Mnaosafiri kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo kuzingatia mambo haya...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kwa mnaosafiri Kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo kuzingatia mambo haya:

1. Hakikisha gari iko vizuri
2. Ukiwa unaendesha na si mzoefu wa safari ndefu ni vizuri kusafiri mchana tu
3. Waza kufika salama na si saa ngapi
4. Epuka mafuta ya vichochoroni
5. Kama kwenu mbali yaani KM 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6. Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho
7. Kuwa makini unapoanza safari na unapokaribia kufika
8. Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9. Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10. Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11. Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12. Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13. Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14. Hakikisha upepo wa matairi uko sahihi wakati wote
15. Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16. Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu, chukua namba kisha mpishe aende
17. Kama sio mzoefu kuendesha safari ndefu hata kama umenunua gari lako jipya chukua dereva….kijijini watajua tu ni lako hata kama sio wewe umeenda unaendesha.
 
Upo sahihi mkuu, safari zangu iwe safari ya mbali au karibu(mkoa mmoja kwenda mwingine) lazima ni Safiri kwa kupumzika, ikizidi sana navuka mikoa miwili, baada ya hapo safari nyingine itaanza kesho yake.
 
Kwa mnaosafiri Kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo kuzingatia mambo haya:

1. Hakikisha gari iko vizuri
2. Ukiwa unaendesha na si mzoefu wa safari ndefu ni vizuri kusafiri mchana tu
3. Waza kufika salama na si saa ngapi
4. Epuka mafuta ya vichochoroni
5. Kama kwenu mbali yaani KM 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6. Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho
7. Kuwa makini unapoanza safari na unapokaribia kufika
8. Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9. Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10. Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11. Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12. Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13. Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14. Hakikisha upepo wa matairi uko sahihi wakati wote
15. Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16. Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu, chukua namba kisha mpishe aende
17. Kama sio mzoefu kuendesha safari ndefu hata kama umenunua gari lako jipya chukua dereva….kijijini watajua tu ni lako hata kama sio wewe umeenda unaendesha.
Vizuri sana
 
Vitu vya msingi Sana hivi kuzingatia hasa kwa kipindi hiki ambacho ajali zimekua nyingi, wasiseme hawaku ambiwa
 
sawa wenye Magari yenu na mimi nimeshanunua flash na nimejanza miziki kabisa kwa ajili ya kusikiliza kwenye gari langu nikiwa nasafir bado kununua Gari tu 💪
 
Umesahau kihatarishi namba moja kwenye siku za mwisho wa mwaka ULABU hii kitu inasababisha ajari nyingi kuliko sababu zingine zote zikiwemo na ulizozitaja hapo juu!

Unakuta mwendesha gari anapark penye kinywaji anatandika chupa zake kadhaa kisha anaingia kwenye gari kuendelea na safari matokeo yake hajifikishi yeye na aliowabeba!
 
Vipi kwa tunaopanda Saratoga, naona kama ushauri unatubagua
Tohoa namba 11 hiyo kaka kuna kitu hapo kwa sisi tusio na magari,badala ya kufakamia mayai,karanga ,maboga,mahindi ya kuchomwa/kuchemshwa,viazi vya kuchemshwa,ndizi njiani, ni bora kujiandalia mwenyewe chakula chako kikavu kv nyama choma au mkate ili kuepusha uhasama na tumbo lako wakati wa safari
 
Hujawa dereva kama bado hujawahi kuendesha gari usiku kupitia barabara ambayo hujawahi kupita, umbali mrefu, mfano kutoka Dar to Mwanza na kurudi salama.
 
Back
Top Bottom