Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Uzuri wa nafsi ya binadamu huwa haidanganyi, unajibaraguza mdomoni lakini ukweli unaujua kwamba ni rushwa ilitumika kuwanunua wabunge. Hata mimi sina ushahidi wa moja kwa moja but circumstantial evidence are sufficient to prove the matter though not in the court of law
Na hii pia inathibisha uhovyo wa chama cha chadema, kisha unaenda kujikomba kwa mzungu kwamba wabunge wetu wamenunuliwa!

Huoni kama unaaibisha chama chako kwamba kina watu wa hovyo wanaonunulika, wanapenda hela kwamba wakiachiwa chochote wanauza hata nchi?

Kiufupi mijitu ya hivi hata mabeberu wenyewe hawawezi kuwaamini, kwasbabu anajua ipo siku watatugeuka akitokea mwingine mwenye dau kubwa zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanalalamika kwanini ameongea hayo hawajiulizi angekufa angeongelea wapi nyambafu
 
Tundu amezidiwa vibaya saana kwenye interview hii. Akili za wazungu usipime[emoji2][emoji2] Wanatujua kwelikweli. Wanajua namna JPM anavyoibadilisha Tanzania na ambavyo kundi la wabunge wa upinzani wanavyokunwa naye hadi wanahamia kwake CCM. Na jinsi atakavyopita kwa kishindo 2020. Tundu anadai eti wote wananunuliwa. Mtangazaji anamwambia kumbuka wewe ni Mwanasheria Mwandamizi, kwanini unatoa allegations zisizo na evidence[emoji2][emoji2] Tundu anabaki bila hoja[emoji2]

Hahahahahh mbombo jilipo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huijui hard talk vizuri.Wewe. Siku zote yeye anataka wewe ufunguke zaidi juu kile unachokipinga,huku yeye akiigiza kuwa sehemu ya kile unachokipinga.Hayo ndio mahojiano bora ambayo wenzetu huyafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushindi wa CCM upo katika kuhakikisha kile walichokiahidi kwenye ilani yao kinatekelezeka kwa asilimia 90 na sio chini ya hapo.

Haya mambo ya kwenda BBC na kuhojiwa ni siasa za muda mfupi, ambazo kadri muda unavyozidi kupita ndivyo zinavyogeuka kuwa sehemu ya jana.

Serikali inayohodhi magogoni ikitaka kuendelea kukubalika ni kuongeza pato la taifa kwa kuanzia na pato la mtu mmoja mmoja.

Kuna suala la zile rada nne, zikishafungwa zitaongeza kwa kiasi kikubwa sana pato la taifa. Pia masuala ya kodi kulalamikiwa na wafanyabiashara, pia ni suala muhimu kutazamwa.

Cha muhimu ni serikali kuendelea kutekeleza kulichomo ndani ya ilani, haya mambo ya mahojiano ni umaarufu wa muda mfupi tu.
Asanteeeeeeee [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] kumbe tuna hazina ya watu wenye mbongo zao zimetulia huku, halafu watu kutwa kubwabwaja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hana ajenda YOYOTE na hata hao wanaomtuma hawana ajenda! Kinachofanyika ni kuwa hawa wanaomtuma wanataka kumpa pesa za kutumia tumia aidha akiwa huko au akisha rudi huku, LAKINI kwa hawa wazungu, HAKUNA FREE LUNCH! Chochote wakupacho lazima UKIFANYIE KAZI, hakuna cha bure! Pia watahitajika kukitolea maelezo with evidence ikiwa ni pamoja na risiti na nani alilipwa, hivyo lazima Lissu atembee huko wanakotaka na aseme kile wanachotaka, LICHA HALI YAKE KUWA BADO MABAYA! Wazungu hawana huruma bana, wao wanachotaka ni wewe uwafanyie kazi yaotu! Hayo mengine ya vyuma miguuni au maumivu utajua wewe uliyekubali pesa zao.
 
Na hii pia inathibisha uhovyo wa chama cha chadema, kisha unaenda kujikomba kwa mzungu kwamba wabunge wetu wamenunuliwa!

Huoni kama unaaibisha chama chako kwamba kina watu wa hovyo wanaonunulika, wanapenda hela kwamba wakiachiwa chochote wanauza hata nchi?

Kiufupi mijitu ya hivi hata mabeberu wenyewe hawawezi kuwaamini, kwasbabu anajua ipo siku watatugeuka akitokea mwingine mwenye dau kubwa zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sioni hoja hapa, hata Magufuli aliwahi kusema majizi yako kwenye vyama vyote, nakubaliana naye kwa hilo, vilevile dhambi ya rushwa ni ya pande zote mbili, pamoja na kwamba mi sina chama corrupt people could be on both sides.
 
Muasisi wa Taifa la Tanzania , Mwl. Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa tumuogope kama ukoma mtu anayetaka kwenda ikulu kwa gharama yeyote. Mtazamo huu wa Mwalimu juu ya watu wa namna hiyo unafikirisha sana na kufanya tutafakari sana na kujiuliza maswali yafuatayo: kama mtu ana ndoto ya kuwa rais, si ataipigania ndoto yake kwa namna yeyote ili aende ikulu kuwa rais? Je, mwalimu aliona nini mpaka kufikia kutoa kauli kama hiyo?

Nimetafakari na kuona kuwa maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa sahihi ya kwamba tumuogope mtu wa namna hiyo kwa sababu kuna wengine wanapelekeshwa na tamaa ya kuwa Rais kuliko matarajio yao na hivyo kutumia kila njia kutimiza tamaa zao na si matarajio yao. Moja ya watu wenye Tamaa hiyo ni Tundu Lissu, tamaa hiyo inampeleka puta haswa hata kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake.

Kiukweli kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha BBC HARDTALK kimeonesha ni kwa namna gani Tundu Lissu akipelekeshwa na tamaa ya urais mpaka kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake. Ni mara nyingi katika kipindi hicho alikuwa akiulizwa kama ana ushahidi wa yale anayoyasema dhidi ya serikali yake kwa shutuma kama hizo na yeye kusema inafahamika hivyo kama jibu.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa mtu kama Tundu Lissu ambaye ni msomi wa sheria kuishutumu serikali imehusika na hiki na kile kwa shutuma kubwa za kuhatarisha amani na usalama bila kuwa na ushahidi. Ni vile tu mwandishi hakusema ila angepata nafasi angemwelezea kuwa kwa kosa kama hilo la kuishutumu serikali bila ushahidi kwa hapa uingereza ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa.

Mwandishi wa kipindi kile kasaidia kwa namna kubwa sana kuamsha hisia za watanzania kwa kufichua ubabaishaji wa Tundu Lissu kwa dunia na uhatari wa anayoyafanya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi. Shutuma anazozipeleka kwa rais wetu ni kubwa na zinahitaji ushahidi wa kutosha kuzitoa kwa sababu zinasababisha wawekezaji na watalii kupungua kutokana na hali mbaya ya kiusalama na uvunjifu wa amani unaoratibiwa na serikali kama Tundu Lissu anavyotaka iwe .

Serikali kama mlinzi namba moja wa usalama na amani ya nchi na raia wake hauna sababu za kueleza sababu za kiusalama kisiasa hasa zile ambazo hawana kithibitisho kuwa zimesababishwa na nini. Katika suala la Tundu Lissu kuna nadharia nyingi juu ya kushambuliwa kwake hivyo Lissu kuishutumu serikali kufanya hivyo moja kwa moja ni kosa na hivyo wenye akili inabidi tujiulize ni kwa nini serikali tu?

Jibu ni kwamba, Tundu Lissu anapelekwa puta na mawazo ya kuwa Rais hivyo ameanza kujipanga taratibu kwa kujenga chuki kwa wananchi kuwa CCM ndio wahusika hivyo wanapata nguvu ya kufanya fujo pale CCM inapowashinda kwenye uchaguzi mkuu wakisaidiwa na wanaowatuma kufanya hivyo.

Tundu Lissu , Dunia nzima sasa inajua lengo lako si zuri kwa nchi yako na waandaaji wa BBC hardtalk wameona aibu kumuhoji mtu ambaye hana data wala ushahidi wa tuhuma anazozitoa kwa serikali ambazo kwao wenyewe wanajua kwa tuhuma kama zile kwa nchi kama uingereza ni makosa makubwa. Umeamua kuichafua nchi yako kwa kupelekwa puta na urais ambao huna hakika utapata ama laaa .

Ushauri

i. Tundu Lissu asinyamaziwe, kwa nguvu ile ile anayoitumia kuichafua nchi kwa shutuma za kuokoteza zisizo na ushahidi ni vyema serikali ikatumia nguvu hiyo hiyo kumjibu . Tundu Lissu ajibiwe kisiasa na kitaalamu.

ii. Tundu Lissu atakapo rudi Tanzania kuandaliwe mdahalo kati ya Tundu LIssu na mwanaCCM mmoja ,watumie jukwaa hilo kumjibu kwa sababu Tundu Lissu hajaichafua serikali katuchafua pia CCM kwa kuwa ndio tunaongoza serikali.

Hitimisho

Tundu Lissu anajiona anajua sana kwa sababu anaamini hakuna mwanaCCM mwenye uwezo wa kumjibu ila akijibiwa atanyamaza kimya. Kila mtanzania mwenye akili timamu anamjua Tundu Lissu anafanya anayoyafanya kwa sababu ya tamaa ya Urais na anatengeneza mazingira mapema ili kushindana na nguvu ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

na Karlo Mwilapwa

Unasikia na kuelewa lugha ya Kiingereza kweli wewe?

Nakuhakikishia kuwa , wewe ni "mjinga" (siyo tusi bali nina maana ya ujinga wa kutoelewa), huelewi, hukuelewa mtiririko wa mazungumzo yote from A - Z

Wenye ufahamu na akili za kuelewa na kuchambua mambo watakucheka na kukunanga tu. Mimi nimejitolea nikuambie ukweli, sitakucheka wala sikunangi....

Na ni bora ungeomba tafsiri ya kipindi chote kwa lugha ya Kiswahili, labda ungeweza kuelewa na pengine ungekuja na mtazamo tofauti wa mtu mwenye uelewa...

Umeonekana kituko zaidi kwa kum - term Tundu Lissu kama "mtu mwenye tamaa ya Urais"...

Nimejaribu kutafakari ili nione msingi wa hoja hii ni mini, nimeshindwa kukuelewa...

Kwako wewe una maana kila atakayeutaka Urais (ukimwacha John Pombe Mega Fool na yeyote huko CCM) wa JMT kwa njia halali, ana tamaa?

Kwanini hawa wawe na tamaa ya Urais na John Pombe Mega Fool na wenzako wote huko CCM nanyi tusiwaone kuwa mna tamaa tu vilevile? Au nyie mna haki miliki na Urais?
 
Mimi nimependa sana yale mahojiano , yalimvua mtu nishai, Tundu Lissu alibaki mtupu kabisa , alikuwa anamung'unya maneno mpaka basi na mara nyingi ameambiwa wewe ni mwanasheria si vizuri kuongea bila ushahidi.
In my opinion he did very well. Tena zaidi ya Mkapa, 2001 ..............!!

Hakumpa nafasi jamaa kucontrol discussion na kuwekwa kwenye kona .... Haya mengine ni propaganda tu kujaribu kumdiscredit!!
 
Utafikiri kuna watu wamepangwa kujaza JF na mjadala juu ya interview ya TAML Hard Talk. Naona kila mtu anamshambulia TAML bila kujali jumuia ya kimataifa inajua mangapi hata kabla ya interview. Kweli kawashika pabaya!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwandishi yule alikuwa na maswali yenye data, mfano Lisu alitaka kusema Magufuli kafukuza wawekezaji, mwandishi akamdaka akamwambia Magufuli alikuwa anasimamia kile alichokiahidi kwamba atahakikisha uwekezaji mfano wa sekta ya madini unanufaisha nchi, akamuuliza Lisu kwamba kwanini wewe unaonekana kupinga hili? Lisu akajibu mm ndio nilianza toka zamani tangu Magu ni waziri wa ujenzi, mwandishi akaona huyu hajui anataka nini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umalaya wako una bei yake ila hauna gharama kuuendesha. Kifupi hujaielewa interview, si wewe peke yako bali na genge lenu lote top to bottom.
Lugha ya malkia ni shida lumumba huenda na jiwe hakuelewa kitu mpaka atafsiriwe
 
Unaelewa maana ya HARD TALK???? Ni hivi They will never, once again Never side with you

All hawataki kukuweka kwenye comfort zone

Ukiona wamekuita kwenye HARD TALK they know you can do it

Lissu did it! Salute you comrade

Huyu mnayemtetea hana kifua cha kukabiliana na haya ndio maana inaitwa HARD TALK -
Language/English (fluent) Confidence Intelligence ndio vigezo vya kuitwa kwenye kiti kile cha Enzi


They will always side na kile unachopingana nacho for you to prove 'your believes/standings'

Msiwe mnasikiliza kama kasuku unless leo kwako ni mara ya kwanza kushuhudia HARD TALK
Wanachotaka ni uanike mapungufu yote ya mtawala na chama chake as much as possible

Nikusaidie kidogo sikiliza HARD TALK za viongozi wa nchi ya Marekani akina Obama Bush Trump ndio uje uandike huu upupu wako.
Uanike mapungufu na ushahidi sio uanike tu kama KASUKU.
 
Kwenda kwa waandishi wa habari kuna njia zaidi ya moja. Unaweza kwenda kwa kupenda au kuomba, ama nafasi yako inaweza kukulazimisha kwenda. Hapa haijalishi unataka ama hutaki. Aina hii ya maswali ndio inayofanya Magufuli asitake kutoka nje, na nina kuhakikishia kwa mazungumzo haya ya Lissu, Magufuli hatakaa akanyage Ulaya.
Kagame unamjua? Museven je? Wale na Magufuli nani hapaswi kwenda ulaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom