Tuna haja kuwa na Ofisi ya Maadili ya Viongozi wa Umma?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,752
Suala la maadili ya viongozi limekuwa ni changamoto. Uwepo wa ofisi ya maadili ya viongozi wa umma ni jambo linalopaswa kuendana na nidhamu za viongozi kiutendaji na kimaadili.

Ripoti za CAG nyingi zilizopita zomeonesha ukiukwaji mkubwa wa uadilifu wa viongozi katika ngazi husika. Imeonekana sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamejikita kwenye kufuatilia ukwasi wa viongozi na hasa hasa kuwalinda kwani taarifa za ukwasi wa viongozi ni siri haziwekwi wazi kwa umma.

Ingawa huku mitaani tunashuhudia watumishi wa umma wakibadilisha maisha yao kuwa ya ukwasi mkubwa wanapokuwa kwenye vitengo au nafasi za uongozi.

Wapo viongozi ambao mwenendo wao wa maisha ni ombwe kubwa la maadili ya uongozi. Wapo viongozi wanatoa kauli ambazo zinalipasua Taifa wanaachwa hawachukuliwi hatua, wapo viongozi ambao wanatumia nafasi au madaraka yao kuingilia ndoa za watu lakini linaonekana ni jambo binafsi.

Wapo viongozi ambao wanatumia madaraka yao kujipatia mali lukuki lakini so long as wanajaza fomu za maadili wanakuwa safe.

Je, kama jamii, hii tume au sekretarieti au ofisi ya maadili ya viongozi wa umma ina tija gani kwa nchi?

Nasbawishika kuomba ifutwe kwani kazi zake zinaweza kufanywa na TAKUKURU kwa ufanisi zaidi.
 
Ipo tume ya maadili ya viongozi wa umma
 
Back
Top Bottom