Profesa Ndalichako aagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwachukulia hatua viongozi wa serikali ya wanafunzi

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Mama hafahamu mwenye njaa haogopi kufa, kwani hata njaa itamuua.

Kuna muda nawaza hawa watu wamesomeshwa na mission nini? Hawajui njaa kabisa. Tuliopitia huu msoto kipindi kile tunaelewa.

=====

1576654093865.png

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), waliotoa tamko la kuipa serikali saa 72, kulipa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, vinginevyo wataandamana.

Juzi Daruso walitoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuhakikisha inatoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Profesa Ndalichako alisema tamko hilo limetolewa kinyume cha utaratibu wa kutoa malalamiko na utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu, ambacho hakiwezi kuvumilika, hivyo ametoa saa 24 kwa UDSM, kuwachukulia hatua na apewe taarifa hatua iliyochukuliwa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu, uongozi wa Daruso unapaswa kuwasiliana na Mshauri wa Wanafunzi, ambaye anachukua malalamiko yao na kuyapeleka kwa Makamu Mkuu wa chuo.

Lakini, taratibu hizo zote hazijafuatwa na uongozi wa chuo hicho kikongwe nchini haujui chochote kuhusu madai na malalamiko hayo. Aidha, alisema wanafunzi 45,000 wa mwaka wa kwanza, walipaswa kupewa mikopo, lakini serikali imeongeza idadi na kufikia 49,485, na Sh bilioni 172 zimetolewa kwa ajili yao na wameshapata mikopo wote waliokidhi vigezo.

Alisema jumla ya wanafunzi 128,697 wa elimu ya juu, wanatarajia kunufaika na mikopo mwaka huu, ambayo kiasi cha Sh bilioni 447 zimepangwa kwa mikopo, na hadi sasa Sh bilioni 202 sawa na asilimia 45 zimeshapelekwa HESLB.

Katika madai ya wanafunzi hao, alisema zipo taratibu za uhakiki wa vigezo na nyaraka wanazopaswa kuwasilisha wanafunzi na hivyo bodi ilikuwa inapitia vigezo na kujiridhisha, ikiwamo uwepo wa wanafunzi yatima, walemavu na uwepo wa wanafunzi waliokata rufaa, ambao taarifa zao zinafanyiwa kazi ili wakikidhi vigezo wapatiwe mikopo.

“Wakati taratibu za uhakiki zinaendelea, wanafunzi wamekuja na tamko ambalo ni utovu wa nidhamu mkubwa tena wanaipa serikali masaa 72 watekeleze madai yao vinginevyo wataandamana, nasema hivi masaa 72 ni mengi waanze maandamano leo, wanatingisha kiberiti, lakini nawaambia kiberiti kimejaa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema amezungumza na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, lakini hajapata malalamiko yoyote rasmi, zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo tamko hilo ambalo halikufuata taratibu ni batili na utovu wa nidhamu.

“Wanafunzi wasiotaka kusoma, waondoke na kuwaacha wanaotaka kusoma, kwa sababu tamko hili kama lina jambo lingine zaidi ya masomo, tamko hili linalenga kuleta vurugu na kuvuruga masomo, tutalishughulikia kikamilifu,” alisema waziri huyo wa Elimu.

Wakati waziri akitoa uamuzi huo, HESLB imesema hadi sasa jumla ya wanafunzi 49,485 wa mwaka wa kwanza, wameshapata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 169.4 na kuvuka lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 45,000.

Imesema kati yao, wanafunzi yatima waliopoteza mzazi au wazazi wote wawili ni 10,383, wenye ulemavu 397, waliofadhiliwa masomo ya sekondari 3,128 na wengine wahitaji 35,577.

Aidha, wanafunzi 78,337 wanaoendelea na masomo, wamepata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 272.1. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema pamoja na malipo hayo, kwa sasa bodi hiyo inakamilisha malipo ya fedha za wanafunzi waliobadilisha kozi, ambayo imepokelewa na HESLB kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) mwishoni mwa wiki na fedha hizo zitawafikia wanafunzi ifikapo kesho.

Alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Menejimenti ya HESLB, Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wawakilishi wa viongozi wa wanafunzi wa chuo hicho juzi jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Makamu Wakuu wa UDSM, Profesa Killian Bernadetha (Utafiti), Profesa David Mfinanga (Utawala), wawakilishi wa serikali ya wanafunzi na watendaji wengine wa UDSM na HESLB.

“Kuna kundi la wanafunzi waliobadilisha kozi wakiwa vyuoni na taarifa hizo zilikuwa hazijatufikia, tumezipokea mwishoni mwa wiki na tu

nakamilisha malipo ambayo yatawafikia siku mbili zijazo,” alisema Badru.

Alieleza kuwa kundi lingine linahusu malipo ya vitabu na viandikwa, ambapo malipo ya awamu ya kwanza ya jumla ya Sh bilioni 13.3 yameshafanyika na awamu ya pili ya Sh bilioni 1.1 itawafikia wanafunzi ifikapo Jumamosi ijayo, Desemba 21, mwaka huu, kwa kuwa wataalamu wanakamilisha uchambuzi.

Profesa Anangisye alisema wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu wanapokutana na changamoto, wasisite kuziwasilisha kwa menejimenti za vyuo ambavyo vitaziwasilisha HESLB au kwa taasisi sahihi.

“Hata nyie (Daruso) mlipaswa kuanzia kwetu na tungeyafanyia yote kazi badala ya kutoa maelekezo ya saa 72,” alisema Profesa Anangisye na kulieleza gazeti hili jana saa 12:04 jioni kwamba walikuwa kikaoni kushughulikia haraka agizo hilo la waziri wa Elimu.

Chanzo: H
abari Leo

====
Maoni ya wadau
Wakati wanatoa tamko nilisikia wanasema kwamba hii ni wiki ya sita hawajapewa hela zao za mikopo na maafisa mikopo hawatoi majibu yanayoeleweka

Sasa hapo wanakosa gani?

Nakumbuka mwaka fulani kule Dodoma wakati UDOM bado haijakamilika, waliohusika na ujenzi walikuwa wachina!

Mwaka huo wanafunzi waliokuwa wanategemea hela ya bodi walicheleweshewa kama hivi hivi!

Kilichokua kinaendelea huko ni huruma tu!

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja na pocket money kama za Sekondari ( elfu 20, 30, 50 +) kila walipokuwa wanaomba kusaidiwa na wazazi ama ndugu zao baada ya kuishiwa hawakueleweka! Na sababu ya kutoeleweka ni rahisi tu! WAZAZI WENGI HAWANA UWEZO!

Baada ya kama mwezi bila kitu kueleweka, wale wachina na baadhi ya vibarua"walijifaidisha" mabinti kwa gharama ya kuwanunulia chakula cha siku kwa mama lishe waliokuwa wanauza chakula kule!

Fikiria unaamka asubuhi hauna hata mia tano mfukoni! Rafiki yako naye hana! Nyumbani ukiomba hawana! Halafu wakati huo huo unatakiwa uwe darasani, ufanye assignment na vitu vingine vingi!

Hivi hapa mambo yataenda? Unadhani watu watatoka na kauli laini?

Ni kweli kabisa kwa hali ya makato ya bodi yanavyoenda kwa waliokwishaanza kurejesha hasa watumishi wanalalamika riba imekuwa kubwa (wanaiita value retention fee) pengine sawa au kuzidi hata mabenki!

Lakini sote tunafahamu hali za watanzania hawakopesheki na mabenki na wengine hawana uwezo kumudu gharama za chuo!

Kwasababu waliingia makubaliano ya kuwahudumia kwa mkopo huo, kwanini wasipewe kwa wakati?

Kwanini wanapodai makubaliano yao kuzingatiwa watishiwe kuchukuliwa hatua?

Hii kweli ni sahihi?

Mbona wao kwenye marejesho hawana subira? Tena hadi figisu zimo! Wengine wamepewa mikopo ya vyuo viwili hadi vitatu wakati kimsingi walisoma chuo kimoja!

Badala ya kushughulika na chuo kilichopokea pesa, wanashughulika na mwanafunzi ambaye kimsingi hakutumia pesa hiyo! Hata pale vidhibitisho vinapotolewa bado muhanga anaendelea kuhangaishwa hadi maika miwili mitatu na makato yanabaki vile vile!

Kwa mtu aliyekulia familia bora, anapata kila atakacho, amesoma bila shida kamwe hawezi kujua shida wazipatazo hawa wanaotegemea HESLB!

Waziri Ndalichako hapo amewatusi wanafunzi, hajawatendea haki!

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wana JF

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na msemakweli ni mpenzi wa Mungu, Dr. John Pombe Magufuli imekuwa ikijinasibu kuwa na pesa nyingi kutokana makusanyo makubwa ya kodi.

Ushahidi wa hili ni miradi mikubwa iliyoanzishwa na kuendeshwa na serikali, mfano ni ununuzi wa madege kwa pesa taslimu, ujenzi wa SGR, umeme wa Stiglers Gorge, flyovers, daraja Busisi nk.

Kama vyote hivi vinafanyika kwa uwezo wetu, nini kimetokea mpaka wanafunzi wa elimu ya juu wakose mikopo yao?

Waziri Prof. Ndalichako kunukuliwa ukijimwambafai kumiliki kiberiti kilichojaa na uko tayari kukitumia ili kuwadhibiti wanafunzi wasidai haki yao ni fedheha kwako wewe na serikali unayoitumikia!

Picha mnayotupa sisi wananchi huku ni kuwa Serikali yetu imejaa ulaghai, haina pesa imefilisika! Serikali tajiri haiwezi kutishia kiberiti wanafunzi!

Serikali wapeni wanafunzi mikopo yao ili mlinde heshima yenu mnayotuaminisha!
Wale waliosoma kwa raha sana miaka ile, ndo hawakumbuki umuhimu wa kulipwa stahiki zote kabla ya masomo kuanza ndo mwanafunzi atulie asome, wamesahau kabisa!! Mtoto katoka Sumbawanga, kapewa pesa ya kula njiani labda 50k, baba anategemea mtoto akifika atalipwa pesa na kuanza masomo; mtoto anafika anakuta eti ndo mipango inaendelea ya malipo, je arudi nyumbani ndo aje baadaye, afunge kula na kulala hadi malipo yawe tayari, au afanyeje?

Mnaojitia kuitetea serikali na Prof. Ndalichako hamjui kwamba hiyo so called Bodi ndio chanzo cha matatizo! Wanazichezea pesa za wanafunzi halafu wanajitia kuwa wakali! Na kwa nini wanafunzi waitwe toka nyumbani, kama mambo hayajakaa sawa?

Halafu ona sasa hii communication breakdown; mwenye chuo anasema kama hujalipa hadi tarehe fulani, basi! Bodi ya Mikopo na Waziri wa Elimu wanajitia wako bize "wanakamilisha mambo"; je, meanwhile, mwanafunzi anapaswa kufanyaje?

Hebu kuweni na busara mtoe mawazo yenye maana ya kuwasaidia wanafunzi. Mnataka wafanyeje ndo mjue wana shida?

Ushauri wangu, bodi ifanye kazi usiku na mchana, mambo yote yawe sawa ndio wanafunzi waitwe kutoka nyumbani kuja kuanza vyuo; short of that, ni ujinga mtupu, ubinafsi na roho mbaya zimetawala!
 
Andamana hata kesho umeambiwa maneno mengi ya nini?
mnapoona wazazi wanafunga mikanda
nyie mnajitia kuvaa milegezo mtaipata fresh.
Sent using Jamii Forums mobile app
Waambie Mkuu hawa watoto wetu hawaelewi kabisa,
leo Mahindi/ makande /unga ni 1,500/ kwa kilo tumeambiwa tusimuingilie Mkulima kupanga bei
wao wanataka mapene ya kununua simu, laptop nk
Waziri na Bodi ya Mikopo safari hii wanachuja haswa
acheni kuvaa milegezo na Tunner bul
 
Mama hafahamu mwenye njaa haogopi kufa,kwani hata njaa itamuua.

Kuna muda nawaza hawa watu wamesomeshwa na mission nini??Hawajui njaa kabisa.

Tuliopitia huu msoto kipindi kile tunaelewa.View attachment 1295151

Sent using Jamii Forums mobile app
Ummy mwalimu, Waziri wa Afya ni jembe. Huyu Prof, sijajua amesomea nini na alipatikana wapi. Hajaweza kumsaidia Mh Rais kwenye sekta ya elimu hata kidogo.aondolewe tu. Mitaala inayotumika vyuo vikuu na shule zote Tanzania haoni kuwa haiendani na soko la ajira hata kidogo, amekaa tu Wala hajaweza kuitafsiri Sera ya Tanzania ya viwanda.

Wala hajiulizi wasomi wanaomaliza kila siku vyuoni wanakwenda wapi Wala kufanya Nini huko duniani.Hajiulizi mikopo ya elimu ya juu inatolewa italipwaje iwapo wasomi waliokopeshwa hawatapata kazi.

Kwa ujumla wake huyu mama kiti alichopewa kukikalia sio saizi take hata kidogo. Ajifunze kwa Mh. Ummy Mwalimu sio Prof Ila ni jembe la kudumu.
 
Waambie Mkuu hawa watoto wetu hawaelewi kabisa,
leo Mahindi/ makande /unga ni 1,500/ kwa kilo tumeambiwa tusimuingilie Mkulima kupanga bei
wao wanataka mapene ya kununua simu, laptop nk
Waziri na Bodi ya Mikopo safari hii wanachuja haswa
acheni kuvaa milegezo na Tunner bul
Haya uliyoandika haya husiani na mada kabisa,mnakwama wapi nyie? Vijana wanateseka huku mtaani wanachuo.
Ningumu sana kuelewa kama hujawahi au ulipita chuo na wazazi wako walitelekeza mahitaji yako bila kutegemea bumu.

Unadhani mtu kutumia kitochi ndiyo kusave? Hapo tu hujui hata umuhimu wa smartphone ktk masomo yake.

Laptop unadhani ni pambo kuwa nayo chuo?
 
Haya uliyoandika haya husiani na mada kabisa,mnakwama wapi nyie? Vijana wanateseka huku mtaani wanachuo.
Ningumu sana kuelewa kama hujawahi au ulipita chuo na wazazi wako walitelekeza mahitaji yako bila kutegemea bumu.
Unadhani mtu kutumia kitochi ndiyo kusave? Hapo tu hujui hata umuhimu wa smartphone ktk masomo yake.
Laptop unadhani ni pambo kuwa nayo chuo?
huo ndio ujinga wenu, mnalazimisha kutumia smartphone na Laptop
sisi mbona hivyo vitu hatukutumia na wala mikopo hiyo haikuwepo
ni bora mrudi nyumbani kuna kazi nyingi sio mtumalizie hela na mje kukosa kazi mtake tena mradi wa chinga barabarani
km mnabisha basi ANDAMANENI KESHO
 
Waambie Mkuu hawa watoto wetu hawaelewi kabisa,
leo Mahindi/ makande /unga ni 1,500/ kwa kilo tumeambiwa tusimuingilie Mkulima kupanga bei
wao wanataka mapene ya kununua simu, laptop nk
Waziri na Bodi ya Mikopo safari hii wanachuja haswa
acheni kuvaa milegezo na Tunner bul
Inawezekana hamuwaelewi wanafunzi.Kama husomeshi tulia.Wanafunzi wamepewa mwisho wa kulipa ada ni Ijumaa na wakishindwa wa ahirishe mwaka unafikiri wafanye nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana hamuwaelewi wanafunzi.Kama husomeshi tulia.Wanafunzi wamepewa mwisho wa kulipa ada ni Ijumaa na wakishindwa wa ahirishe mwaka unafikiri wafanye nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
NAWAELEWA SANA, NA NINASOMESHA
Kuna member kawaambia tunafunga mikanda hela hakuna au zinachelewesha malipo, wapo tunaoidai Serikalini tumeambiwa tusubiri wana mipango yao tutalipwa
Wao wanfunzi ni nani wavuruge mipango ya Serikali kwanza vipaumbele
HAWAWEZI WAANDAMANE ndani ya hayo masaa 72 wataziona hizo hela
 
huo ndio ujinga wenu, mnalazimisha kutumia smartphone na Laptop
sisi mbona hivyo vitu hatukutumia na wala mikopo hiyo haikuwepo
ni bora mrudi nyumbani kuna kazi nyingi sio mtumalizie hela na mje kukosa kazi mtake tena mradi wa chinga barabarani
km mnabisha basi ANDAMANENI KESHO
Mkuu usilazimishe kisa ulitembea pekupeku wakati unasoma na watoto wako watembee ivyoivyo,kila jambo na wakati wake acha mawazo mgando na ya kishamba,yaani unacomment kabisa hapa kwa kujiamini "eti mbona sisi tulisoma bila smartphone na laptop?
Mkuu umesoma mpaka level gani na mwaka gani?

Watu wa karibu yako hasa wadogo zako nawaonea huruma sana
 
Ifike mahali wanaosomeshwa na bodi chuo kikuu wawe ni wale walopata div.1 tu na kozi zenye uhitaji wengine wasaidiwe kusoma vyuo vya ufundi ili wajiajiri,sioni sababu ya kupanga bajeti kubwa kusomesha watu wanaorudi mtaani na kulia njaa eti hawana ajira na pesa hazilipwi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi nilishawahi kuongelea kuhusu hili..tena masomo ya Arts ni wengi mno..kusomesha mtu huku ukijua hutaweza kumuajiri ni wizi..hizi hela zinazosomesha hili kundi kubwa ambalo halitasaidia jamii kwa namna yoyote ile ni bora wangewekeza kujenga facilities/vyuo vingine vya ufundi....kwa watu ambao hawajapata Division one ama two wakasomee ufundi maisha yaendelee
 
Mkuu usilazimishe kisa ulitembea pekupeku wakati unasoma na watoto wako watembee ivyoivyo,kila jambo na wakati wake acha mawazo mgando na ya kishamba,yaani unacomment kabisa hapa kwa kujiamini "eti mbona sisi tulisoma bila smartphone na laptop?
Mkuu umesoma mpaka level gani na mwaka gani?

Watu wa karibu yako hasa wadogo zako nawaonea huruma sana

Umesema ukweli mkuu...
 
Back
Top Bottom