Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amjibu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu karipio la kuongeza ubeti kwenye Wimbo wa Taifa

Pale inapothibitishwa kuhusu weledi wa majaji wetu ikiwa vitu vidogo kung'amua ni shida.
Heshima kubwa kwa Tundu Lissu
 
Nadhani Lissu aache tit for tat, hazimsaidii

Watanzania hawapendi arrogance/much know.

Angeweza kupeleka maoni yake kwa mwaanasheria wa chama, kisha Chama kikatoa statement, siyo yeye kuingia front na kuanza malumbano

Lissu ajue kuwa yeye sasa ni potential president inabidi aact presidentially, siyo kama mere activist.

Siyo lazima aseme kila kitu!

Mzunguko wote huo wa nini sasa?

Hii hii inatosha, tumemwelewa...

Na kwa taarifa yako, hii ndiyo namna bora na sahihi ku - deal na CCM na allies wao.
 
Mimi nampa tu angalizo huyo Mutungi. Amekuwa akifumbia macho uvunjaji wa wazi wazi wa Katiba unaofanywa na uongozi wa juu kabisa wa CCM kwa kofia ya serikali. Halafu leo kama mlevi anakurupuka na matamshi yasiyo na msingi kisheria utadhani hakuona milango ya shule. Safari hii lazima achunge sana ulimi wake asije akaonekana kituko. Kabla ya kumjibu Mh. Tundu Antiphas Lissu atulie na apime kauli zake kabla ya kuropoka hovyo. Ni hilo tu.
 
Lissu is sharp

Kinachompoza ni kukosa filter au breki kwenye mambo yake

Sometimes sio kila kitu ajibu yeye

Chama kina msemaji

Unahitaji filter na break gani kwenye mazingira haya kwa mtu ambaye anaku - accuse wrongly hadharani...??

This is the best way to deal na CCM na allies wao...

Na kama hujui au kutambua ni kuwa hawa jamaa wamejibanza kila kona kuvizia na kuokoteza kila aina ya vijikosa ili mradi tu wawa - confuse na kuwapotezea focus ktk mipango yenu...

Mbinu na njia hii ni sahihi kabisa kwa wanaotafutwa, CHADEMA na ACT WAZALENDO.....

Na Bahati mbaya kwao ni kuwa, wameweka vijana wajinga wajinga sana, wasio na weledi wowote ktk nyanja za kijamii, uchumi na kisheria kuifanya kazi hii....

Ni weupe vichwani, hawajui hata kujenga hoja zao kutetea mabwana zao wanaowatuma. Utaweza kuthibitisha hili kwa kuwasoma humu na ktk social medias zingine nyingi...

Dawa yao ndiyo hii. Wanaibua ujinga wao, na hapohapo unapanguliwa. Hakuna kusubiri siku mbili au tatu. Ni TIT 4 TAT....
 
Mimi nampa tu angalizo huyo Mutungi. Amekuwa akifumbia macho uvunjaji wa wazi wazi wa Katiba unaofanywa na uongozi wa juu kabisa wa CCM kwa kofia ya serikali. Halafu leo kama mlevi anakurupuka na matamshi yasiyo na msingi kisheria utadhani hakuona milango ya shule. Safari hii lazima achunge sana ulimi wake asije akaonekana kituko. Kabla ya kumjibu Mh. Tundu Antiphas Lissu atulie na apime kauli zake kabla ya kuropoka hovyo. Ni hilo tu.
Jaji kasema hili swala ameiachia mamlaka husika
 
Je tunaweza kuwiita ni umbu mbumbu wa viongozi wetu waliopewa madaraka ya juu ya Inchi ambao hawatofautishi kati ya Siasa na Sheria.
Wanataaluma wengi baada ya kuwekwa kwenye nafasi za uongozi kwenye taasisi za serikali wamekuwa wavivu wa kurejea vifungu vya Sheria na kanuni wanapojibu hoja mbali mbali.
Kiongozi mkuu wa taasisi muhimu anasema, Sheria imevunjwa bila kutaja kifungu cha Sheria kilichovunjwa.
Kiongozi mkuu anasema wimbo wa Taifa umenajisiwa wakati ne no najisi halipo katika vifungu vya Sheria bali hutumika katika misahafu ya Dini.
Huyu anawaza udini zaidi kuliko Sheria.
Siku zote Viongozi wetu wapendwa wajue kuwa Tundu Lissu anapotoa ne no ambalo wengi wanatafasiri ni tusi au kashfa anakua anajua mahali pa kutokea kisheria.
Kwa mfano anapotaja vipaya Rais wa Inchi bila kutaja jina lake.
Ukimpeleka mahakamani anakuambia kuwa Tanzania kuna marais wengi wa kuchakuliwa, kwa umueleze ni yupi ambaye alimkashifu. Kuna rais wa TFF, TLP, pi kuliwawahi kuwa na Rais wa Yanga. nk
Tunakuomba Tundu Lissu the great, wewe sasa hivi ni maarufu sana , fanya busara na hekima katika uongozi wako wa Kisiasa kwa manufaa ya watu wa Singida ambao tumeachwa nyuma kimaendeleo.
Hatuna chuo kikuu hata kimoja ambacho kingeongeza mzunguko wa pesa kidogo na akina mama wa sokoni wakauza nyanya zao.
Sasa hivi serikali inakuheshimu na ukikaa nao vizuri watafanya yote unayotaka hata bila kuwa Rais.
 
Jaji mstaafu hajui sheria za nchi.... Asije kuwa ni wale wa group la kupata maelekezo toka juu.
 
Mi ndo maana nasema upinzani Tanzania kutawala bado Sana,Sasa kilichofanya waongeze ubeti ni nini hasa,?Mi Sina mzuka na CCM lakini uropokaji na kiherehere Cha upinzani kinaboa na vinawaponza kila siku hawakomi.Hadi wanaonekana kama wahuni tuu.

Hao walioingia mikataba ya wizi nchi hii ndio wanajua kuimba huo wimbo wa taifa kwa usahihi, kwanini kama wanajua umuhimu wa huo wimbo waliingia mikataba ya wizi?
 
Mwambieni Msajili wa Vyama vya Siasa akasome Sheria ya Nembo za Taifa ya 1971 ili ajiridhishe kama Wimbo wa Taifa ni mojawapo ya Nembo za Taifa zinazolindwa kisheria kabla hajatoa vitisho vya bure kama hivi. Ataje Sheria iliyovunjwa, kama ipo, kabla hajatoa kauli za aina hii. - Tundu Lissu

Kwa hiyo wimbo wetu wa taifa unaweza ukachezewa ovyo ovyo, kwa kuingiza beti za futuhi, za kingwendu nk au za mapenzi moto moto za Diamond nk?
Eti siyo nembo ya taifa. Tangu lini wimbo ukawa nembo? Wimbo wa Taifa lo lote unaheshimika sana na unapoimbwa watu hukaa mguu sawa na kutulia. Sasa utaufanyiaje mzaha kwa kuuimba kifutuhi?
Huyu jamaa alishamzihaki mara kadhaa hata baba wa taifa letu Mwalimu Nyerere kwa kisingizio hicho hicho kwamba yeye si nembo ya taifa! Kama si kuchanganyikiwa akili itakuwa ni nini?
 
Mtu anagombea urais! Badala awe bize na mambo makubwa makubwa, yeye anahangaika na Mutungi.

He can’t be serious
Mambo makubwa ni yapi?
Hili la Mutungi kutishia nyau ni dogo?
Wewe kupigwa nao kisha ukakaa kimya kisa tu unataka upate jambo kubwa (utajiri) kusikufanye ufikirie wote wapo kama wewe.
Leo mtu ataanza kwa kukukanyaga,ukikaa kimyaa,kesho "singi",ukipiga kimyaa tena,basi kesho kutwa unapigwa dole.
Chora mstari mapema ili watu wasikuchezee.
 
Kama mteuliwa wa kugombea nafasi ya urais, Tundu Lisu anapaswa kuacha siasa za aina hii.

Angewasiliana na msajili moja kwa moja kuweka heshima kwenye nafasi yake kama mgombea wa nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Aache mipasho isiyo ya lazima, tunafahamu anaifahamu sheria, sasa avae u candidate.
Msajili ndiye aliyetakiwa kuwaandikia CDM barua juu ya suala hilo. Sasa yeye anajiropokea tuu kama enzi zile tulipokuwa naye Dom kama msajili tukigombania watoto wa Dom Sec,Central Sec na CBE pale Kisasa nyumba 300.
 
Back
Top Bottom