Inasikitisha kuwa Assad alionewa lakini inasikitisha zaidi kuwa watu walishindwa kuhoji chochote kipindi cha Magufuli. Nina yakini kama Magufuli angekuwa hai leo hii, achilia mbali hukumu hata hiyo kesi isingesikilizwa.
Kama taifa tuna kubwa la kujifunza juu ya mustakabali wa maisha yetu. Ikiwa mahakama ambayo ni muhimili unaojitegemea unashindwa simamia haki kwa kuogopwa mtu mmoja, tujiulize wangapi walihukumiwa/waliwajibishwa pasi kuwa na hatia.
Kuna kina Assad wengi wataendelea kuwepo kupitia tawala zote zijazo endapo katiba haitobadilishwa. Mamlaka ya raisi yamekuwa makubwa mno kiasi cha kujisahau nae ni binadamu.