Ndugu zangu,
Maandalizi yoyote yanakuwa na mantiki pale unapopata matokeo mazuri. Hapa ndipo utakapogundua maana ya kocha wa yanga mkongomani Mwinyi Zahera alipoona mambo yatakuwa magumu kwenye kombe la mapinduzi akaja na propaganda ya kuwa ''atapeleka kikosi B'' kwa sisi watu wazima tuliupata ujumbe.
Turudi kwenye hoja, huenda maandalizi ya kuongea na media za kimataifa yalikuwa mazito na yamegharimu mamilioni ya dola. Inapotokea matokeo yanakuwa madogo sana kulinganisha na uwekezaji tusipeleke ''timu A''.
Ndugu zangu, kule CNN akienda Lissu atakutana na Richard Austin Quest , huku mambo yatakuwa mabaya zaidi kuliko yalivyokuwa kwa Stephen Sackur. Kwani Richard atapata wasaa wakuangalia mahojiano baina ya Steve na Tundu na hapo kazi itakuwa imekwisha, hata akiuliza maswali yale yale hali itakuwa mbaya zaidi.
Hapa ndipo mantiki ya kuitimia timu B, ambapo hapa ndipo Mange Kimambi 'anafit'. kwanini Mange? angalau ana cha kuzungumzia kuhusu maandamano yake yaliyoshindwa ya 26 Aprili, 2018.
Pili, kama kweli Lissu bado anaumwa si busara, Chadema watumie sababu hii kukwepa kiti moto pale CNN kwani kushindwa kwake ni kuanguka kwa chama na aibu zaidi kwa kukosa misingi ya kujenga hoja kimataifa.
Nimalizie tu kwa kusema, 'mzima nguo ikidondoka chutama', sisi wenyewe ni mashaidi wafuasi wengi wa Bavicha hawasherehekei clips za BBC sasa mkiongeza mziki wa CNN ya Richard Quest hali itakuwa mbaya zaidi.
Mahojiano ya CNN aende Mange na sio Lissu kuepuka aibu zaidi.