Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

haiwezekani wauaji wakufuatilie wiki sita mfululizo halafu ushindwe kutoa ushahidi usio na mashaka. Dereva aliposema analijua gari na aliwaona, eti akaenda kumkinga Lissu na risasi badala wamuache aende kuhojiwa wamemkimbiza ubelgiji kutibiwa ugonjwa wa saikolojia.
Mi huwa nawauliza sababu za mcng za kukimbia na dereva ni zipi kama mnajua cctv zitawaumbua?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Mnatuchosha...!
Naona ni Usajiri mpya huu toka Lumumba kwa ajiri ya 2020!
Sijui mmeokotwa wapi, Maneno mengi hafu pointless!

Nyie si ndo wenye Kila kitu....! Mpelekeni Mahakani mkamshtaki kwa kusema Uongo na kuleta Taharukuki mixer kupandikiza chuki kwenye JAMII..... kama ambavyo imefanyika huko nyuma!
Sasa Tundu alalamike, nyie pia wenye Chama Dola mlalamike.....Mnatuchosha.
analalamika kwa anayemtuhumu kwa tuhuma za kutunga?
 
Hicho ndo kitu watu wasichotambua, wamezoea waandishi wetu wasiofanya maandalizi
Mkuu yani mtu anaulizwa habari za wabunge wake kuhamia ccm yeye anasema wamenunuliwa, anaambiwa onesha ushahidi yeye anaanza kuongelea mambo ya kibiti!

Kiufupi Lisu kwenye hii interview kafeli vibaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mzungu anageuka kuwa mtanzania mzalendo kuliko mtanzania anayehojiwa, anamwaga data halafu TL anaanza kazi nzito ya kujenga hoja!.

Mzungu mwaka 1884 Berlin alikuwa anaijua afrika kuliko muafrika anavyoijua, muafrika anahaingaika na moto wa vijiti mzungu tayari anao umeme na anajua afrika inaanzia wapi na inaishia wapi!

Yule mtangazaji wa BBC alikuwa anamchora TL kiaina, tangu alivyomkaribisha unaona kabisa anamtazama katika jicho la kumjua kwa undani.

Halafu mzungu alivyo nyoko, siku zote akikudharau huwa anaongea kwa kunyenyekea ili usimgundue kuwa anachokifahamu ni zaidi ya unachokifahamu.

Sasa hapo Lissu amepata shida kwa maelezo, je pata picha angekuwa anahojiwa Magufuli ingekuwaje. Je unaamini kwa dhati ya moyo wako huyo mzungu mzalendo akimuhoji Magufuli atapata majibu stahiki?
 
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
Na mwisho wa hii drama yote ya TAL ninaiona kabisa

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Sasa hapo Lissu amepata shida kwa maelezo, je pata picha angekuwa anahojiwa Magufuli ingekuwaje. Je unaamini kwa dhati ya moyo wako huyo mzungu mzalendo akimuhoji Magufuli atapata majibu stahiki?
Magufuli hajawahi kulialia kwa wazungu kama Tundu na Chadema, mara kadhaa ameweka msimamo mkali, hata Steve amekubali. Kwani Lissu aliitwa au alienda mwenyewe?
 
Lumumba buku Saba wanazani mtangazaji kawabeba kwa kumbana lissu kwa follow up questions,kumbuka wale wako vizuri kiteknolojia wana setelite na source nyingi za kupata habari.Na Huyo mtangazaji anajua kula kitu ameamua kupotezea tu kama strategy isije onekana wazungu wanasapoti upinzani,ambapo ki ukweli hakuna taifa linalomsapoti Jiwe,kumbuka waraka wa bunge la umoja wa ulaya na baraza la seneti wewe unafikiri Steven sacur hayajui hayo.Wanasubiri right time to shoot.mark my words.
 
Sasa hapo Lissu amepata shida kwa maelezo, je pata picha angekuwa anahojiwa Magufuli ingekuwaje. Je unaamini kwa dhati ya moyo wako huyo mzungu mzalendo akimuhoji Magufuli atapata majibu stahiki?
Magufuli anawatumia vyema wasaidizi wake kwenye masuala kama hayo. Huwezi ukamkuta akiwa kwenye mahojiano ya aina hiyo.

TL alikwenda studio kwa nia ya kuchafua nchi yake akakutana na mzungu mwenye taarifa nyingi tu za Tanzania.
 
Alafu kwa mfano kama hili la kibiti, asichokijua Lisu ni kwamba hata hao wazungu wanaweza kuwa wanajua kwamba kilichokuwa kinatokea kule ni kulinda maslai ya nchi, kitu ambacho hata wao hufanya sana.

After all, hata huo ushahidi wa hao watu kuuawa huko kibiti hana, hivyo yule mwandishi angembana na hapo ninauhakika Lisu angekimbia swali tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu ameongea vizuri kwenye usaili wake, ila kilichomtoa kwenye reli ni ushahidi/uthibitisho kwa kile alichoongea mwenyewe,

Simshangai kukosa uthibitisho kwenye kauli zake mwenyewe, ila nawalaumu watanzania kwa kupenda na kuamini habari za udaku zisizo na ushahidi

Tabia hii ya watanzania imesababisha hata viongozi wetu wasione kama kuna maana ya kuongea vitu vinavyothibitika bila kuacha shaka

Jambo hili limemfanya lissu ajiamini kuingia kwenye usaili bila kua na hofu ya kuombwa uthibitisho akijua anaemsaili hatakua tofauti na watanzania

NB: watanzania tubadilike, tupende kuhoji kila tunacholetewa, tabia hii itawajenga viongozi wetu pia.
 
Mkuu yani mtu anaulizwa habari za wabunge wake kuhamia ccm yeye anasema wamenunuliwa, anaambiwa onesha ushahidi yeye anaanza kuongelea mambo ya kibiti!

Kiufupi Lisu kwenye hii interview kafeli vibaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Uzuri wa nafsi ya binadamu huwa haidanganyi, unajibaraguza mdomoni lakini ukweli unaujua kwamba ni rushwa ilitumika kuwanunua wabunge. Hata mimi sina ushahidi wa moja kwa moja but circumstantial evidence are sufficient to prove the matter though not in the court of law
 
Sikiliza mahojiano ,Lisu alizidiwa mbinu na yule mzungu.

Mzungu yuko bize kuzungumza positive kuhusu Tanzania ,Lisu yuko bize kuzungumza negative tu kuhusu nchi yake!!

Alafu mwishoni anamalizia kwa kuiomba serikali imlinde!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom