Tume na Kamati hizi zote za nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume na Kamati hizi zote za nini?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Aug 16, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Natumaini kila mmoja ni mzima.

  Hivi Tanzania ni li-inji lililofilisika kabisa kuwa hakuna mwenye kufanya kazi mpaka tume au kamati iundwe?

  Majuzi kulikuwa na Tume ya Vazi la Taifa, wakimbiza upepo wetu Beijing nilitegemea wangekula Rubega, wamevaa trakisuti.

  Kamati ya Mwakyembe, Tume ya Bomani, Tume ya Epa, Tume ya kuchunguza Mgololo, Tume ya Muhimbili I ya mgonjwa wa kichwa kupasuliwa goti na wa goti kupasuliwa kichwa, sasa tume ya kuchunguza mgonjwa wa akili ambaye madawa yaliisha nguvu akachukua tayarodi na kubomoa wenzake ambao nao walifikiri ni maigizo mpaka pale waliporudisha namba!

  Bado kutakuwa na tume ya TFF kuchunguza Aden Rage kushinda TFF Tabora, Kamati ya kuichunguza Yanga kuwagomea Simba, Tume kumchunguza Mwanakijiji, FMES na Kuhani kwa nini hawaoni kwa jicho moja, na hata ile tume ya kumtafuta Mchungaji ipeni pesa nyingi tuu na Padiemu za kutosha!

  Tume ya Chura ilishamaliza kazi, tume ya Bunge kudai mjusi kafiri ujerumani bado haijaanza kazi, tume kuchunguza kauli ya Mfipa kuwa "Wagunya" hawana nchi, tume kuchunguza ushuzi wa Manji na Mengi upi unaharibu mazingira zaidi!

  Bado kuna Tume ya Wangwe kumchunguza marehemu na uhusiano wake na mtuhumiwa, tume ya Masau kutafiti kama kweli anajua kupasua moyo na THI yake, tume, kamat, tume, kamati, tumekamatitumekamatitumekamatiiii...

  What the heck? Sasa hata tume kuchunguza mahandaki yaliyoko kwenye barabara Dar!

  What in the hell is going on with Tanzania? nothing works efficiently and no one is accountable and responsible enough until a Kamati or a Tume is created!

  Naingia mafichoni wakati mnasubiri tume kuchunguza waliomdanganya Raisi kuwa Daraja limekamilika, Kamati kuuchunguza mtumbwi ambao ulikuwa umvushe mto na tume maalum kuchunguza kwa nini Wakwere ni waoga wa maji huku wamezaliwa kando ya bahari!

  Msisahau tume ya kuchunguza pesa alizopewa Mtikila na RA na Kamati ya kupinga mahakama ya Kadhi!

  Peace!

  By the way naunda tume kuchunguza kama kweli Mazese (Maxence DeMello) ameoa au ni danganya toto! ongezea kamati ya kumsaidia JMushi asifungiwe tena na wasiopenda wachaga!
   
  Last edited by a moderator: Aug 17, 2008
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Aug 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha mimi nadhani inabidi tuunde tume kukuchunguza mchungaji kwanini unapinga uundwaji wa tume muhimu katika Taifa letu.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tuanze kwa kamati ya kuchunguza matumbo ya hawa jamaa hapa chini, je ni Ufisadi au ni Kwashiakor, Utapiamlo...

  There is nothing muhimu again in Tanzania, if we had anything muhimu and we had right minds, attitude and focused, we would not have need a Tume or a Kamati for anything!

  [​IMG]
   
 4. m

  mgirima Member

  #4
  Aug 16, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUME ni njia mojawapo ya kuahirisha na hivyo kulivunja nguvu tatizo lililopo.

  Hivi ile ripoti ya TUME ya Brig. Mbita kuhusu mauaji ya Wapemba mwaka 2000 iliishia wapi au kujadiliwa na nani! Nakumbuka huyu bwana alitunukiwa ubalozi Zimbabwe baada ya hiyo ripoti.
   
 5. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #5
  Aug 16, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Rev. Kishoka,

  Hahahahaha..no comment.
  Jamaa wameshiba kupindukia..sidhani ni utapiamlo.
  Watamaliza nchi kabla vijana hawashika hatamu za uongozi jamani!!!

  Amani iwe nawe pia.
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mgirima,

  Ndiyo maana nauliza kwa nini watu wasifanye kazi zao inavyopaswa na si kusubiri Tume na Kamati zitoe mapendekezo ambayo ni kusema watu wafuate kanuni za kazi?

  Mfano wa BOT na EPA, wakaguzi wa Deloitte Touche walisema BOT hawafuati kanuni zao za kazi na kanuni na sheria za nchi na za mahesabu. Waziri na Gavana wakalalia chini, akaja Ludoviki Utouh akasema hilo hilo, bado Serikali ikakaa kimya na kuifanya hakuna kitu, ikaundwa tume ya Ernest and Young, ikatoa majibu yale yale waliyotoa Deloitte Touche na kisha Ludoviki, Kikwete kapewa faili, anaunda tume, ya Mwanasheria, Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Takukuru, kupitia waliyoyasema Deloitte Touche, CAG-Utouh na E & Y, kisha wafikire la kufanya!

  Njoo hili la Mgonjwa wa akili Muhimbili (Kichaa), je kilichotokea ni lazima kiundiwe tume kuchunguza sababu za mgonjwa wa akili kuchanganyikiwa zaidi na kupasua vichwa vya wenzake?

  Tayari tumesikia Kivuko huko Ruvuma au Mtwara kimezama, kisa matengi yanayowezesha Kivuko kuelea kwenye maji yametoboka na KUOZA, je tuunde tume kuchunguza ni vipi mtumbwi/stima/boti/merikebu/meli/mashua ulipata kutu na kuoza? je si wajibu wa wenye kumiliki kivuko hichi kukifanyia matengenezo na ukaguzi kila baada ya muda fulani ili kuhakikisha kuwa kivuko ni salama? Je kingezama huku kikiwa kimebeba abiria tungemtafuta mnunuzi kumlaumu kama tulivyofanya kudai Mzee Munanka ndiye alaumiwe kwa kuzama MV. Bukoba?

  Jamani si tuna methali, Kinga ni bora kuliko matibabu?

  Nanukuu kutoka magazetini kuhusu tume ya kumchunguza kichaa!

   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mara nyingi tume zinatumika kuhalalisha majungu.
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Juzi hapa kuna mnene mmoja wa polisi ameamuriwa arudishe gari alilonunua ktk mnada fake,ripoti ya tume iliyochunguza mauaji ya vijana wale anayo nani? Nashauri tuunde tume kuchunguza ile ripoti anayo nani.

  Tume ni nyingi mpaka basi.Kwa ufupi hiyo ndiyo bongo,aah nimesahau ile tume ya kuleta mvua toka Thailand iliishia wapi vile?
   
 9. C

  Choveki JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2008
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nadhani ni bora kwanza tuunde tume ya kuchunguza kama kuna umuhimu wa kuwa na tume zinazoundwa.
   
 10. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..za ku-past time!
   
 11. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Reverend,

  Ninakubaliana na wewe kwamba hizi tume na kamati zinazoundwa kila siku hazileti tija kwa sababu kwanza; Zimekuwa zikiundwa kwa wingi mno kila sensitive issues zinapolikabili taifa wakati the majority ya hizo issues zina-deserve kuwa dealt-with more effficiently kwa kutumia Presidential executive judgment. Na Pili; Zimeshaundwa tume nyingi ambazo zimetoa mapendekezo mazuri ambayo hayajafanyiwa kazi mpaka leo. Nafikiri kuna haja ya kuji-evaluate wenyewe kama kweli tunahitaji tume ili kupata recommendations za ku-solve problems, kitu ambacho mimi binafsi nakichukulia kwamba kina uwalakini.

  Mheshimiwa Reverend, naona ulipozungumzia tume umesahau kitu kimoja sugu ambacho kinali-cost taifa letu trillions of shillings ambazo zingeweza kuwa channeled elsewhere kuwapatia ahueni wananchi. Kuna kitu kinachoitwa "Committee Meetings" ambazo mwanzoni mwa mwaka huu, kwa mfano, tulisikia watu wa benki kuu wakikizungumzia kwamba kitu hiki kinai-cost benki kuu billions of shillings. Swali langu kwenye suala hili ni - Wafanyakazi taasisi mbalimbali katika nchi yetu (mfano wakurugenzi, mameneja ama wakuu wa vitengo) mara kadhaa huwa wanachaguliwa kwenye special committees katika sehemu zao za kazi kutengeneza ama kurekebisha miongozo/taratibu za taasisi zao. Watu hawa hukutana mara kadhaa, tena katika mda wa kazi (sio weekends), kutengeneza hizo taratibu. Mara zote wanapokutana, hata kama ni kwa nusu saa, huwa wanalipwa mapesa mengi ambayo mtu ukitumia akili nzuri utaona kwamba hawa watu hawakupaswa kulipwa hayo mapesa kwa sababu walikuwa wakitekeleza majukumu ya kuajiriwa kwao ambayo mara zote huwa yamewekwa wazi kwenye job descriptions zao kabla watu hawa hawajaajiriwa. Don't you see mheshimiwa Reverend kwamba hapa kuna tatizo kubwa sana ambalo ni rahisi mno kuli-solve? Why hawa watu walipwe extra money kutekeleza majukumu yao wanayoyatekelewa katika mda wa kazi?

  Mungu ibariki Tanzania
   
 12. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #12
  Aug 17, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kila Jamii Duniani Inaishi Kwa Uhuru Na Utashi Wake Tanzania Pia Ni Jamii Nayo Inaishi Kwa Uhuru Na Utashi Wake , Kuunda Kamati Ni Uhuru Wa Jamii Ya Watanzania Wao Ndio Wanalilia Kamati Kila Kitu Kikitokea Wao Ndio Wamepiga Kura Kuwaingiza Hawa Madarakani Wakati Wanapiga Kura Walikuwa Na Utashi Fulani Hivi Walikuwa Wanajua Yote Haya Yatatokea Sasa Kwanini Tulalamike

  Hata Wewe Kishoka Si Ulipiga Kura ?
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Shy,

  Hivi nilimchagua nani vile? nikumbushe basi!
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ufufuko,

  Hilo suala la watu kulipwa ujira wa ziada kufanya kazi zao nimelisema mara nyingi. Hata katika Waraka wa Mchungaji, nimeliongelea kwa kina.

  Tunajihujumu wenyewe kwa kuweka mianya mibovu ya ulaji na uzembe ili kukidhi ufinyu wa mishahara.

  Watu hawataki kufanya kazi zao za kawaida lakini wanakimbilia kugombea kuwa kwenye Tume, Kamati, Kamisheni na bodi za ukurugenzi!

  We need strong reforms Tanzania, we need mental reforms to become progressive!
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu Shy,
  Hao watanzania wanaolilia kuundwa kamati hizo ni akina nani na walilia kupitia forum ipi?
  Kuna kamati za bunge - hizo kweli ni " watanzania" kwa maana wawakilishi wao - wabunge
  Je hizo za kuangalia kwanini jengo la ghorofa kadhaa liliangua na kuua watu; kichaa kaua wenzie wodini,na nyinginezo wewe kama mtanzania mlipa kodi - kodi hii itakayawalipia ada ya kuketi wanapojadili uliulizwa ukaafiki kuundwe tume??

  Na ukichunguza nani wanakuwemo kwenye hizo tume - ni mada nyingine tena. Iweje wawe ni walewale? na je kwanini wigo wa ushiriki kwenye hizo tume haupanuliwi kusudi hata akina pangu pakavu nitilie mchuzi washiriki au mawazo yao hayana maana? i dont think u need rocket science kupata majibu ya masuala yanayochunguzwa kwenye hizi "tumechoka" na "kamatika"
   
 16. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  mradi wa kula na kutafuta scapegoats
   
 17. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hizi tume ni mbinu ya kufunika kombe mwanaharam apite. Si kwa nia ya dhati ya kutatua kero na matatizo ya watanzania. Kila inshu inayohusu maslahi ya wanyonge utasikia inaundwa tume. Lakini ikitokea inshu inayotishia maslahi ya wakubwa, utaona hatua zinachukuliwa bila hata kamati au tume kuundwa. Huu ni ubabaishaji. Jamani mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenzake, sana atamuonesha njia ya kutokea. CCM hawaaminiki tena, wameshashindwa kuongoza ila hawataki kukiri, kazi yao ni kuiba kura na kung'ang'ania madaraka basi, uongozi kwao ni ajira na si kuonesha njia, ndo sababu wanafanya uozo mtupu. Watanzania tuamke sasa na kwa kuanzia tuwaoneshe hasira zetu 2010 ndo watapata adabu na kujifunza kuwa hawana hati miliki ya uongozi ktk taifa hili. Mungu wabariki watanzania wananchi na si viongozi wa CCM. Amin.
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Aug 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tume Hizo Zitaendelea Kuundwa Na Kuwepo Ili Mradi Watanzania Wameridhia Na Kutaka Wenyewe , Serikali Haijalazimisha Tume Na Hao Hao Wananchi Ndio Wametaka Ziundwe Kwahiyo Kwahiyo Kama Hle Zinaliwa Kila Mtu Na Kamba Yake Kama Wewe Yako Fupi Jitahidi Kuikata Kidogo Kidogo
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Aug 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wewe Si Ndio Ulipigia Kura Ccm Na Kuhubiri Makanisani Kuhusu Unabii Wa Kikwete ?

  Sasa Muache Yeye Na Watu Wake Watimize Torati
   
 20. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hizi tume zinaundwa ili watu wapate sitting allowance na fedha za ziada ili wapate fedha kwa ajili ya kumalizia vibanda vyao.
  They are always full of crap!
   
Loading...