Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Madini yaweze safirishwa kwa ghrama kidogo.

Madini yasafirishwe kwa gharama kidogo kutoka Chato, gharama ya nani?

Nani huwa anagharimika kusafirisha madini?

Yanatoka wapi yanaenda wapi?

Madini ya nani?
 
Lisu ameanika chuki yake hadharani aibu kubwa sana kwa mwanasheria wa muda mrefu kama yeye kuwekeza hoja zake kwa allegations ambazo hazina ushahidi wowote.

Jambo lililowazi ni kuwa International community ipo well informed kwa yote yanayoendelea Tanzania ndio Maana wanashangaa ni kwa namna gani mtu anaweza kupinga mambo mazuri kabisa Serikali ya sasa inayoyafanya.
 
Kuhusu mdahalo wa Tundu Lissu na mwanaccm hilo yuko tayari na hata mkitaka mpelekeni mwenyekiti wenu kama ana uwezo wa mdahalo na majibu stahiki. Hakuna mwanaccm anayeweza kumjibu Lissu kwenye mdahalo hasa hilo shambulio lake. Lissu kutaka urais ni haki yake na tutampa kura zetu kwani tunautambua uzalendo wake.
YAANI MNAKAA KUONGEA PUMBA TUPU HAMNA KAZI ZA KUFANYA? TOBO ANAUWEZO GANI WA KUSHIKA URAIS ? MNAFIKIRI KITI CHA URAIS NI CHA KUJARIBISHA? MSITULETEE MAMBO YA AJAMBUHAPA NCHINI WAPO WATU WENYE UWEZO KUONGOZA NCHI NA WAMO NDANI YA CCM TU
 
Kuanzia swali la kwanza mpaka la 6 yalihusu moja kwa moja shambulio la risasi alilofanyiwa Dodoma na maswali 18 yalijikita kwenye kukubali au kukataa kuhusu umadhubuti wa serikali ya Dr Magufuli kasoro la 22 ambalo lilikua mahususi kuhusu mapenzi ya jinsia moja hasa ushoga.

Kwa hiyo, umeeleza kulikuwa kuna maswali ya aina tatu:

1 ) kupigwa risasi
2 ) umadhubuti wa serikali ya Magufuli, Lissu abishe au akubali
3) issue za ushoga na mimba za wanafunzi

Je, hili swali la tuna dili vipi na udikteta unaliweka kundi gani?

Au ukandamizaji, repression, ni umadhubuti wa Magufuli?

"It faces you with a choice though, because the government even with its latest legislation, which wants to repeal the Political Parties Act, to make it much more difficult for opposition political parties to conduct what's been called activism on the street, you then face a choice, are you going to confront this government and its repressive legislation openly and that could of course lead to violence or are you going to find ways which are peaceable rather than potentially confrontational?"
 
Nilishawahi kuandika humu kuwa Tundu Lissu siyo presidential material.

Sasa hii majuzi baada ya mahojiano yake kwenye kipindi cha BBC HARDtalk, ambapo alibanwa mbavu kuhusu tuhuma zake mbalimbali dhidi ya Rais Magufuli, CCM, na watu wengine, tuhuma ambazo hajatoa ushahidi wowote, kumeibuka mjadala kana kwamba hiyo ndo ilikuwa mara ya kwanza kwa Lissu kuulizwa ushahidi juu ya hizo tuhuma zake uko wapi.

Pengine labda jukwaa lililotumika kumhoji huo ushahidi ni kubwa zaidi, lakini kiukweli tupo baadhi yetu humu JF ambao tumekuwa tukisema kuwa Lissu mpaka sasa hajaonyesha ushahidi wowote ule juu ya hizo tuhuma zake nyingi anazoporomoshaga.

Mpaka wakati mwingine huwa nafikiria labda akipandagwa na mzuka huwa anasahau kabisa mipaka na misingi ya taaluma yake na kuchanganya madesa ya uanaharakati na uanasiasa.

Nashukuru imechukua kipindi cha kimataifa kumhoji kile ambacho sie wengine tumekuwa tukikihoji humu kwa muda mrefu sasa.

Mtu unaibuka unadai flani na flani wamenifanya hivi au flani kanunuliwa na flani, halafu ukiambiwa onyesha ushahidi wa unachokidai, unaishia kucheza mduara.

Ahsante sana mwendesha kipindi cha HARDtalk.
 
Najua huko aliko nyuma ya nondo anawaza kummaliza Lissu kisiasa na anajuta kwanini Lissu amepata nafasi ya kuongea na Media kubwa duniani,anaiona shida inayokuja mbeleni kwa mustakabali wa Chama,Lissu anajijengea wigo na umaarufu mbele ya wanachama ili aipoke nafasi ya mwenyekiti na ugombea uraisi ameshawashtukia wana kindai kuwa wana dalili zote za kutaka kukivuruga chama kama alivyomsikia mwana kindai mwingine akisema mchakato wa mgombea uraisi ndani ya chadema lazima uwe wazi,
Hivi sasa ni Chadema inamtegemea Lissu kuliko hapo mwanzo Lissu alipokuwa anaitegemea Chadema
Lissu sasa ni maarufu kuliko hata Chairman na hata mtu yeyote ndani ya Chadema
Lissu kwa umaarufu alioupata anaweza kuweka shinikizo lolote likakubalika kwa kuwa sasa ni wakati wake,
Namuona mzee wa kushughulikia watu akimshughulikia Lissu kwa mara ya pili,namuona Chairman akimuwekea kauzibe Lissu ya kugombea uraisi nakiona chama kikisambaratika kwakuwa wana kindai watajiengua baada ya kunyimwa fursa
Hongera Lissu Hard talk imekuweka juu kuliko Lowassa,
Kuliko Mbowe
Kuliko Chadema
Tulio upande wa pili tunaomba upate hiyo nafasi ili muendelee kujimaliza!
 
Ndugu zangu,

Maandalizi yoyote yanakuwa na mantiki pale unapopata matokeo mazuri. Hapa ndipo utakapogundua maana ya kocha wa yanga mkongomani Mwinyi Zahera alipoona mambo yatakuwa magumu kwenye kombe la mapinduzi akaja na propaganda ya kuwa ''atapeleka kikosi B'' kwa sisi watu wazima tuliupata ujumbe.

Turudi kwenye hoja, huenda maandalizi ya kuongea na media za kimataifa yalikuwa mazito na yamegharimu mamilioni ya dola. Inapotokea matokeo yanakuwa madogo sana kulinganisha na uwekezaji tusipeleke ''timu A''.

Ndugu zangu, kule CNN akienda Lissu atakutana na Richard Austin Quest , huku mambo yatakuwa mabaya zaidi kuliko yalivyokuwa kwa Stephen Sackur. Kwani Richard atapata wasaa wakuangalia mahojiano baina ya Steve na Tundu na hapo kazi itakuwa imekwisha, hata akiuliza maswali yale yale hali itakuwa mbaya zaidi.

Hapa ndipo mantiki ya kuitimia timu B, ambapo hapa ndipo Mange Kimambi 'anafit'. kwanini Mange? angalau ana cha kuzungumzia kuhusu maandamano yake yaliyoshindwa ya 26 Aprili, 2018.

Pili, kama kweli Lissu bado anaumwa si busara, Chadema watumie sababu hii kukwepa kiti moto pale CNN kwani kushindwa kwake ni kuanguka kwa chama na aibu zaidi kwa kukosa misingi ya kujenga hoja kimataifa.

Nimalizie tu kwa kusema, 'mzima nguo ikidondoka chutama', sisi wenyewe ni mashaidi wafuasi wengi wa Bavicha hawasherehekei clips za BBC sasa mkiongeza mziki wa CNN ya Richard Quest hali itakuwa mbaya zaidi.

Mahojiano ya CNN aende Mange na sio Lissu kuepuka aibu zaidi.
 
Ile interview imethibitisha pasi na shaka kuwa Lissu hajui na hana hakika na waliompiga risasi bali ana hisi tuuu....na watu tulitegemea sasa pale ndio amwage ushahidi lakini alibaki na maneno matupu ambayo hayana tofauti na ya kina Salary Slip...Yani Lissu anaulizwa ushahidi ana leta maneno ya kwenye nyuzi za kina Salary Slip....
Hahahahaha


Halafu alipata bahati nzuri alipewa maswali ya kumuelekeza kabisa.....lakini hakuna chochote kipya ambacho ameongea Lissu ambacho kuna mtu hakuwai kukisikia kutoka kwake au kwa wengine....lakini unaweza shangaa wengine wana shangilia as if hayo maneno hawakuwai kuyaona kwenye nyuzi za Salary slip
 
nimeshasema kwenye nyuzi zangu, 2020 chadema itapangaranyika na kuvurugika si kwa sababu wametaka bali wanachama watagawana fito za nyumba ambayo wameijenga na hapo ndipo tutapata CCM ushindi mkubwa sana. Mpaka sasa chadema hawajui ni lowassa, lissu au nyarandu kuelekea 2020
 
Kuna muda tutumie akili tu kuelewa
wale waliomuuliza lissu kila kitu wanafanyia uchunguzi hata mende wakiongezeka huku mtu kapigwa risasi 200 wenye mamlaka ya kufanya uchunguzi hawataki
kisha unataka mtu aliyekuwa hospital ndio athibitishe watesi wake
wabongo mbona hatuna akili
wabongo mbona tunatiana aibu
Naona aibu kusoma wanaomponda lissu badala ya kuiponda serikali kwanini uchunguzi haufanyiki
Tunakwama wapi ?
Lissu ndio tunamchukia lakini sio kwa hili
 
Najua huko aliko nyuma ya nondo anawaza kummaliza Lissu kisiasa na anajuta kwanini Lissu amepata nafasi ya kuongea na Media kubwa duniani,anaiona shida inayokuja mbeleni kwa mustakabali wa Chama,Lissu anajijengea wigo na umaarufu mbele ya wanachama ili aipoke nafasi ya mwenyekiti na ugombea uraisi ameshawashtukia wana kindai kuwa wana dalili zote za kutaka kukivuruga chama kama alivyomsikia mwana kindai mwingine akisema mchakato wa mgombea uraisi ndani ya chadema lazima uwe wazi,
Hivi sasa ni Chadema inamtegemea Lissu kuliko hapo mwanzo Lissu alipokuwa anaitegemea Chadema
Lissu sasa ni maarufu kuliko hata Chairman na hata mtu yeyote ndani ya Chadema
Lissu kwa umaarufu alioupata anaweza kuweka shinikizo lolote likakubalika kwa kuwa sasa ni wakati wake,
Namuona mzee wa kushughulikia watu akimshughulikia Lissu kwa mara ya pili,namuona Chairman akimuwekea kauzibe Lissu ya kugombea uraisi nakiona chama kikisambaratika kwakuwa wana kindai watajiengua baada ya kunyimwa fursa
Hongera Lissu Hard talk imekuweka juu kuliko Lowassa,
Kuliko Mbowe
Kuliko Chadema
Tulio upande wa pili tunaomba upate hiyo nafasi ili muendelee kujimaliza!
Kuliko ccm, kuliko wewe na Baba ako! Lissu for president!
 
Ile interview imethibitisha pasi na shaka kuwa Lissu hajui na hana hakika na waliompiga risasi bali ana hisi tuuu....na watu tulitegemea sasa pale ndio amwage ushahidi lakini alibaki na maneno matupu ambayo hayana tofauti na ya kina Salary Slip...Yani Lissu anaulizwa ushahidi ana leta maneno ya kwenye nyuzi za kina Salary Slip....
Hahahahaha


Halafu alipata bahati nzuri alipewa maswali ya kumuelekeza kabisa.....lakini hakuna chochote kipya ambacho ameongea Lissu ambacho kuna mtu hakuwai kukisikia kutoka kwake au kwa wengine....lakini unaweza shangaa wengine wana shangilia as if hayo maneno hawakuwai kuyaona kwenye nyuzi za Salary slip

Mimi nimefurahi tu kuona kuwa kumbe wapo na wengine wanaoona kuwa Lissu anaropoka tu bila ushahidi wowote ule!
 
Mwacheni akajimalize basi, mbona Ndugai anahangaika ? Angenyamaza aendelee kuumbuka kama usemavyo wewe na wengine!
Halafu hilo lako la kumchokonoa Mange kwa kebehi unadhani hasomi hapa?
Unataka kumponza Juliana Shonza bure! au unadhani hajui?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muda tutumie akili tu kuelewa
wale waliomuuliza lissu kila kitu wanafanyia uchunguzi hata mende wakiongezeka huku mtu kapigwa risasi 200 wenye mamlaka ya kufanya uchunguzi hawataki
kisha unataka mtu aliyekuwa hospital ndio athibitishe watesi wake
wabongo mbona hatuna akili
wabongo mbona tunatiana aibu
Naona aibu kusoma wanaomponda lissu badala ya kuiponda serikali kwanini uchunguzi haufanyiki
Tunakwama wapi ?
Lissu ndio tunamchukia lakini sio kwa hili

Lissu mwenyewe ndo anasema Magufuli anahusika moja kwa moja na hilo shambulio.

Sasa kilicho kibaya katika kumwuliza ushahidi ni kipi?
 
Kufuatia mahojiano ya Mhe. Tundu Lissu na Mtangazaji wa BBC kipindi cha Hard Talk nina tamani kuona mdahalo wa Rais Magufuli na Tundu Lissu siku moja kabla Rais Magufuli hajaondoka madarakani.Mhe.Lissu kama kawaida yake ameonyesha umahiri wa ajabu katika kujieleza,kujibu maswali na kujenga/kupanguahoja za mwendesha kipindi. Hakika ilikuwa ni burdani tosha.

Kwa vile hoja inajibu kwa hoja,ni wakti wa serikali kupeleke mtu kwenye kipindi cha BBC Hard Talk akajibu au kupangua hoja za Mhe. Lissu. Hili litakuwa jambo la busara badala ya sasa kumtishia Mhe. Lissu kurtaka kumfukuza Ubunge kwa kisingizio atI anazurura na kuichafua nchi huko ughaibuni...!!!!

Lakini pia kuna haja siku moja kuandaliwa kipindi cha Mdahalo Maalumu kati ya Mhe. Rais John Magufuli na Mhe.Tundu Lissu ambao utaendeshwa kwa Lugha ya Kiingereza ili kupima uelewa, ufahamu, ujuzi, busara na hekima wa kujibu hoja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kiulinzi kwa nchi yetu Tanzania. Mdahalo huu unaweza kuandaliwa na chombo chochote cha Habari kutoka Tanzania au nje ya Tanzania kama BBC, CNN, VOA, DW n.k.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom