ITEGAMATWI
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 5,362
- 4,125
Nadhani wanamzushia huyu mzee kwakweli!Kama kauli hii imetoka kinywani mwake basi naanza kudhani kuwa madai ya udini yanayotolewa na magamba juu ya CDM yanakaukweli fulani hivi!!
Hivi kiukweli z'bar hakuna wakristo. Maana serikali yote,bunge lote, tume ya katiba wote dini moja. Utasema hakuna cha kujadili hapa, acheni kufikiri kij....
Muasis wa CHADEMA mzee MTEI,amesema kuwa tume ya katiba iliyoundwa hivi karibu na JK imejaa waislam wengi!
SOSI:JAMBOLEO
Mimi nilichoona ina wazanzibari wengi.
duhh mzee nilikuwa namheshimu sana, kwa hili natafakari upya, kwani hiyo tume ni ya kutuswalishaa....? achunge maneno yake kwa umri na heshima alojijengea, hata kama anakerekwa ajaribu kujifichaficha, inamaana magamba wako sahihi, kuwa cdm ni chama cha udini.
Hoja ya waislamu wengi haina mashiko.issue hapa ni Wazanzibar wengi. Wanamikoa sita sisi tuna 30 lakini tunakuwa na idadi sawa ya wajumbe, hii haijakaa vyema..
Zanzibar ni nchi kama ilivyo Tanganyika. Hata kama ina watu laki moja.
Mimi nilichoona ina wazanzibari wengi.
Na wazanzibar wengi ni waislam
Asalaam Aleykum.
hata Mtei hajaongelea waisalm wengi ameongelea wazenji wengi, naona mtoa maada kaamua wazenji wengi imaanishe waislam wengi
Jk anatupeleka pabaya
sijui viongozi wa ccm watumia akili gan kufikiria,sijaona umuhimu wa kuwajaza wazenji kwenye swala la katiba kabsa-yaani kifupi jionsi walivyochangua tu wameshaniboaHoja ya waislamu wengi haina mashiko.issue hapa ni Wazanzibar wengi. Wanamikoa sita sisi tuna 30 lakini tunakuwa na idadi sawa ya wajumbe, hii haijakaa vyema..
Wana JF tusiwe kwenye "state of denial" , lazima tuingalie kwa makini kauli ya Mzee Mtei kuwa haikutakiwa kutolewa na mtu kama yeye kwanza akiwa ni mzee makini na pia muasisi wa CDM ambayo tunahangaika kutwa kucha kuitafutia uhalali katika maeneo yenye waislam wengi kwa vile hata tukichukua Nchi leo hatutaweza kuongoza kwa ufanisi bila kuungwa mkono na jamii pana ya ndugu zetu waislamu. Itakuwa jambo baya kama kila kitu tutadai kiwe sawa au wakristo wazidi, tunajua katika mfumo wa serikali kuna wakristo wengi sana mpaka baadhi ya ndugu zetu waislam wanaiita "christian bureaucracy" tafadhali tusifike mahala tukakiangalia kila kitu kwa mtazamo wa kidini kufanya hivyo unajipambanua kuwa wewe ni mdini bali tupime kwa vigezo vya weledi na uadilifu. Mwisho kauli ya Mtei ni kauli yake binafsi na wala si ya CDM!