tracy martins
JF-Expert Member
- Aug 5, 2014
- 3,532
- 1,484
Elimu ipo kichwani na sio kwenye makaratasi...kuna mjomba wangu alipitia gereji miaka mingi iliyopita....baada ya kuona maisha ya ufundi hasa wa mitaani ni magumu sana akakimbilia mwanza kwa kaka yake....kwa kuwa hakuwa na elimu ya darasani....akafanikiwa kupata kibarua kwenye kampuni flani ya kuchimba madini kama mlinzi......alikaa getini kwa miaka minne....ndipo siku moja kuna mtambo mmoja ulileta hitirafu...yule injinia alihangaika sana na mavitabu yake....alipekuwa mpaka vidole vikatoa jasho.....ndipo yule bwana wakati anapiga doria za kawaida akapita karibu na hilo eneo yule injinia akamwita akiwa na mzungu ili amshikie vifaa wakati akiwa anahangaika....ulipotimia muda la lunch yule injinia akaenda kupata lunch kwa mbwembwe...huku nyuma alibaki yule mzungu na yule mlinzi....wakati yule mzungu akiwa anatafakali cha kufanya maana ule mtambo ni muhimu sana kwa shughuli za pale mgodini.....yule mlinzi ambaye alikuwa anautazama ule mtambo kwa umakini wa hali ya juu...akamwambia yule mzungu kuwa anaweza akamtengezea....yule mzungu bila ubishi akamkabidhi vifaa jamaa akazama uvunguni...ambapo alikaa kama dakika kumi...alipotoka uvunguni akamwambia mzungu awashe mtambo....katika hali iliyomshangaza yile mzungu ule mtambo uliwaka na kuanza kufanya kazi...mpaka anakuja yule injinia anakuta yule injinia anakuta mtambo unafanya kazi hakuyaamini macho yake pale alipoambiwa kuwa aliyefanya kazi hyo ni huyo mlinzi alichoka kabisa....kiilichotokea baada ya hapo ni kuwa mjomba ambaye ni mlinzi alikabidhiwa mitambo yote ya pale aisimamie......alilipwa mshahara ambao kwake ulikuwa kama ndoto...
saafi hiyo