Tume ya mabadiliko ya katiba

Unapinga tume ya katiba...kweli wewe ni m-binafsi na hulitakii mema taifa...
Mzee Mtei, ume kula chumvi tena kwa amani....hebu ondoa choko choko zako ili watoto na wajukuu zako wapitie hatua kama zako kwa AMANI...
Ulaaniwe na fikra zako za kidini na uchochezi!!!
 
Kweli nchi hii ina mambo!!! Hivi Mzee Mtei ni Mzanzibar? Maana haya madai yake yalitakiwa yaletwe na wakristu wa Zanzibar kwamba hawakutokea wa kutosha kwenye tume kwa upande wao, sasa inakuwaje yeye wa huku bara ndiye anayelalamika!!! Kwani huku bara waislam ni robo ya wakristu? Mbona idadi yao ni almost robo kwa upande wa bara? Swali la tatu, hivi waislam hawana uwezo wa kuwa viongozi wa juu kwenye tume? Mbona viongozi wakuu si wao? Pamoja na yote hayo waislam wa bara wameonyesha ninachokiita ustaarabu mkubwa kabisa kwani sisikii wakilalamika ila yeye Mtei. Ninachokiona hapa ni Mzee wangu Mtei kuchochea chuki za kidini kwani wanaostahili hasa kulalamika kutoka pande zote wako kimya ila yeye sasa anawachokoza. Pia atufahamishe kuwa yeye anataka uwiano mzuri wa kidini au anataka wakistu wapendelewe? Kama ni uwiano mzuri wa kidini basi angeongelea pande zote ikiwemo bara ya kwamba waislam hawakutendewa haki, hapo tungejua anatetea haki na si upendeleo wa kule aliko. Ina maana yeye angekuwa ndiye Rais, angeiundaje hii tume!!! Moja ya makosa makubwa kabisa ambayo amekifanyia chama chake katika hili ni kutilia uzito tuhuma wanazozitoa watu kwa chama chake muda mrefu ya kwamba ni cha kidini. Ikumbukwe kuwa yeye ni katika waasisi wa chama hicho. Watu wanapata shaka kuwa huenda ametakiwa tu kumfunga paka kengele ili waliomtuma waangalie 'reactions' za watu. Kama ziko positive kwa upande wao, basi walivalie njuga na kama ni negative kama ilivyo sasa basi wajifanye hawahusiki na yale ni mawazo yake binafsi. Hapa kuna kitu kimejificha ila wengi hawafahamu. Inaonekana Tanzania kama watu hawatabadilika na pia viongozi wa dini kujizuia na kujenga chuki za dini nyingine kwa wafuasi wao, basi kutakuja kutokea vita ya kidini hapo baadaye. Hatuombei litokee hili. Mzee Mtei hawezi kukwepa kuwa ameamua kutumika kuwa kikaangio cha vita ya udini nchini.

Niko tayari kukosolewa.

Benito.
 
hawa makafiri achana nao kwa kweli uongozi wa nchi nzima wao ndo wameshika madaraka kwa asilimia 85 haya hawayaoni ila waislamu wakiwa wengi kumbe huumia ama kweli nyani haoni kunduleeeeeeeeeeeeeeeee
Mkuu bila kujali kama maneno haya kweli ni ya mtei au si ya mtei, ukiangalia utaona kuwa issue hapa ni katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si ya Tanganyika. Kama tuna nia ya kweli ya kuwa na katiba ambayo ni ya watu wote, si ya wanasiasa tu, ni vema watu WOTE(si wanasiasa tu) wakahusishwa. Na kuhusihwa kwa watu hakuna maana ya idadi tu. Zanzibar inaweza kuwakilishwa na wanasheria mazuzu 100 lakini wasifanye lolote la maana kutetea maslahi ya wazanzibar, lakini inaweza kuwakilishwa na mmoja tu aliyewiva na maslahi ya Zanzibar yakazingatiwa ipasavyo. As always mkristo, mhindu na msukusu wakieleza maoni yao kuhusu representation yao ni udini lakini waislamu wakilalamika wanalalamika kuhusu ukandamizaji dhidi yao.

Weka mbali, udini na ujinga mwingine, ukweli ni kuwa hakuna kipya kwenye tume ya katiba ya sasa. kazi yote ilifanyika na vipengele vyote vya katiba vinavyotakiwa kubadilishwa vinafahamika, so inawezekana kuwa ni mchezo unafanywa ili kujustify katiba itakayowafavour watawala.
 
Mzee Mtei,
Upande wa Waislam umetumia majina kuwajua ulivyokuja upande wa pili unasema kuna Wakiristo na wengine hawana dini...ebu tutajie nani hana dini kwenye hiyo tume ya mabadiliko ya katiba.
Barega
 
Mzee Mtei kaongea pointi 100%. Wanaompinga wanawaza tu kwenye dini. Kwa maana kuwa ndio wadini wenyewe. Je, ingekuwa tume ina wakristo asilimia 80 na akasema hilo ni dosari si hoja hiyo? Alichokikosea mzee huyu ni kwanini waislamu wanakuwepo wengi. Ni kwa sababu tume inazipa asilimia sawa Tanzania bara na visiwani. Hili ni kosa kubwa na limetumiwa makusudi na ccm. Hawa wenzetu wazanzibar wametumiwa tu kwa mgongo wa nyuma huku wakishangilia lakini hawajui malengo ya ccm ni nini. Na kwa kuwa wengi wao hawana maslahi yoyote na kuwepo Tanzania bara kwenye muungano huo muundo wa tume wanaufurahia. Utawafanikishia malengo yao lakini pia itafanikisha malengo ya ccm.
Mimi kwa kweli sina imani kabisa na tume hii. Tume inaongozwa na watu wa ccm, waliowahi kuwa viongozi wa ccm. Tume ingeajiri wataalamu wa katiba kuiongoza si wanasiasa hawa ambao chama chao ndio kizingiti cha katiba mpya.
 
naukumbuka vizuri sana huu uzi, uzi huu ni ushahidi wa udini wa chini kwa chini uliotamalaki nchini kwetu.
 
Back
Top Bottom