Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Tundu Lisu ana sifa moja kuu, anapenda kujenga hoja bila kuweka chuki au uadui. Hana adui wa kudumu na kutokuwa na adui hakujawahi kumfanya awe mnafiki kama walivyo wanasiasa na wanazuoni wengine.
Anapotamka wazi kwamba Magufuli hakuuza nchi kwa mikataba mibovu anasema ukweli. Anaposema Mkapa na Jk waliuza nchi na mifano anakupa.
Hayati Magufuli alikuwa adui wake mkubwa; na hapa amecheza mchezo mkubwa sana kuona kwamba wapo sukuma gang wanahitaji faraja kwa Hayati Magufuli.
Alipoona yupo kanda ya Ziwa kwanza kuwapanga Sukuma Gang na amefaulu kila uzi umejaa maneno ya Lissu. Huyu ni nguli wa kuchanga karata, amebobea kwenye mikakati. Watu wa kanda ya ziwa walimwona Hayati Magufuli kama mkombozi wao; Lisu anatambua ilo na sasa ameamua kwenda Chato kuona kaburi la Magu.
Kwa wataalamu wa fasihi anataka kuwaambia Dunia kwamba hana adui wa kudumu na Dunia nzima itafuatilia tukio la yeye kwenda kwa Hayati Magufuli. Ugumu wa safari yake to Chato ni kwamba anakwenda kumuuliza hivi ndiyo CCM uliyokuwa unaipigania?
Natambua hatapata majibu ila kisiasa anapeleka ujumbe kwamba ukiwa mwanasiasa usiimarishe chama cha siasa kuliko nchi; tengeneza mifumo ya nchi. Hiyo itadumu milele na malengo yako yatakuwa malengo ya Taifa.