Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,833
Tundu Lissu kwa maneno yake mwenyewe na kwa kujiamini alisema Magufuli ndiye aliyeagiza apigwe risasi kwa madai kuwa alikua msaliti bahati nzuri akapona.
Lissu alidai tena aliponea kuuawa mara ya pili baada ya uchaguzi kumalizika na akaokolewa na ubalozi wa Ujerumani.
Rais Samia ambaye ndiye kiongozi pekee aliyemtembelea Tundu Lissu alipokuwa amelazwa Nairobi, alikubali pia kumtembelea Tundu Lissu nchini Ubelgiji alipokuwa katika ziara ya kikazi.
Tundu Lissu baada ya hapo alisema Samia alimlipa stahiki zake za Ubunge na kumwambia atamlipa pia na hela zake za matibabu akikamilisha kupeleka vielelezo.
Ukizingatia nchi ilipokuwa imetoka kabla ya Samia kuwa Rais kitendo cha Samia kukutana na Lissu iliwashtua sana CCM na CHADEMA, kwa kuwa kulikuwa na uadui mkubwa sana.
Rais Samia pamoja na hayo alifanya mengi ambayo yalikuwa kinyume na msimamo wa chama chake kilichokuwa na msimamo mkali dhidi ya Chadema kwa manufaa ya Chadema na nchi kwa ujumla.
Alifuta kesi nyingi zilikuwa zinawakabili kutoka awamu ya 5, kuwakaribisha nchini waliokuwa wamekimbia nje, kuwapa malimbikizo ya ruzuku, kuruhusu kufanya mikutano ya hadhara iliyokuwa imezuiwa, kufungulia vyombo vya habari, na hata kuahidi kufufua mchakato wa katiba mpya, ambao mtangulizi wake alikataa hata kusikia.
Sasa leo nikaona tweet ya Lissu akimkebehi Samia kuwa hajafanya la maana lolote halafu ameweka bango.
Labda pengine Lissu na wanaharakati wengine wa Chadema hawajui kwamba Samia angeweza kuendeleza aina ya utawala wa Magufuli ambao ndio wengi katika CCM wanataka na ila akatumia busara, na sadly wasingekuwa na la kufanya.
Sasa kiongozi akionyesha busara na nyie onyesheni busara, kuna mengi ambayo bado Chadema na Lissu wanaweza kuwa wanadai au hayaendi kwa spidi kama wanavyotaka lakini kukejeli jitihada za Samia ni kuwapa nguvu wahafidhina ndani ya CCM.