Tumjibu Askofu Gwajima Kisayansi na si Kisiasa, tuache kumshambulia na kumtishia. No research no right to speak

Halafu mavuvuzela wa Gwajima Chameleon wengi karibu wote ukiwauliza kwa nini wanataka uthibitisho wa chanjo miaka 10 mbele na kwanini isiwe 20, 30,au 50 au miaka 5 jibu watakuambia
dawa ndio muda wa uthibitisho.
Nani kapanga hiyo miaka waulize wakupe jibu.

Kwa ugunduzi wetu au wa hao hao wanaotupa dawa na chanjo kila siku !!?

Je chanjo ba dawa tutumiazo toka tuwe nchi huru tulishadai uhakika wa miaka 10 mbele.

Wajinga sana. Wanasahau computer zenye nguvu kabisa zimegunduliwa ndani ya miaka ya 50 tu iliyopita.

1970 windows computer hata mouse yenyewe au cd au dvd vitu hivi havikuwepo duniani, labda kwa Billgates huko.

Flash ilipotea bongo watu wengine walikuwa wanazivaa shingoni kwenye chain. !!! Ilikuwa uvbuzi wa kutisha 60mb !!!!

Lakini upuuzi wowote wa Gwaji Chameleon wanapiga vuvuzela sijui ndg zetu mmelogwa na huyu Chameleon.

Sambamba na uvumbuzi na ugunduzi ni kuokoa muda.

Muulizeni alipokuwa anaanza kile kanisa pale hunters pub ubungo alikuwa anaenda na Tablet au smartphone.
Ile clip ya kwichikwichi hatujaisahau pia.
 
Kwenye kesi yoyote ‘mshtaki’ ndio anaanza kwa kuthibisha uhalali wa mashtaka yake, na sio upande wa ‘utetezi’ unaanza kwa kujibu.

Wewe kama mfuasi wa Bishop Gwajima chukulia hii ni fursa adimu serikali imempa kupeleka ushahidi wa madai yake na kama maelezo yake yanajitosheleza mbele ya sheria ajibiwe.

Vinginevyo unataka serikali ipoteze muda kujibizana na kila mtu atakaekuwa anajitungia mambo tu.
Waziri wa afya ana watumishi wengi wenye sifa na ufahamu mkubwa, siyo tu wa chanjo ya UVIKO-19, zaidi ya 1m ya chanjo iliyoletwa awamu ya kwanza. Kama hao, ambao ndio wanapaswa kutoa mfano kuoonesha ubora na usalama ya chanjo, wanasita, kwa nini Gwajiboy abebeshwe lawama. Yeye, Gwajiboy anachukua tahadhari ili kondoo wake wasiangamie
 
THE HUNGRY MAN IS ANGRY.... 😂😂😂😂😂 NJAA MBAYA SANA.
Ndio maana kuna watu walipopata uongozi tu walitengeneza mkakati wa kuiba tu kwa miradi ya kinguvu hakika njaa mbaya sana hasa ukikulia sehemu yenye dhiki unakuwa na roho mbaya sana.
 
Waziri wa afya ana watumishi wengi wenye sifa na ufahamu mkubwa, siyo tu wa chanjo ya UVIKO-19, zaidi ya 1m ya chanjo iliyoletwa awamu ya kwanza. Kama hao, ambao ndio wanapaswa kutoa mfano kuoonesha ubora na usalama ya chanjo, wanasita, kwa nini Gwajiboy abebeshwe lawama. Yeye, Gwajiboy anachukua tahadhari ili kondoo wake wasiangamie

Umeshaambiwa kuchanja ni hiyari.

Ugonjwa wenyewe ni mgeni changamoto ya wizara zote za afya duniani ni kutoa elimu kuhusu huo ugonjwa na umuhimu wa chanjo kuondoa sintofahamu watu wajilinde.

Sasa wewe na huyo Gwajima wenu kutwa kupinga kwa hoja za kuokota okota mitandaoni.

Kwanza sioni kwanini unatetea Bishop Gwajima kukwepa fursa aliyopewa kuthibitisha madai yake; si ndio atawaumbua zaidi serikali.

Hiyo ni nafasi nzuri kwake sio tu kuonyesha ingredients za kwenye chanjo but also proving mawaziri walichanja maji mbele ya camera. You can do that aombe aletewe vaccine antibody test damu ya waziri itajibu kama kuna protein za kupambana na COVID kama amna mpaka leo basi yale yalikuwa maji.

Ifike mahala mjue upotoshaji una madhara, umeshaambiwa kuchanja sio lazima sasa kwanini uzidi kuogopesha watu; wakati mitungi ya oxygen ikikosekana hospitali watu wanailalamikia wizara na serikali sio kanisa la mtu.
 
You can go and eat your own feces, we don't have time to swallow anymore nonsense.

Hakuna cha SARS wala bibi yake na SARS. Tanzania is safe and will continue to be that way.

Anyone who seeks to destroy our country with fake diseases shall be equally destroyed with fierce and ferocity.

Take this to the bank!
Wow,I like this!
 
Ukweli uko wazi, chanjo hazijapitia stage zote zinazotakiwa kwa chanjo kukamilika.
Hawawezi kujibu kisayansi kwa sababu kisayansi hawajatimiza hatua zinazotakiwa.
Most likely, wanapoulizwa maswali magumu kama hayo wanakimbilia kwenye vitisho; usipochanjwa utaambukizwa, ukiambukizwa utakufa, nk.
Hakuna anayejua kwa hakika 'long term effects' za hizi chanjo.
Tunaohoji tusitishwe, tuna uhuru wa kuhoji.
Tengeneza yako na wewe
 
Ndio maana kuna watu walipopata uongozi tu walitengeneza mkakati wa kuiba tu kwa miradi ya kinguvu hakika njaa mbaya sana hasa ukikulia sehemu yenye dhiki unakuwa na roho mbaya sana.
THE HUNGRY MAN IS ANGRY.... 😂😂😂😂😂 NJAA MBAYA SANA
 
Sijui kwanini kila nikimwona Askofu Gwajima anahubiri au anazungumza mahala popote pale hudhani ni Mgonjwa wa Akili amezidiwa na anahitaji Tiba ya haraka ili asije akafanya tukio baya kwa wenye Akili timamu.

Hata P kaunga mkono, basi hoja hizi afikishiwe na bi nanihii.
naunga mkono hoja.
p
 
Umeshaambiwa kuchanja ni hiyari.

Ugonjwa wenyewe ni mgeni changamoto ya wizara zote za afya duniani ni kutoa elimu kuhusu huo ugonjwa na umuhimu wa chanjo kuondoa sintofahamu watu wajilinde.

Sasa wewe na huyo Gwajima wenu kutwa kupinga kwa hoja za kuokota okota mitandaoni.

Kwanza sioni kwanini unatetea Bishop Gwajima kukwepa fursa aliyopewa kuthibitisha madai yake; si ndio atawaumbua zaidi serikali.

Hiyo ni nafasi nzuri kwake sio tu kuonyesha ingredients za kwenye chanjo but also proving mawaziri walichanja maji mbele ya camera. You can do that aombe aletewe vaccine antibody test damu ya waziri itajibu kama kuna protein za kupambana na COVID kama amna mpaka leo basi yale yalikuwa maji.

Ifike mahala mjue upotoshaji una madhara, umeshaambiwa kuchanja sio lazima sasa kwanini uzidi kuogopesha watu; wakati mitungi ya oxygen ikikosekana hospitali watu wanailalamikia wizara na serikali sio kanisa la mtu.

Simtetei Gwajiboy ila nailaumu Serikali, hasa Mawaziri wa afya kudai anapotosha. Hana kesi ya kujibu kwa sababu ni swala la afya na uhai wa kila mtu. Kama chanjo ni bora na salama pasingekuwa na mijadala kote duniani. Kwa kauli yako, kote duniani, wanaohoji wakamatwe kuthibitisha?

Kama ni kuogopesha watu, Serikali ndio iko mstari wa mbele. Mawaziri wa Afya na wataalamu wao wanapaswa kuelimisha jamii kuhusu ubora na usalama wa chanjo ili wampuuze Gwajiboy. Kinyume chake nami nitaendelea kuhoji ubora na usalama wa chanjo, kwa SAUTI KUBWA

Ili kuthibitisha ubora na usalama wa chanjo hao Mawaziri wafanyiwe wafanyiwe hiyo "vaccine antibody test" kuthibitisha wana kinga ili jamii iamini na Gwajiboy aumbuke. Vinginevyo Gwajiboy ataendelea kuwapiga nyundo
 
Kabla ya kama atajibiwa au la awajibike kwa insubordination.
Hoja yeyote aliyonayo alitakiwa ajiuzulu kwanza. Hiyo ndio sheria. Tuanzie hapo.
Kuna mengi ambayo nae yanamhusu e.g. vyanzo vya taarifa zake, utalaan ktk fani hiyo na kithibitisha hoja zake kwamba viongozi wamechanjwa kimagumashi kuwazuga watz n.k, lakini kabla ya yote awajibike. Naona mnampa big up sana huyu gwajima chameleon bila kuliangalia hilo.

Kauli nyingine ya kipuuzi ya huyu chameleon ni ile ya kusema potelea mbali ubunge.
Angekuwa hachukui posho angekuwa na hiyo jeuri

Edwin Mtei aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu alipoona Nyerere hataki ushauri wake kwenye masuala ya IMF alijiuzulu kesho yake.

Hapa huyu bw anatakiwa ajiuzulu kwamza wote mnaompigia debe hamlioni hilo haijalishi kama chanjo ni sawa au sio sawa.

Kama hajali sana Ubunge mbona anakomba hizo m11 na ushee kila mwezi.
Kama chanjo ni bora na salama, wahusika waelimishe jamii na hakika Gwajiboy atapuuzwa.

Je, wanaohoji ubora na usalama wa chanjo, dunia nzima wanatakiwa kuthibitisha? Ni wajibu wa mtengenezaji kuthibitisha. Hiyo ndiyo kanuni kuu katika tiba.
 
Simtetei Gwajiboy ila nailaumu Serikali, hasa Mawaziri wa afya kudai anapotosha. Hana kesi ya kujibu kwa sababu ni swala la afya na uhai wa kila mtu. Kama chanjo ni bora na salama pasingekuwa na mijadala kote duniani. Kwa kauli yako, kote duniani, wanaohoji wakamatwe kuthibitisha?

Kama ni kuogopesha watu, Serikali ndio iko mstari wa mbele. Mawaziri wa Afya na wataalamu wao wanapaswa kuelimisha jamii kuhusu ubora na usalama wa chanjo ili wampuuze Gwajiboy. Kinyume chake nami nitaendelea kuhoji ubora na usalama wa chanjo, kwa SAUTI KUBWA

Ili kuthibitisha ubora na usalama wa chanjo hao Mawaziri wafanyiwe wafanyiwe hiyo "vaccine antibody test" kuthibitisha wana kinga ili jamii iamini na Gwajiboy aumbuke. Vinginevyo Gwajiboy ataendelea kuwapiga nyundo

Waziri keshasema yeye binafsi yupo tayari kwenda nae popote kuthibitisha madai yake. Ataje mtu aliechanjwa maji atapelekwa atapimwa antibodies mbele yake.

Ina maana hata akitajwa yeye (waziri) yupo tayari kupimwa antibody, mbele ya mchungaji kuonyesha uongo wake.

Ndugu kuhusu usalama wa chanjo kuna nchi zishachanja 80% ya adults over the age 18 sasa hivi wapo kwenye majaribio ya chanjo kwa under 17.

Human trial ya under 17 years nimekuwekea video jana imeanza five months ago, sasa hivi bado wana monitor reactions za volunteers waliochanja, go ahead ya kuanza kuwachanja hilo kundi lote bado.

Kila kitu kinakwenda kutokana na medical requirements, hakuna short cuts.

Ngoja nikupe testimony yangu ya COVID mimi nilipata sasa kuna wengine reaction yao ni tofauti na hata hayo maelezo ya wataalamu wanaotupa ndio maana wanasema ni ugonjwa mpya ata wao wataalamu bado wanajifunza with new information.

Sasa what happened to me, to cut the story short mie nilipata mid March mwaka jana na elimu tuliyokuwa tukipewa attack ni siku 7-14 hiyo kwa wale wataopata homa. Basi homa kali likanitandika kama kwa siku 10 hivi ya 11 nikapona nikawa fresh kabisa.

Upumbavu wangu siku ya 12 nikanywa vodka (anyway nilikuwa najiona, poa kabisa) kilichotokea kesho yake ilirudi homa kali ya mara ya kwanza afadhali. Na hii ya safari ya pili nilikaa nayo kuanzia late March- mpaka mid May 2020, kwenye hizo siku leo unaamka asubuhi mzima jioni homa. Kesho siku nzima mzima, keshokutwa upo hoi na homa yaani ni up and down for six to seven weeks.

Na baada ya kupona in May nilikuwa sitoi makamasi kabisa yaani hata nikijaribu unatoka mvuke tu na aushuki unabaki juu baada ya dakika kadhaa huo mvuke unaganda inabidi uchokonoe pua kukakwangua ndio utoke na ukiushika ukoko wenyewe ni mgumu kama jiwe.

Hiyo hali nimeenda nayo mpaka mwaka huu April 2021 nilipopata jab ya kwanza, baada ya sindano usiku huo huo ndio makamasi yalianza kuchuruzika for the first baada ya karibu mwaka (bila ya kusahau ata mkojo wangu ulikuwa ni wa njano tu, ule wa rangi ya dehydration indication ata ninywe maji vipi).

Sasa nina uhakika kwa wale COVID iliyotupiga kwa homa ya week 6-7 kila mtu ana story yake; kuna dada namjua na yeye aliugua muda sawa na mimi; yeye mpaka December mwaka jana alikuwa kuna siku moja au mbili kwenye mwezi homa linamwendea mpaka alipochanjwa yeye ni nurse December ndio hiyo hali ilipoisha, kama mimi side effects zangu zilivyopotea.

So what am I trying to say COVID 19 bado wanasayansi wanajifunza madhara yake, however vaccine helps asikwambie mtu.

Tatizo la huyu Gwajima sio kupinga with merit na uongo juu anawatungia wahusika to justify his position, now that is just stupid.
 
Kwanza kabisa tuache kutishiana kuhusu covid 19 japo kama una kinga dhaifu au kama una other risk factors ya kuambukizwa na kufa kwa ugonjwa wa uviko 19 jaribu kukaa mbali na watu ambao unahisi wanaweza kukuambukiza covid 19 au kama unahiari ya kupata chanjo ya covid 19 nenda ukachanjwe . Risk factors za kufa kwa ugonjwa wa Covid 19 ni kama ifuatavyo:unene uliyopitiliza,magonjwa ya presha na moyo,kisukari,ukimwi,umri mkubwa,utapiamlo,pumu,kansa,magonjwa yanaoathiri mapafu,upunguvu wa damu,kuwa na kinga pungufu mwilini.kama uko ndani ya makundi hayo jaribu kwa kipindi hichi cha ugonjwa huu kuwa makini sana au ikipidi kama una hofu tafuta chanjo ambao unahisi yaweza kukufaa

Nimetangulia kusema kuwa tusitishane kwa sababu hizi zifuatazo.
Tangia ugonjwa huu umekuwepo early jarunary 2020,walioambukizwa ni 206,958,371,na waliyokufa ni 4,357,179. yani kati watu 100 wanaombukizwa,wanaokufa ni asili mia 2.1.

kwa hiyo hata ukiambukizwa usiingize hofu,wahi hospitalini.na watoa huduma tusiogope kuwahudumia wagonjwa wa aina hii.ukimnyapaa ndiyo unakuwa unamuua kabisa.

Globally, as of 12:23pm CEST, 16 August 2021, there have been 206,958,371 confirmed cases of COVID-19, including 4,357,179 deaths, reported to WHO. As of 11 August 2021, a total of 4,428,168,759 vaccine doses have been administered.

Na ukiangalia kidunia waliaambukizwa ugonjwa huu ni 206,958,371, kati ya watu bilioni 7.8 wanaoshi duniania.sasa piga mahesabu ni asilimia ngapi ya watu waliyombukizwa ulimwenguni kote.

Ndiyo maana,tunatakiwa kutoingiza hofu bali tuchukue tahadhali na kufuata ushauri mzuri wa watoa huduma za afya.kama uko kwenye kundi hatarishi jitahidi sana kujikinga kwa kadri iwezekanovyo lakini pia acha hofu.wahi hospitalini endapo utahisi umeambuikizwa.

Nikizungumzia kuhusu kinga .kuna primary prevention na secondary prevention primary prevention ni pamoja na kuacha tabia hatarishi,kufuata ushauri wa watoa huduma za afya namna ya kujikinga,kupata chanjo safi na salama.

chanjo safi na salama inapatikana kwa kufuata hatua zilizoanishwa na shirika la afya duniani kwa kushirikiana na taasisi zengine kama CDC na FDA.

Utengenezwaji wa chanzo unaanza kwa kutafiti kisababishi cha ugonjwa husika,muundo wa kirusi au bacteria,tabia yake,kuzaliana kwake etc .Hii inaitwa exploratoty stage .Baada ya kukielewa kirusi au bacteria alivyo ndipo watalaam wanatengeneza chanjo.chanjo ikishapatikana inajaribishwa kwanzamaabara au kwa wanyama.this is mandatory.hii inaitwa pre clinical stage.

sasa swali ambalo Mh Askovu GWAJIMA amekuwa akiuliza ni hili .je?chanjo hii ilipitia kwa wanyama kwanza?tumjibu kisayansi na siyo kisiasa.

Ukitoka preclinical stage unakuja phase one clinical stage ambabo chanjo inajaribiwa kwa watu 20-80 wenye kuwa na ugonjwa huo huo au unaofanana na huo.Akofu GWAJIMA ana haki ya kuuliza kama hili lilifanyika.

i:The goals of Phase 1 testing are to assess the safety of the candidate vaccine and to determine the type and extent of immune response that the vaccine provokes".

ukishatoka clinial trial phase unaingia clinical trial phase ambapo chanjo inatolewa kwa mamia ya watu.lengo likiwa hili"The goals of Phase II testing are to study the candidate vaccine’s safety, immunogenicity, proposed doses, schedule of immunizations, and method of delivery.""Hapa wamesema schedule of immuizations.yani chanjo itolewe lini,mara ngapi,kwa watu gani,.nimeona jinsi watu wanavyojikanyaga mana leo wanasema ati wapewe high risk group mara wapewe watu wote mara sijui.Hili linaleta maswali mwengi.

Ukitoka phase 2 clinical trial unaingia phase 3 ambapo chanjo inatolewa kwa maelfu ya watu.maengo ya pahse 3 yakiwa haya:
One Phase III goal is to assess vaccine safety in a large group of people. Certain rare side effects might not surface in the smaller groups of subjects tested in earlier phases. For example, suppose that an adverse event related to a candidate vaccine might occur in 1 of every 10,000 people. To detect a significant difference for a low-frequency event, the trial would have to include 60,000 subjects, half of them in the control, or no vaccine, group (Plotkin SA et al. Vaccines, 5th ed. Philadelphia: Saunders, 2008).

Vaccine efficacy is tested as well. These factors might include 1) Does the candidate vaccine prevent disease? 2) Does it prevent infection with the pathogen? 3) Does it lead to production of antibodies or other types of immune responses related to the pathogen?

ASKOFU GWAJIMA anauliza chanjo ya nini ikiwa nikichanjWa nitaambukizwa,nitambukiza nitakufa kwa ugojwa huo huo.Tumujibu kisayansi siyo kisiasa.watengenezaji wasiingize siasa kwa maisha ya watu .wamesema hata ukichanja utaambukizwa,utaambukiza ,unaweza ukafa kwa ugonjwa wa covid.na pia usiache kufuata zile measures nyengine kama kuvaa barakoa,kunawa mikono,social distancing .ATI MAKALI YA UGONJWA YANAPUNGUA UKIJIPATIA CHANJO YA UVIKO.

Kwa kuzungu ni hivii:
Safe and effective vaccines are a game-changing tool: but for the foreseeable future we must continue wearing masks, cleaning our hands, ensuring good ventilation indoors, physically distancing and avoiding crowds.

Being vaccinated does not mean that we can throw caution to the wind and put ourselves and others at risk, particularly because research is still ongoing into how much vaccines protect not only against disease but also against infection and transmission. See WHO’s landscape of COVID-19 vaccine candidates

Mashirika ya CDC ,FDA,WHO,yameweka wazi kuwa chanjo ni hiari.sasa kwa nini wanasiasa ambao mahala pengine hawajasomea mambo ya afya,layman kabisa wanalazimisha chanjo klutolewa kwa nguvu.embu jiulize MBUNGE wa tanzania ambaye amemaliza la saba,sijui form 4,form 6 ,mwanasheria ,mwalimu wa kawaida kabisa yani mtu hajawahi kufanya utafiti wowote anataka kulazimisha chanjo kwa nguvu.!!!!!!common.embu heshimuni taluma za watu.na kama wewe unataluma ya afya au ni mtafiti weka uzalendo kwanza mbele achana na siasa kichani.madaktari wanaelewa ninacho kisema.yani medical ethics.Hata kipimo huwezi kukifanya kama mgonjwa hataki.HUWEZI KUMPA MGONJWA DAWA KAMA HATAKI SEMBUSE CHANJO???

Kwa kizungu ni hivi"that they have the option to accept or refuse the vaccine""

How will vaccine recipients be informed about the benefits and risks of any vaccine that receives an EUA?​

FDA must ensure that recipients of the vaccine under an EUA are informed, to the extent practicable given the applicable circumstances, that FDA has authorized the emergency use of the vaccine, of the known and potential benefits and risks, the extent to which such benefits and risks are unknown, that they have the option to accept or refuse the vaccine, and of any available alternatives to the product. Typically, this information is communicated in a patient “fact sheet.” The FDA posts these fact sheets on our website.

sasa povu la nini na kumtishia askofu GWAJIMA.siasa za nini?chanjo ni hiari.acheni kulazimisha watu.kama wewe unaona ni lazima kupata chanjo nenda ukachanjwe .ASKOFU GWAJIMA anachokifanya ni ku compliment missing doubtful information about the vaccine.

kama chanjo imetolewa under EMERGENCY USE UUTHORIZATION kwamba wanayoitoa wahakikishe wanamonitor chanjo hiyo kwa sababu ni" Under an EUA, FDA may allow the use of unapproved medical products, or unapproved uses of approved medical products in an emergency to diagnose, treat, or prevent serious or life-threatening diseases or conditions when certain statutory criteria have been met, including that there are no adequate, approved, and available alternatives""" KOSA LA ASKOFU GWAJIMA LIKO WAPI?

sisi wanasiasa tuache siasa kwa afya za watu.chanjo ni hiari.nashauri kama kuna mtu atalazimishwa chanjo fungua kesi mahakamani na nakuhakikishia utawashinda mapema kabisa

AFYA NI HAKI YAKO .KUTOA ELIMU NI HAKI .

NIWAKUMBUSHE WATU WOTE HASA WANASIASA KUWA KILA CHANJO NI HIARI YA MTU KUKUBARI AU KUKATAA KUCHANJWA.na KAMA CHANJO INAFANYA KAZI INAVYOTAKIWA INATAKIWA IKUKINGE NA UGONJWA.NDIYON MAANA CHANJO NI HIARI .KWAMBA WEWE UNAYECHANJWA HUTAAMBUKIZWA AU UKIAMBIKIZWA USIFE.

Mbona hepatitis B Vaccine hatualazimishani?kwani hepatititis B Hiuwi?

Jioni njema
Kitu kinaniuma kabisa ni mwanangu wa form one wakike eti kachanjwa sindano ya kinga ya kansa ya kizazi...siku hiyo katoka shule ananiambia mama tumechoma sindano asee niliumia na bado naumia..mpaka nataman nikafungue kes mahakamani...hata cjui hatma ya mwanangu akiwa mkubwa walah..
 
Waziri keshasema yeye binafsi yupo tayari kwenda nae popote kuthibitisha madai yake. Ataje mtu aliechanjwa maji atapelekwa atapimwa antibodies mbele yake.

Ina maana hata akitajwa yeye (waziri) yupo tayari kupimwa antibody, mbele ya mchungaji kuonyesha uongo wake.

Ndugu kuhusu usalama wa chanjo kuna nchi zishachanja 80% ya adults over the age 18 sasa hivi wapo kwenye majaribio ya chanjo kwa under 17.

Human trial ya under 17 years nimekuwekea video jana imeanza five months ago, sasa hivi bado wana monitor reactions za volunteers waliochanja, go ahead ya kuanza kuwachanja hilo kundi lote bado.

Kila kitu kinakwenda kutokana na medical requirements, hakuna short cuts.

Ngoja nikupe testimony yangu ya COVID mimi nilipata sasa kuna wengine reaction yao ni tofauti na hata hayo maelezo ya wataalamu wanaotupa ndio maana wanasema ni ugonjwa mpya ata wao wataalamu bado wanajifunza with new information.

Sasa what happened to me, to cut the story short mie nilipata mid March mwaka jana na elimu tuliyokuwa tukipewa attack ni siku 7-14 hiyo kwa wale wataopata homa. Basi homa kali likanitandika kama kwa siku 10 hivi ya 11 nikapona nikawa fresh kabisa.

Upumbavu wangu siku ya 12 nikanywa vodka (anyway nilikuwa najiona, poa kabisa) kilichotokea kesho yake ilirudi homa kali ya mara ya kwanza afadhali. Na hii ya safari ya pili nilikaa nayo kuanzia late March- mpaka mid May 2020, kwenye hizo siku leo unaamka asubuhi mzima jioni homa. Kesho siku nzima mzima, keshokutwa upo hoi na homa yaani ni up and down for six to seven weeks.

Na baada ya kupona in May nilikuwa sitoi makamasi kabisa yaani hata nikijaribu unatoka mvuke tu na aushuki unabaki juu baada ya dakika kadhaa huo mvuke unaganda inabidi uchokonoe pua kukakwangua ndio utoke na ukiushika ukoko wenyewe ni mgumu kama jiwe.

Hiyo hali nimeenda nayo mpaka mwaka huu April 2021 nilipopata jab ya kwanza, baada ya sindano usiku huo huo ndio makamasi yalianza kuchuruzika for the first baada ya karibu mwaka (bila ya kusahau ata mkojo wangu ulikuwa ni wa njano tu, ule wa rangi ya dehydration indication ata ninywe maji vipi).

Sasa nina uhakika kwa wale COVID iliyotupiga kwa homa ya week 6-7 kila mtu ana story yake; kuna dada namjua na yeye aliugua muda sawa na mimi; yeye mpaka December mwaka jana alikuwa kuna siku moja au mbili kwenye mwezi homa linamwendea mpaka alipochanjwa yeye ni nurse December ndio hiyo hali ilipoisha, kama mimi side effects zangu zilivyopotea.

So what am I trying to say COVID 19 bado wanasayansi wanajifunza madhara yake, however vaccine helps asikwambie mtu.

Tatizo la huyu Gwajima sio kupinga with merit na uongo juu anawatungia wahusika to justify his position, now that is just stupid.

Pole kwa kupitia athari za kuambukizwa na kuugua UVIKO-19.

Maelezo yako ya kupona, baadhi ya athari za ambukizo, baada ya kupata chanjo yanazua maswali mengine ya kisayansi.
︎ kwamba ukiambukizwa ugonjwa wa kirusi ukapona unakuwa na kinga ya huo ugonjwa, je, iweje kuwe na ulazima wa chanjo?
︎ hizo athari za ambukizo baada ya kupona (homa, mafua makavu, nk) yaonekana ni baadhi ya madhara ya ugonjwa, je, wataalamu wa afya walikushauri nini kabla ya kupata chanjo?

Kwamba So what am I trying to say COVID 19 bado wanasayansi wanajifunza madhara yake, however vaccine helps asikwambie mtu inazua maswali anayouliza Gwajiboy. Isije kuwa chanjo kwako imekupa nafuu ya athari za kuambukizwa kuliko ambaye hajaugua kabisa?

Kwamba Tatizo la huyu Gwajima sio kupinga with merit na uongo juu anawatungia wahusika to justify his position, now that is just stupid ni maoni yako binafsi lakini kwangu maswali yake yamenisaidia kufanya maaumuzi sahihi kuhusu kuchanjwa au la.

Msimamo wangu uko palepale kuwa waliochanjwa, hasa viongozi walioonesha mfano wa kuchanjwa, akiwemo Rais SSH, wafanyiwe vipimo kuthibitisha kuwa miili yao imetengeneza kinga. Kinyume chake nami nitaendelea kuamini walichanjwa "placebo"

VIONGOZI watupe majibu ya kisayansi kuhusu ubora na usalama wa chanjo ili watu kama Gwajiboy wapuuzwe
 
Ukweli uko wazi, chanjo hazijapitia stage zote zinazotakiwa kwa chanjo kukamilika.
Hawawezi kujibu kisayansi kwa sababu kisayansi hawajatimiza hatua zinazotakiwa.
Most likely, wanapoulizwa maswali magumu kama hayo wanakimbilia kwenye vitisho; usipochanjwa utaambukizwa, ukiambukizwa utakufa, nk.
Hakuna anayejua kwa hakika 'long term effects' za hizi chanjo.
Tunaohoji tusitishwe, tuna uhuru wa kuhoji.
Hizo stages haziwezi kuwa fupi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia? Kama unaamini hizo stages kuwa inabidi zifuatwe, kwanini ushindwe kuamini hao walioziweka wanavyotwambia kuwa chanjo ni salama?
 
Angalia na hiyo documentary imetengenezwa kabla COVID kulipuka. Kwa hawa wenzetu ata intervention zao sio kwamba za kukurupuka watu walishafanya simulations zao ikitokea pandemic wana handle vipi.

Kwenye hiyo documentary utaona dawa zimekuja haraka kwa sababu nchi nyingi zilikuwa na research zao za kinga ambazo zimejikita ni kwa namna gani wanaweza tweak existing vaccine to fight future similar viruses wakishawaelewa kwa haraka.

So research nyingi azijaanzia from scratch kulikuwa na ongoing work already. Nachokubaliana na wewe ni kutokulazimishana chanjo.

Hila Gwajima lazima adhibitiwe he is too much, he has to behave.
Pia anawazushia viongozi kuwa wamehongwa na mabeberu na pia walifeki kuwa wamechanja.
 
Back
Top Bottom