Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Nimeangalia ile clup ya hard talk zaidi ya mara tatu. Sijaamini kile wazungu wamemfanyia jamaa. Alibaki anajikanyaga kanyaga tu bila kuwa na hoja zilizonyooka. Nasema ile interview imewaumbua sana chadema. Aibu yao wenyewe. Walitehemea maswali direct yenye mrengo wa kuiabisha nchi lakini jamaa alichokutana nacho ni hatari tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha
Atafune uwembe tu walahi
Wadhungu wanajua jamaa linataka pochi, walalishtukia, wakalipiga pin walahi
 
Hii interview imethibitisha kuwa Lissu hajui walio mpiga risasi sema ana hisi tuu na amekuwa akihituhumu serikali bila ushahidi wowote hahahahah
Anaulizwa una ushahidi umepigwa risasi na serikali ana baki kujiuuma uma ooooh the area.... the area hahahah
Tulia hajui dhana ya circumstantial evidence.
 
Mtaweweseka sana nabado ilo ni pigo moja tu la bbc mmechanganyikiwa ivo, nawaambien laana ya Mungu juu ya Damu ya Lissu haitawaacha salama, labda nikukumbeshe urejee mahojiano ya rais wetu mtarajiwa Lissu,alisema doctor wake akimruhusu tu siku ya pili atakuwa dar esalaam
Kweli kamanda ngoja arudi. Mashoga wamepata mtetezi sasa
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Haya yananikumbusha ya maalim seif kuzunguka dunia nzima kwa miaka zaidi ya 15 kupinga SMZ hadi leo hajafanikiwa.
 
Issue ya CIG imekufa baada ya hard talk, leo Lumumba FC dau limepanda hadi msimbazi kuanzisha nyuzi za Lissu, poleni mesage imefika ss ni zamu ya Rais wa wanyonge kwenda akahojiwe tusikie kituko cha karne.
 
ha ha ha mgonjwa anaulizwa 'Magufuli amefanikiwa kudhibiti wawekezaji wa sekta ya madini'..'Mgonjwa anatoka povu akipinga hatua za serikali mwishowe anasema mimi ndiye nilianza lakini hawakuniunga mkono. Ni dhahiri kachemka!
Umechemka wewe nenda na wewe kahojiwe umsifie Magufuli kwani umekatazwa? yeye hakwenda kuabudu na kusifu.
 
m

Tundu lissu limejionyesha mbele ya ulimwengu lilivyo jinga. He has been grilled like meat. Chezea hardtalk stephen sackur. Alifikiria atawadanganya hardtalk kama anavyowadanganya nyumb wa cdm. Hardtalk yuko well versed kuhusu mambo ya tanzania. Hapo lissu ni kingereza tu ndio anajua lakini siasa ni kibaraka takataka. Imeacha walimwengu wakijua jpm anapendwa na amefanya makubwa nchini. Sasa hapo lissu limepata nini. Nimefurahi sana huyu mpuuzi kwenda hardtalk.
Kwa kifupi ameitangaza vizuri serikali ya JPM.
 
Kajitahidi ila siku zote open ended questions( Interview) huwa ngumu sana hasa ukikutana na mbobezi na mfukunyuzi wa habari kama walivyo kina Tim Sebastian na Stephen Sackur.

Wanapokuuliza swali usifikiri wanahitaji majibu yako bali wanahitaji kuoma umeenda mbali zaidi( Extraordinary defence) kwa kile unachokijua ...

Hata tundu Lisu alilitegemea hilo hata kabla ya mazungumzo kuanza kwani anamfahamu fika Stephen Sackur ndo mtu pekeee ambaye huwa anafanya research kuhusiana na taarifa nyingi za kiintelijensia na kidiplomasia huku akiwa amesheheni majibu na data tosha kuhusu mazungumzo yenu ..

HARDTALK ni kipindi au programme ngumu sana kuihandle kwa baadhi ya wanasiasa au watu ambao wanajikuta katika nafasi ile ,ndo mana wakati mwingine wataalamu wa kiplomasia wanakwambia kuwa HARDTALK ni kipindi ambacho unapaswa kujitoa mhanga kwani maswali yake huwa yanakulazimu kufunguka hata siri ambazo hukutegemea kama jamaa wangekuuliza ABC kuhusu inshu flani...

Ni kipindi ambacho mwanasiasa anaweza funguka mengi kutokana na system ya uendeshaji wa maswali kwani ni open ended questions...

Ni Provocative interview ambapo mhanga anaweza kujikuta analopoka mengi ila badae akitoka anaanza kujuta kwa alichofunguka...


Sent using Nokia 8 Plus
Stephen Suckur anazijua habari za Tz kana kwamba ni Mbongo alafu mdadisi sana cheki alivyombana Lisu atoe ushaidi wa kuwa ameshambuliwa na Serikali ? Hapa Lisu hajajibu vizuri amebaki na ushaidi tu wa mazingira

Alafu jamaa sometimes anaongea mambo na yuko na Statistical data angalia wakati mnahoji kuusu achievements za serikali ya magufuli kusuhu kuondoa watumishi hewa kwenye payroll? na kuongezeka kwa ukanyaji wa mapato

Bwana Stephen ni jembe sana yuko aware na political situation ya Tz lakini hata Lisu yuko vizuri sana hajaburuzwa kwenye interview alikuwa Straight forward hana hesitations yuko fluent in short naweza sema ilikuwa ni battle of words sio interview ya kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,

Kama wazungu wanatambua kuwa tuhuma za akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na wenzao kuwa ni za 'kutengeneza' basi wabadili mbinu.

kitendo cha waandishi wa media za kimataifa kuyaita madai ya Lissu kuwa ni ''base less allegations'' au ''inflamatory statement ni dhahiri wapo uchi.

Huenda Zitto Kabwe naye hajatupa mrejesho wa Mwenyekiti wa jumuiya za madola baada ya kuambiwa ''your allegations against Hon.Ndugai with respect to CAG are utter baseless''

Tuliwahi kusema hapa uongo haudumu na ndicho kilichotokea na zaidi umewaumbua watu mchana.

Ni dhahiri hata ule mpango wa akina Ngurumo kutafuta ''hadi ya ukimbizi'' Finland umeshindwa.

Tanzania yetu sote, tuipende,tuikumbatie.
Yale yanaitwa maswali chokonozi, anamwambia Lissu ni 'baseless' ili Lissu atoe ushahidi, na Lissu alifanya hivyo kwa umakini mkubwa.

Niseme tu Lissu aliwin the show, he was so composed, he looked so knowledgeable and extremely intelligent hata kuweza kujibu kwa ufasaha sana. Lissu is my hero.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu amezidiwa vibaya saana kwenye interview hii. Akili za wazungu usipime[emoji2][emoji2] Wanatujua kwelikweli. Wanajua namna JPM anavyoibadilisha Tanzania na ambavyo kundi la wabunge wa upinzani wanavyokunwa naye hadi wanahamia kwake CCM. Na jinsi atakavyopita kwa kishindo 2020. Tundu anadai eti wote wananunuliwa. Mtangazaji anamwambia kumbuka wewe ni Mwanasheria Mwandamizi, kwanini unatoa allegations zisizo na evidence[emoji2][emoji2] Tundu anabaki bila hoja[emoji2]

Hahahahahh mbombo jilipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!!! nimeisikiliza hii hard talk lakini naona Mh. Lissu kaniangusha sana sehemu 1 muhimu, pale alipoulizwa atoe evidence kuwa wabunge wananunuliwa na sio kwamba wanaenda kuunga mkono juhudi za President Magufuli.
Nilitegemea swala la video ya uthibitisho iliotolewa na Lema na Nassari ambayo alikabidhiwa mkurugenzi wa takukuru ingetumika kama ushahidi wa kununuliwa kwa madiwani na kwa kuwa haikufanyiwa kazi na hakukuwahi kuwa na uthibitisho wowote kuwa ilikuwa fake kama alivyojitanabaisha mmoja wa wanunuliwaji Ole Sabaya ingetumika kama strong evidence lakini Mh. Tundu alimiss hyo opportunity. BTW maybe next time atajiandaa vyema maana hii mechi yake na Stephen ilikuwa kama AS Vita vs Simba walioenda na matokeo yao Kinshasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unafikiri wazungu ahawaelewi kinachoendelea huku kwetu? Jiwe anavyo soma meseji za wengine na wao wanasoma zake! Kwa akili ya kawaida kabisa haiwezekani mbunge akaachia ubunge wake akagombee tena ubunge sehemu nyingine. Na hakuna anae hoji hizo garama za kurudia uchaguzi ni nani anae zibeba.
 
Back
Top Bottom