Act ndio chama gani hiki,mbona cha hovyo kiasi hicho!chama akijui hata nguvu ya rais aliyonayo kwenye tume ya uchaguz bila katiba mpya usitegemee ccm kutoka madarakani.TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI
Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.
Utangulizi.
Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.
Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.
Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.
Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?
Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!
Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!
Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!
Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?
Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.
Tunaanza na Tume Huru!
Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;
1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.
2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.
3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.
4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.
Tume Itapatikanaje?
Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.
ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.
Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?
1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.
2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.
3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.
4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.
5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.
6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.
7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.
Katiba Mpya Itapatikanaje?
Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.
Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.
Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.
Hitimisho.
Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Hawala" kingereza mnaitwa concubine wa ccm au siyo mwami?TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Tume huru utaipataje chini ya Raisi mfalme, kwanza Raisi apunguzwe nguvu, ndo tume itakuwa huruTUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Ndio maana nasema ACT wazalendo sijui kama wanajua tatizo ni nini!..tatizo haliko ktk tume ya uchaguzi peke yake.
..tatizo liko ktk MNYORORO mzima wa uchaguzi hapa nchini.
..mfumo mzima unatakiwa ufumuliwe kuanzia ktk uandikishaji wapiga kura, kuteua wagombea, kampeni, ...mpaka hatua ya mwisho.
True!..kwa maoni yangu, michakato yote miwili ianze kwa pamoja, lakini ni lazima MFUMO WA UCHAGUZI uwe umebadilishwa kwa kuboreshwa kabla ya 2024.
ACT wanafanya siasa za kuifurahisha CCM, ACT inataka ifanye siasa za kuonekana wastaarabu mbele ya CCM. Ukitazama vizuri kwa sasa, ACT inafanya siasa za Zito alizokuwa anazifanya miaka yote alipokuwa CDM. Ni vyema wapinzani wa kweli wakawa makini sana na siasa za ACT/Zito, ambazo ni za ghiliba. Wapinzani wa kweli wabaki na hoja kuu ambayo ni katiba mpya na sio kutekeleza matakwa ya CCM ya tume huru ya uchaguzi, ambayo lengo ni kuipa ACT viti kadhaa lakini CCM ikijihakikishia inabaki madarakani kwa shuruti.
Kujadili sinema za Zitto Kabwe ni kupoteza muda wenu bure.ACT ni zao la CUF chini ya hayati Maalim Seif.
Mwaka 2010 CUF na CCM walikubaliana uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa (GNU)
Walikubaliana uwepo wa TUME HURU ya Uchaguzi, iliyoundwa na Wajumbe kutoka CCM na CUF
Mwaka 2015 Tume ikiwa karibu kutangaza matokeo ambayo CUF Walishinda, Mwenyekiti Bw Jecha akabanwa na '' kuhara na kubebwa na watu maalumu kisha kupata matibabu'' TV Zanzibar akibatilisha matokeo
Serikali ya CCM na vyombo vyake vikakubali uhuni uliofanyika.
Mahakama haikuwa na nguvu, maamuzi ya Tume huru iliyokuwa na CUF hayahojiwi mahakamani.
CUF ambayo ni ACT ya leo wakapoteza uchaguzi na Maalim Seif akabaki kuwa mhanga hadi kifo
Tume huru haihakikishi uchaguzi huru. ACT wameshiriki chaguzi nyingi hawakuhujumiwa na Tum
Kazi ilifanywa na vyombo vya dola kwa baraka.ACT hawajashinda hata mtaa mmoja
Serikali za mitaa hazisimamiwi na tume! ACT hawakumbuki uhuni uliofanywa
Kama kuna kundi linalohujumu katiba mpya, ACT ni sehemu kubwa sana na muhimu ya kundi hilo
Kuna jambo la kujiuliza ikiwa ACT wanakumbukumbu, wanafikiri sawasawa au Wanatumika
JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla Matola
ACT ni CUF ya zamani, hakuna kilichobadilika. Hoja ya CUF ya Maalim ni Zanzibar yenye mamlaka kamili. Hoja hiyo ya CUF na shinikizo la CDM ndivyo vilimshinikiza JK kuanzisha mchakato wa Katiba
Mchakato wa katiba ulilenga kurekebisha mifumo ya nchi ikiwemo wa kupata Tume huru ya uchaguzi. Tume ni zao la Katiba kwani uwepo wake umeanzishwa na Katiba.
CUF ya Maalim walienda Bunge la Katiba chini ya Ukawa. Mwanasheria mkuu wa SMZ alikuwa Maosud Othman. Mwanasheria (AG) alijiuzulu kufuatia kutokubaliana na mambo ambayo serikali ya CCM iliyafanya ikiwemo kuhujumu mchakato wa katiba mpya
Masoud Othman sasa ni VP akitembea na ving'ora , ulinzi na kila faraja za uongozi, kasahau alisimamia nini na kwanini alijiuzulu kuwa AG.
Mh Masoud ambaye ni kiongozi wa ACT yeye na wenzake hawakumbuki madhila yaliyomkuta maalim Seif chaguzi nyingi ikiwemo ya CUF kuwa sehemu ya tume ya uchaguzi , Jecha akatenda
Masoud Othman kuongoza CUF kuingia makubaliano na CCM inachekesha wala haifikirishi
Kwamba lini CCM wamekuwa wema sana kwa wapinzani katika Taifa hili ?
Wale wanaohisi tu kuwa kuna kutumika na ''quid pro quo' ni ngumu sana kuwashawishi hakuna
ACT hawajiulizi ni kwa mapenzi yapi CCM wanataka Tume huru ya uchaguzi ikiwa hata mikutano hawaruhusiwi? Juzi kule Pemba Polisi wameshushwa vyeo kwa kuruhusu mikutano ya ACT, bado ACT wanadhani ipo namna tofauti na zile zilizofeli huko nyuma
Kwahili, ACT wanaharibu mchakato wa katiba, na kuna kila sababu ya kuamini lipo jambo!
Kwa mtu makini ''hesabu' za ACT Wazalendo hazieleweki kwa namna yoyoteHao Wapemba walioko ACT wameingizwa mkenge na siasa za Zito, watatumika hadi wakija kustuka muda utakuwa umekwisha.
Umesema yote mkuu,tukisema Zitto hamna kitu kichwani na yuko upande CCM,mtu wa siasa maslahi,mnakasirika.Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!
Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusika na uchaguzi mkuu.
Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi ikiwa ni pamoja na ninyi ACT wazalendo.
Wanafuata kwa sababu za udini tuHao Wapemba walioko ACT wameingizwa mkenge na siasa za Zito, watatumika hadi wakija kustuka muda utakuwa umekwisha.
ACT nyinyi ni hopeless kabisa. Utapataje tume huru ya uchaguzi bila kufumua katiba ya nchi ???Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!
Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusika na uchaguzi mkuu.
Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi ikiwa ni pamoja na ninyi ACT wazalendo.
Yan Zitto ni Yuda IskarioteTUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI