Japo siafikiani na mawazo ya Mtei kwenye hili ila ana point. Na kama tukimbeza mzee Mtei na kutaka kuanza kucheza siasa kwa malengo kumalizana kivyama, Ni wazi kuwa zitakazoumia ni Nyasi (mchakato wa kupata katiba bora). Kama ambavyo JK aliwahi kusema wakati wa kampeni kuwa nchi sasa inaanza kuchagua watu kwa kuangalia dini, basi Mtei nae ana haki ya kuongea alichoongea. Sitaki kusema kuwa password yake imekuwa hacked na si yeye ila naandika nikiwa naamini kuwa mwanzilishi wa thread ni mzee Mtei.
Anachoongea Mtei hadharani ni ambacho watu wengi wanakiongelea faragha. Mchakato huu umepelekwa kibabe bila ya kuwa na national concesus ya jinsi ya kuufanya kwa kuwa tu chama fulani kinajiona kina hati miliki. Hivi kwa mfano katika kuunda tume JK angepewa nafasi ya mwisho tu katika mchakato mzima yaani kutia saini ama kukataa ila pia kama 75% ya tume wakikubali anakuwa over ruled na mambo mengine yote yafanywe kwa kutunga sheria nzuri ya mchakato angekosa nini?. Mfano sheria ingetaja wazi makundi yote ya jamii yaliyo Tanzania kushiriki katika tume na idadi yao na Rais awe mratibu yaani apokee majina yote toka sehemu zote na kuyatangaza angekosa nini?
Mfano sheria ingesema Tume iwe na idadi ya wajumbe watakaotokana na makundi haya
- Serikali ya muungano wajumbe 5
- Serikali ya mapinduzi wajumbe 5
- Madhehebu yote ya kiislam wajumbe 3
- Madhehebu yote ya kikristo wajumbe 3
- Wasikuwa na imani ya dini hizo mbili hapo juu wajumbe 3
- Wakulima wajumbe 3
- Wafanyakazi wajumbe 3
- Wafanya biashara wajumbe 3
- Vyama vya siasa vyenye wabunge wajumbe 3 kila chama bila kujali idadi yao
- Walemavu wajumbe watatu 3
- Wasomi wajumbe 3
Pia katika sheria iweke minimum qualification ya wajumbe ni at least first degree, na kuwataka vikundi husika wawakilishe majina matatu kwa Rais ambayo yatakuwa vetted na kuangaliwa kama wamekidhi sifa za kwenye sheria na kama hawajakidhi basi majina yatakatwa na hakuna replacement. Tungeepusha manung'uniko kama haya ya Mzee Mtei. Huu mchakato tusipokuwa makini utakuwa ni igizo tu na Katiba kamili itapatikana baadae watanzania watakapokuwa na utashi wao.