Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

nimeshasema kwenye nyuzi zangu, 2020 chadema itapangaranyika na kuvurugika si kwa sababu wametaka bali wanachama watagawana fito za nyumba ambayo wameijenga na hapo ndipo tutapata CCM ushindi mkubwa sana. Mpaka sasa chadema hawajui ni lowassa, lissu au nyarandu kuelekea 2020
Adui yako muombee njaa!
 
Mmepigwa kipigo cha mbwa koko then mnakimbilia kuleta propaganda kama za slowslow, au hukuangalia kipindi then umesimuliwa na slow slow, jipangeni kwani Watanzania wote washawashitukia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi nimefurahi tu kuona kuwa kumbe wapo na wengine wanaoona kuwa Lissu anaropoka tu bila ushahidi wowote ule!
Ukimuangalia mtangazaji unaoana kabisa hakutarajia kuwa Lissu hana ushahidi usio tia shaka au kaja mikono mitupu hahaha... Hivi kwa maneno matupu yenye shaka namna ile pamoja nakupewa maswali ya kuelekeza lakini bado hakuna alicho jibu.......... Lile swali la mazuri ya Magufuli ndio limemdhalilisha kabisa Lissu maana mtangazaji amejua kabisa huyu ni pinga pinga tuu hana ushahidi wowote.... hahaha
 
Ngoja nimzikilize kwanza lakini nafahamu kuna kitu kinaitwa Circumstantial evidence. Ngoja nimsikilize nifahamu kaongea nini katika hili! Nilikuwa sijamsikiliza... ni thread ya Pascal Mayalla ndiyo imenifanya nitafute mazungumzo haya!!!

Lakini itoshe tu kusema kwamba, si kila ushahidi ni LAZIMA uwe DIRECT EVIDENCE!

Kama kuna mwingine na yeye alikuwa hajasikiliza, video husika ni hii hapa:-



UPDATES:​

Tundu Lissu anasema anaishi ndani ya government compund kwenye nyumba za serikali ambazo zipo highly guarded 24/7. Na siku anamiminiwa risasi, alimininiwa hapo mchana wa jua kali ng'ombe anakula majani! Watu wenye silaha walimfuata kuanzia bungeni hadi hapa ambapo pia wanaishi viongozi wa juu wa serikali!

Lakini ch ajabu, siku anashambuliwa, hapakuwa na ulinzi wowote!!!

Hoja yangu ambayo yashasemwa sana huko nyuma:-

Nimesikiliza A-B... to be honest, nashangazwa na wale wanaohoji suala la Lissu kuongea bila ushahidi!! Kwa mfano, Tundu amesema wazi eneo alikopigwa risasi ni 24/7 heavily guarded compound by the government!

Sasa how come eneo kama hilo, high profile figure anaweza kumiminiwa risasi 16 bullets on target na zingine 22 off-target na bado vyombo vya usalama wasiwe na clue yoyote for almost 15 months now?!

Wakati mnamtaka Tundu Lissu atoe ushahidi, je vyombpo vya serikali vimefikia wapi kwenye uchunguzi wao?!

Lissu amesema jambo ambalo kila mmoja analifahamu kuhusu kupotea kwa watu huko MKIRU lakini maiti zikiwa zinaokotwa baharini na mtoni!!

Sasa kama serikali ahihusiki, vyombo vya usalama vimefanya uchunguzi wowote kufahamu victims ni nani na possible suspects ni nani?!

Ikiwa watu kama akina Ben Saanane wamepotea kwa takribani miaka 2 sasa... je, uchunguzi wa vyombo vya usalama umefikia wapi na possible suspects ni akina nani?!

Kwa ufahamu wangu, unless referenced otherwise, hadi sasa hakuna suala hata moja kati ya hayo ambayo vyombo vya usalama vinalifanyia kazi seriously na hakuna hata moja ambalo kuna suspects!

Je, hayo yametokea kwa sababu vyombo vya usalama vipo COMPLETELY WEAK au ni kwa sababu vyombo vya usalama haviwezi kujichunguza vyenyewe?! Kama vyombo vya usalama vipo completely weak, ni kwa vipi basi President Magufuli ambae tunaambiwa havumilii udhaifu serikalini lakini bado ameamua kuuvumilia udhaifu mkubwa kama huo bila kufanya lolote?!

Ni kwamba President Magufuli ameamua kuvumilia udhaifu wote huo wa vyombo vyake vya usalama au hawezi kuchukua hatua dhidi ya "VITENDO VYA KIDHALIMU" vilivyofanywa na vyombo vyake vya usalama usalama kwa sababu vina baraka ya serikali yake kwa namna moja au nyingine?!
 
Apeleke ushahidi kwani pale studio ni Mahakamani..........
Muulize muendesha kipindi aliomuuliza kama ana ushahidi yeye aka refer uzi wa salary slip na comment za jf....aliulizwa ushahidi usiotia shaka yeye analeta hisia... hivi kwa majibu yale usipo ambiwa kama huyu ni Mwanasheria unaweza jua ni mwana sheria? Hivi amejibu nini kipya ambacho kina mtofautisha yeye na Salary slip?
 
Nianze kwa kuandika, Mwanaharakati ni mtu yeyote anayejitolea kupigania na kutetea jambo fulani katika jamii liwe zuri au baya kama vile adhabu ya kifo iondolewe, haki za watoto, kutetea ushoga, mazingira, utawala bora, nk. Mara nyingi huwa hana msaada/nguvu kubwa ya kisheria zaidi ya ile ya kikatiba ya uhuru wa kuongea.

Lengo kuu la Mwanaharakati ni kuikosoa serikali na kulisemea kundi ambalo anadhani halitendewi haki na serikali bila hata ya kujali maslahi mapana ya jamii/wananchi au serikali. Anachotaka wananchi wote wawe sawa.

Mwanasiasa ni mtu yeyote anayejishughulisha na siasa kama kazi kupitia msingi wa itikadi na sera. Kwa sababu siasa ni kazi basi mwanasiasa ni mtu anayeangalia fursa za kisiasa kwa lengo la kutawala au kupata madaraka.

Wanasiasa wengi ni waongo wakati wanaharakati wengi ni wakweli.

Maisha ya mwanasiasa hutegemea maoni ya wengi wakati maisha ya mwanaharakati hutegemea imani yake hata kama wengi wanapinga.

Mwanasiasa hawezi kuwa Mwanaharakati lakini Mwanaharakati anaweza baadaye kuwa Mwanasiasa.

Jibu alilotoa Tundu Lissu baada ya kuulizwa na Mtangazaji wa kipindi cha HARDtalk, Stephen John Sackur kuhusu ushoga haliwezi kutolewa na mtu anayetaka kushinda nafasi ya Ubunge achilia mbali Urais wa nchi katika nchi yenye kushikilia ''ukale'' kama Tanzania.

Ushoga kwa Tanzania ni tendo ambalo bado ni haramu (taboo) na mwiko kwa Watanzania wengi.

Kwa sababu ushoga ni taboo nchini huwezi kumsikia mwanasiasa mbele ya vyombo vya habari anasema kuwa sheria za Tanzania kuhusu ushoga zinavunja haki za faragha ambazo ziko kwenye katiba na kwa sababu hiyo lazima zifutwe.

Ni Mwanaharakati ndiye anaweza kupinga sheria ya ushoga nchini mbele ya vyombo vya habari kwa sababu anaamini inawanyima haki baadhi ya wananchi lakini kikubwa zaidi anafanya hivyo kwa sababu nia yake sio kupewa madaraka bali usawa kwa wananchi wote.

Lissu kwa sababu bado ni Mwanaharakati ndio maana ameweza kusema mbele ya chombo cha habari kuwa anafikiri sheria kuhusu Ushoga nchini inavunja haki za faragha.

BBC News wameandika, ‘’ Mr Lissu also said he believed Tanzania's laws against homosexuality violated people's right to privacy and so were unconstitutional.
"We should never allow the government to start peeping into people's bedrooms,
" he said’’.


Ukitaka kusoma habari yoye GONGA LINK>>>Tundu Lissu ready to run for Tanzania Presidency

Jibu la Tundu Lissu ninanikumbusha Mwanajamii forums mmoja aliwahi kusema;

Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

Ukitaka kusoma habari yote GONGA LINK>>>Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Alichokisema Tundu Lissu kuhusu Mwl. Nyerere hata kama ni ukweli lakini kwa Tanzania bado ni taboo. Huwezi kumsikia Mwanasiasa akisema mbele ya vyombo vya habari alichokisema Tundu Lissu lakini yeye alikisema kwa sababu ni Mwanaharakati.

Nimalizie kwa kuandika, Mahojiano ya Tundu Lissu na Mtangazaji wa kipindi cha HARDtalk, Stephen John Sackur yamedhihilisha kuwa bado ni Mwanaharakati.
 
Lissu mwenyewe ndo anasema Magufuli anahusika moja kwa moja na hilo shambulio.

Sasa kilicho kibaya katika kumwuliza ushahidi ni kipi?
hakuna kibaya mbona
kibaya ni wale wenye mamlaka ya kufanya uchunguzi wanapokaa kimya
hivi uchunguzi ungefanyika kisha washtakiwa na wahusika wakakamatwa angeongea vile ?
 
Nilishawahi kuandika humu kuwa Tundu Lissu siyo presidential material. Nikasema yeye ni rabble rouser. Ni gadfly tu.

Sasa hii majuzi baada ya mahojiano yake kwenye kipindi cha BBC HARDtalk, ambapo alibanwa mbavu kuhusu tuhuma zake mbalimbali dhidi ya Rais Magufuli, CCM, na watu wengine, tuhuma ambazo hajatoa ushahidi wowote, kumeibuka mjadala kana kwamba hiyo ndo ilikuwa mara ya kwanza kwa Lissu kuulizwa ushahidi juu ya hizo tuhuma zake uko wapi.

Pengine labda jukwaa lililotumika kumhoji huo ushahidi ni kubwa zaidi, lakini kiukweli tupo baadhi yetu humu JF ambao tumekuwa tukisema kuwa Lissu mpaka sasa hajaonyesha ushahidi wowote ule juu ya hizo tuhuma zake nyingi anazoporomoshaga.

Mpaka wakati mwingine huwa nafikiria labda akipandagwa na mzuka huwa anasahau kabisa mipaka na misingi ya taaluma yake na kuchanganya madesa ya uanaharakati na uanasiasa.

Nashukuru imechukua kipindi cha kimataifa kumhoji kile ambacho sie wengine tumekuwa tukikihoji humu kwa muda mrefu sasa.

Mtu unaibuka unadai flani na flani wamenifanya hivi au flani kanunuliwa na flani, halafu ukiambiwa onyesha ushahidi wa unachokidai, unaishia kucheza mduara.

Ahsante sana mwendesha kipindi cha HARDtalk.
Heko..comment maridadi. Imefika muda huyu bwege adhibitiwe kwa hoja ili aondoe mzuka kichwani kwake.
 
Kuna muda tutumie akili tu kuelewa
wale waliomuuliza lissu kila kitu wanafanyia uchunguzi hata mende wakiongezeka huku mtu kapigwa risasi 200 wenye mamlaka ya kufanya uchunguzi hawataki
kisha unataka mtu aliyekuwa hospital ndio athibitishe watesi wake
wabongo mbona hatuna akili
wabongo mbona tunatiana aibu
Naona aibu kusoma wanaomponda lissu badala ya kuiponda serikali kwanini uchunguzi haufanyiki
Tunakwama wapi ?
Lissu ndio tunamchukia lakini sio kwa hili
Huo uchunguzi unatakiwa uanzie wapi sasa kam sio kwake yeye mwenyew na waliokuwa jiran nae wakat tukio linatokea.
Bavichaa Acheni kutapatapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom