Baada ya Mahakama kuu kutoa Hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Asad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba katiba ilivunjwa, Viongozi katika maeneo mbalimbali ya Serikali mnajifunza nini?!
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Asad kuondolewa katika nafasi Ya CAG;
Kwanza baada ya Hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Asad, nilivuta picha ya siku Prof. Asad alipokabidhi Ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka!!
Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.
Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za Serikali acheni kuwaonea walio chini yenu kwani malipo ni hapahapa duniani, lazima utadhalilika.
2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa walio chini yetu.
3. Cheo ulicho nacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.
4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.
Ushauri;
Prof. Asad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT.