Tume ya mabadiliko ya katiba

Tume ya mabadiliko ya katiba

Pasco, mimi nakuandama kwa sababu wewe unajifanya kuwa well informed and knowledgable kuliko watu wengine kwa muda mrefu sasa. Lakini, bahati mbaya sana, wewe ni sawa na nabii wa uongo tu. Ninakumbuka mifano miwili ili kuthibitisha tuhuma yangu kwako:
(1) Ulisema: Kuna tume ya uchunguzi, iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ugonjwa wa Mh Dr Mwakyembe, na ya kwamba tutashangaa, Dr Mwakyembe hakuwekewa sumu, bali ugonjwa wake wa sasa unasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za ugonjwa wake alio nao kwa siku nyingi. Sasa hiyo tume haipo..na wewe ulitusihi kuvuta subira..thus, this is nonsense of yours
(2) Kama miezi miwili iliyopita kabla ya campaign za ubunge huko Arumeru, ulitabiri kuwa: "hadi sasa uchaguzi umekwisha, kinachongojewa ni kumtangaza tu Siyoi kama Mbunge wa Arumeru! Sasa hivi Mbunge ni Mh Nasari...Je, unabii wako uko wapi? Wewe ni nabii wa uwongo na unatuudhi sisi watu wazima

You are becoming too much on all false alarts & predictions..Pasco, stop it immediately .. its nonsense of you

Kule kwenye thread ya Mzee nimejibu na hapa najibu tena!

Kazi ya tume ni kukusanya maoni, hoja ya msingi sio dini za wajumbe wa hiyo tume bali competences zao!. Upatikanaji wa katiba nzuri, utategemea maoni tunayoyatoa na uwezo wa mkusanyaji kuya compile na sio dini yake!.
Pasco

Pasco, hapa unataka kutuaminisha nini tena? Kwani ni lini maoni ya wa-Tz yaliwahi kuzingatiwa? Multi-partism tulivote against it by 80% mbona hatukupewa? Mwaka juzi watu wali-vote out wabunge wengi wa CCM wakatangazwa kwa nguvu..nani anasikiliza wakulima na wafanyakazi siku hizi? Tunachoona sasa hivi ni viongozi kutumia udini, rushwa na maguvu ili kuendelea kubaki kwenye uongozi. Je, watu wanapoanza kuwa na mashaka na composition ya tume na kamati hizi wewe unafikiri wanaleta udini sana? No, udini umeleywa na hao unao wateetea. Wananchi sasa wamefahamu hila zao na wanataka kufahamu..wasikilizwe.

Ukiiangalia hiyo Kamati iliyoundwa unapata masuali mengi na mengine yameulizwa ..
(1) Je, kwanini Prof Shivj hakuwekwa kwenye hiyo Kamati? na sisi wote tunajuwa uzalendo wake na ufaham wake mkubwa katika mambo ya sheria na katiba? Je, ni kweli rais anataka Kamati yenye uwezo wa kufanya kazi ? au Kamati yenye uwezo wa kuibeba serikali tu
(2) Kwanini %-ge kubwa ya wajumbe wa Kamati ya Katiba ni kutoka chama tawala tu? Kwani Katiba tunayotaka ni ya CCM?
(3) Tatizo la uwingi wa wajumbe wa dini moja linaonesha mwendelezo wa mchezo na mbinu anazotumia Dkt Kikwete, na hii ndio sababu watu tunalalamika hapa. Kwa nini wewe unajifanya kuvaa miwani ya mbao? Je, unatafuta kupewa ubwabwa
(4) Uwepo wa Warioba na Dkt Salim haimaanishi hiyo Kamati ni nzuri na itakusanya maoni yetu bila hila za kuilinda CCM yako

..Natishwa na "the motive behind" wa hii karata ya udini kwenye tume ya katiba na sasa kuinganisha na suala la IOC na Mahakama ya Kadhi!. Mimi ni Mkisto tena Mkatoliki die hard!, kwenye suala la matumizi ya "protection", nimetofautiana na msimamo wa kanisa langu, vivyo hivyo sina tatizo na Tanzania kujiunga OIC au kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi, kwani mahakama hiyo ilikuwepo enzi za mkoloni, mahakama hiyo ipo Zanzibar, Kenya na Uganda!.Pasco

Wewe ni Mkatoliki kwa jina tu, lakini tayari umeukana u-Katoliki wako kwa kutofautiana na misingi ya kanisa. Wewe anza kuvaa baraghashia ili tukujuwe wazi. Usijifanye Mkatoliki die hard na mtetezi wa Mahakama ya Kadhi na OIC...unatuzuga tu hapa..

Kumbuka kuwa, sisi ni Tanzania, hatupo hapa kuiga kile kinachofanyika Kenya, Uganda, Zanzibar na serikali ya Mkoloni. Sisi tunataka Katiba inayotuunganisha kama nchi ili tukae kwa amani kama hapo awali. Mahakama ya Kadhi ni suala la kidini na wa-Islam hawazuiliwi kuanzisha hiyo Mahakama ya Kadhi. Hata wa-Katoliki wana Mahakama yao na Sharia (canons) zao lakini hawajalazimisha zitambuliwe katika sheria ya nchi na katiba.

Tanzania inafuata utaratibu wa kutenganisha serikali na dini. Nchi haina dini isipokuwa raia zake wana dini zao

Hivyo kitakachoingizwa kwenye katiba mpya hakitokani na wajumbe wengi ni wa imani gani, bali Watanzania waliowengi wanataka nini. Hata kama wajumbe wote 28 wa tume hiyo wangekuwa Wakristu, halamu maoni ya asilimia 30% ya Watanzania wakaitaka mahakama ya kadhi, mahakama hiyo itakuwepo!. Sambamba na suala la uwepo wa muungano, hata kama Wanzanzibari asilimia 99% hawaitaki na asilimia 0.1% tuu ndio wanautaka, muungano utaendelea!.

Kinachohitajika sasa more than anything else ni elimu kwa umma kuhusu zoezi hili!.

Please stop this "udini" nonsense!Pasco

Sasa hapo ndio unaongea nini sasa? Yaani hakuna uwezo wa kuleta mabadiliko, siyo? Yaani hata kama hatutaki Muungano hatutaweza kuuvunja? Hilo ndio tunaloogopa. Ndiyo maana tunaituhumu Kamati ilivyoundwa.

Elimu kwa umma ni pamoja na watu kuhoji composition ya Kamati. Tunahoji mambo yote bila mipaka ili tupewe majibu ya kuridhisha. Hapo nyuma tumevurugwa, na kupoteza imani na matumaini. Tuna mashaka na watu kama wewe wanaongea vitu ambavyo hawana uhakika navyo. Kesho mambo yakiwa tofauti hatuna pa kukuhoji na kukuwajibisha

ama kweli this is nonsense
 
sio ishu wazazi,hata wangejaa wapagani sawa tu
 
Muasis wa CHADEMA mzee MTEI,amesema kuwa tume ya katiba iliyoundwa hivi karibu na JK imejaa waislam wengi!
SOSI:JAMBOLEO
Mbona CDM ina wachaga na wakristo wengi na bado akina sie tusio wakristo na wachaga tunaipenda?? Aache fikra zake potofu na hii inapelekea tuwekee mashaka hata kuimani CDM yenyewe(hidden agenda). Siamin kama muasisi Mtei anaongea vapour hadharani kiasi hicho. Chamsingi ni kuangalia je haki itatendeka kny tume basi. Jirekebishe mzee Mtei.
 
WanaJF
Nimeshtushwa na taarifa zilizopewa uzito wa juu na gazeti Jambo Leo.Limeripoti katika habari kuu leo kwamba muasisi wa CDM Mzee Edwin Mtei ameiponda kamati ya katiba iliyoundwa na Rais kwa madai kwamba imejaza Waislam wengi kwa hiyo haifai na inapaswa kupingwa na watanzania wote hasa wakristo.

My Take.
Hii ni aina mbaya kabisa ya uandishi wa habari.Gazeti limeonyesha wazi linataka kufarakanisha watanzania kwa misingi ya dini.Pili gazeti linaonekana wazi kuichafua CDM katika jamii ya kiislam.Tatu gazeti linataka watu waache kujadili maudhui ya tume ya katiba badala yake lijadili dini za wajumbe.
Nadhani Mzee Mtei ajitokeze mbele ya wanahabari leo akanushe upuuzi huu wa Jambo Leo.
 
Source ya habari ni Jambo leo halafu mnahangaika kujibishana kweli?malengo ya gazeti hilo yanafahamika. Anaweza kuwa kaulizwa,jee mzee Mtei ktk kamati ile waislam na wakristo nani wengi? Unategemea jibu lingekuwa nini?sasa hilo jibu mwandishi mwenye malengo yake lina kuwa HEADING ya story yake. Mtei ni kubwa janja na hawezi kuzungumza kuwa na msimamo wa kidini katika siasa kiasi hicho.Hiyo habari ya Jambo Leo maLengo yake yanafahamika wazi.Ni mkakati maalumu ila wenye akili wanang'amua
 
Ni kweli haya maneno yalisemwa na Mzee Mtei, humu JF bahati nzuri yeye mwenye ndio alianzisha thread kwa ID yake.

Gazeti alijamchafua Mzee Mtei labda cha kushangaza tu hilo gazeti la Jambo Leo kuchukuwa habari zake JF.

Tafuta thread ya Mzee Mtei utakutana na hiyo habari.
 
JK kawapendelea waislam. Na hii ina implication kubwa sana...
 
Wenye tafakuri nzuri watajua Jambo leo ni wazushi haijalishi ni watu dini gani, na hao ndo tunaowitaji katika kipindi hiki.
(WATU WENYE KUTAFAKARI KWA MANTIKI NA SIO MSUKUMO WA UDINI)
 
Hao Jambo Leo wamefanya mahojiano na Mzee Mtei? Kuna mdau anatumia jina la Edwin Mtei hapa JF alitoa maoni kuhusu hiyo tume. Kama JF wametumia hiyo hoja ya Edwin Mtei wa JF bila kumhoji yeye binafsi basi ni tuna tatizo! Walitakiwa wamhoji Mzee Mtei mwenyewe na kujiridhisha kuwa hayo ndiyo maoni yake.
 
Ni kweli haya maneno yalisemwa na Mzee Mtei, humu JF bahati nzuri yeye mwenye ndio alianzisha thread kwa ID yake.

Gazeti alijamchafua Mzee Mtei labda cha kushangaza tu hilo gazeti la Jambo Leo kuchukuwa habari zake JF.

Tafuta thread ya Mzee Mtei utakutana na hiyo habari.

Weka link hapa mkuu
 
Source ya habari ni Jambo leo halafu mnahangaika kujibishana kweli?malengo ya gazeti hilo yanafahamika. Anaweza kuwa kaulizwa,jee mzee Mtei ktk kamati ile waislam na wakristo nani wengi? Unategemea jibu lingekuwa nini?sasa hilo jibu mwandishi mwenye malengo yake lina kuwa HEADING ya story yake. Mtei ni kubwa janja na hawezi kuzungumza kuwa na msimamo wa kidini katika siasa kiasi hicho.Hiyo habari ya Jambo Leo maLengo yake yanafahamika wazi.Ni mkakati maalumu ila wenye akili wanang'amua
Mkuu mzee Mtei anatakiwa akane hii kauli kama sio kweli vinginevyo ataanza kufukuza wanachama wake wa CDM nikiwemo mie mwenyewe na jopo lote la wapiganaji kata yetu. Huwa tunajitoa kupita kiasi hata kupelekea kuonekana watovu na waislamu wenzetu hasa kipindi kile cha uchaguzi iliposambaa habari CDM ni ya wakristo, lakini tulipuuza na kuiamini CDM, hii habari nimeisikia kijiweni kwetu ambapo waislamu ni wengi na pia kuna tawi la CDM jirani,nikasema nije JF nipate uhakika naiona sasa hii habari. I am shocked na hii news na tumekuwa dissapointed na mzee Mtei. Surely bila kuja kukana tutakuwa mbele kukilaani CDM na kuona ni wasaliti wa harakati zetu.No matter gazeti gani limeandika aje akane sababu kuchezea/kugusa imani ya mtu ni kitu hatari sana. Non sense Mtei na usipokuja utakuwa janga la taifa kama Lusinde.
 
Hilo gazeti wamechukua humu humu JF, hiyu thread imetumwa jana na mtu anayejiita Edwin Mtei.
Maxence una uhakika kweli huyo aliefungua hiyo ID ni Mzee Mtei mwenyewe??
Umejaribu kuwasiliana nae???
 
Hivi kiukweli z'bar hakuna wakristo. Maana serikali yote,bunge lote, tume ya katiba wote dini moja. Utasema hakuna cha kujadili hapa, acheni kufikiri kij....

Ametafuta akampata Jaji Brig. Augustino Ramadhani akampa umakamo angefanyaje sasa?
 
Mimi Ninachokijua kwa Zanzibar Kuna Minority Group ambao Ni Wakristu!! Sasa Katika uwepo wote wa ofa ya wajumbe 15 (Kumi na tano) wanashindwa hata kuwateua wakristu wawili (2) kuwakilisha Jamii ndogo ya Wakristu?? Kweli Hii sio sawa Kabisa!! Namuunga Mkono Mzee Mtei!!
 
Back
Top Bottom