Tunaanza na Tume Huru Kwanza

Wasi wasi wa ACT ni kuwa kuna uchaguzi wa serikali za mitaa 2024. ACT wanaamini watashinda chaguzi hizo. Hivi wakipata viti 5000 dhidi ya 40,000 kuna maana gani?
ACT wanaamini kuna uchaguzi 2025 na Tume huruikiwepo watashinda. Hivi wakishinda viti 50 vya ubunge dhidi ya 200 vya CCM wataleta mabadiliko gani? Hapo si ndipo watapiga mhuri kwa CCM kufanya mauza uza yao.

Kosa la ACT ni lile walilofanya Chadema mwaka 2010. JK alitangaza kuanzishwa mchakato wa katiba mpya. CDM wakasema Rais amefanya jambo jema na Wamefarijika. Tuliwaambi kuwa hiyo si njia sahihi, mchakato ulitakiwa uanzie Bungeni ili waweze kuuratibu

Matokeo yake mchakato ukawa mali ya 'Rais' na matokeo yake tunayajua
Hilo ndilo kosa la ACT kutaka Tume huru na Wajumbe wake wapatikane kwa mazingira ya sasa

Haraka ni ya nini ACT?
Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde. Kuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.

Fatma Karume alitoa pendekezo zuri sana kuhusiana na cheo cha Spika. Kwa vile inaelekea Spika anajiona kuwa ni Rais mtarajiwa basi anaona ni muhimu ajipendekeze kwa mamlaka yenye nguvu ya kuteua mgombea urais. Fatma alishauri kuwa ili kuepukana na tamaa hizo, Katiba imzuie Spika kugombea nafasi yeyote ya kisiasa muhula wake utakapoisha.

Hii itaondoa uwezekano wa kuwa corrupted kwa ahadi ya cheo cha kisiasa. Mimi nashauri iwe hivi kwa Jaji Mkuu, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na ile ya Vyama vya Siasa. Aidha, wasimamizi wote wa uchaguzi na wakuu wa vyombo vya usalama nao wasiruhusiwe kugombea kwenye chaguzi kuu mbili baada ya kutoka kwenye nafasi yao. Kwenye uspika, iwekwe wazi kuwa sio lazima kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na mara ukichaguliwa hauruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa za chama chako ( hamna mambo ya kuwa mjumbe wa NEC n.k.).

Mheshimiwa Rais anyang'anywe pia mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao (kwa kuwapa kazi nyingine, kuwapandisha vyeo n.k) bila kutoa sababu inayoeleweka ambayo itakubaliwa na Tume itakayoundwa (kama Spika, tume iwe na maspika kutoka Jumuia ya Madola). Nadhani tukifanya hivi tutapata watumishi ambao wataweka taifa mbele na sio chama chao cha siasa.

Amandla...
 
Mimi hata siwaelewi wakina Zitto. Pamekuwa na chaguzi kiasi toka ile ya 2020 na ACT wameshiriki kikamilifu. Kama sikosei ACT wameshinda moja tu tena kwa mbinde.
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapa
Kuna chaguzi nyingine huku bara wamelalamika kufanyiwa ubabe ule ule wa 2020. Ya mwisho ndio hawakupata hata kura 200. Sasa ikiwa wanachezewa rafu katika nchi ambayo wao ni washiriki kwenye utawala nini kinawaamisha kuwa 2025 hali itakuwa tofauti? Labda kama wanategemea hisani.
Huku bara si kwamba wameshindwa tu, bali pia walipigwa sana. Hawajaambulia chochote
Hapa ndipo tunawauliza haya yote yamefanywa si kwa idhini ya Tume bali vyombo vya dola, sasa wao wanadhani Tume ina nguvu gani kubwa kuliko vyombo vya dola?

Jecha si alichukuliwa na vyombo vya dola, Tume ilifanya nini!
Ndio msingi hasa wa sisi wengine kuhoji, huko ACT Wazalendo kuna watu wanafikiri ?
Fatma Karume alitoa pendekezo zuri sana kuhusiana na cheo cha Spika. Kwa vile inaelekea Spika anajiona kuwa ni Rais mtarajiwa basi anaona ni muhimu ajipendekeze kwa mamlaka yenye nguvu ya kuteua mgombea urais. Fatma alishauri kuwa ili kuepukana na tamaa hizo, Katiba imzuie Spika kugombea nafasi yeyote ya kisiasa muhula wake utakapoisha. Hii itaondoa uwezekano wa kuwa corrupted kwa ahadi ya cheo cha kisiasa. Mimi nashauri iwe hivi kwa Jaji Mkuu, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na ile ya Vyama vya Siasa. Aidha, wasimamizi wote wa uchaguzi na wakuu wa vyombo vya usalama nao wasiruhusiwe kugombea kwenye chaguzi kuu mbili baada ya kutoka kwenye nafasi yao. Kwenye uspika, iwekwe wazi kuwa sio lazima kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na mara ukichaguliwa hauruhusiwi kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa za chama chako ( hamna mambo ya kuwa mjumbe wa NEC n.k.). Mheshimiwa Rais anyang'anywe pia mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao (kwa kuwapa kazi nyingine, kuwapandisha vyeo n.k) bila kutoa sababu inayoeleweka ambayo itakubaliwa na Tume itakayoundwa (kama Spika, tume iwe na maspika kutoka Jumuia ya Madola). Nadhani tukifanya hivi tutapata watumishi ambao wataweka taifa mbele na sio chama chao cha siasa.

Amandla...
Ni moja ya msingi mkubwa wa kuwa na katiba. Tunakumbuka Mwenyekiti wa NEC aliwahi kuchukua fomu za kugombea Urais kupitia CCM.

Kinachotakiwa ni kuwa na sheria kwamba kuna nafasi hazitaruhusiwa kugombea nafasi za kisiasa au utumishi katika serikali

Nafasi hizo ni pamoja na za Spika na Naibu wake na kwamba takayechaguliwa kuwa Spika wa bunge atakuwa amepoteza uanachama wake wa chama cha siasa na hataruhusiwa kufanya siasa tena katika maisha yake. Hii inawezekana kwa kuzingatia kuwa masilahi yao ya leo hii yanawahakikishia maisha mazuri hadi kufa

Jaji mkuu na Majaji wa Mahakama kuu wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au utumishi katika serikali kwa muda wa maisha yao yote.

Kwamba mtumishi katika ngazi ya Jaji wakimaliza muda wao wa utumishi wasiteuliwe tena katika Taasisi za Umma au serikali katika maisha yao yote.

Mwenyekiti wa NEC asiruhusiwe kuwania nafasi ya Urais au uongozi katika serikali katika maisha yake. Wajumbe wa NEC nao wapewe muda wa miaka 20 kabla ya kujiunga na siasa tena

Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wajumbe wa NEC wala uwezo wa kutengua.
Kazi ya Rais iwe kusaini majina yanayofikishwa 'vetting' kwa namna yoyote

Polisi katika ngazi za Kamishna kwenda juu wasiruhusiwe kushiriki siasa baada ya utumishi wao

Hayo ni baadhiya mambo yatakayohakikisha kuwa wale wanaoteuliwa kwa majukumu kadhaa wapo committed na nchi na hawatakuwa compromised na mambo au mtu mwingine.
 
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal , wakawapa...
Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni.

Nimeyapenda sana mapendekezo yako juu ya viongozi. Ni muhimu kukata huu mlango wa kuzunguka kati ya utendaji na siasa. Kwenye hili tuwaige waingereza sio wamarekani.

Amandla...
 
Mimi nawashangaa sana ACT. Wamepigwa, Ado Shaibu na wenzake wameswekwa ndani lakini kimya. Wanaugulia tuu maumivu yao wakitumaini ushindi Zanzibar utawapa uongozi wa upinzani Bungeni...
Kule Pemba kuna Polisi kawa demoted kwa kuruhusu mikutano ya ACT.
ACT wanaamini tatizo hilo litamalizwa kwa kuwa na Tume huru

Kinachonishangaza ni ufupi wa kumbu kumbu. Walishakuwa sehemu ya tume huru kupitia CUF. Walipokwa matokeo na Jecha na hawakumfanya lolote.

ACT wanasahau jinsi CUF ilivyouawa. Haikuwa Tume ya uchaguzi, ni ile taasisi nyingine ya vyama.
Wamepigwa sana kila uchaguzi mdogo. Hawakupigwa na Tume bali vile vyombo vyetu

ACT wanakaa na Msajili wa vyama wala hawamuulizi sheria ya kuzuia mikutano imeandikwa wapi!
Wanakaa na msajili hawaulizi kwanini kuna vyama vikitoa matamko ya mauaji havichukuliwi hatua!

ACT wanakaa na NEC hawawaulizi Wabunge 19 wapo Bungeni kwa sheria gani

Wanachoamini wao ni kuwa Tume huru itatoa haki, zile zile wanazonyimwa sasa!

ACT wajiulize hivi Othman Masoud si alikuwa mtu wa katiba ya serikali tatu, leo mbona kimya

Sidhani Zitto anayafanya haya kwa mapenzi, nadhani ACT kuwa na nguvu Zanzibar kunamweka Zitto katika wakati mgumu. Anajua wazi kinachofanyika si sahihi lakini kule si yupo Othman Masoud na ving'ora! Kelele za ving'ora zinamziba macho na masikio.

Katika sheria mbovu zilizopo na mfumo mbovu uliopo hata Tume ya uchaguzi ikiundwa na ACT/CDM/NCCR bado CCM watashinda kwa kishindo. Ndivyo walivyoshinda kule Zbar halafu wakamwambia Mbunge ajiuzulu na kuwapa kiti ACT. Yaani CCM wanaamua nani ashinde na inakuwa

Tunaposikia ACT wamekaa meza moja tena kujadili Katiba pendekezwa na Tume huru inasikitisha sana. Tunaweza kuwalaumu lakini huenda ni uwezo wa kufikiri na kupambanua! inasikitisha sana
 
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Utangulizi.

Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.

Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?

Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!

Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!

Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!

Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?

Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.

Tunaanza na Tume Huru!

Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;

1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.

2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.

3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.

4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.

Tume Itapatikanaje?

Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.

6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Katiba Mpya Itapatikanaje?

Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.

Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.

Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.

Hitimisho.

Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
1647433626699.png
 
Inatakiwa tushawishiwe kwa hoja Katiba ni ya wananchi sio ya wamiliki wa vyama vya siasa

Bila maridhiano hakuna Katiba mpya na wakushaiwishiwa ni CCM na si mwingine

Shida iliyopo ni Chama kimoja kuona kina haki ya kupata Katiba mpya kitu ambacho ni NDOTO , bila mtawala kuridhia ni ngumu na mtawala anatakiwa ashawishiwe kwa hoja vinginevyo utakuwa wimbo tu wa miaka na miaka

Mtawala ndio Nani? Nchi Ni Mali ya wananchi na sio mtawala ambaye anakula na kuvaa kwa Kodi ya wananchi. Na baa ya miaka mitano anakuja kuomba aongoze Tena.
 
Hujaelewa Act wanataka tume huru ianze ili uchaguzi ujao uwe huru ILI UPINZANI UPATE VITI VINGI BUNGENI,
Maana si mnasemaga ccm huwa wanaiba, ila upinzani wanashindaga miaka yote
Huwezi kupitisha katiba unayoitaka kama huna watu

Tume Huru nje ya Katiba mpya Ni kujilisha upepo. Utakuwaje na Tume huru wakati structures zipo vile vile Kama zamani?. Tusiingie kwenye mtego wa ACT na Zitto Kabwe, hatujui wamehaidiwa nini. Kama walipewa Jimbo Pemba kwa makubaliano ya kutokuongelea katiba mpya nani ajuaye.
 
Sasa unadhani katiba unaipataje bila kuwa na number bungeni?.
Hiyo sheria tu ya kuanza mchakato unadhani nani anaitunga?

Kisheria Bunge la kawaida halipitishi katiba mpya Bali, bali Bunge Maalum la Katiba ndilo linalojadili rasimu na kuipitisha. Bunge la kawaida Lina badilisha tu vipengere vya katiba.
 
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Utangulizi.

Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.

Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?

Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!

Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!

Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!

Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?

Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.

Tunaanza na Tume Huru!

Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;

1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.

2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.

3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.

4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.

Tume Itapatikanaje?

Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.

6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Katiba Mpya Itapatikanaje?

Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.

Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.

Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.

Hitimisho.

Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Kwa mujibu wa Katiba Tume Tuliyo nayo ni Huru
 
Ile chaguzi wala hawakushinda kwa kampeni, lile ni jimbo lao na walitishia kujitoa. CCM waliona isiwe tabu ili kuendelea kuudanganya ulimwengu jimbo moja si deal ...
Act kwa Sasa wameshakaribishwa mezani (serikali ya nusu mkate huko Zenji) na wamejihakikishia ruzuku ya kudumu.

Kwa Sasa Zitto ameshapata ajira ya miaka 9 ndani ya kikosi kazi hivyo kelele zake zitapungua.

Kiufundi Act na Zitto wameshapata wanachokitaka
 
Nyie ACT Mama naye kawauliza Nini maana ya Tume Huru mmeshindwa kujibu mkabaki mnacheka.
 
Act kwa Sasa wameshakaribishwa mezani (serikali ya nusu mkate huko Zenji) na wamejihakikishia ruzuku ya kudumu.

Kwa Sasa Zitto ameshapata ajira ya miaka 9 ndani ya kikosi kazi hivyo kelele zake zitapungua.

Kiufundi Act na Zitto wameshapata wanachokitaka
Nakubaliana nawe . Tatizo ni kwamba wanatumika kukwaza au wanatumika kama mpini

VP Othman Masoud alikuwa AG wakati wa Bunge la katiba. Maoud alijiuzulu nafasi yake kwasababu takwa la rasimu ya Warioba la katiba mpya halikutimizwa.

Othman alikuwa miongoni mwa viongozi wa UKAWA waliojiondoa Bunge la katiba

Leo kapewa ving'ora(Shaka anasema) hawezi tena kusimamia alichokiani

Majuzi waliadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha maalimu.

Maalim aliamini katika katiba mpya na muundo wa serikali za muungano

Maalim alifarikia akipigani haki hiyo. Leo akina Othman na Zitto wameusaliti umaalim wanautukuza katika mikutano tu. Matendo yao ni kinyume kabisa

Lakini si Masoud na Zitto, unafiki upo kwa Wazanzibar.

Kesho akija Rais mwingine utasikia kelele zinaanza tena,kwasasa wametulia kwasababu wanachotewa tu kutoka Hazina Dar es Salaam, hawahitaji kwenda kazini au kuvua, hakuna shida tena ya katiba mpya wala muungano! ni starehe kwenda mbele

Zitto ametumika kupitia TCD na tulimuonya kuwa hataweza mbinu za dola.
Mkutano wake wa TCD ndio umezaa tume za akina Sheikh Alhad na Mkandala na yeye akiwemo

Zitto anafahamu 'usaliti' alioufanya kwa Upinzani, tazama kila mahali Task force ya Mkandala inapojitokeza Zitto ananekana kuwa na shaka na asiye ana furaha.

Nafsi inamsuta sana akijua amesaidia sana ''kuuza ghala la silaha''

ACT Wazalendo watakuwa washirika wa CCM huko Zanzibar hawatashika dola hata siku moja, kwa mtu wa bara anayetafakari sawa sawa ACT Wazalendo inatia shaka sana na haina lengo jema na Taifa hili.

Hatuwezi kumsema Mrema wa TLP au Cheyo wa UDP tukameza maneno kwa Zitto wa ACT. Hawa wanasafiri katika chombo kimoja , ni maswahiba wa Lumumba

JokaKuu
 
Kesho akija Rais mwingine utasikia kelele zinaanza tena,kwasasa wametulia kwasababu wanachotewa tu kutoka Hazina Dar es Salaam, hawahitaji kwenda kazini au kuvua, hakuna shida tena ya katiba mpya wala muungano! ni starehe kwenda mbele
Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.
 
Inawezekana Wazenji wametulia kwa sababu kero za muungano zimepatiwa ufumbuzi.
Swali ni kuwa kero hizo zimepatiwa ufumbuzi kwanini imekuwa siri?

Yapi yamejadiliwa na Rais wa Zanzibar na Rais wa JMT Mzanzibar kuhusu Tanganyika?

Je, makubaliano yapo kisheria? Kama hayapo kisheria mbele ya safari akija mwingine na kugundua kuna madudu ''tunayodhani'' yapo ya kuwaumiza Watanganyika na Rais huyo akayaondoa Wazanzibar watalalamika?

Watanganyika wajiulize, ni kipi kimewatuliza Wazanzibar kwa miezi 12 iliyopita kiasi hata cha 'kumsaliti'' Maalim Seif? Kuna kitu gani?

Watanganyika hawahoji kwanini makubaliano ni siri ya Wazanzibar tu! Kuna nini

Ukiangalia kwa ujumla kuna unafiki mkubwa sana!
 
Ukweli tuanze na tume huru. Sababu

1. Ndio itasimamia kura ya maoni ya wananchi kuridhia rasimu ya warioba.
Tukienda na tume tuliyonayo tutatumia fedha zetu na matokeo tutaambiwa wana 70% wameikataa.

Tutaanza upya.
2. Tume hii itasimamia zoezi la uchaguzi iwapo kutakuwa na ucheleweshaji wa katiba mpya.

Ni mawazo tu mimi si mtaalamu wa sheria.

Matusi hapana
 
Back
Top Bottom