Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
 
KATIBA MPYA NDIO SULULISHO, tusipende kujifanya kama tatizo halipo
Hata hiyo mpya wakubwa wataivunja na hakuna cha kuwafanya. Hakuna katiba itakayokuja kutungwa kudhoofisha mamlaka ya Rais. Wanaodhani hivyo wanaota ndoto za Alinacha na kuwa na hekaya za Abunuasi.
 
Kwel ujinga mzigo mzto
Asad alipaswa tena kufukuzwa kabisa hakufaa. Mi naona hata uteuzi walikosea kumteua mtu ambaye ni fundamentalist ambaye anaamini ktk kile anachoamini yeye.

Ndiyo maana mfumo ndiyo ulimuondoa wala siyo Dkt Magufuli. Ukikumbuka kuna hela fulani nadhani zilikuwa za kitengo yeye Asad akaomba azikague wakamuambia hapana utaratibu siyo huo, akakomaa ila kaenda kusoma ripoti asubuhi hakukuta kitu hahaha. Hii habari alisimulia yeye mwenyewe.

Kikubwa Asad siwezi kumtetea ni moja ya wasomi majanga wasiokuwa na mchango wa taifa. Kila jambo lina mipaka yake, halafu kibaya kabisa akawa anatumika kupindisha report.
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.


Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Nilicho jifunza kikubwa ni kwamba Mahakama zinatakiwa zitoe maamuzi wakati Muhusika/culprit yupo Hai.
 
Nilidhan watumia logic kumbe kuna chuki za kidin????pole sana
Wewe ndo jitu usiejua Zito na Asaadi walikuwa na ajenda gani kuhusu Magufuli.Zito na Asaadi na mambo yao ya udini ndo yanasumbua.Na kama Zitto na Asaadi walivyowadini walikuwa na ajenda mbaya sana na mpaka leo inaendelea.Hii ajenda inaanzia kwa Asaadi alipokuwa mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma na kuasisi migogoro ya kidini ikiwemo kutaka kujengwa msikiti maeneo ya chuo na Magufuli ndio aliyekuwa rais wa kwanza kupinga taasisi za dini kujiingiza katika maeneo ya taasisi za elimu za serikali badala yake watumie madarasa yaliyopo kufanya ibada then mambo mengine yaendelee.Sasa katika kujibu mapigo Asaadi akatumia cheo Cha CAG kujibu mapigo kwa taarifa za kizushi kwa kumtumia Zito ila JPM akawashtukia mapema akampinga chini Asaadi ndo maana hadi leo Zito bado anaangaikaKama sio udini baada ya hii kesi au akamuunge mkono Mbatia kuendeleza kesi kwanini Ndugai avuliwe usipika bila kufata katiba
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana

Ww umekaa zako buza huko na kifurushi cha jero na msamart kitochi chako unataka kujifanya unataka uambiwe kila kitu, ww Nani?

Baba yako mwenyewe akwambii kila kitu sembuse serikali
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu
Assad ana kiburi. Huwezi kuona katiba ni supreme kuliko watumiaji wa katiba wenyewe. Kile kiburi cha Assad ni cha kishamba. Huwezi kuwa na kiburi juu ya watu ambao huwezi kuwafanya chochote NA WANAWEZA WAKABADILI HIYO KATIBA BILA KUWAFANYA CHOCHOTE. Waliokuwa wakimpa kibri wako wapi? Wamemsaidia nini? Kama kufa, kila mtu atakufa kwa wakati wake.
 
Magufuli hakumfukuza kazi Asaad. Alichofanya ni kutokumpa mkataba wa pili pale mkataba wa kwanza ulipoisha. Na sheria ya National Audit Act ilimruhusu Magufuli kufanya hayo. Na hiyo sheria ilitungwa na kupitishwa kabla Magufuli hajawa Rais wa JMT. Walichosema High Court ni kwamba hiyo sheria inapingana na Katiba. Hapo Magufuli kosa lake ni lipi? Hiyo sheria hakuitunga yeye mbona?

..kosa la Magufuli ni kutumia sheria inayopingana na katiba.

..hata kama alishauriwa vibaya bado maamuzi ni ya kwake.

..nchi inakwenda kuingia hasara kwa makosa aliyoyafanya.
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Prof Assad hakufukuzwa kimakosa. Prof. Assad ni jeuri. Prof. Assad alimshutumu Magufuli kwamba alipokuwa Waziri wa Ujenzi aliuza nyumba za serikali kiholela. Shutuma hizo alizitoa(mara tu) BAADA ya Magufuli kuchaguliwa kuwa mgombea urais. CCM kwa tuhuma hizo ingeweza kubatilisha uteuzi wa Magufuli bila lawama kutoka kwa mtu yoyote. Lakini CCM haikufanya hivyo. Kwa hiyo Prof. Assad amecheza kamari ameshindwa. Ashukuru kwamba kichwa chake bado kipo juu ya shingo lake.
Kama anaendelea na rufaa, I am not complaining. Lakini lazima tuwafunfishe watu waache kuwa reckless.
Unaweza kuleta criticism ukawa quite correct. Lakini lazima ujiulize kama hayo mambo ungeweza kuyasema ungekuwa na Rais kama Kagame au Rais kama Putin?
 
..kosa la Magufuli ni kutumia sheria inayopingana na katiba.

..hata kama alishauriwa vibaya bado maamuzi ni ya kwake.

..nchi inakwenda kuingia hasara kwa makosa aliyoyafanya.

Hasara ya Aina gani.? Umesoma report mzima ya kesi..?
 
Kama dhaifu ni dhaifu tu hata uwe mfalme,vp zile mbwembwe zake zipo tena yule mbilikimo wa Kongwa?????
upumbavu aliokuwa akiufanya asad hata rais angekuwa kichaa namna gani asing mvumilia yaani yeye ndiyo alikuwa anajiona kidume mtenda haki anayejuwa kila kitu unawezaje kumuita hata spika eti ni dhaifu yaani upumbavu mtupu ni sawa na baba wa familia aje mtu akuambie mbele ya familia yako wewe ni mpumbavu nani anaweza kuvumilia kama siyo kumpatia ndoige za kutosha huyo mpuuzi aende tu shamba akalime alichezea shilingi chooni
 
Kama hutaki kosolewa ongoza familia yako na co nchi,huyo kiongozi wa familia akizinguwa anapewa za uso itakuwa wa nchi????
Jitahidi kutokuwa mjinga hasa ktk umr uliofikia ucje kufa nao
Ww umekaa zako buza huko na kifurushi cha jero na msamart kitochi chako unataka kujifanya unataka uambiwe kila kitu, ww Nani?

Baba yako mwenyewe akwambii kila kitu sembuse serikali
 
Hasara ya Aina gani.? Umesoma report mzima ya kesi..?

..tumbua-tumbua ina hasara zake ambazo Watz hatukuelezwa.

..kwa mfano, ukimteua mtumishi kuwa katibu mkuu wa wizara, halafu ukamtumbua, mtumishi huyo huendelea kupokea mshahara wa katibu mkuu mpaka atakapostaafu.

..hasara ninayoiona mbele yetu ni ya serikali kulazimika kulipa mshahara kwa CAG wawili.
 
Back
Top Bottom