Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.


Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake ya CAG.
 
Inasikitisha kuwa Assad alionewa lakini inasikitisha zaidi kuwa watu walishindwa kuhoji chochote kipindi cha Magufuli. Nina yakini kama Magufuli angekuwa hai leo hii, achilia mbali hukumu hata hiyo kesi isingesikilizwa.

Kama taifa tuna kubwa la kujifunza juu ya mustakabali wa maisha yetu. Ikiwa mahakama ambayo ni muhimili unaojitegemea unashindwa simamia haki kwa kuogopwa mtu mmoja, tujiulize wangapi walihukumiwa/waliwajibishwa pasi kuwa na hatia.

Kuna kina Assad wengi wataendelea kuwepo kupitia tawala zote zijazo endapo katiba haitobadilishwa. Mamlaka ya raisi yamekuwa makubwa mno kiasi cha kujisahau nae ni binadamu.
 
Baada ya Mahakama kuu kutoa Hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Asad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba katiba ilivunjwa, Viongozi katika maeneo mbalimbali ya Serikali mnajifunza nini?....

Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
 
Inasikitisha kuwa Assad alionewa lakini inasikitisha zaidi kuwa watu walishindwa kuhoji chochote kipindi cha Magufuli. Nina yakini kama Magufuli angekuwa hai leo hii, achilia mbali hukumu hata hiyo kesi isingesikilizwa...
Hii kesi Zitto aliifungua January 2020. Sasa unaposema angekuwepo Magufuli wasingehoji unamaanisha nini?
 
Hii kesi Zitto aliifungua January 2020. Sasa unaposema angekuwepo Magufuli wasingehoji unamaanisha nini?
Hukumu imetoka 2022.

Rejea nilichoandika mbali ya kuhoji nimesema kusikilizwa na kutolewa hukumu. Toka January 2020 hukumu imekuja kutolewa 2022. Inamaanisha ilichimbiwa chini ya uvungu.

Dhamira sio kumkandamiza Magufuli hapa hivyo hifadhi utetezi wako. Magufuli alikuwa muhanga (nasema muhanga sababu ya kupewa nguvu kubwa na katiba kupelekea makosa aliyofanya) wa madaraka makubwa kiasi cha kutia dosari dhamira yake njema ya uzalendo.

Endapo kungekuwa na katiba stahiki ambayo ingeweza kum control Magufuli kwa hakika angefanya makubwa zaidi pasikuwa na kasoro.

Nguvu nyingi humpa hata aliye muungwana kiburi.

Point sio Magufuli bali nguvu kubwa aliyopewa yeye, waliomtangulia na waliopo sasa na katiba iliyopo.
 
Baada ya Mahakama kuu kutoa Hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Asad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba katiba ilivunjwa, Viongozi katika maeneo mbalimbali ya Serikali mnajifunza nini?...
Asad alipaswa tena kufukuzwa kabisa hakufaa. Mi naona hata uteuzi walikosea kumteua mtu ambaye ni fundamentalist ambaye anaamini ktk kile anachoamini yeye.

Ndiyo maana mfumo ndiyo ulimuondoa wala siyo Dkt Magufuli. Ukikumbuka kuna hela fulani nadhani zilikuwa za kitengo yeye Asad akaomba azikague wakamuambia hapana utaratibu siyo huo, akakomaa ila kaenda kusoma ripoti asubuhi hakukuta kitu hahaha. Hii habari alisimulia yeye mwenyewe.

Kikubwa Asad siwezi kumtetea ni moja ya wasomi majanga wasiokuwa na mchango wa taifa. Kila jambo lina mipaka yake, halafu kibaya kabisa akawa anatumika kupindisha report.
 
Back
Top Bottom