Kenya 2022 Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) inajitengenezea bomu kupitia kile wanadhani ni Uhuru wa Vyombo vya Habari

Kenya 2022 General Election

Wazo Kuu

Senior Member
Oct 21, 2018
114
293
Habari wakuu!

Najua kwa siku mbili tatu baadhii yetu tumekuwa tukifuatilia kile kinachoendelea katika uchaguzi wa Majirani zetu Kenya. Kwa tathmini fupi utabaini kwamba watu wengi nchini kenya na Tanzania wamepongeza kile ambacho IEBC imefanya kwa kuruhusu vyombo vya habari kujumlisha na kutangaza matokeo ya ugombea wa Urais.

Kwa kifupi mchezo uliofanywa na IEBC unaonekana kupongezwa ila ni wa hatari kiusalama kuliko inavyodhaniwa kwani kitendo cha kila chombo cha habari kujumlisha kisha kutangaza matokeo kimesababisha matokeo kupishana na kingine jambo ambalo litaacha mtafaruku mkubwa iwapo Tume itakapotoa matokeo tofauti na mwelekeo wa vyombo hivyo.

Ni kweli Uhuru wa habari ni mzuri lakini lazima uwe na mipaka, hili jambo sio la kuliombea nchini kikubwa ni kuwaombea Mungu matokeo ya Tume yasiwe tofauti sana na matokeo yanayowasilishwa kinyume na hapo majirani watachapana soon.

ANGALIA CHINI TOFAUTI YA TAKWIMU BAINA YA VYOMBO VYA HABARI.

NB: HADI MATOKEO YANAYOENDELEA HAYAHUSISHI KURA ZA MAGEREZANI NA BALOZI MBALIMBALI.

NTV.jpeg
KBC.jpeg
K24.jpeg

===SASA WENYE JAMBO LAO WAEANZA KUTOA TAKWIMU ZA MATOKEO...NAWASIHI TUSIKIMBIANE NA MEDIA ZENU ZIMEFIKA ASILIMIA 99 YA KURA ZOTE ZIME STUCK ....

FZ5zqxIWAAMZhRK-1.jpg
 
Ambacho huelewi ni kwamba,kila chombo cha habari kina maripota wake kwenye maeneo yote, kwahiyo taarifa za matokeo ya awali haziwezi kulingana. Ila matokeo ya jumla yatalingana,shida unaonekana umemzoea mfumo mfu wa CCM kufanya uhesabuji wa kura kuwa siri.

Kama kweli Tanzania inapenda democracy,ijifunze kutoka Kenya,no janja janjaa.
 
Asipokuelewa basi tena tutajua ana udumavu wa akili.
 
Tatizo jingine ni kila chombo cha habari kuwa na interest za kumpigia debe mgombea mmojawapo. Hivi vyombo vya habari vya kenya vinaleta mkanganyiko wa ni yapi ndio matokeo ya kweli
 
Mkuu nadhani ni kwa muda tofauti kura zina tofautiana kuna wakati Ruto anaongoza kuna kipindi Raila anaongoza sasa wewe ulileta screenshot ya KTN wakati Raila alipoongoza ni KBC ukaona Ruto anaongoza kumbe ni wakati na katika majimbo jofauti.

Wakenya wana akili hawawezi kuchanganywa na hilo labda kwa nchi ya wajinga Tanzania
 
Mwisho idadi ya kura inatakiwa iwe ileile ifanane.Ulitaka wazime mitandao ya kijamii na wajifungie sehemu ili wafanye wizi?

Alitaka wanahabari wakamatwe wapotezwe, vyombo vya habari wasifie chama tawala mda wote, wanajeshi wavalishe uniform za police wazagae mitaani na kupiga watu kama kule Zanzibar, wazime mpaka mitandao kama hapa Bongoland, ila Tanzania kuna ujinga mwingi mpaka naona aibu kua Mtanzania.
 
Na hiyo akili imewaingia vichwani mwao sana.Alaaniwe aliywafundisha ujinga huo.Laana kum kabisa!
 
Back
Top Bottom