Tunaanza na Tume Huru Kwanza

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Utangulizi.

Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.

Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?

Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!

Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!

Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!

Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?

Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.

Tunaanza na Tume Huru!

Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;

1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.

2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.

3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.

4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.

Tume Itapatikanaje?

Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.

6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Katiba Mpya Itapatikanaje?

Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.

Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.

Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.

Hitimisho.

Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusika na uchaguzi mkuu.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi ikiwa ni pamoja na ninyi ACT wazalendo.
 
Tatizo lenu hiyo "ndoa" mliyopo inawafanya muwe watumwa wa mawazo ya wengine, Samia kusema Katiba Mpya isubiri naona na nyie mmedandia hapo hapo sasa mnadai ianze Tume Huru.

Hii Tume Huru mnaitakia nini? au mnaitaka baada ya ule ubinafsi wenu wa kwenda kinyume na makubaliano ya wapinzani wengine kutoshiriki uchaguzi mpaka Tume Huru ipatikane kugonga mwamba.

Nakumbuka mlijaribu kule Mbagala mawakala wenu wakaishia kupigwa mateke, sasa ndio mnaona bora kwanza Tume Huru ianze ili muendelee kuokoteza majimbo kadhaa huku lile la msingi zaidi [Katiba Mpya] mkitaka lisubiri, wacheni utapeli.
 
SUALA LA KATIBA MPYA NI SUALA LA MARIDHANO YA KITAIFA NA SIYO SUALA LA NANI ATASHIDA NA NANI ANASHINDWA,HIVYO BASI KUFIKILIA KUWA NA KATIBA MPYA NDO NJIA SHAIHIA YA KUPATA KATIBA MPYA SIDAHNI KAMA NI HOJA .KAMA WATAWALA HAWATATAKA BASI HATA HIYO TUME HURU INAWEZAKULAZIMISHWA KUTANGAZA VITU TOFAUTI
 
Mawazo ya ACT nimeyaelewa ni maoni mazuri. Lakini kwa mujibu wa Katiba iliyopo tutazuia vipi makucha ya Mwenyekiti wa chama cha ccm ktk kupenyeza watu wake ndani ya tume huru ya uchaguzi??

Hiyo sheria ya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi itatekelezwa na watu gani, na bunge gani sio hili hili?
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi ikiwa ni pamoja na ninyi ACT wazalendo.
Kweli tupu
 
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Utangulizi.

Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.

Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?

Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!

Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!

Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!

Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?

Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.

Tunaanza na Tume Huru!

Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;

1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.

2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.

3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.

4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.

Tume Itapatikanaje?

Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.

6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Katiba Mpya Itapatikanaje?

Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.

Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.

Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.

Hitimisho.

Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Inayotakiwa kuanza ni Katiba mpya ila kwakuwa mmefunga ndoa na ccm (mmeolewa) kule Zanzibar na kiongozi wenu wa chama ni mjasiamali wa siasa ndo mana mmeziba masikio
 
Kwanza jibu maswali haya

1. Kati ya Sheria za uchaguzi na katiba ipi ina nguvu?

2.Kama katiba ina nguvu na katiba inampa Rais mamlaka ya kufanya chochote wakati wowote hiyo tume itakuwa vipi huru?

3. Katiba ni hitaji la watanzania tume huru ni hitaji la kisiasa nyie ACT hamuoni kuwa ni uroho wa madaraka unaowafanya mkimbilie tume huru huku mkiacha hitaji namba moja la wanachi?

4. Vyama vingine vya siasa vimekuwa vikidai katiba mpya na nyinyi ACT ambao mna ndoa na CCM kule Zanzibar hamuoni hii kama ni mpango wa mme/mke wenu (CCM) kuharibu na kuua agenda ya katiba mpya na nyie kama ACT mnatumika kutimiza malengo?

5. Kwanii hoja ya tume huru ije sasa kipindi ambacho hoja ya katiba mpya imeshika kasi?
 
Tatizo linaanza hapo kwenye Kamati ya Uteuzi wa Tume maana karibu wote wanaopendekezwa wameishakuwa au wanaweza kuwa compromised katika mazingira ya sasa. Ndio maana watu wanadai Katiba Mpya ambayo itaruhusu uundaji wa Kamati ambayo wananchi watakuwa wana imani kuwa haiegemei upande wowote.
Ni bora kusubiri kuliko kuunda Tume ambayo italeta matokeo yale yale ya 2020 ingawa labda safari hii hawatarudia kosa la kukipa chama kimoja ushindi wa 99%. Wapinzani wenye staha watapewa viti vya kutosha kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani na hivyo kuweza kudai kuwa hata Katiba itakayopendekeza itakuwa na uhalali.

Amandla...
 
TUNAANZA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

Hoja ya ACT Wazalendo Juu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Utangulizi.

Tangu kurejeshwa upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, hoja ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi imetawala medani ya siasa nchini.

Tume ya Jaji Nyalali ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi iliweka bayana kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, ni lazima kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya.

Hoja hizi zimeendelea kutawala medani ya siasa katika miaka 30 ya uwepo wa siasa za Vyama vingi nchini.

Kikao cha Wadau wa Tasnia ya Siasa Dodoma: Ukurasa Mpya?

Utawala wa Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ulijipambanua bayana kuwa dhidi ya vyama vya upinzani. Wito wa viongozi wa upinzani wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa na maridhiano ya kisiasa ulipuuzwa. Haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa uhuru iliangamizwa. Shughuli halali kama vile mikutano ya hadhara ziliharamishwa!

Katika mazingira hayo, ni dhahiri kuwa Kikao cha Wadau wa Siasa Tanzania Kujadili Hali ya Demokrasia Tanzania kilichofanyika Jijini Dodoma kati ya tarehe 15 hadi 17 Desemba 2021 kilikuwa mwanzo mpya uliokosekana katika miaka sita iliyopita!

Kikao hicho kilichowakutanisha viongozi waandamizi wa vyama vya siasa, Mawaziri wenye dhamana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini kilikuwa ni jukwaa muafaka la kutafakari tulipojikwaa kwenye chaguzi zilizopita, hasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 na kutafakari kwa pamoja mwelekeo unaopaswa kuchukuliwa na Taifa kurekebisha dosari hizo kwa maslahi mapana ya Taifa. Makosa hurekebishwa kwa watu kukutana, kuambiana ukweli na kuwa na utayari wa kubadilika!

Kwa Hali yetu, Nini Kianze? Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba Mpya?

Moja ya masuala ambayo yalijadiliwa kwa uwazi na kina kwenye Kikao cha Wadau wa Siasa cha Dodoma ni kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Baada ya kikao, masuala haya mawili, hasa kuhusu nini hasa kinapaswa kutangulia yamepata mjadala mkubwa.

Tunaanza na Tume Huru!

Kalenda ya Uchaguzi inaonesha kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na 2025 Uchaguzi Mkuu. Kwa maoni yetu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa tunapaswa kwanza kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi kisha Katiba Mpya. Sababu zetu zipo wazi;

1. Mchakato wa Katiba Mpya unahitaji kutungwa kwa Sheria Mpya ya kusimamia suala hilo kwa sababu Sheria iliyokuwepo imeshapitwa na muda. Kutokana na unyeti wa suala hilo, ACT Wazalendo tungefurahi jukumu hili nyeti, litekelezwe na Bunge lililochaguliwa Kidemokrasia na Wananchi tofauti na Bunge la sasa ambalo asilimia kubwa ya Wabunge wake ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hawakutokana na matakwa (will) ya Wananchi.

2. Kura ya maoni ya Katiba Mpya itasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Hatuna imani kuwa Tume ya Uchaguzi inaweza kusimamia zoezi hilo nyeti kwa weledi na haki. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itasimamia mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Mpya. Tume hiyo ni lazima iundwe sasa.

3. Hata baada ya Katiba Mpya kupitishwa na Wananchi kwenye kura ya maoni, Katiba haitaanza kutumika mara moja. Kutakuwa na kipindi cha mpito kisichopungua Miaka minne. Katika kipindi hicho Sheria mbalimbali zitafanyiwa marekebisho ili kuendana na Katiba Mpya. Kipindi hicho cha mpito lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025 na chaguzi ndogo zozote zitakazokuwa zinatokea kabla ya Katiba Mpya kuanza kutumika.

4. Iwapo kwa sababu zozote zile, Mchakato wa Katiba Mpya hautakamilika hadi wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, Tume Huru itakayoundwa itaweza kusimamia chaguzi hizo kwa uhuru na haki.

Tume Itapatikanaje?

Tume ya Uchaguzi ni zao la Katiba na Sheria. ACT Wazalendo tunapendekeza kuandikwa upya kwa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi. Tunapendekeza kuwa Tume Huru ya Uchaguzi iwe na uwezo wa kuajiri Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi zote na kuondokana kabisa na Mfumo wa sasa wa makada wa Chama tawala kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi.

ACT Wazalendo tunapendekeza Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba na ya Katiba Pendekezwa Kuhusu Tume ya Uchaguzi yachukuliwe kama yalivyo au na marekebisho kulingana na hali ya sasa. Msingi wa hoja hii ni ukweli kuwa maoni hayo yanatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi Wapatikanaje?

1. Sheria mpya ya Uchaguzi (National Elections Act 2022) iweke utaratibu kuwa Watanzania wanaotaka kuwa Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi waombe kazi kufuatia tangazo la wazi kwa umma.

2. Sheria mpya ya Uchaguzi ianzishe Kamati Maalum ya Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi.

3. Kamati ya Uteuzi ifanye usaili (interview) kwa uwazi kwa waombaji wote na kuchuja majina ambayo yatapelekwa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi.

4. Mara baada ya wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi kupatikana wataajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye nafasi itatangazwa, kufanyiwa usaili wa wazi na kisha jina kupelekwa kwa Rais kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi.

5. Kamati ya Uteuzi wa Tume itamkwe kisheria kuongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kama Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Zanzibar kama Makamu wa Mwenyekiti, Wajumbe wawe ni Rais wa Tanganyika Law Society, Rais wa Zanzibar Law Society, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mtu mmoja atakayeteuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na kama hakuna Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni basi kutoka chombo kinachojumuisha Vyama vyenye Wabunge Bungeni, Mtu mmoja kutoka Asasi ya Kitaifa ya masuala ya Sheria na Haki za Binaadam Tanzania Bara na mtu mmoja kutoka asasi kama hiyo Tanzania Zanzibar. Kwa vyovyote vile angalau theluthi ya wajumbe wa Kamati ya Uteuzi lazima wawe Wanawake.

6. Kutakuwa na sifa maalum za Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanakuwa watu wenye weledi na hawaegemei upande wowote.

7. Baada ya kuteuliwa na Rais, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume wataidhinishwa na Bunge kwa utaratibu utakaowekwa na Sheria ya Uchaguzi. Kisha watakula kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Masuala haya, na mengine yatakayoonekana yanafaa kutokana na mashauriano ya wadau, yanaweza kujumuishwa kwenye Sheria Mpya ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Katiba Mpya Itapatikanaje?

Katiba Mpya ni jambo pana! Inahitaji kuwepo kwa muafaka wa kitaifa juu ya jambo hilo.

Jambo la kutia matumaini, mchakato wa Katiba Mpya ulikwishaanza. Tume ya kukusanya maoni ilikwishaundwa, maoni yalishakusanywa na kuwasilishwa kwenye Bunge la Katiba ambalo lilitoka na Katiba Pendekezwa. Changamoto pekee ni kuwa Katiba Pendekezwa haikutokana na maoni ya pande zote kwa sababu Wabunge wengi wa Upinzani walisusia upigaji kura.

Hivyo basi, Taifa litahitaji Katiba Pendekezwa kufanyiwa maboresho. Mchakato wa namna ya kuifanyia maboresho lazima uelezwe kwenye Sheria ya Mchakato wa Katiba Mpya itayoandikwa upya na Bunge. Bunge linaweza kuamua kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu (Committee of Experts) ili kutafuta namna nyingine ya kumalizia mchakato bila kuligharimu Taifa.

Hitimisho.

Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni chanda na pete, vinategemeana. Kwa mazingira yetu kama Taifa kwa sasa, kutangulia kupata Tume Huru ya Uchaguzi kunaweka mazingira mazuri ya kupatikana kwa Katiba Mpya inayotokana na maoni na matakwa ya Wananchi.
Mtoto Anapo dai kumzaa baba yake!
 
Hiyo sheria ya kuiunda hiyo Tume huru itatungwa na Bunge gani kama sio hili hili. Kama mnaliamini kwa sheria iwe hivyo kwa katiba Mpya.
Nifikiliavyo mimi katiba ikimuondolea Rais hayo manguvu na kuhakikisha check and balance ya uhakika automatic Tume huru itakuwa imejitengeneza.
 
ACT Wazalendo wanafaidi matunda ya ndoa yao mpya na CCM kule upande wa Zanzibar. Hawana ufahamu kuhusu machungu ya ndoa ndani ya kutalikiwa, kusalitiwa, kutelekezwa, kuachwa, kufukuzwa pengine hata kufumaniwa

Hawajifunzi kutoka kwa mwanandoa CUF ambaye alimtangulia katika ndoa kama yake. Siku za fungate zinahesabika, pale zitakapo kwisha msije kuja na visingizio vipya vya madai ya katiba mpya.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Tume huru ambayo mwenyekiti wake atariport kwa Rais wa nchi...Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia atakuwa mgombea Urais 2015. Tume ambayo ikitangaza matokeo huna mamlaka ya kuyahoji popote pale...ok !!

Watanzania amkeni.
 
Back
Top Bottom