nyomi? Ukweli ni kwamba tulipopita pote tunampiga Magufuli mapema sana. Tunampiga Mwanza, Geita, Kigoma. Na wakiiba hatukubali.. Kitanuka. Tunataka kama ni kushindwa tushindwe kihalali.
Aendelee tuu Sasa anapayuka nini😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ndio maana walitaka kumchukua mapema wanajua mziki wake!!!!! Sasa naelewa. Huyu jamaa anajielewa na anajua haki zake. Ni kama raia wa Kenya huyu ndugu
 
Consequence zakuendelea kufanya kampeni zinaweza ku justify hatua ingine kubwa zaidi na ya kuumiza.Naamini NEC wakimkata kuendelea na uchaguzi hakuna kitakachotokea (kama ilivyotokea kwa JECHA).Atumie busara na ajenge hoja!!
Kama hilo linawezekana ni bora afanye hivyo ili wamuengue mapema. Maana najua hata akishinda hawatamtangaza
 
Kama haiamini tume kwanini ashiriki uchaguzi? Si angeacha? Hiyo ingeleta maana kuwa kuna matatizo kwenye tume. Ni sawa na muumini anayemuomba Mungu bila kujua kuwa Mungu anaweza kufanya hicho anachokiomba. Wote wanaomuomba Mungu wanatumaini kuwa yupo na anaouwezo.

Kubahatisha hakufai
Mnatumia udhaifu huo kukandamiza watu? Eti asishiriki ili mpite bila kupingwa?

Muache atuonyeshe njia na kujua namna ya kupambania haki zetu.

Mbali ya kampeni, Lissu anatufungua macho
 
ngoja niwaambie kwa upole tuu MTAKAO UMIA NI NYINYI MISKULE yake hamuwezi kujifanya arrogant sababu ya icj
huu mchezo hauitaji hasira na huu ni mtego mnajiingiza kichwakichwa kubishana na vyombo halali

Mtachapika na asitokee mtu wa kuwasaidia

naona serkali ishajivua na lawama kama zitatokea vurugu + serkali inapata uhalali wa kuwashughulikia perpendicular

hapa lisu amekurupuka!!
Unadhani hayo yakitokea wewe na familia yako mtabaki salama?

Acheni kuchochea watu kuumizana kwa maslahi ya watu wachache
 
Anatafuta triggering factor...ya kuanzisha vurugu. Yawezekana ni moja ya kazi alizopewa, maana inasemwa si mwananchi mwenzetu yule. Fuatilieni ukweli wa hili.
Kazungumza kwa mujibu wa sheria. Kama mmefuata sheria, mpeni vifungu.

Acheni kujificha kwenye koti la vurugu
 
Nashangaa sana na Comment za humu.

Wengi wanaona kama LISSU ni Mkorofi na anatafuta chokochoko ; Ukweli ni kwamba CCM ni dhulumati na wana siasa za kishamba zilizopitwa na wakati, yaani Ujima.

CCM Hii Hii ndio iliyofuta uchaguzi Zanzibar kwa kuendekeza dhulma na kuuficha ukweli. Kitendo kile ni jibu tosha nani si mwema katika nchi.

Kabla ya kuwaza kwamba Lissu anataka kuharibu Amani ya Nchi; tuwaze kwanza CCM ndio chama chenye kuleta Vurugu. Yaani CCM inajiona ina haki kila mahala. Ni ulofa kwa Karne hii. Tukuwe watu wazima basi.

Kama uchaguzi , CCM itashinda hata kwa mkono ; sasa upuuzi wa nini ! Si wamuache huyo Lisu afanye linalomfaa. Yaani siasa za Kitanzania ni Ufala sana .
 
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini..
ogopa sana mtu aliyebishana na kifo,usibishane nae atakuumiza kwa kila kitu.
 
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini...

Sawa Bw Mahera umesikika..
 
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini...
Umezoea kuroga mnaroga mpaka mchana
 
UPUUZI MTUPU!! Mbona huyo anayejiita KICHAA yeye hiyo Tume FAKE haimsumbui pamoja na kukiuka taratibu kila siku?

Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar. 9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini....
 
Consequence zakuendelea kufanya kampeni zinaweza ku justify hatua ingine kubwa zaidi na ya kuumiza.Naamini NEC wakimkata kuendelea na uchaguzi hakuna kitakachotokea (kama ilivyotokea kwa JECHA).Atumie busara na ajenge hoja!!
Huo uwezekano hakuna kabisaaa. Sumu haijaribiwi kwa kuimeza
 
Uchaguzi hauendeshwi na maagizo wala matamko ya tume ila ni kwa mujibu wa sheria, kwo wakifuata sheria na yeye atafuata ila vinginevyo haiwezekani kabisa kumtii shetani hatakama umemkuta madhabahuni
Hafati maelekezo ya tume,anashindana na tume
 
166 Reactions
Reply
Back
Top Bottom