Tunapigwa sana na Wachina 🥲

Tunapigwa sana na Wachina 🥲

Naumkza sana kuona raslimali za nchi kama madini, gesi, nk. badala ya kuinufaisha nchi! Zinawanufaisha wageni huku wananchi wakiongezewa kodi na tozo kila mwaka ili serikali hiyo hiyo iishi maisha ya kifahari!

Kwa hali hii tukubali tu Waafrika tuko hapa duniani kwa bahati mbaya.
Hukumsikiliza vizuri Samia Suluhu Hassan, aliyosema Kigoma. Huhitaji kabisa kuumizwa na haya, wakati yeye analinda AMANI ya nchi hii.
 
Hukumsikiliza vizuri Samia Suluhu Hassan, aliyosema Kigoma. Huhitaji kabisa kuumizwa na haya, wakati yeye analinda AMANI ya nchi hii.
Na hapo kwenye "amani ya nchi" maana yake anaongelea ishu ya kuyalinda madaraka yake yeye binafsi na yale ya chama chake kwa gharama yoyote ile, ikiwemo ya kuuza raslimali za nchi kwa wageni!

Kwa maana hiyoBwatunwa aina hii wako tayari kufanya chochote ili tu waendelee kubakia madarakani. Hili ni jambo la kusikitisha.
 
Habari za Jf siku hizi ni kama umbea tu,hakuna details ni mipasho tu!

BTW:Maeneo yote yenye dhahabu kwa sasa wachina huwakosi Geita,Kahama,Chunya.

Airstrips kwenye migodi wala siyo habari,ipo pote tu hata migodi ya wazungu
 
Ila waTanzania hawana habari na wala hawana uchungu kabisa na nchi yao. Inasikitisha sana. Wao waonge hela ndogo tu wape kushabikia muziki, mpira na ujinga wa kina Mwijaku na uwatishe kuwa wapinzani wanaleta fujo na kutaharibia amanai basi the rest you can do whatever you want ata kama kuchukua kipande cha nchi yao wao sawa tu. Hiyo ndo Tanzania
Hapo si kuwalaumu watanzania maana mfumo wa nchi ndio umejengwa hivyo kuwa hutakiwi kushoboka la sivyo utaona cha mtema kuni sasa hii imefanya watu wengi kuana kuwa mali za nchi sio mali zao na haziwahusu zaidi ya serikali.
 
Ila waTanzania hawana habari na wala hawana uchungu kabisa na nchi yao. Inasikitisha sana. Wao waonge hela ndogo tu wape kushabikia muziki, mpira na ujinga wa kina Mwijaku na uwatishe kuwa wapinzani wanaleta fujo na kutaharibia amanai basi the rest you can do whatever you want ata kama kuchukua kipande cha nchi yao wao sawa tu. Hiyo ndo Tanzania
Ni kwamba mkuu hukuona Watz waliojitoa MO29? Na wakauliwa?
 
Sio Mpanda tu, Kanda ya Ziwa yote milima yenye dhahabu wamepewa Wachina. Wachina wamejaa wanavuna dhahabu tu. Wachimbaji wadogo wanafukuzwa kila sehemu.
 
APo wangekuwa wamewekeza nchi za magharibi mimi nisingechangia chochote sababu najua angalau jamaa wana utu na ubinadamu apo wakazi wa mpanda wangechimbiwa visima vya maji na bado wangetoa hela kwa ajili ya kufanyia maendeleo bila kusahau wangaeawaajili watu wakalipwa vizuri na ku treatiwa vizuri tofauti na wachin washenzi sana awa jamaa cha kwanza wanachukua kila kitu apo kwenye mgodi hawana ubinadamu na watawalipa hela mbuzi wafanyakazi ..
 
Unaokota tweet za huko X kuja kupandikiza chuki dhidi ya Wachina waliowekeza Tanzania?

Hata kama ni uongo basi mpe credit mwenye hiyo tweet
Watu tupo field tunayaona haya wachina ni wababaishaji hawana ubinadamu na watesaji tu iyo.migodi wangepewa wazungu watu wangefaidika sana apo kwa kulipwa vizuri na kufanyiwa baadhi ya maendeleo kwenye eneo husika
 
Wewe unatuongezea tu msongo wa akili; kana kwamba yaliyopo hayatoshi kuumiza roho za watu.

Sasa tueleze basi tuelewe unasema nini na ushahidi ulionao wewe; hata wa kimazingira tu.

Ni nani asiyejuwa wizi wa waChina, lakini sasa si wizi tena, ni kama wanazoa tu mali isiyokuwa na mwenyewe!

Tumeharibikiwa sana, lakini hasa sijui kwa nini wananchi nasi ni kama tumegandishwa akili kabisa ili tusistuke!

Kelele zote zile alizopiga Magufuli kuhusu mali zetu, hakuna hata moja iliyotuingia kichwani?
Na kwa wale wazee je, mafunzo yote ya Mwalimu Nyerere kuhusu raslimali za taifa hili, hata wao hawakumbuki kabisa lolote?

Tumebaki na akina Stphen Wassira na akina Kibudu Kalamaganda, wakiwa mstari wa mbele kunadi mali za waTanzania, kana kwamba hawakuwepo kabisa wakati wa mafunzo?

Sasa tufanyeje, nani ataliokoa taifa hili!
Ni wananchi wenyewe kuamka kutoka usingizini bila hivyo Tanzania itabaki kufaidisha na kustawisha mataifa mengine tu.
Tatizo CCM ilichofanikiwa ni ku put Tanzanians' mind into captivity kuona kwamba maliasili (dhahabu, almas, gas, misitu, mafuta, mbuga za wanyama etc) ni mali za serikali sio mali za watanzania. Ndio maana ukiongea na watu wazee kwa vijana hadi wasomi wanakwambia hayo mambo ya maliasili ni vitu vya serikali mimi mwananchi nahusikaje hapo. Kwa hiyo unaona kabisa waTanzania hawako connected kabisa na maliasili zao. We have a very long way to go
 
Back
Top Bottom