Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

IMG-20261101-WA0009.jpg
 
Taarifa za kusikitisha zimetufikia SasaLive zikithibitisha kifo cha Wakili Allute Lissu Mughwai, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa,Tundu Lissu, kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

Habari za ndani za kuaminika zimeweka wazi kuwa msiba huo upo mkoani Arusha, ambapo taratibu za awali za msiba zinaendelea kuratibiwa na wanafamilia na ndugu wa karibu.

Hadi kufikia sasa, ratiba ya mazishi imepangwa kufanyika katika Kijiji cha Mahambe mkoani Singida, huku ikielezwa kuwa mazishi hayo yatasubiri kwanza kukamilika kwa hukumu ya kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inayotarajia kusomwa tarehe 06 Novemba 2026.

SasaLiveinaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa zaidi kutoka kwa viongozi wa familia na wanasheria ili kuwajuza wananchi na wadau kuhusu hatua nyingine zote za msiba huu mzito.

#AlluteLissu #TunduLissu #Chadema #Arusha #Singida SasaLive
1793517568074.jpg
 
Mdogo wake na Tundu Lissu, Ikota Lissu, amesema kuwa kumfikishia taarifa za msiba wa kaka yake Tundu Lissu ,marehemu Alute Lissu, ilikuwa kazi nzito kihisia kutokana na uhusiano wa karibu uliokuwapo kati yao kwa kuwa marehemu, alikuwa mlezi na mshauri wa Lissu katika masuala mbalimbali, yakiwamo sheria na siasa.

Akisimulia tukio hilo, Ikota amesema walifika Gereza la Ukonga asubuhi wakiwa watu wanne, wakiwamo yeye, Jenerali Ulimwengu, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na mpwa wa Lissu, lakini uongozi wa gereza uliwaruhusu ndugu wawili pekee kuingia kumfikishia taarifa hizo.

Amesema walipokutana na Lissu, hawakuhitaji kutoa maelezo marefu, kwani baada ya kusalimiana na kuulizana hali za nyumbani, mpwa wake alimtajia jina la Alute, jambo lililomfanya Lissu kuelewa mara moja kuwa kaka yake amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Ikota, baada ya kupata taarifa hizo, jambo la kwanza Lissu alilosisitiza ni kuhakikisha marehemu anapata mazishi yanayostahili, huku akiahidi kutoa Sh.15 milioni kugharamia shughuli hizo.

Pia, Lissu aliwaelekeza ndugu zake kushirikiana na mapadri, askofu, viongozi wa Kanisa Katoliki mkoani Singida na marafiki wa marehemu katika kuratibu mazishi hayo, akisisitiza umuhimu wa kumpa heshima kaka yake.
1793671599219.jpg
 
‼️UJUMBE KUTOKA GEREZA LA UKONGA‼️

Anaandika Wakili Paul Kisabo

Nimetoka Ukonga kuzungumza na Mhe. Lissu, he is fine na anawasalimia wote, amesema

"I remain optimistic about tomorrow but am also prepared for the worst, so if the best comes, I will go straight to Arusha to take my brother home. If the worst happens, then the struggle will continue. It will not be the end of the world; it will just be a new chapter in the struggle for justice and democracy in this country" akaongezea kuwa I am sustained by the line of a famous Kenyan freedom fighter Koigi wa Wamwere who authored the autobiography I Refuse to Die: My Journey for Freedom na Mhe. Lissu amemalizia kuwa TL insoumiese "

Tafsiri ya Ujumbe wa Mhe. Lissu kwa Kiswahili.

“Ninaendelea kuwa na matumaini kuhusu kesho, lakini pia nimejiandaa kukabiliana na habari mbaya. Hivyo, ikiwa mambo yataenda vizuri, nitaelekea moja kwa moja Arusha kumpeleka kaka yangu nyumbani lakini ikiwa vinginevo basi mapambano yataendelea.

Huo hautakuwa mwisho wa dunia; utakuwa tu mwanzo wa sura mpya katika mapambano ya kudai haki na demokrasia katika nchi hii.

Aliongeza kuwa anapata nguvu na faraja kutokana na maneno ya mpigania uhuru maarufu wa Kenya, Koigi Wamwere, ambaye aliandika kitabu chake cha wasifu binafsi kinachoitwa I Refuse to Die: My Journey for Freedom (Ninakataa Kufa: Safari Yangu ya Kupigania Uhuru).
Mheshimiwa Lissu alihitimisha kwa kusema: "TL insoumiese" …”

INSOUMISE ni neno la kifarasa maana yake ni mtu, asiyekubali kunyenyekea, asiyetishika wala huwezi kumtawala.
1793885078913.jpg
 
INSOUMISE ni neno la kifarasa maana yake ni mtu, asiyekubali kunyenyekea, asiyetishika wala huwezi kumtawala.View attachment 3705118
 
TAL SUBMISSION ON MITIGATION;

" Waheshimiwa Majaji Kwa bahati mbaya meamua kuniwekea Kosa... na Hiki mlichofanya ni kutumika kuwa Mahakama na Sehemu ya Mapambano ya Kisiasa... Pia Historia haijawahi kuwa Rafiki ( History is never Kind to Judges who agree to be used). Kwenye Historia hili mlilofanya lilifanyika kwenye Mahakama ya Kenya Mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta na Wenzake hata Hivyo I feel inside my heart you have Conviction already..."

Tundu Lissu: "Siku 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Muhaini kosa ambalo kwa katiba ni kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leo mnaniita mchochezi kwa kosa ambalo halina adhabu yani baada ya kukaa siku 577 kusubiri kitanzi , mmeniita mchochezi na wakili wa serikali mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake.

Hii maana yake ni nini waheshimiwa majaji?

Maana yake ni kwamba kosa nililoshtakiwa nalo halikua kosa "

Ushahidi wangu umethibitisha hii ilikua ni kesi ya kisiasa, kugeuza mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.

Ni political persecution.. kwa hiyo inabidi visababu vitengenezwe kumfunga huyu mgomvi wetu wa kisiasa.

Na visababu vyenyewe ni kosa la.uchochezi ambalo mmelitengeneza sikushtakiwa nalo .

Nje ya uhaini nilishtakiwa kusambaza taarifa za uongo na hilo mmesahau.

Ninajua mna hukumu na mmeshakubaliana na hukumu.

Kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Mzee Jomo Kenyatta na wenzake 6.

Mnaadhibu mtu ambaye hana hatia.

UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI UTALIPONYA TAIFA.

BAK MWABUKUSI.
 
HUKUMU YA MH. LISSU

Mh. Lissu amehukumiwa kwa kosa ambalo
1. Hakushitakiwa nalo
2. Hakusomewa Hati ya Mashitaka
3. Kesi Haikuwa na Mlalamikaji
4. Kesi Haikuwa na Mashahidi wa pande zote 2
5. Kesi haikufunguliwa Polisi kama Makosa ya Jinai yalivyo
6. Mshitakiwa Hajawahi Kukamatwa na Polisi ila ni Majaji tu wamemuokota Mahakamani
7. Kesi haikusikilizwa ila imesomwa tu Hukumu
8. Kosa lina dhamana ila kwa kuwa kesi imeanzia Hatua ya Hukumu Mtuhumiwa hakupewa haki ya Dhamana
9. Mtuhumiwa hakupewa haki ya kujitete au kuweka wakili wa kumtetea!
10. Majaji wamesoma Hukumu ambayo Haikuwa na Hati ya Mashitaka!!
11. Kesi hakupita Hatua ya Mention
12. Kesi hakupita Hatua ya PH
13. Kesi haikupita Hatua ya Rulling ( case to answer au no case to answer)

Hii ni zaidi ya aibu na hata Maelekezo kutoka juu huwa hayoko hiv!!!
 
Wakili Jebra Kambole ameweka wazi pazia la kile kilichotokea chumbani mwa mahakama kati ya mawakili na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, mara baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uchochezi na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne jela, tarehe 6 Novemba 2026.

Katika ushuhuda aliouweka wazi kupitia mtandao wa X, Wakili Kambole ameeleza kuwa Lissu aligomea mpango wa mawakili wake wa kuomba kupunguziwa adhabu (mitigation), akahoji iwapo hatua hiyo ingebadili uamuzi ambao tayari aliamini ulishapangwa, kabla ya kuamua kusema kile kilichokuwa moyoni mwake.
Wakili Kambole ameelezea mazungumzo hayo ya faragha yaliyojiri mahakamani hivi:

"TAL! Baada ya kukutwa na hatia aliomba kuongea na mawakili wake, tukamzunguka kila mtu akawa anampa mitigation facts, akasema kwani hamjui wana hukumu?, tukamjibu tunajua!, akasema nikifanya mitigation itabadili hukumu yao?, tukajibu hapana! Akasema let me speak my mind!"

Maelezo hayo yanaonyesha msimamo usioyumba wa Lissu mbele ya vyombo vya sheria, ambapo alichagua kueleza mtazamo wake bila woga badala ya kufuata taratibu za kawaida za kisheria za kuomba huruma ili kupunguza miaka ya kifungo.

Ushuhuda huu wa Wakili Kambole unaendelea kuongeza joto katika mjadala mpana kitaifa na kimataifa kuhusu uwazi, utawala wa sheria, na mazingira ya kisiasa nchini Tanzania kufuatia hukumu hiyo ya Novemba 6.

#SasaLive #JebraKambole #TunduLissu #Mahakama #DemokrasiaTanzania HakiZaBinadamu Siasa
1794063163011.jpg
 
#SasaLive #JebraKambole #TunduLissu #Mahakama #DemokrasiaTanzania HakiZaBinadamu SiasaView attachment 3706149
 
Back
Top Bottom