Tume ya mabadiliko ya katiba

Tume ya mabadiliko ya katiba

Siamini kama haya ni maneno ya Mzee wetu mtei.
Katika mambo ambayo yameturudisha nyuma waafrika kwa takribani karne nzima ni haya ya udini.Hizi dini zimetugawa tumeshindwa kuaminiana hata kuheshimiana.Tumefikia mahali pakuanza kunyoshean vidole sio kuhusu ufanisi wa mtu bali yeye ni wa dini gani.

Sinzani kama ni sahihi kuanza kubaguana kidini

Mtoa mada (Mtei) ana habari kuwa hao waisilamu walio wengi wamepta elimu wakiwa shule zenye misingi ya kikristo ama shule za mchanganyiko wakristo na waislamu!. Muisilamu ama mkristo huwezi mtambua kwa jina ,tupo wengi sana tz wenye majina tofauti na dini zetu. Ni dhahiri waafrika tulio wengi ambao wamepata elimu dunia suala la udini halina nafasi kama alivyoonyesha mtoa mada (Mtei).
 
Naona kuna magamba amejaribu kutumia identity ya mtei ili kumchafua.namshauri mtei alishitaki gazetila jambo leo. Awadai kama 100billioni hivi
 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.

Mkuu bila kujali kama maneno haya kweli ni ya mtei au si ya mtei, ukiangalia utaona kuwa issue hapa ni katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si ya Tanganyika. Kama tuna nia ya kweli ya kuwa na katiba ambayo ni ya watu wote, si ya wanasiasa tu, ni vema watu WOTE(si wanasiasa tu) wakahusishwa. Na kuhusihwa kwa watu hakuna maana ya idadi tu. Zanzibar inaweza kuwakilishwa na wanasheria mazuzu 100 lakini wasifanye lolote la maana kutetea maslahi ya wazanzibar, lakini inaweza kuwakilishwa na mmoja tu aliyewiva na maslahi ya Zanzibar yakazingatiwa ipasavyo. As always mkristo, mhindu na msukusu wakieleza maoni yao kuhusu representation yao ni udini lakini waislamu wakilalamika wanalalamika kuhusu ukandamizaji dhidi yao.

Weka mbali, udini na ujinga mwingine, ukweli ni kuwa hakuna kipya kwenye tume ya katiba ya sasa. kazi yote ilifanyika na vipengele vyote vya katiba vinavyotakiwa kubadilishwa vinafahamika, so inawezekana kuwa ni mchezo unafanywa ili kujustify katiba itakayowafavour watawala.
 
Tunatafuta katiba ya Tanzania.Mie naongea kama Mtazania bara kuwa tume yetu imejaa Wakirsto wengi.
Jibu zuri pamoja na kwamba umechukuwa muda kujibu, kama tunatafuta katiba ya Tanzania, mimi naongea kama mtanzania kuwa tume yetu imejaa waislam wengi.
 
Mlitaka asiseme? yale yale ya mkataba wa muungano hayakusemwa na kuwekwa wazi wakati ule baadae leo ndio tunalalamika. Acheni kila kitu kiwe wazi hii ni katiba ya watanzania si ya watu wachache au kikundi fulani kipendelewe. Maana haiingii akilini Zanzibar asiwepo hata mkristo mmoja, hata kama 99% ni waislam hao 1% wana haki ya kuwakilishwa mawazo yao. Tumeona juzi wawakilishi wanataka kuwabagua watanganyika, tunasikia makanisa yanachomwa nani basi atawasemea kwenye kamati hata mmoja asiwepo? hapana.

Naungana na Mtei, kuna haja ya kuendelea na majadiliano hata baada ya kuundwa kwa katiba mpya.
 
Udini umeanzishwa na Kikwete mwenyewe anataka kuturithisha kupitia katiba kitu ambacho nafikiri hatoweza ni sawa na kuchezea kiberiti karibu na pipa la petrol.
Feedback,
Mwalimu siyo kwamba alikuwa anazuia udini, ukimsoma vyema, utagunduwa alikuwa vitani kujaribu kuutokomeza.Udini ulikuwepo na bado upo.
 
Hakuna sababu ya kukwepa ukweli kuwa hakuna hisia za kidini katika hiyo tume ya katiba!

Kupuuza kwa kujifanya kuwa ati udini umetutenga katika masuala ya msingi kwa miongo kadhaa ni upofu na kuipindisha kweli iliyo dhahiri, fanya utafiti rahisi tu hata hapa JF wale wanaojinasibu kama waislamu wamekuwa wakitetea viongozi kwa dini zao ni tofauti na upande wa pili, tumeshuhudia kina Mkapa & co. wakisulubishwa kwelikweli na watu wa dini zao tokana na makosa yao katika jamii!!

Mzee Mtei ana point, take it from me!! Otherwise lets wait and see 'zao' la tume hii ya katiba. Watu wengi wanaopingana na hoja za mzee huyu huenda hawataki kutafakari makusudi au wanaficha ukweli kupitia mwamvuli wa ubaguzi(udini, ukabila, jinsia et al) lakini kwa maslahi mapana ya taifa letu ni bora tufikiri nje ya bongo zetu.

Kasoro za tume hii ni nyingi sana ila baadhi kwa mtazamo wangu ni
  1. tume ina taswira ya kidini
  2. taswira ya kichama
  3. haijazingatia ulali wa uwingi wa watu- this is not political warfare rather it is MATHS.
Endapo tutapuuzia masuala haya ya kimsingi ni wazi kabisa katiba itayokuja itakuwa na mgogoro mkubwa na huenda hawhawa CCM wakaipigia chapio isipite kwa kutumia Udini huohuo sababu kwa namba hii tutegemee kuwa na mambo kama mahakama ya kadhi n. k

Matokeo ya tume hii hayatapita na watasema tuendelee na katiba ile ile ya zamani!!!
 
Wengi wanaopingana naye si watu walioko "free minded" chunguza utaona huwa wana mwelekeo gani.
Wengi wao wana hisia kali sana za kidini, yaani double standard balaa!
 
Feedback,
Mwalimu siyo kwamba alikuwa anazuia udini, ukimsoma vyema, utagunduwa alikuwa vitani kujaribu kuutokomeza.Udini ulikuwepo na bado upo.
Ndio nakubali kuwa udini ulikuwepo tangu enzi za mwalimu lakini umekuja kuwa wazi zaidi wakati wa Kikwete anauchekelea na anaupenda kwa vile wanamsifia, mbona wakati wa Mkapa haukuwa wazi namna hii?
 
Watu wanasema, ooh "hawa wajumbe wanaenda tu kukusanya maoni"

Sasa kama unataka kutengeneza fruit punch, halafu una watu kama watano, wengi wao wanapenda "mapapai", ukiwatuma wakalete matunda ya kutengeneza fruit punch, ambayo huwa inatumia matunda ya tofauti, wakikuletea mapapai mengi utashangaa?

Je itakuwa fruit punch?
 
Wana JF tusiwe kwenye "state of denial" , lazima tuingalie kwa makini kauli ya Mzee Mtei kuwa haikutakiwa kutolewa na mtu kama yeye kwanza akiwa ni mzee makini na pia muasisi wa CDM ambayo tunahangaika kutwa kucha kuitafutia uhalali katika maeneo yenye waislam wengi kwa vile hata tukichukua Nchi leo hatutaweza kuongoza kwa ufanisi bila kuungwa mkono na jamii pana ya ndugu zetu waislamu. Itakuwa jambo baya kama kila kitu tutadai kiwe sawa au wakristo wazidi, tunajua katika mfumo wa serikali kuna wakristo wengi sana mpaka baadhi ya ndugu zetu waislam wanaiita "christian bureaucracy" tafadhali tusifike mahala tukakiangalia kila kitu kwa mtazamo wa kidini kufanya hivyo unajipambanua kuwa wewe ni mdini bali tupime kwa vigezo vya weledi na uadilifu. Mwisho kauli ya Mtei ni kauli yake binafsi na wala si ya CDM!

leo umekuwa msemaji wa cdm sio?.au ww ni mnyika?.wacha wafu wazike wafu wao.
 
Mkuu ritz, Mzee Mtei ametahadhalisha kitu ambacho ni mhimu kabisa kwamba udini unaolinyemelea taifa la TZ ni mhimu kuondokana nalo kwa kuziba ufa kuliko kukubali kujenga ukuta. Ritz mapovu yamekutoka humu kwa sababu za ajenda yenu ya kutaka serikali ya TZ ifungamane na dini ya Kiislam period! kwa kuanzia na Mahakama ya Kadhi, OIC, na baadaye mudai kwa nguvu taifa la TZ kuwa la kiislam. Bila kumung'unya maneno waislam hamtakuwa tayari kuwavumilia wakristo, kwa kuwanzishia vikundi vya mauji kama vile vya Bhoko Haram, Mjahideen, alkkaida alshababu; Hivyo kuanza kuwaua wakristo kwa kuwalipua kwa mabomu.

Note: Kwenye serikali za Kiislamu wakristo hunyongwa kwa kosa la kumhubiri Yesu tu. Nani awe tayari kuingia kwenye mtego wenu huu? Angalia kule Naigeria kikundi cha kiislam cha Bhokoharam wanavyowaua wakristo kwa kuwalipua kwa mabom bila kosa lolote.

Hoja hafifu sijapta ona katika maisha yangu.Kwenye red ni TOTAL UPOTOSHAJI.Kimsingi mkuu jitahidi kuficha ujinga.
 
Kama ni nchi mbili sawa sawa mbona hakuna katiba ya Tanganyika? ,Mbona hakuna rais wa Tanganyika?
Watanganyika tudai katiba yetu kwanza, baada ya hapo tuandike katiba ya Muungano.
 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.

Zanzibar sio nchi kamili, ni sehemu ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania
 
Wengi wanaopingana naye si watu walioko "free minded" chunguza utaona huwa wana mwelekeo gani.
Wengi wao wana hisia kali sana za kidini, yaani double standard balaa!
Ni kweli mi sioni cha kuficha hapo!!

Udini umejaa hiyo tume...

Hakuna tofauti kati ya JK na King Mithridates VI Eupator, King of Pontus (123-63)

Yatubidi tukae chonjo na kufahamu tu ya kwamba hakuna tofauti kati ya Mwislamu wa Bara na yule wa Zanzibar, wanazungumza Lugha moja, tukipuuza tuwe tayari kuendlea na katiba hii hii!!
 
Watu wengi humu wanaoitetea hii tume ya sasa, wengi wao ukiangalia kiundani, wamekuwa wakilalamika kuwa dini yao inanyanyaswa.

@werea, nakubaliana na wewe, hao wanaodai bara kuna wakristo wengi kwenye tume ya uwakilishi, wanasahau kuwa bara haina katiba yake na si nchi kama ilivyo Zanzibar.
 
Back
Top Bottom