Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Asad alipaswa tena kufukuzwa kabisa hakufaa. Mi naona hata uteuzi walikosea kumteua mtu ambaye ni fundamentalist ambaye anaamini ktk kile anachoamini yeye.

Ndiyo maana mfumo ndiyo ulimuondoa wala siyo Dkt Magufuli. Ukikumbuka kuna hela fulani nadhani zilikuwa za kitengo yeye Asad akaomba azikague wakamuambia hapana utaratibu siyo huo, akakomaa ila kaenda kusoma ripoti asubuhi hakukuta kitu hahaha. Hii habari alisimulia yeye mwenyewe.

Kikubwa Asad siwezi kumtetea ni moja ya wasomi majanga wasiokuwa na mchango wa taifa. Kila jambo lina mipaka yake, halafu kibaya kabisa akawa anatumika kupindisha report.
Pole
 
What if 1.5 zilinunua vifaa vya jeshi?

Kwani ni lazima yy ambiwe? But magu sio mjinga amtoe Kwa kuhoji 1.5 lazima kuna kitu na sio muhimu Sisi kujua, as long as mambo yameenda vizuri
Yule jamaa hakupenda ukweli alipenda majungu zaidi ndiyo maana asilimia 80% ya wateule wake walikuwa watu wa majungu majungu.
 
Magufuli hakumfukuza kazi Asaad. Alichofanya ni kutokumpa mkataba wa pili pale mkataba wa kwanza ulipoisha. Na sheria ya National Audit Act ilimruhusu Magufuli kufanya hayo. Na hiyo sheria ilitungwa na kupitishwa kabla Magufuli hajawa Rais wa JMT. Walichosema High Court ni kwamba hiyo sheria inapingana na Katiba. Hapo Magufuli kosa lake ni lipi? Hiyo sheria hakuitunga yeye mbona?
Kukiuka sheria mama(KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA 1977)
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Point of correction Magu amezikwa na cheo chake cha uraisi. Hajawahi staafu hiko cheo
 
Assad anaamini yeye yupo sahihi kuliko wengine wote, alijiona yeye ni kama boss wa nchi nzima kwa hiyo nafasi ya kuwa CAG, na kama nae angekuwa rais pengine angekuwa ni majanga zaidi na mwisho Assad nae ni mtu wa visasi.
Lakini haki imemlinda yule mtu ambaye hakupenda haki korona ilienda naye.
 
Assad ana kiburi. Huwezi kuona katiba ni supreme kuliko watumiaji wa katiba wenyewe. Kile kiburi cha Assad ni cha kishamba. Huwezi kuwa na kiburi juu ya watu ambao huwezi kuwafanya chochote NA WANAWEZA WAKABADILI HIYO KATIBA BILA KUWAFANYA CHOCHOTE. Waliokuwa wakimpa kibri wako wapi? Wamemsaidia nini? Kama kufa, kila mtu atakufa kwa wakati wake.
Kumbe wew ni mpumbavu,hivi kati ya Rais na Katibu ni nini SUPREME? Katiba imemweka rais lakini rais hawezi kuiweka katiba,Katiba ni Jamhuri,Rais ni Taasisi inayolindwa na Katiba.Ndiyo maana tunabishana sana kwa sababu watu bado tongotongo za ujinga hazijaisha.Bila hivyo kusingekuwa na uchaguzi kama Katiba iko chini ya Rais.
 
Assad ana kiburi. Huwezi kuona katiba ni supreme kuliko watumiaji wa katiba wenyewe. Kile kiburi cha Assad ni cha kishamba. Huwezi kuwa na kiburi juu ya watu ambao huwezi kuwafanya chochote NA WANAWEZA WAKABADILI HIYO KATIBA BILA KUWAFANYA CHOCHOTE. Waliokuwa wakimpa kibri wako wapi? Wamemsaidia nini? Kama kufa, kila mtu atakufa kwa wakati wake.
Na amekufa kweli kwa ushamba wake lakini Assad yupo anatamba mtaani na wakati wowote ule anaweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Prof Assad hakufukuzwa kimakosa. Prof. Assad ni jeuri. Prof. Assad alimshutumu Magufuli kwamba alipokuwa Waziri wa Ujenzi aliuza nyumba za serikali kiholela. Shutuma hizo alizitoa(mara tu) BAADA ya Magufuli kuchaguliwa kuwa mgombea urais. CCM kwa tuhuma hizo ingeweza kubatilisha uteuzi wa Magufuli bila lawama kutoka kwa mtu yoyote. Lakini CCM haikufanya hivyo. Kwa hiyo Prof. Assad amecheza kamari ameshindwa. Ashukuru kwamba kichwa chake bado kipo juu ya shingo lake.
Kama anaendelea na rufaa, I am not complaining. Lakini lazima tuwafunfishe watu waache kuwa reckless.
Unaweza kuleta criticism ukawa quite correct. Lakini lazima ujiulize kama hayo mambo ungeweza kuyasema ungekuwa na Rais kama Kagame au Rais kama Putin?
Pumbavu.
 
Jitu kwa kukosa maarifa linamtetea Magufuli, tuonyeshe basi kivipi hakuvunja katiba- hawezi. Eti oooh mzalendo, wapi pameandikwa ukiwa mzalendo ruksa kuvunja katiba
Jina unalotumia ndio linalifanya uwe zuzu kwa kiwango cha juu..hukumu ya hao majaji bado imekaa kisiasa sana..
"Kama kuondolewa kwa Assad kulikiuaka katiba iweje Uteuzi wa "Kichere uwe halali"?

Tuna wanasheria waoga na wahovyo mnoo ndani ya nchi hii..CAG anayekuwa kwa vipindi na sio mfalme...
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Aliyemuonea ashitakiwe na amlipe haki zake
 
Jitu kwa kukosa maarifa linamtetea Magufuli, tuonyeshe basi kivipi hakuvunja katiba- hawezi. Eti oooh mzalendo, wapi pameandikwa ukiwa mzalendo ruksa kuvunja katiba
Kutokupandisha madaraja na kuwanyima ongezeko la mishahara kila mwaka watumishi wa umma kumeathiri maisha yao, nawashangaa watumishi kutokudai haki zao za kisheria ikibidi aliyesababisha alipe hata kwa kupiga mnada mali zake.
 
Unajua maana ya kiapo cha SITO TOA SIRI?

sasa Kwa mfano mtu anataka kuhatarisha usalama wa taifa zima unataka bado awepo Tu just because akitolewa katiba inavunjwa?

Kuna mambo mengi zaidi viongozi wanafanya Kwa ajili ya manufaa ya wanainchi
Kusema kuna udhaifu wa bunge kunavujisha siri gani za serikali?
 
Wewe mataga uliwezaje kubadilika nyuzi 180 na upepo mpya??!
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
 
Mzalendo Assad amepitia misukosuko mingi sana kutoka kwa "wenye nchi" kwa kutimiza wajibu wake tu.
Mahojiano yake kule New York niliyasikia vizuri tu. Na ndicho kilichowakera wanaojiona wenye nchi. "IKIWA SISI (CAG) TUMEONYESHA UBADHIRIFU SERIKALINI NA HATUA HAZIKUCHULIWA BASI UTAKUWA NI UDHAIFUWA BUNGE" Kwani sisi kazi yetu ni kuionyesha bunge, na bunge ndiyo inaichukulia hatua serikali kikatiba. Sasa hapa kosa la Asad lilikuwa wapi ?!

Na kama ni hizo fedha za kitengo ndiyo ilikuwa ni tatizo. Ujue ndiyo kichaka cha ubadhirifu. Kutumia kodi za wananchi bila kulitolea maelezo ni ufisadi ule ule. Kitengo lazima kiwe adilifu ili kutoa mfano. Siyo kichaka cha kufichia matumizi mabaya serikalini.
 
Hukumu imetoka 2022.

Rejea nilichoandika mbali ya kuhoji nimesema kusikilizwa na kutolewa hukumu. Toka January 2020 hukumu imekuja kutolewa 2022. Inamaanisha ilichimbiwa chini ya uvungu.

Dhamira sio kumkandamiza Magufuli hapa hivyo hifadhi utetezi wako. Magufuli alikuwa muhanga (nasema muhanga sababu ya kupewa nguvu kubwa na katiba kupelekea makosa aliyofanya) wa madaraka makubwa kiasi cha kutia dosari dhamira yake njema ya uzalendo.

Endapo kungekuwa na katiba stahiki ambayo ingeweza kum control Magufuli kwa hakika angefanya makubwa zaidi pasikuwa na kasoro.

Nguvu nyingi humpa hata aliye muungwana kiburi.

Point sio Magufuli bali nguvu kubwa aliyopewa yeye, waliomtangulia na waliopo sasa na katiba iliyopo.
Katiba inatoa freedom of expression sasa ni wapi Professor Assad alivunja katiba?
 
Back
Top Bottom