Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,413
- 31,403
Tume ya Nyalali ilisema '' ni lazima kwanza kuwe na Tume huru ya uchaguzi na kuandikwa katiba mpya''. ACT wanakubali mambo hayo yanaenda sambamba!Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Jeshi la Polisi linaingiaje kwenye mambo ya siasa? Kazi ya jeshi ni kusimamia sheria za nchi.Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!
''Kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika''. Kule Zanzibar kumefanyika miafaka mingapi na hali ipoje leo hii. Kuna utayari gani kwa CCM waliopora chaguzi! utayari wanaozungumzia ACT ni upi huo
ACT wanaamini kukiwa na Tume huru basi Wabunge watachaguliwa kwa uhuru.Tunaanza na Tume Huru!
Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;
1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.
Hapa ndipo ninapoona ACT wana tatizo la kufikiri. Hivi si waliwahi kuwa na Tume huru Zanzibar?
Kwa mamlaka gani Jecha aliharibu uchaguzi alioshinda Maalim?
ACT hawakumbuki Jecha aliondolewaje, alipelekwa wapi na aliamriwa aseme nini?
Tume huru haina uhusiano na uhuni unaofanywa. Mtu akiporwa Form si tatizo la tume ni uvunjaji wa sheria na wahusika ni Polisi. Hujuma za mawakala si tatizo la tume ni uratibu wa CCM, Polisi na vyombo vya usalama.2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.
Tunarudi pale pale kwamba wao wanaamini uchaguzi unahujumiwa na Tume. Hawana habari kuwa uratibu wa hujuma za uchaguzi ni wa mfumo mzima.3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.
Kule kule wanaamini Tume huru itamaliza tatizo la uhuni. Hawakumbuki Jecha alifanya nini kwa msaada wa nani na kwanini hakukuwepo na hatua dhidi yake. Si Jecha alikuwa na Tume huruiliyowashirikisha CUF ambao ni ACT4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.
Katiba pendekezwa iliandikwa na CCM, kusema kwamba maoni ya Tume ya Warioba yachanganywe na uhuni wa CCM ni ku adulterate maoni ya Wananchi.ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.
ACT Katiba pendekezwa ni mali ya CCM. Wananchi wanataka kurudi ktk Tume ya Warioba
Kumbe tayari kuna sheria imeandaliwa!!Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?
1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.
Kwanini Rais awe na mkono wa uteuzi? Rais anatakiwa aidhinishe jina. Rejea tume ya uchaguzi ya Ghana. Rais hana mamlaka yoyote ya kuteua majina au kupewa lundo la ma3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.
Forget about katiba pendekezwa. Turudi kwa Rasimu ya Warioba.Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.
ACT hii katiba pendekezwa iliandikwa na CCM
ACT katiba pendekezwa iliandikwa na CCM na haihitaji maboresho yoyote. Hii ilifuta maoni ya Tume ya Warioba ambayo ni maoni ya wananchi. Katiba pendekezwa si maoni ya Watanzani, ni Bunge la CCM.Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.
Ninatilia shaka uelewa wa ACT Wazalendo! kuna tatizo kubwa wanajitahidi kulisukuma mbele
Huwezi kuwa na Tume huru ya uchaguzi katika mfumo wa dhulma ACT!Hitimisho.
Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Kuna tatizo kubwa sana na nadhani kuna kitu kipo nyuma! mtakuja baini ikiwa ni too late
ACT na CCM wanaserikali ya pamoja kule Zanzibar, huku bara hatuna GNU na ACT wasijaribu kututumbukiza katika matatizo hayo. Kuna motive behind , ipo siku watu wataelewa tunamaanisha nini. Kuna kitu!