Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Kama hutaki kosolewa ongoza familia yako na co nchi,huyo kiongozi wa familia akizinguwa anapewa za uso itakuwa wa nchi????
Jitahidi kutokuwa mjinga hasa ktk umr uliofikia ucje kufa nao

Nyie ndio mliingia jf bila kusoma umri wa kujiunga
 
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi

Rais ndio mtu wa kwanza anaye takiwa kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi.
Sasa Kiongozi wa juu akivunja katiba hawa wa chini watafanyaje? siwata inyea kabisa!!

Kulinda na kuifuata katiba sio jambo la hiari ni lazima.

kuheshimu utawala wa sheria na kulinda haki za binaadamu.
 
Magufuli alikuwa na uchungu kweli na maendeleo ya hii nchi. Shida ni pale alipoamini kuwa ni yeye pekee alikuwa anajua kila kitu. Ule ulikuwa ni ubinafsi.
Aheri ubinafsi wenye manufaa kwa Taifa,badala ya Ushirikiano wa kulifilisi Taifa!

Magufuli alikuwa mwiba wa kikundi hiki kilichorudi kwa kasi kuendeleza ufilisi wa nchi hii.
 
Prof asad yupo. Ila yule kakufa zake
Na kwani huyo Assad atabaki milele?

Unaweza jua ni nani kati yako na yeye atamtangulia mwenzake?

Mawazo ya cheti fake utayajua kwa urahisi sana!
 
Unajua maana ya kiapo cha SITO TOA SIRI?

sasa Kwa mfano mtu anataka kuhatarisha usalama wa taifa zima unataka bado awepo Tu just because akitolewa katiba inavunjwa?

Kuna mambo mengi zaidi viongozi wanafanya Kwa ajili ya manufaa ya wanainchi
Kati ya hayo mengi unaweza kuyataja machache mkuu!?

Kama huyajui basi acha kufikiri kwa hisia
 
Kesi km hizi zinatakiwa hikumu itolewe mapema ili haki itendeke, sasa mgoni wako hayupo ndiyo unavua shati upigane ni upumbavu mtupu.Walimuogopa sana yule jamaa.
 
Hiyo kesi ilifunguliwa na nani mahakamani?

Nani pia wanufaika wa kesi hii?

Lengo la kesi likikuwa nini?

Wengi pia walitenguliwa pengine bila kufuata utaratibu, mbona kimya hakuna kesi kuwahusu?

Asad yeye ni nani hasa mpaka kesi ifunguliwe?

Namna alivyoondoka Ndugai nfivyo alivyoondoka Asad na wengine wengi kabla ya hawa, nini cha mno, mpaka Asad anahangaika huku na huku? Je ni uroho wa madaraka, je ni roho ya kisasi na kutotaka mambo yapite na kuzikwa kwenye kaburi la sahau ama ni mtazamo wenye kiburi wa kujiona na kudhani yeye ni mtu safi, mkamilifu na huwa hakosei!? Ushauri ambao narudia tena kwa Asad, yaliyotokea yametokea, kile kipindi na ile mandhari na hadhira haitokuwepo tena, ni ksma harusi ikisheherekewa ukumbini lile tukio na hadhira ile ile haitorudia tena. Inakuwa historia. Hata kama kuna jambo liliharibika hakuna wa kulinyoosha. Inabaki historia, labda cha muhimu ni kujaribu kufikiria namna ya kuboresha. Asad aache kuhangaika na yaliyopita kwa maana kusamehe na kusahau kuna mpa faida sana yule anayefanya hivyo, kuliko yule anayesamehewa.
Pia Assad anavyong'ang'ana na yaliyo pita ni kana kwamba anataka kujiinua na kutaka utukufu na sifa kutoka kwa wanadamu, ili yeye aonekane ni msafi na muadilifu na asiye na mawaa yoyote. Kumbe hayo yote ni ubatili. Mwenyezi Mungu anawahesabia waja wake haki hata wasipopigania haki. Yeye huona mpaka ndani ya mioyo yetu.
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Watanzania tunataka kujua SINGASINGA jambazi ameachiwa huru na Samia kwa katiba na sheria gani ? Pia ununuzi wa mabehewa ya mitumba tena kwa bei kubwa sawa na bei ya mabehewa mapya ni sheria gani SAMIA KATUMIA
 
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida.
HAPA NA..!!

Sheria hutenguliwa kwa sheria nyingine...

Kwa hili hakukuwa kwa national interests bali ilikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka ya u - Urais kwa Magufuli..

And by all means elewa kubwa ni KOSA LA UHAINI kwa kiongozi yeyote awe Rais au Waziri ama nani kuvunja na kukiuka kiapo cha kuilinda katiba ya nchi..!!
Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa..
It doesn't matter alikuwa na kosa gani. Katiba imetanabaisha clearly namna ya kumwondoa ktk cheo cha kikatiba kiongozi yeyote..

Vyeo vya kikatiba ni kama Rais mwenyewe, CAG, PM, Majaji wa mahakama kuu & rufaa nk nk..

Hawa wamewekewa utaratibu maalumu namna ya kuwaondoa ktk nafasi zao iwapo imelazimika kwa sababu ya makosa mbalimbali..

Mathalani Rais utaratibu wake ni kupitia Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani maarufu kwa kiingereza kama impeachment...

Ni kosa la uhaini kutaka kumwondoa Rais nje ya utaratibu huu. Rais Magufuli naye alifanya kosa kumwondoa CAG Assad bila kufuata utaratibu wa kikatiba hata kama kwa mtazamo wake aliona kosa kwake...
And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
Kosa la CAG Assad ni kuhoji uhamishaji wa fedha za umma kwenda kusikojulikana usiozingatia utaratibu wa kibajeti eti tu kwa sababu Rais kataka....

We don't go that way...!

Na hii ilitokea kwenye zile 1.5trn. Hili lilimchanganya sana John P. Magufuli akawa kama mwehu wa kuuliza hadharani "eti wewe fulani hujui ziliko 1.5trn...??"

Loooh..!! Hiyo ilikuwa kali kwelikweli. Mwisho wa siku jibu likawa, ASITUZINGUE HUYU, TUMTUPE NJE NA TUWEKE MTU WETU TU...!
 
Unajua maana ya kiapo cha SITO TOA SIRI?

sasa Kwa mfano mtu anataka kuhatarisha usalama wa taifa zima unataka bado awepo Tu just because akitolewa katiba inavunjwa?

Kuna mambo mengi zaidi viongozi wanafanya Kwa ajili ya manufaa ya wanainchi
Zipo njia sahihi za kudeal na mtu anayehatarisha usalama. Sio kwa staili ile. Hivi rais akihatarisha usalama tunamshughulikiaje?? Au tunamuachia Mungu ashughulike nae kama alivyofanya kwa Magu!
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu,Rushwa ni adui wa haki Mungu alishakataa,Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu kwa manufaa yangu na jamii inayonizunguka na Binadamu wote ni sawa mbele ya sheria(Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Ibara ya 12 na 13)
 
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
Yule alivunja Katiba kwa Benefits zake hasa kuifanya Chato kuwa makao makuu ya nchi.
 
Hukumu imetoka 2022.

Rejea nilichoandika mbali ya kuhoji nimesema kusikilizwa na kutolewa hukumu. Toka January 2020 hukumu imekuja kutolewa 2022. Inamaanisha ilichimbiwa chini ya uvungu.

Dhamira sio kumkandamiza Magufuli hapa hivyo hifadhi utetezi wako. Magufuli alikuwa muhanga (nasema muhanga sababu ya kupewa nguvu kubwa na katiba kupelekea makosa aliyofanya) wa madaraka makubwa kiasi cha kutia dosari dhamira yake njema ya uzalendo.

Endapo kungekuwa na katiba stahiki ambayo ingeweza kum control Magufuli kwa hakika angefanya makubwa zaidi pasikuwa na kasoro.

Nguvu nyingi humpa hata aliye muungwana kiburi.

Point sio Magufuli bali nguvu kubwa aliyopewa yeye, waliomtangulia na waliopo sasa na katiba iliyopo.
Mbona wenzie hawakufanya kama yeye pamoja na kuwa Katiba mbovu.
 
Back
Top Bottom