wewe Graduate unayelalamika na kupiga Makelele hakuna ajira hebu pitia hapa ujifunze kitu

young MathematiciAn

Senior Member
Oct 31, 2016
160
361
Leo hii ukimuuliza mwanafunzi yeyote wa O level,A level ndoto yake ni ili awe nani au anasoma ili afanyaje 95% watakupa jibu wanasoma ili aajiriwe kitengo chochote aidha serikalini au sector binafsi.Wapo watakuambia wanataka kuwa wahasibu,wengine watakuambia wanataka kuwa madaktari,wahandisi,walimu,wakurugenzi nk

"Graduates na wanafunzi kuna kitu huwa mnasahau"

1.Kila mwaka wanafunzi wanahitimu vyuoni na hapa Tanzania tuna vyuo vingi vinavyotambulika na TCU kuna UDSM,SUA,MZUMBE,IFM,UDOM,TIA,na vingine vingi.

*wewe graduate uliyosoma Bcom,Uhasibu,finance nk fahamu kwamba kila mwaka graduates wa kozi hizo wanahitimu.Mzumbe kila mwaka wahasibu wanahitimu,IFM,TIA,CBE hivyo hivyo kila mwaka kuna watu wanahitimu ,wewe uliyosomea Bcs na IT fahamu ya kwamba kila mwaka UDOM,SUA,UDSM,IFM,nk kuna watu wanahitimu hizo kozi.

Sasa fikiria tokea 2000-2016 kuna wahitimu wangapi wa kozi ya uhasibu,IT kuna fani nyingi ndani ya hizo fani kuna wahitimu wangapi waliobobea kwenye security,web developer,networker nk,wahandisi wangapi wamehitimu,na kila aina ya kozi unayoifahamu piga hesabu tokea 2000-2016 ni wangapi wamehitimu na bado wengine wapo vyuoni wanasubiri kuhitimu.

*Tujiulize nafasi ya kazi kwenye ngazi ya uhasibu zipo ngapi nchini na wahitimu tupo wangapi?
*Mawakili kuna nafasi za kazi ngapi serikalini na sisi wahitimu tupo wangapi?

Kama wewe ulisoma ili ukishahitimu hapo hapo uajiriwe utakuwa na matatizo exclude madaktari na walimu "hawa wanahitajika sana na jamii" ,labda uwe na ndugu atakaye kufanyia mpango ya kukuweka kwenye kitengo .

*Inawezekana kila siku tunapiga makelele kuhusu ajira lakini tumejiuliza je, nafasi za kazi zinaendana na idadi ya wahitimu nchini.

kuna njia nyingi ya kutatua haya matatizo ya ajira lakini tatizo hatujajiwekea mikakati ya kuondokana na hili wimbi la kelele la ajira

*Hivi nyie wahitimu wa fani ya uwakili mnaotambulika na chombo chenu cha uwakili mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu.Kila siku watu wanataka kugongewa mihuri na ukienda ofisi za mawakili itabidi utoe si chini ya Tsh 10,000 na wanaotaka kuanzisha biashara,kampuni kupata mhuri wa wakili ni tsh 50,000++.

* nyie mliosomea web designing,system administrators,Programmers mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu,watu kibao hawajui kutengeneza websites,kuna watu wanashida kibao mngetumia fursa hiyo mngekuwa mbali saizi.

*Wasanifu majengo mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu kuna mifano nimeiona huku ninapoishi kuna vijana graduates wa Ardhi walianzisha kampuni yao saizi wanatembelea ma range rover tu na ofisi zao zipo mtaani tu frame 2 tu ukiona ofisi yao unaweza kuwadharau lakini kila siku wanasafiri nchini kwenye sites mbali mbali.

wengine watatoa sababu mtaji tutapata wapi??

1.Adama Barrow Rais aliyechaguliwa Gambia alikuwa mlinzi wa getini ilhali alikuwa degree holder wa BBA lakini saizi anaendesha biashara zake kubwa tu

2.Waziri wa India alikuwa konda wa daladala japo alikuwa graduate lakini saizi ana cheo kikubwa serikalini.

''Vision without Action is merely a dream.
vision with Action can change the world.

Structural Unemployment-Ni ile hali ambayo hakuna ajira kutokana na sababu mbalimbali za ki uchumi labda sababu ajira haitoshi kwa watu wote hivyo idadi kubwa ya wasomi,wenye ujuzi wanabaki wanahangaika.Inawezekana mtu huyo akahangaika kwa kipindi kirefu lakini akakosa ajira labda sababu ya uzoefu mdogo,nafasi za kazi zimejaa nk sasa mtu huyu akikaa kwa kipindi kirefu bila ya kujishughulisha na fani yake pindi ajira zikitoka mpya anaweza kukosa sifa sababu ujuzi wake utakuwa umefifia,umeyeyuka kutokana hakujishughulisha na fani yake kwa kipindi kirefu hivyo sifa akakosa na akafeli kwenye interview..kuondoa hiyo tatizo njia sahihi ni kutumia ujuzi wako kujiendeleza kama mifano iliyotolewa kuanzisha kampuni zenu binafsi hata siku ukienda kuomba kazi kwenye CV yako utakuwa na Experience ya kutosha.

Volunteer/Temporary Job-Ki uchumi Temporary job ni aina ya kazi ambayo mhitimu anafanya huku akisubiria nafasi za ajira katika fani yake.Mfano mhasibu anaamua kufanya kazi yeyote ile ambayo haiendani na fani yake/anajishikiza sehemu yeyote ile hata kama mshahara hautoshi huku akitafuta kazi inayoendana na fani yake ya uhasibu .

Vijana wengi waki Tanzania na masikitiko makubwa unamkuta kijana kasoma Uchumi A level mpaka chuo na haya masuala ya Volunteer jobs anayajua,frictional unemployment anayafahamu lakini unamkuta analalamika ajira hakuna ,steps zipi ulichukua kukabiliana na tatizo la ajira???

Vijana tubadilikeni

Ushauri mzuri na pia kila mmoja anawaza kama unavyoshauri. Ila tatizo linarudi mwanzo kuwa nyenzo za kuanzisha huo mradi au kazi ya kujitegemea lazima uwe na pesa ya kutosha.. Huwezi kuendelea kwa kuwa na idea tu, lazima nyenzo za kuiweka idea into practice ziwepo
 
mkiwa wa 4 au 5 mnaweza kusaidiana na kutengeneza kitu kikubwa.
siamini mkiwa wa nne mtashindwa kwa pamoja kupata nyenzo.
mkiaminiana na kuwa na team work naamini pesa haitokuwa kikwazo
 
Rc na Rpc atabaki kuwa moja kila mkoa , C.A.G atabaki kuwa moja, mkuu wa Tra au hospitali atabaki kuwa moja tu, mkemia mkuu atabaki kiwa moja tu Tz nzima, na nafasi zote za kazi zitabaki vilevile sasa ukiangalia uwiano na wahitimu dah yani ajira chache wahitimu wote hawawezi kupata.......
 
Tanzania unaweza ukaambiwa mtoa Uzi kaajiriwa kwa ufupi ushauri Mzuri wanaombea mkuu wa kaya awatimue labda vijana watapata ajira
 
Leo hii ukimuuliza mwanafunzi yeyote wa O level,A level ndoto yake ni ili awe nani au anasoma ili afanyaje 95% watakupa jibu wanasoma ili aajiriwe kitengo chochote aidha serikalini au sector binafsi.Wapo watakuambia wanataka kuwa wahasibu,wengine watakuambia wanataka kuwa madaktari,wahandisi,walimu,wakurugenzi nk

"Graduates na wanafunzi kuna kitu huwa mnasahau"

1.Kila mwaka wanafunzi wanahitimu vyuoni na hapa Tanzania tuna vyuo vingi vinavyotambulika na TCU kuna UDSM,SUA,MZUMBE,IFM,UDOM,TIA,na vingine vingi.

*wewe graduate uliyosoma Bcom,Uhasibu,finance nk fahamu kwamba kila mwaka graduates wa kozi hizo wanahitimu.Mzumbe kila mwaka wahasibu wanahitimu,IFM,TIA,CBE hivyo hivyo kila mwaka kuna watu wanahitimu ,wewe uliyosomea Bcs na IT fahamu ya kwamba kila mwaka UDOM,SUA,UDSM,IFM,nk kuna watu wanahitimu hizo kozi.

Sasa fikiria tokea 2000-2016 kuna wahitimu wangapi wa kozi ya uhasibu,IT kuna fani nyingi ndani ya hizo fani kuna wahitimu wangapi waliobobea kwenye security,web developer,networker nk,wahandisi wangapi wamehitimu,na kila aina ya kozi unayoifahamu piga hesabu tokea 2000-2016 ni wangapi wamehitimu na bado wengine wapo vyuoni wanasubiri kuhitimu.

*Tujiulize nafasi ya kazi kwenye ngazi ya uhasibu zipo ngapi nchini na wahitimu tupo wangapi?
*Mawakili kuna nafasi za kazi ngapi serikalini na sisi wahitimu tupo wangapi?

Kama wewe ulisoma ili ukishahitimu hapo hapo uajiriwe utakuwa na matatizo exclude madaktari na walimu "hawa wanahitajika sana na jamii" ,labda uwe na ndugu atakaye kufanyia mpango ya kukuweka kwenye kitengo .

*Inawezekana kila siku tunapiga makelele kuhusu ajira lakini tumejiuliza je, nafasi za kazi zinaendana na idadi ya wahitimu nchini.

kuna njia nyingi ya kutatua haya matatizo ya ajira lakini tatizo hatujajiwekea mikakati ya kuondokana na hili wimbi la kelele la ajira

*Hivi nyie wahitimu wa fani ya uwakili mnaotambulika na chombo chenu cha uwakili mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu.Kila siku watu wanataka kugongewa mihuri na ukienda ofisi za mawakili itabidi utoe si chini ya Tsh 10,000 na wanaotaka kuanzisha biashara,kampuni kupata mhuri wa wakili ni tsh 50,000++.

* nyie mliosomea web designing,system administrators,Programmers mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu,watu kibao hawajui kutengeneza websites,kuna watu wanashida kibao mngetumia fursa hiyo mngekuwa mbali saizi.

*Wasanifu majengo mnashindwa vipi kujikusanya na kuanzisha kampuni yenu kuna mifano nimeiona huku ninapoishi kuna vijana graduates wa Ardhi walianzisha kampuni yao saizi wanatembelea ma range rover tu na ofisi zao zipo mtaani tu frame 2 tu ukiona ofisi yao unaweza kuwadharau lakini kila siku wanasafiri nchini kwenye sites mbali mbali.

wengine watatoa sababu mtaji tutapata wapi??

1.Adama Barrow Rais aliyechaguliwa Gambia alikuwa mlinzi wa getini ilhali alikuwa degree holder wa BBA lakini saizi anaendesha biashara zake kubwa tu

2.Waziri wa India alikuwa konda wa daladala japo alikuwa graduate lakini saizi ana cheo kikubwa serikalini.

''Vision without Action is merely a dream.
vision with Action can change the world.

Structural Unemployment-Ni ile hali ambayo hakuna ajira kutokana na sababu mbalimbali za ki uchumi labda sababu ajira haitoshi kwa watu wote hivyo idadi kubwa ya wasomi,wenye ujuzi wanabaki wanahangaika.Inawezekana mtu huyo akahangaika kwa kipindi kirefu lakini akakosa ajira labda sababu ya uzoefu mdogo,nafasi za kazi zimejaa nk sasa mtu huyu akikaa kwa kipindi kirefu bila ya kujishughulisha na fani yake pindi ajira zikitoka mpya anaweza kukosa sifa sababu ujuzi wake utakuwa umefifia,umeyeyuka kutokana hakujishughulisha na fani yake kwa kipindi kirefu hivyo sifa akakosa na akafeli kwenye interview..kuondoa hiyo tatizo njia sahihi ni kutumia ujuzi wako kujiendeleza kama mifano iliyotolewa kuanzisha kampuni zenu binafsi hata siku ukienda kuomba kazi kwenye CV yako utakuwa na Experience ya kutosha.

Volunteer/Temporary Job-Ki uchumi Temporary job ni aina ya kazi ambayo mhitimu anafanya huku akisubiria nafasi za ajira katika fani yake.Mfano mhasibu anaamua kufanya kazi yeyote ile ambayo haiendani na fani yake/anajishikiza sehemu yeyote ile hata kama mshahara hautoshi huku akitafuta kazi inayoendana na fani yake ya uhasibu .

Vijana wengi waki Tanzania na masikitiko makubwa unamkuta kijana kasoma Uchumi A level mpaka chuo na haya masuala ya Volunteer jobs anayajua,frictional unemployment anayafahamu lakini unamkuta analalamika ajira hakuna ,steps zipi ulichukua kukabiliana na tatizo la ajira???

Vijana tubadilikeni

OK vizuli
 
Ushari mzuri mkuu

Japo hata Dr. Rutengwe alishauri tujiajiri alipotenguliwa akaanza kulia tena kama sisi.
 
Back
Top Bottom