Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Kilichotokea katika mahojiano yale ni; mwandishi wa BBC kuhoji doubts zote zilizopo na zinazo ongelewa na Chama tawala na Tundu Lissu akazijibu. Ilikuwa kama jukwaa la mpambano kati ya washindani wawili, mmoja akiigiza nafasi ya mtawala na mwingine akiwa upande wa upinzani. Nafikiri tunahitaji majadiliano kama haya ndani ya taifa letu. Tumemiss mpambano wa hoja kama ule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikia Lissu, BBC Steven Sanker's command of knowledge of goings on in Tanzania has belittled Tundu Lissu just like a piriton tablet. So pity to Lissu. So sad that Lissu has dillydallied to answer a question regarding his party's position on homo sexuality.
 
Muasisi wa Taifa la Tanzania , Mwl. Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa tumuogope kama ukoma mtu anayetaka kwenda ikulu kwa gharama yeyote. Mtazamo huu wa Mwalimu juu ya watu wa namna hiyo unafikirisha sana na kufanya tutafakari sana na kujiuliza maswali yafuatayo: kama mtu ana ndoto ya kuwa rais, si ataipigania ndoto yake kwa namna yeyote ili aende ikulu kuwa rais? Je, mwalimu aliona nini mpaka kufikia kutoa kauli kama hiyo?

Nimetafakari na kuona kuwa maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa sahihi ya kwamba tumuogope mtu wa namna hiyo kwa sababu kuna wengine wanapelekeshwa na tamaa ya kuwa Rais kuliko matarajio yao na hivyo kutumia kila njia kutimiza tamaa zao na si matarajio yao. Moja ya watu wenye Tamaa hiyo ni Tundu Lissu, tamaa hiyo inampeleka puta haswa hata kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake.

Kiukweli kwenye mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha BBC HARDTALK kimeonesha ni kwa namna gani Tundu Lissu akipelekeshwa na tamaa ya urais mpaka kufikia hatua ya kuichafua nchi yake na Rais wake. Ni mara nyingi katika kipindi hicho alikuwa akiulizwa kama ana ushahidi wa yale anayoyasema dhidi ya serikali yake kwa shutuma kama hizo na yeye kusema inafahamika hivyo kama jibu.

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa mtu kama Tundu Lissu ambaye ni msomi wa sheria kuishutumu serikali imehusika na hiki na kile kwa shutuma kubwa za kuhatarisha amani na usalama bila kuwa na ushahidi. Ni vile tu mwandishi hakusema ila angepata nafasi angemwelezea kuwa kwa kosa kama hilo la kuishutumu serikali bila ushahidi kwa hapa uingereza ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa.

Mwandishi wa kipindi kile kasaidia kwa namna kubwa sana kuamsha hisia za watanzania kwa kufichua ubabaishaji wa Tundu Lissu kwa dunia na uhatari wa anayoyafanya kuwa yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi. Shutuma anazozipeleka kwa rais wetu ni kubwa na zinahitaji ushahidi wa kutosha kuzitoa kwa sababu zinasababisha wawekezaji na watalii kupungua kutokana na hali mbaya ya kiusalama na uvunjifu wa amani unaoratibiwa na serikali kama Tundu Lissu anavyotaka iwe .

Serikali kama mlinzi namba moja wa usalama na amani ya nchi na raia wake hauna sababu za kueleza sababu za kiusalama kisiasa hasa zile ambazo hawana kithibitisho kuwa zimesababishwa na nini. Katika suala la Tundu Lissu kuna nadharia nyingi juu ya kushambuliwa kwake hivyo Lissu kuishutumu serikali kufanya hivyo moja kwa moja ni kosa na hivyo wenye akili inabidi tujiulize ni kwa nini serikali tu?

Jibu ni kwamba, Tundu Lissu anapelekwa puta na mawazo ya kuwa Rais hivyo ameanza kujipanga taratibu kwa kujenga chuki kwa wananchi kuwa CCM ndio wahusika hivyo wanapata nguvu ya kufanya fujo pale CCM inapowashinda kwenye uchaguzi mkuu wakisaidiwa na wanaowatuma kufanya hivyo.

Tundu Lissu , Dunia nzima sasa inajua lengo lako si zuri kwa nchi yako na waandaaji wa BBC hardtalk wameona aibu kumuhoji mtu ambaye hana data wala ushahidi wa tuhuma anazozitoa kwa serikali ambazo kwao wenyewe wanajua kwa tuhuma kama zile kwa nchi kama uingereza ni makosa makubwa. Umeamua kuichafua nchi yako kwa kupelekwa puta na urais ambao huna hakika utapata ama laaa .

Ushauri

i. Tundu Lissu asinyamaziwe, kwa nguvu ile ile anayoitumia kuichafua nchi kwa shutuma za kuokoteza zisizo na ushahidi ni vyema serikali ikatumia nguvu hiyo hiyo kumjibu . Tundu Lissu ajibiwe kisiasa na kitaalamu.

ii. Tundu Lissu atakapo rudi Tanzania kuandaliwe mdahalo kati ya Tundu LIssu na mwanaCCM mmoja ,watumie jukwaa hilo kumjibu kwa sababu Tundu Lissu hajaichafua serikali katuchafua pia CCM kwa kuwa ndio tunaongoza serikali.

Hitimisho

Tundu Lissu anajiona anajua sana kwa sababu anaamini hakuna mwanaCCM mwenye uwezo wa kumjibu ila akijibiwa atanyamaza kimya. Kila mtanzania mwenye akili timamu anamjua Tundu Lissu anafanya anayoyafanya kwa sababu ya tamaa ya Urais na anatengeneza mazingira mapema ili kushindana na nguvu ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

na Karlo Mwilapwa

Usimtumie Nyerere kwenye utetezi wako kwani linapokuja suala la kung'ang'ania madaraka yeye ni mmojawapo. Yeye alikaa madarakani miaka 24 akisema hakuna mtu sahihi kitu ambacho si kweli. Usimtumie Nyerere hapa maana ana mazuri yake mengi, hivyo tumeyafumbia macho mabaya yake.

Tuje hapo kwa Tundu Lisu. Anachokifanya ni kueleza kile kilichomkuta kwenye shambulizi lake na mwitikio wa serekali kwenye hilo shambulio. Kama ukweli anayosema itazuia watalii basi wakulaumiwa hapo ni serikali kwa kutotimiza wajibu wake. Huko uingereza huwezi toa tuhuma bila ushahidi hilo ni kweli, lakini shambulio lake ingekuwa ni uingereza, sasa hivi walioshambulia mpaka waliowatuma wangekuwa wamefahamika. Tundu Lissu haichafui nchi bali anaonyesha udhaifu wa serekali.

Kuhusu mdahalo wa Tundu Lissu na mwanaccm hilo yuko tayari na hata mkitaka mpelekeni mwenyekiti wenu kama ana uwezo wa mdahalo na majibu stahiki. Hakuna mwanaccm anayeweza kumjibu Lissu kwenye mdahalo hasa hilo shambulio lake. Lissu kutaka urais ni haki yake na tutampa kura zetu kwani tunautambua uzalendo wake.
 
Base Less Alegation, Inamaana Madai Yasiyo Na Msingi, Kama Kusoma Hawajui Hata Picha Hawaoni?, Risasi 16, Suggery 32, Bado Madai Hayana Msingi?
Wewe ndio hujaelewa!
Mwandishi alikuwa anamwambia Lisu athibitishe kwa ushahidi kwamba selikali inahusika. Yeye akabaki kusema mara mawaziri wote wanakaa eneo lile na blabla nyingine, amesahau kwamba hata Osama aliua watu karibu na pentagon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Mgonjwa lakini sio mgonjwa mahututi. Hiyo hospitali anaruhusiwa kufanya mazoezi mepesi hivyo kwenye hayo mazoezi mepesi anaweza kuendelea na mambo yake binafsi.
Umejaribu kuhoji lengo la yy kufanya hiyo ziara ni nini Na nini manufaa kwa Taifa?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
ha ha 'mere allegations'.. haya ndiyo aliokuwa anaambiwa Tundu na Steve, mnatuhumu bila ushahidi.
Kwahiyo ulitaka wakati Mh Tundulisu anapigwa lisasi achukue video kama ushahidi!!!
Hivi kunamtu anahitajiushahidi wa watu kuuawa amakupotea TZ? Serikali ndiyo yenye dhamana ya kulinda watu na mali zao, kama imeacha ombwe lakutoa ama kufanya uchunguzi juu ya uovu hii lawama abebe nani?
 
Hakika Kwa Interview AliyoFanyiwa TUNDU LISSU angefanyia JIWE NGOSHA angejiharishia Maana English Ya Lissu iko Vizuri Balas Ila mzee wetu wa Intrepreneur angekabwa na Kigugumizi Tu.m

Sent using Jamii Forums mobile app
Rejea interview yake ya Uganda ikabidi Museveni amfanyie ukalimani jiwe alitingwa sana maneno ya kutafuta tafuta full hesitations

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeangalia ile clup ya hard talk zaidi ya mara tatu. Sijaamini kile wazungu wamemfanyia jamaa. Alibaki anajikanyaga kanyaga tu bila kuwa na hoja zilizonyooka. Nasema ile interview imewaumbua sana chadema. Aibu yao wenyewe. Walitehemea maswali direct yenye mrengo wa kuiabisha nchi lakini jamaa alichokutana nacho ni hatari tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
irudie tena na ufuatilie maana ya HARDTALK au msingi wa kile kipindi.hawaulizi maswali ya TBC japo wanajua jambo huwa hawapendi kuchukua nafasi yako na siku zote hawapendi ionekane wao wamekushawishi kusema lakini wewe ndio umesema.Jiulize kwa nini maswali mengi yaliyokuwa yanaulizwa yamechukuliwa kwenye statement za viongozi wa serikali
 
For the first time Maelezo haya kuhusu Mh.Tundu Lissu hayana watu wanaomusapoti? Imekuwaje sasa? Nyie watu ndo munasema 2020 agombee uraisi wa nchi kweli hamutasahau kumpigia kura? Nilitegemea comment zakumutia moyo lakini munapita tu kama hamuoni majibu ya Mh.wetu? Yetu macho .......
 
Sijapenda alivyokua anamkatisha TALB kila alipokua anajibu maswali japo kasema ambacho dunia ilipaswa kukijua
 
Wote hao nawajua, hakuna anayezuiwa. Ila wanauwezo wa kujibu maswali mazito pamoja na sifa ya kuimudu lugha ya kiingereza. Je hapa kwetu uwezo huo upo?
Katika ziara zao huko ulaya na kwineko mfano Kagame walipokutana na Trump pembezoni mwabmkutano flan mwaka jana uliona akimuhoji lolote kuhusu yanayoendelea Rwanda?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na uwezo wake huo huo alionao, anaifaa nchi kuliko hao madalali wa wazungu. Vipi kuhusu MIGA, lini tunashtakiwa?.

Utashitakiwa huko MIGA umezuia maslahi gani ya mzungu? Hao Acacia na Barrick mpaka leo wapo na hawajalipa hata shilingi na bado wanaendelea na shughuli zao. Wakushitaki kwa lipi? Hakuna kiongozi yoyote ambaye hajawahi kuifaa nchi, bali ni kiwango gani anaifaa nchi hilo ndio jambo la msingi. Hata Hitler aliifaa nchi yake japo aliwaingiza matatizoni.
 
Utashitakiwa huko MIGA umezuia maslahi gani ya mzungu? Hao Acacia na Barrick mpaka leo wapo na hawajalipa hata shilingi na bado wanaendelea na shughuli zao. Wakushitaki kwa lipi? Hakuna kiongozi yoyote ambaye hajawahi kuifaa nchi, bali ni kiwango gani anaifaa nchi hilo ndio jambo la msingi. Hata Hitler aliifaa nchi yake japo aliwaingiza matatizoni.
Cha muhimu tuendelee kuwapa uhuru wa kupiga kazi wale ambao ilani yao imekubalika na wengi.
 
Tundu Lissu Kasoma Shule Ya Msingi Mahambe, O-Level Ilboru Kisha Advance Galanosi Lakini Anahojiwa Nusu Saa Na Anaongea Kingereza Kilichonyooka Alafu Kuna Mtu Kasoma Mpaka PhD, Hajui kuongea Kingereza Ukimuuliza Kwanini Anakwambia "Mimi Mtoto Wa Maskini" Ndugu Wewe Ni MJINGA!!

Swali la ushoga mtego. Lissu kajibu kwa akili sana. Interviews kama Hard Talk ni ngumu jamani. Kama hauko vizuri kichwani au kama lugha inakupiga chenga, bora usiende. Kweli Tundu Lissu anajua kingereza na kichwani yuko vizuri. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Ndugai na Makonda hawajawahi kujihangaisha na Lissu - hata kwa kumuandikia ujumbe wa pole mbali ya kutokwenda kumuona hospital lakini leo wamekuwa wa kwanza kumtaka arudi Nchini. Wamejipa kazi ya Utabibu na Udaktari and in their medical opinion, TL ameshapona. Unafiki ulioje!

Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan, aliwahi kusema kwamba serikali huwa hazitatui matatizo bali huyapanga upya tu. Ukifikiri kwa undani,kuna ukweli dhahiri. Tizama matatizo yaliyopo leo. Hayakuwepo siku za nyuma? Kama yalikuwepo na bado yapo, serikali inatatua?

mr mkiki.
 
*LISSU ATAABIKA SANA, AISHIA KUAIBIKA LONDON, ABANWA VIKALI NA KUTOA MAPOVU*

_NA Mwamba wa Kaskazini_

Leo ndio msemo kuwa Kiingereza sio maarifa umethibitika.

Tundu Lissu ana uwezo wa kutosha tu kuongea Kiingereza lakini asubuhi ya kuamkia leo kukosa maarifa kujawa na umbea, uongo na uzushi na uzandiki dhidi ya nchi yake kumemtokea puani akifanya mahojiano na Kipindi cha Hard Talk cha BBC.

Sikiliza haya.

*1.Aonesha Chuki Binafsi Kwa Magufuli*

Kosa la kwanza ni kutojadili hoja bali mtu.Kila alipoulizwa aliishia kutaja jina la Magufuli hata asipohusika.

Mtangazaji mzungu akabaki anashangaa na kumbana kwa maswali zaidi akaishia kutoa macho maskini.

*2.Lissu Hakutegema*

Hakika hata mimi sikutegema kama yule mzungu angefanya utafiti kiasi kile na kuyajua mengi ya Tanzania kiasi cha Lissu mwanzoni tu kubabaika na kuanza kuzusha uongo.

*3. Jaribio la kumdanganya Mzungu lakwama*

Baada ya kuzoea kuandika viwaraka vyake na kuwapa akina Martin Malera wa Tanzania Daima au Ibrahim Yamola wa Mwananchi leo Tundu Lissu kakutana na mwanahabari wa level nyingine.

Akajikuta anakosa ushahidi...anaambiwa unalalamika kila siku Serikali imekushambulia, unaushahidi gani anasema niliona gari inanifuatafuata, mzungu akambana kwani gari ziko ngapi na mtu yeyote si anaweza kukufuatilia kwani umeshafanya kazi ngapi za kukuweka katika risk ikiwemo kuwa wakili, Lissu akajikuta anakiri kuwa ni kweli hana ushahidi wa moja kwa moja bali ushahidi wa mazingira.

Asante sana mzungu, huyu Bwana leo baada ya mbwembwe nyingi sasa kakiri hana ushahidi zaidi ya mazingira tu ambayo pia yanaweza kuonesha chama chake kinahusika au hata dereva wake.

*4.Akosa maarifa kwenye madini*

Maskini hapa ndio jamaa alitoa mimacho tu baada ya mzungu kumbana kuwa yeye alipigania sana masuala ya nchi kufaidika na madini haoni kuwa JPM anachukua hatua nzuri?

Kwa hakika na mimi hapa nilipoteza Kiingereza changu[emoji3][emoji3]Sikumbuki hata Lissu alikuwa anajibu nini, aliishia maskini kutaabika na kuruka ruka huku na kule.Mzungu akaona isiwe shida, akahamisha mada!

Kwa kifupi hapa Lissu alijikuta anatamani kumpinga Magufuli, lakini pia akawaza anampinga kwa lipi?Kurekebisha mikataba ili nchi ifaidike? Akabaki anataja taja tu majina mara uwanja wa ndege Chato wakati nchi nzima vjwanja zaidi ya 15 vinajengwa[emoji3][emoji3]

*5.Mtangazaji aamua kutaja mwenyewe mazuri ya Tanzania.*

Baada ya kuona Lissu hana analolikubali katika nchi yake mzungu wa watu akaamua kutaja mwenyewe mageuzi makubwa yanayoendelea Tanzania.

Akataja mapambano dhidi ya rushwa, akataja kuongezeka kwa mapato akataja kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu.

Usiniulize wakati wote huu mzungu anashusha nondo Lissu alikuwa kwenye hali gani[emoji3][emoji3]Kumbuka mwenyewe kisa cha chura aliyebanwa na mlango[emoji3]


*6. Atoa mfano wa kitoto, wamuumbua*

Akieleza kwa nini wapinzani wenzake wamekuwa wakirejea CCM kuunga mkono juhudi za JPM Lissu aliishia kirusha matuhuma ambayo hadi mtangazaji akamuonya aache kuropoka bil ushahidi.


Lakini yotrme hii ni kwamba alishachanganyikiwa. Sasa sikia hii: akapewa mfano wa Masha aliyetoka CCM na kwenda upinzani (ingawa badae alirudi CCM) kama naye alihongwa huko upinzani? Usiniulize Lissu alikuwa katika hali gani hapa tena[emoji3]

*7.Akata fahamu, aunga mkono ushoga*

Akiwa hoi bin taaban na kisaikolojia akionekana mtu anayetamani mahojiano yaishe tu, Lissu akaulizwa ukiwa kiongozi wa upinzani na siku ukiingia Ikulu utafuta sheria zinazoelezwa kuwa kandamizi zinazoufanya ushoga kuwa kosa la jinai?

Maskini, mwisho wa zama ukatimia, baba la watu likajikanyagaaaa mwishowe likaingia kingi eti litafuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.Maweeeee[emoji17]

Rasmi Lissu kaunga mkono ushoga. Hakika ametaabika sana.

Kwa nini utaabike lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu aina kama yako ni hatari kwa taifa ,tutarajie wajukuu zetu kurithi ujinga mwingi kutoka kwa watu kama hili jitu[emoji115]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom