Tunapofika mwisho wa mwaka, haya ni mambo ambayo tunapaswa kujihadhari nayo

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,102
2,717
Tunapofika mwisho wa mwaka, inafaa tujadili mambo tunatakiwa kujihadhari nayo tunapokwenda mbele.

Nasita sasa kulihusisha jina la Nyerere na mambo ninayotaka kuyaandika sasa.

Lakini wote tunataka maendeleo ya kiroho kwa hiyo ni bora tuyajadili mambo ambayo yanaweza kutukwamisha.

Ni mambo gani ambayo tunapaswa kuyaepuka?

Nataka nitoe maoni, from my vantage point, kutokana na mazingara ninayoyaona. Mtu mwingine, aliyepo pengine, ataona mambo tofauti.

Tatizo la kwanza watu wanalopaswa kuepuka ni ngono za jinsia moja. Pia watu waache uzinzi. Utawasikia mapadre na masheikh wanakemea uzinzi.

Ni jambo zuri kukemea uzinzi. Lakini tunapoongea kuhusu uzinzi, nadhani, wakati mwingine tunaongea kuhusu mambo ambayo hayajakatazwa kisheria. Kwa hiyo jambo kubwa la kuzingatia kwanza ni kuwakataza watu wasifanye ngono za jinsia moja.

Sasa, watu lazima waamini kwamba maisha bila laana yanawezekana. Kama itakuwepo hali ya kukata tamaa kuhusu matatizo ya ngono, haya matatizo hayataondoka.

Nilisema tutamsikia Nyerere anaongea jinsi ambavyo hatujamsikia anaongea.
Tatizo lingine ni ulevi. Watu wanahangaishwa sana na ulevi. Sheikh wa Kiislamu mara nyingi namsikia anasema,"Nawausieni ninyi na kuiusia nafsi yangu." Kwa hiyo, kama wapo watu katika familia ya Nyerere walevi, naomba waache ulevi.

Tatizo lingine ni fitina. Fitina imezidi katika jamii. Fitina, maneno ya uongo yanasemwa, yanaleta taharuki katika jamii. Again, masheikh wa Kiislamu, natazama transcripts za Khutba za Masjid Kuu ya Makka, naona neno "fitna"linatajwa tena na tena.

Kwa hiyo nikitazama naona kwamba haya ni mambo ambayo tunapaswa kujihadhari nayo.

Nawatakia wote Happy New Year.
 
Poppy Hatonn nafasi gani ya uteuzi kwa sasa ukipewa unazani utaimudu zaidi. Na utafanya vitu gani pengine vya kukumbukwa kwa kipindi ambacho utakuwa ukitumika kwa hiyo nafasi?
 
Ahsante Poppy Hatton kuna ulevi wa madaraka na ubinafsi uliopitiliza huo nao unapaswa uwekwe kwenye bandiko hili.
 
Hapo "kama" kuna walevi kwenye familia ya Nyerere, hilo neno "kama" liondoe tu halina nafasi kabisa.
 
Umeongea mambo ya msingi sana, ni dhahiri saa mbovu kuna wakati inafika kwenye ukweli.
Happy New Year Mkuu.
 
Ushauri mmzuri sana.

Ingawa Kwa jinsi ambavyo kuna mmomonyoko mkubwa WA maadili mambo Kama ulevi, uzinzi plus unafiki (fitna) vimekuwa ni sehemu ya maisha yetu.

Watu wanajisifu kunywa pombe Kali

Watu wanajisifu kufanya ngono zembe, kununua Malaya, kuchepuka watu wanaona ndio mtindo sahihi WA maisha...

Unafiki uchonganishi plus uchawa

Mungu aturehemu.
 
Back
Top Bottom