Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Mbona upelelezi hadi leo hakuna CCTV camera za nyumbani kwa Lissu zilipelekwa wapi
Nilishawahi kuandika humu kuwa Tundu Lissu siyo presidential material. Nikasema yeye ni rabble rouser. Ni gadfly tu.

Sasa hii majuzi baada ya mahojiano yake kwenye kipindi cha BBC HARDtalk, ambapo alibanwa mbavu kuhusu tuhuma zake mbalimbali dhidi ya Rais Magufuli, CCM, na watu wengine, tuhuma ambazo hajatoa ushahidi wowote, kumeibuka mjadala kana kwamba hiyo ndo ilikuwa mara ya kwanza kwa Lissu kuulizwa ushahidi juu ya hizo tuhuma zake uko wapi.

Pengine labda jukwaa lililotumika kumhoji huo ushahidi ni kubwa zaidi, lakini kiukweli tupo baadhi yetu humu JF ambao tumekuwa tukisema kuwa Lissu mpaka sasa hajaonyesha ushahidi wowote ule juu ya hizo tuhuma zake nyingi anazoporomoshaga.

Mpaka wakati mwingine huwa nafikiria labda akipandagwa na mzuka huwa anasahau kabisa mipaka na misingi ya taaluma yake na kuchanganya madesa ya uanaharakati na uanasiasa.

Nashukuru imechukua kipindi cha kimataifa kumhoji kile ambacho sie wengine tumekuwa tukikihoji humu kwa muda mrefu sasa.

Mtu unaibuka unadai flani na flani wamenifanya hivi au flani kanunuliwa na flani, halafu ukiambiwa onyesha ushahidi wa unachokidai, unaishia kucheza mduara.

Ahsante sana mwendesha kipindi cha HARDtalk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pyeeeeee
Lisu ameanika chuki yake hadharani aibu kubwa sana kwa mwanasheria wa muda mrefu kama yeye kuwekeza hoja zake kwa allegations ambazo hazina ushahidi wowote.

Jambo lililowazi ni kuwa International community ipo well informed kwa yote yanayoendelea Tanzania ndio Maana wanashangaa ni kwa namna gani mtu anaweza kupinga mambo mazuri kabisa Serikali ya sasa inayoyafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye Enzi Mungu ameshatukabidhi baraka zote Mama Tanzania na adui yetu ni adui wa Mwenye Enzi Mungu walahi
Downfall ya lissumsaliti ni straight kaburini walahi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile interview imethibitisha pasi na shaka kuwa Lissu hajui na hana hakika na waliompiga risasi bali ana hisi tuuu....na watu tulitegemea sasa pale ndio amwage ushahidi lakini alibaki na maneno matupu ambayo hayana tofauti na ya kina Salary Slip...Yani Lissu anaulizwa ushahidi ana leta maneno ya kwenye nyuzi za kina Salary Slip....
Hahahahaha


Halafu alipata bahati nzuri alipewa maswali ya kumuelekeza kabisa.....lakini hakuna chochote kipya ambacho ameongea Lissu ambacho kuna mtu hakuwai kukisikia kutoka kwake au kwa wengine....lakini unaweza shangaa wengine wana shangilia as if hayo maneno hawakuwai kuyaona kwenye nyuzi za Salary slip
Hahahahah pale msomi kama lisu anapotumia madesa ya akina Salary slip, BAK au Gsam ni hatar sana. Hawa jamaa wakishapandishwaga mizuka kwenye hizi social networks uamini wamemaliza kila kitu.Sawa na akina Fatuma na zito wanajazwa upepo insta wanaona tayar washashinda kesi,haoooo mbio mahakaman wakifika huko wanapigwa KO.Wanarudi insta maagizo kutoka juu. Huyo muuliza maswali wa BBC angekua Bongo ungesikia maagizo kutoka juu hahahahahahah.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Lissu Nilikuwa namkubali sana wakati akiwa lawyer kabla hajaingia siasa. Ila naona siasa haijamtendea haki kwani baadaye anaonekana kuwa mzushi badala ya mtu aliyekuwa evidence oriented. Jaribio la kuchukua maisha yake kweli ni jambo linalohitaji kulaaniwa sana na watanzania wote bila kujali itikadi zao, na kweli sikufurahishwa na kitendo cha Bunge kushindwa kumlipia gharama za matibabu yake kama ni kweli. Lakini sasa hivi yeye kuwa anayoosha vidole sehemu yoyote bila ushahidi kweli inakatisha tamaa kwa mtu wa kiwango chake. Ametumia muda mwingi negatively kwa kila aliloulizwa bila kutoa matumaini (hope) yoyote. I am sorry

Ndo matatizo ya siasa hayo. Ukishajiingiza kwenye hiyo fani kuna mambo flani flani ya integrity na probity inabidi uyaweke kando!
 
Teh teh teh

Hapo nilicheka sana aisee.

Ila ndo ujue Tanzania fani ya uandishi wa habari bado sana.

Na kusema ukweli, fani zote, ukiondoa labda umbea na uzushi, ni bado sana.

Kwa sababu, Lissu eti ndo anaonekanaga ni bonge la maana sheria lakini kumbe hata namna ya kujibu maswali hajui!!!
Mkuu;
Hata uzushi nchini bado sana kwa sababu uzushi wa Watanzania ukiusoma kama una fikra pana unagundua mara moja kuwa ni uzushi.

Labda tuko vizuri kwenye umbea! hahahah
 
Ona aibu kuandika vitu usivyo vijua. Richard Quest mambo yake ni ya fedha na uchumi. Bora hata ungemtaja mkongwe Larry King.
Kwa kweli Lissu amewaumiza sana. Maswali yote aliyoyauliza Sakkur si mageni hata kidogo. Nia ya Sakkur ilikuwa ni kuonyesha uongozi wa hovyo uliopo hivi sasa Tanzania, kwa International Community.
Mimi mwenyewe nimesoma nikaona huyu mleta mada ni mkurupukaji tu..Quest ni mbobevu wa mambo ya uchumi na biashara..na kwenye mahojiano anayoyafanya anabase kwenye sehemu hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu mwenyewe ndo anasema Magufuli anahusika moja kwa moja na hilo shambulio.

Sasa kilicho kibaya katika kumwuliza ushahidi ni kipi?
Nachojua lisu ilikua ni kumwaga ushahid usioacha shaka. Sasa kaendelea kuruka ruka tu

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Hahaha labda TBC international. SOFT talk.

Nanye Go,
Umenichekesha sana....kumbe kuna TBC International SOFT Talk...!!!!Hii sijui inapatikana masafa gani ili siku moja ni-tune pengine naweza kumwona Jiwe akibonga Kiswanglish cha kutoka pande za Geita Golid Mainingi...!!!
 
Muulize muendesha kipindi aliomuuliza kama ana ushahidi yeye aka refer uzi wa salary slip na comment za jf....aliulizwa ushahidi usiotia shaka yeye analeta hisia... hivi kwa majibu yale usipo ambiwa kama huyu ni Mwanasheria unaweza jua ni mwana sheria? Hivi amejibu nini kipya ambacho kina mtofautisha yeye na Salary slip?

Ushahidi ni mhakamani Mkuu, yeye siyo Jaji, hivyo ushahidi wa mazingira ndicho alichopaswa kuelezwa....
 
as vita 5-0 simba, naweka record sawa tu, tuendelee na mjadala, kama CNN aliitakuwa mbaya na wew umeshajua kwanin usiende wew badala ya lisu?
 
Back
Top Bottom