Tume ya mabadiliko ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya mabadiliko ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Edwin Mtei, Apr 8, 2012.

 1. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Licha ya kwamba J.K. kajitahidi kuwa na vigogo kweli kweli, na Katiba ya sasa imezingatiwa ktk kuandaa m'badala wake, muundo wa hii Tume umedhihirisha kwamba demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania wa leo. Kama tunanuia kwa dhati kuwa na Demokrasis ya kweli, itabidi Watanzania wanaoamini kwamba hilo ni muhimu, waendelee na juhudi za kuandaa hata Mabadiliko kwa Katiba Mpya ijayo.

  Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.

  Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.

  Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.
   
 2. K

  King kingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kiongozi heshima kwako
  Kwa mtazamo wangu, Tanzania ya leo waislamu/wakristo ni wachache sana wengi wetu tumebeba majina tu ya hizo dini ila hatufanani kabisa na imani wala matendo yake.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

  Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

  Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
  Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mzee Mtei,

  Heshima Kwako. Kwanza kabisa mimi nakuunga mkono asilimia zote na kiukweli Tume hii imebeba Wazanzibari wengi kuliko watanzania bara ile hali katiba inayobadilishwa ni ya Tanzania Bara... Sidhani kama zanzibar wana matatizo zaidi ya tunayopata sisi.

  Nilchokiona hapa ni dhamira ya kuwa Katiba mpya haipo kwa hawa CCM lasivyo kuna malengo ya Mtu fulani au upande fula yanataka kutimizwa kupitia tume hii...

  Hivi ina maana watu wote tanzania Bara wakihiji jambo fulani liwepo kwenye katiba mpya maana yake ni hadi ridhaa ya watu 1.5mil siyo..

  Hii haikubaliki na hata kama ni kwa gharama ya kuvunjika kwa muungano.

  Mimi ni Raia wa Kawaida na sioni nachofaidika na muungano zaidi ya wanasiasa.. Watanzania Bara tusiogope na tuwe na Moyo. Kwa sasa nachokiona kwa CCM nikuhakikisha wanatimiza kila kinachotakiwa kwenye ule muungano
  '
  MIMI NINGESHAURI KAMA INAWEZEKANA WATUMIE ILE RATIO YA WABUNGE WA BARA NA ZANZIBAR KWENYE BUNGE LA MUUNGANO KATIKA TUME HII, NA KATIKA MAAMUZI KUHUSU MAMBO YA BARA WAAMUE WANAOTOKA BARA NA ISSUE ZA Z'BAR WAAMUE WA KULE.

  Hii tume utafikiri tuna idadi sawa ya eneo na watu. Zaidi mimi naona itafika mahali tutakuwa na 50% kwa kila kitu bila kujali nini.
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ukweli unabakia pale tu hata kama huutaki.. Acha kumhangaisha mzee wa watu wakati kasema point na ushahidi upo. Refer kwenye majina ya tume.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu namuhangaisha vipi wakati kaleta mjadala jamvini namuheshimu Mzee Mtei kama unavyomuheshimu tunajadili alichokileta.

  Kuna watu wengine kutoka Tanganyika wanalalamika pia kuwa JK kachagua Wakiristo wengi kuliko Waislam.

  Waislam wa 4 tu wakati Wakirsto 15 na wakuu wa tume wote wakiristo Jaji J, Warioba, Jaji A. Ramadhan.
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo wewe hukubaliani na huu uteuzi siyo? Basi kumbe tuko pamoja sasa ndiyo toa mawazo yako na sii kunyooshea kidole kwa mwingine....
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mie sijamnyooshea kidole mtu mwingine nimeandika nachokiamini.
   
 9. S

  SURURU Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa we ndo Mdini
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mzee Mtei,
  Heshima mbele Kamanda! Kesho nakuja Arusha kikazi ntakuja kukutembelea nyumbani.
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mzee Mtei asante kwa maoni yako

  Hata mimi JK amenihuzunisha na kunisikitisha sana kwasababu zifuatazo:

  a. Viongozi wote wa juu wa tume ni Wakristo tena fundamentalistis kama wewe..hivyo nategemea katiba hii kujaa mambo ya kikanisa..

  b. Ukiangalia wajumbe wa 15 kutoka Tanganyika 4 tu ndio waislamu hii inaonyesha dhahiri kuwa Tanganyika wanawajali zaidi wakristo kuliko waislam, hivi Tanganyika ni nchi ya kikristo???

  c. Kuhusu wajumbe 15 vs 15 kutoka pande zote za muungano hiyo ni kwa mujibu wa sheria; ndio maana wakati ule chama kilipoenda kunywa joice ikulu niliwauliza kitu hasa mmekibadili kwenye sheria?? kama kawaida pro-chadema wanaogopa kuwauliza makamanda wao..(hivyo hoja yako ni dhaifu sana mzee wangu)
   
 12. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mzee Mtei..! heshima yako! ila nadhani unakosea pale unapoangalia majina na kuhusisha ni watu wa imani flani..! kuna kina Abdallah.. ambao ni waislam jina jina!... kuna kina john ambao ni waislam majina tu!..

  tuweke huu udini pembeni....
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mzee Mtei kasema mambo ambayo watu wengi wanayasema, tofauti ni kwamba yeye amekuwa na ujasiri wa kumwaga mboga hadharani na sio kuguna kichinichini. Wakubwa wanaweza kuamua kumwaga ugali au kuuchuna.
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mmmhhhh!!! hata mimi siamini mzee Mtei kweli ndiye anaweza kuandika kilichoandikwa hapo juu.

  Naamini ni msomi mzuri ambaye kabla ya kuandika lazima aziangatie facts mbalimbali zilizo wazi. Tunaweza kupinga uwingi wa watu kutoka Tanzania visiwani kwenye tume hiyo. Hilo ni suala la katiba zaidi na perception of fairness. Ili katiba ikubalike sehemu zote ni muhimu kwa Tanzania visiwani kuhisi wameshirikishwa ipasavyo.

  Sasa tukiacha hilo, asilimia 99 ni Wazanzibari ni Waislam kwa majina pamoja na dini. Hivi kweli ulitegemea kwenye tume ambayo ina uwakilishi sawa wa bara na visiwani majina ya kislam yafanane na ya kikristo? Hii haiwezekani logically and factually.

  Ili premise yako ya kuwa na uwiano wa majina ya Kiislam na Kikiristo ifanane ni lazima majina yote ya Kiislam yaondolewa kwa watu wa bara au watu wenye majina ya kikristo watafutwe zanzibar hata kama hawana sifa. Hiyo less than one percent ya Wazanzibar wakristo wawakilishe nusu ya tume kwa Zanzibar. kwa mawazo nyangu hilo haliwezekani.

  Hizi dini za kuletewa na wageni inaelekea zimeingia sana vichwani mwetu.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mzee Mtei,
  Upande wa Waislam umetumia majina kuwajua ulivyokuja upande wa pili unasema kuna Wakiristo na wengine hawana dini...ebu tutajie nani hana dini kwenye hiyo tume ya mabadiliko ya katiba.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  FJM,
  Hakuna ujasiri wowote mzee wetu kateleza kwenye ili.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,564
  Likes Received: 18,298
  Trophy Points: 280
  Mzee Mtei, mimi nakuita baba kwa sababu nimesoma darasa moja na mtoto wako Meli.

  Pili nakupongeza kwa kutoa maoni yako kuhusu hii tume, bali lazima nikiri wazi, baba umeanza kuzeeka!.

  Hii ni tume, kazi ya tume sio kutupatia katiba bali ni kukusanya maoni, hii inamaanisha kazi ya tume hii ni kutusikiliza sisi Watanzania tunataka nini, halafu ndipo iya compile maoni hayo, sasa wewe wasiwasi wako wa nini?.

  Hoja zako zote mbili baba, hazina mashiko.

  1. Hili la uwiano, wa wajumbe 15 kutoka bara na 15 kutoka Zanzibar, sio la JK, hili ni takwa la kisheria ambalo ni lazima litimizwe!. Rais hapa hakuwa na choice ametimiza jinsi sheria ilivyosema.

  Kijana wako Tundu Lissu hili alilipigia sana kelele mpaka akaonekana ni mpinga maendeleo. Kwa vile wewe ni miongoni mwa visima vya hekima, busara na uzoefu tulivyo navyo, ungetoa hoja binafsi kuwa kutokana na uwingi wa watu na ukumbwa wa eneo, muungano wetu uendeshwe kwa proportional representation na sio equal basis kama ulivyo sasa!. Naamini ungesikilizwa!.

  Hizi haki za Zanzibar ndani ya muungano, zimekuwa zikikiukwa kwa miaka mingi mpaka tujajisahau kwa kudhania Tanzania bara ndio yenye haki kubwa ndani ya muungano kutokana na wingi wa watu na ukubwa wa eneo, kitu ambacho sii sawa. Tanzania na Zanzibar ni two partners wenye haki na hadhi sawa ndani ya muungano wetu kama zilivyo ndoa za kiserekali mkishaoana, siku mkiachana, mnagawana mali pasu kwa pasu na mkeo, hata kama ni wewe ndio ulikuwa umechuma hiyo mali na mkeo ni mama tuu wa nyumbani!.

  Zingatia simaanishi hii ndio uwiano bora, ila hapa rais Kikwete ametimiza matakwa ya kisheria!.

  2. Hili la pili la udini pia halijakaa vizuri, kwa vile idadi ni watu 14 toka kila upande tena kwa rais kupelekewa mapendekezo ya majina, hakuna shaka kuwa asilimia 99% ya Wanzanzibari ni Waislamu, hivyo ili kuweka uwiano wa dini, jee ungetaka hao wajumbe 14 toka Zanzibar ndio wawe Waislamu halafu wale 14 wa bara ndio wawe Wakristu?.Au hata kama hakuletewa hata jina moja la Mkristu kutoka mapendekezo ya Zanziabar, basi rais angejitafutia japo Mkristu mmoja amteua ili ionekane Zanzibar nayo ina Wakristo?!.

  Kwa vile katiba tunayoitafuta ni katiba ya nchi na sio katiba ya uendeshaji wa ibada wala kupanga utaratibu wa swala, naomba tuipe imani, hata kama inawajumbe wengi kutoka dini fulani, hadidu za rejea hazionyesha kama aumuzi wa nini kiwepo kwenye katiba mpya na nini kisiwepo, utaamuliwa kwa wajumbe hao kupiga kura, hivyo Wakristo watashindwa!. Hoja hii ya uwiano wa bara na visiwani na Ukiristu na Uislamu, utakuwa na mashika wakati wa uundaji wa bunge maalum la katiba ambalo ndilo litaamua nini kiwepo na nini kisiwepo kwa kupiga kura, na wa mwisho kabisa ni sisi wananchi, kupiga kura ya maoni "referendum" kuikubali au kuikataa!.

  Naamini yule mdogo wako mule kwenye tume, atayasimamia maslahi yako ipasavyo hata kama yuko yeye mmoja tuu!.

  Namalizia kwa kuomba radhi tena kama kutaonekana ukosefu wowote wa adabu kwa wakuu wetu.

  Asante.

  Pasco.
   
 18. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwako Pasco,

  Labda tu niseme hivi, kama tume ina dosari lazima katiba itakuwa na dosari kwa sababu ya mapungufu yaliyoko kwenye tume.

  Na lazima mambo haya tuyapigie kelele... Unajua sisi watanzania tulikuwa kimya muda mrefe tangu baada ya mwalimu kung'atuka tukafika tulikofika hadi sasa tunaonekana taifa la wendawazimu mtu unatoka huko duniani unachukua unachokita au unafanya unachokitaka na kuondoka bila kuulizwa na mtu yeyote.

  Juzi tu wakati wa Kampeni hadi baada ya uchaguzi CCM walikuwa wanasema hakuna haja ya katiba mpya mpaka ilipofika kila mwananchi kila kona ya TZ anadai katiba mpya ndiyo JK akaona ngoja aanzishe mchakato wake.

  Mchakato ambao baadaye ulitekwa tena na genge lile wahalifu wa nchi hii na kupenyeza muswada wao bado watu wakapiga kelele ndiyo tukafika tulikofika sasa.

  Nachojaribu kukueleza ni kuwa kupata Katiba mpya mikononi mwa watu wanaonufaika na katiba ya sasa ni vita viali sana kama alivyowah kusema Prince Bagenda pale UDSM kuwa kupatikana kwa katiba mpya ni mapambano.

  Kwa hiyo usitegemee tukanyamza tu, huu mchakato waliuanzisha na kuusimawa na CDM kwa hiyo ni wadau wakubwa na hasa wananchi wanaisikiliza CDM inasema nini kama hamamini basi mtakuja kuona.
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo tuseme waislam wapo 19 ukijumlisha bara na visiwani kisha wakristo wapo 11 ukijumlisha bara na visiwani
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama hakuna uwiano wa sawa sawa na Muungano uvunjike.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...