Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Mbona uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo namna hii!!!

Hapo no need ya uchambuzi ni Jambo simple la kuelewa

Ndio maana hata rais aliwahi kusema Jambo wanaloamua viongozi au kwenye baraza la mawaziri ni lao wote, hakuna kujitenga

Ww Una uwezo mkubwa wa kuchambua mambo but hauna uwezo mkubwa wa kuelewa
 
Mahakama imerule kuwa jiwe alivunja katiba
Wewe unatetea nini sasa!!!
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Sidhani kama kuna funza maana matukio ya uvunjifu wa katiba na sheria hayajaanza leo na hayataisha na bado watanzania tunaona ni sawa tu, mbaya zaidi bunge halina meno,ni wazee wa zidumu fikra za mwenyekiti
 
Kama Mahakama imetamka kuwa katiba ilikiukwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022, lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.
Kwahiyo kwa sasa tuna CAG wawili!?
 
Huwezi kwenda Marekani kulisema bunge letu eti ni dhaifu alafu wewe ukajibatiza eti ni muhimili na bado Magufuli akakuangalia tu.
Ila ukweli kuna hizi sheria zilizopitishwa na jungu kuu ni ngumu kumeza
1. Mf: umpe dereva lori apeleke mzigo zambia, wakati anarudi apakie mkaa, hukumu yake ni Lori litaifishwe kweli? kwa hiyo unahukumu gari badala ya mtenda kosa
2. Hiyo ni sawa na uajiri Daktari atoe dawa isiyo sawa; hukumu yake iwe kutaifisha hospitali
au Mwalimu aliyeajiriwa afanye kosa, hukumu yake iwe kutaifishwa Shule?

Hapo nimegusa moja tu; Mungu tuhurumie
 
Kws hiyo Zitto alikwenda mahskamani kwa ajiri ya nini?
Zitto alishamwambia Assad kuwa asingefanywa chochote na ndicho alichotafuta mahakamani. Hivi wewe uliwahi kusikia hii kesi imefunguliwa wapi na ilizungumzwa lini na mashahidi waliitwa lini na ndio hukumu ikatolewa? Kulikuwa na usiri mkubwa sana kwenye hii kesi naifananisha na ile ya Richmond ambayo ni wazi serikali ilitaka ishindwe.
 
..kosa la Magufuli ni kutumia sheria inayopingana na katiba.

..hata kama alishauriwa vibaya bado maamuzi ni ya kwake.

..nchi inakwenda kuingia hasara kwa makosa aliyoyafanya.
Hiyo sheria inayopingana na katiba ilianza kutumika kabla Magufuli hajawa rais
 
... Mahakama ya juu ime-rule out kwamba Katiba ya Jamhuri ilivunjwa; wewe unatuletea porojo! Uko smart upstairs kisheria kuliko jopo la majaji watatu wa High Court waliofikia uamuzi huo? Sheria ikipingana na Katiba nini kinatakiwa?
Hii kesi iliendeshwa kisirisiri sana . Kumbe ni jopo la majaji watatu walitoa huo uamuzi?
 
Hiyo sheria inayopingana na katiba ilianza kutumika kabla Magufuli hajawa rais

..Ccm wametengeneza matobo mengi kwenye sheria na katiba ili waweze kutekeleza uovu wao.

..Ni kweli sheria hiyo iliandikwa kabla Magufuli hajaingia madarakani, lakini bado aliwajibika kuiepuka kwasababu iko kinyume na katiba.

..Kwa maoni yangu, aliyekuwa Waziri wa Sheria Prof.Kabudi, na aliyekuwa AG Prof.Kilangi, wanastahili lawama kubwa zaidi kwa kushindwa kumshauri na kumuongoza Rais Magufuli ktk suala hili.
 
[QUOTE="Midimay, post: 44533694,Kama kufa, kila mtu atakufa kwa wakati wake.[/QUOTE]

Shida ipo kwa anayetangulia.

Ila wafu hawajui lolote linaloendelea kwenye maisha waliyoyaacha.
 
Kwahiyo kwa sasa tuna CAG wawili!?
Hapana CAG ni mmoja tu ambaye ni Prof. Asad kwa mujibu wa katiba.

uteuzi ulio fanywa kwa CAG mwengine bila kuzingatia utaratibu ni "batili tangu alipo teuliwa".
 
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Mkuu mahakama siyo mama yako
1. Aliye fungua mashtaka hakuomba Assad arudishwe; yeye aliomba mahakama itamke kuwa kuondolewa kwake kulivunja katiba
2. Kama ilivyoombwa mahakama imesema kuondolewa kw Assad kulivunja katiba
 
Baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu yake na kubaini kuwa Prof. Assad aliondolewa katika nafasi yake ya CAG kimakosa, kwamba Katiba ilivunjwa, viongozi katika maeneo mbalimbali ya serikali mnajifunza nini?

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika sakata la Prof. Assad kuondolewa katika nafasi ya CAG;

Kwanza baada ya hukumu ya Mahakama Kuu kutamka kuwa katiba ilivunjwa kumuondoa CAG Assad, nilivuta picha ya siku Prof. Assad alipokabidhi ofisi na kubeba kilicho chake kweye gari yake ndogo na kisha kuondoka! Picha ya siku ile ilinihuzunisha sana na ilionesha kuwa kulikuwa na uonevu na udhalilishaji mkubwa.

Jambo la kujifunza;
1. Viongozi mliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali ya taasisi za serikali acheni kuwaonea waliyo chini yenu kwani malipo ni hapahapa Duniani, lazima utadhalilika.

2. Tuache uonevu na unyanyasaji kwa waliyo chini yetu.

3. Cheo ulichonacho leo ni dhamana tu huwezi kuzikwa nacho, watendee mema walio chini yako.

4. Tuheshimu katiba na sheria za nchi.

Kama Mahakama imetamka kuwa katiba/sheria hazikufuatwa wakati wa kumtoa kwenye nafasi yake maana yake hadi sasa hivi tunapo jadili hoja hii Prof. Asad ni CAG.

labda atenguliwe kuanzia sasa hivi/leo hii trh 6/12/2022 (kwa kuzingatia katiba) lakini kutokana na Hukumu ya Mahakama ni wazi kabisa CAG ni Prof. Asad.

Ushauri:
Prof. Assad arudishwe kwenye nafasi yake au apewe nafasi ya juu zaidi, ikiwezekana awe hata Gavana wa BOT kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.
Mtu aliyewahi kushika nafasi ya CAG hawezi kushika Madaraka mengine ya Umma
 
Back
Top Bottom