MWANAHARAKATI MWEMA
Senior Member
- Dec 16, 2022
- 192
- 270
Nawasalimu Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa kusamehe, nawashukuru wazazi wangu Kwa kunizaa hivi nilivyo nashukuru.
Mimi nimekuwa miongoni mwa watu ambao nimezaliwa nikajikuta nina moyo ambao muda wote unaitaji amani, na sipendi kuonea mtu wala sipendi kuona mtu mwingine akionewa.
Nimekuwa katika maisha haya kuanzia utoto mpaka ukubwani na mpaka nimeajiliwa nipo vilevile.
Shida kubwa kabisa ambayo nimeiona ofisi nyingi za umma ni Ile hali kwamba endapo utakuwa tofauti na mitazamo na wenzako ambao wao wanaweza kuwa wazee wa madili, unakuta mtu anafanya jambo mpaka unashangaa ukimuuliza anakwambia wewe unadhani mimi nimekuja kucheza hapa.
Yaani mitazamo ya walio wengi kwenye ofisi za umma ni kwamba "CHUKUA CHAKO MAPEMA" lakini ukiangalia watu wanaoumia ni wananchi wa hali ya chini, na ikitokea wewe ambaye una hofu ya mungu unataka kulifanya jambo lile kwa haki unachukiwa huku ukipewa majina ya hajabu, utaitwa mjuaji, bush loyar, mzee wa protocol, mlokole nk.
Sasa Kuna nyakati huwa najiuliza hivi kama sisi tutakuja kujikomboa kweli kwenye hali hii inayoitwa ya umaskini au ndio bhasi tuendelee kuumizana mpaka Mungu mwenyewe atakapoamua kututoa kwenye hili janga.
Ni kweli kwamba asilimia kubwa ya watu ambao wanakula na kuchezea ofisi za Umma ni watu wanamaisha mazuri na wale wanaopenda haki wengi ni maskini ata maisha yao ya kawaida sana, sasa hali hii ndio inafanya wachache wapate mali na wengi wanaishia kwenye umaskini.
Na hakuna kitu kinakela sana kama mtu ukiwa unakibiashara flani ambacho wewe kama mtumishi umekianzisha na kinakulunguzia shida ,maneno utakayopewa ni kukatishwa tamaa tu, yaani watu hawaami katika kujiwekeza badala yake wanakutengenezea mazingira ukwame kiukweli inasikitisha sana.
Asanteni.