Tume ya mabadiliko ya katiba

Tume ya mabadiliko ya katiba

Mkuu hao wanaolialia na kukemewa waache udini huwa hawataki dini yao ndio wawe wengi HAPANA, wanataka uwiano sawa kama anavyotaka Mtei......... two wrong

Naaw!Still irrelevant mkuu!

Mbona hawataki uwiano sawa kwenye katiba ya Tanzania kama hapo kwenye bold pana ukweli wowote?

Ama wewe unaizungumzia katiba ipi?

Umeipitia hii thread vyema toka mwanzo?
 
The worse part I always see behind this ID is hipocricy, idiocy, doublestandard, political arrogance et al!

The good part is that this ID is dented with Intellectualism.

Ushauri: Kuwa muwazi na mkweli kwa faida ya nchi yetu...

I reserve my comment on this Mkuu
 
UKWELI?..........ukweli upi mkuu unaouzungumzia wewe hapa
Haya ni maoni yake tu mkuu, na hapa tunazungumzia impact ya maoni yake katika jamii kutokana na influence yake
The open fact is waislam 23 na wakristo 11 huo ndio ukweli wenyewe.
 
Licha ya kwamba J.K. kajitahidi kuwa na vigogo kweli kweli, na Katiba ya sasa imezingatiwa ktk kuandaa m'badala wake, muundo wa hii Tume umedhihirisha kwamba demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania wa leo. Kama tunanuia kwa dhati kuwa na Demokrasis ya kweli, itabidi Watanzania wanaoamini kwamba hilo ni muhimu, waendelee na juhudi za kuandaa hata Mabadiliko kwa Katiba Mpya ijayo.

Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.

Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.

Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.
I hope haya ni mawazo na mtazamo wa Mzee Mtei na sio ya chama Chadema.
 
Mzee Mtei asante kwa maoni yako

Hata mimi JK amenihuzunisha na kunisikitisha sana kwasababu zifuatazo:

a. Viongozi wote wa juu wa tume ni Wakristo tena fundamentalistis kama wewe..hivyo nategemea katiba hii kujaa mambo ya kikanisa..

b. Ukiangalia wajumbe wa 15 kutoka Tanganyika 4 tu ndio waislamu hii inaonyesha dhahiri kuwa Tanganyika wanawajali zaidi wakristo kuliko waislam, hivi Tanganyika ni nchi ya kikristo???

c. Kuhusu wajumbe 15 vs 15 kutoka pande zote za muungano hiyo ni kwa mujibu wa sheria; ndio maana wakati ule chama kilipoenda kunywa joice ikulu niliwauliza kitu hasa mmekibadili kwenye sheria?? kama kawaida pro-chadema wanaogopa kuwauliza makamanda wao..(hivyo hoja yako ni dhaifu sana mzee wangu)

vp ulisahau kama rais alisema watu wapeleke majina ikulu wao walikua wapi jk kasema kateua watu kutokana na mapendekezo ya majina aliyo pelekewa aisee nyiny pipo...
 
The open fact is waislam 23 na wakristo 11 huo ndio ukweli wenyewe.

Yes ofkoz,,,,,, that is the fact waislam23, wakristo11 na hili sio tatizo

Tatizo ni kwanini iwe kichekesho kwa Mtei, kwanini itakuwa ndoto kufikia demokrasia kwa mujibu wa Mtei?...........is this u called FACT?

Hiki ndicho tunajadili.
 
Yes ofkoz,,,,,, that is the fact waislam23, wakristo11 na hili sio tatizo

Tatizo ni kwanini iwe kichekesho kwa Mtei, kwanini itakuwa ndoto kufikia demokrasia kwa mujibu wa Mtei?...........is this u called FACT?

Hiki ndicho tunajadili.
Hebu jisome kwenye red naona umeshajijibu.
 
I hope haya ni mawazo na mtazamo wa Mzee Mtei na sio ya chama Chadema.

Nyika kayakanusha hayo kuwa sio msimamo wa chadema lakini tunajua nguvu na ushawishi wa mtei katika chama kwa hiyo tunaelewa bila shaka kuwa huu ndio msimamo wa chama. FULL STOP
 
Hebu jisome kwenye red naona umeshajijibu.
Mkuu acha kuruka vihunzi bana, i know you can tackle this..........come again
Yes ofkoz,,,,,, that is the fact waislam23, wakristo11 na hili sio tatizo

Tatizo ni kwanini iwe kichekesho kwa Mtei, kwanini itakuwa ndoto kufikia demokrasia kwa mujibu wa Mtei?...........is this u called FACT?

Hiki ndicho tunajadili.
 
Mkuu acha kuruka vihunzi bana, i know you can tackle this..........come again
Wewe unajitungia swali unategemea mimi nilijibu. Mimi nimesema facts ni waislam 23 na wakristo 11, hayo mengine ni yako.
 
yaani nimesoma hii thread mpaka mwisho, I was hoping nitakuta post ya mzee Mtei on the way, ikikanusha kuwa si yeye aliyeanzisha hii thread.
issue ya udini ni very delicate, especially kwa CDM ambao wamekuwa accused several times kuwa chama chao ni cha kidini. Kwa sababu hiyo sidhani kama huyu mzee ameoverlook hii issue kwa kutoa msimamo alioutoa, unless otherwise ana malengo fulani.
Nawaasa watanzania wenzangu, muwe makini sana na vyama vya siasa vinavyoanzishwa na hawa wazee (former CCM & govt officials). Wengi wao unakuta ni Usalama wa Taifa, wapo kazini kutudistruct watanzania.

Thank you for listening
 
Fact zipi mkuu?
Fact nyingine ni wazanzibari 1.5milion kuwakilishwa na wajumbe 15 sawa na watanganyika milion 42 kuwakilishwa na idadi sawa ya wajumbe wewe huoni tazito hapo.
 
Kwa wenye akili timamu tuliisha tambua Mzee Mtei kachemka
Na kwa barua hii rasmi ya CDM inaonyesha pia CDM wametambua kuwa mzee wao kapotoka

Kwangu mimi ili mradi CDM wameliona hili hadi kufikia kulitolea tamko ni ishara tosha kuwa Mzee wetu amaeghafikirika kidogo hadi chama kikaamua kumnawa mapema.
Nashukuru CDM kuliona hili mapema

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwamba maoni binafsi ya viongozi na wanachama wasiokuwa na mamlaka kwa mujibu wa katiba, kanuni na itifaki ya chama kuwa wasemaji wakuu wa masuala ya chama katika ngazi husika yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa taarifa hii kufuatia maoni binafsi ya muasisi na mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA juu ya wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba yanayoelezwa kutolewa katika mtandao wa jamii wa Jamii Forums kutafsiriwa kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa mwito kwa wachangiaji katika mitandao ya kijamii na wananchi kwa ujumla kuzingatia kuwa CHADEMA bado haijatoa kauli juu ya wajumbe wa tume husika kwa kuwa bado CHADEMA inaendelea kufanya uchambuzi juu ya wasifu wa wajumbe wa tume husika na mchakato wa uteuzi wao kama tulivyoeleza kwenye taarifa kwa umma tuliyotoa tarehe 7 Aprili 2012.

Hata hivyo, izingatiwe kwamba uchambuzi wa wasifu wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika unaoendelea kufanywa na CHADEMA hauhusu dini za wajumbe wa tume kwa kuwa CHADEMA hakiamini katika udini bali unahusu uwezo na uadilifu wa wajumbe husika na iwapo umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Izingatiwe pia kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya 3B kifungu cha 3.1.9 ikiwa ni sehemu ya misingi iliyopo kwenye itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati, CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola na na misingi mingine ya CHADEMA ya kujenga chama na taifa lenye kutoa fursa kwa kuzingatia uwezo na uadilifu bila kujali tofauti zingine.

Pamoja na kujulisha umma kwamba CHADEMA kinaendelea kufanya uchambuzi wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika, tulieleza kuwa CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Tunasisitiza umuhimu wa Serikali kutoa kauli kwa umma kuhusu ratiba ya marekebisho ya awamu nyingine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 kwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Bunge imetangaza kuwa Mkutano wa Bunge utaanza tarehe 10 Aprili 2012 bila marekebisho ya sheria ya katiba kuwa sehemu ya orodha ya miswada ya sheria inayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa saba wa Bunge.

Tunarejea kuutarifu umma kuwa Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 itafanya kikao chake karibuni mara baada ya uchambuzi kukamilika kupitia taarifa ya uchambuzi unaofanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Imetolewa tarehe 09 Aprili 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Zanzibar sio nchi kamili, ni sehemu ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania

Mkuu inategemea unatumia definition gani ya nchi. Ukiangalia unaweza kuona kuwa Zanzibar ina rais, waziri Mkuu, spika wa bunge, baraza la mawaziri, mahakama yake na NGO zake. Ina taasisi zote za kuifanya iwe na sifa ya kuwa nchi. Lakini Tanganyika haina taasisi kama hiyo hata moja, ninachofahamu ni kuwa kuna kitu kinaitwa Tangayika Law Society, hicho pekee haina maana yoyote, kwanza kinaweza kuwa na members kutoka Znz kwa hiyo hata ule utanganyika wake haupo So Tanganyika kimsingi imekufa, labda ifufuke kwanza ndio tunaweza kusema kuwa kuna Tanganyika.

All in all katiba inatakiwa kuwa ya maana, ya sasa iliyopo ni ucharwa, na hata make up ya wajumbe wa katiba inatia shaka sana kama kutakuwa na genuine change of the contents tunazolalamikia.
 
Ningekuwa natumia pc ninge copy official statements ya Mnyika
 
Back
Top Bottom